Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Katika hali iliyoshangaza wengi, Waziri wa Vijana nchini Uganda ametoa ufafanuzi wa kutatanisha kuhusu sababu za kukatika kwa huduma ya mtandao wakati huu wa mchakato wa uchaguzi mkuu nchini humo.
Soma pia: Uganda yatangaza kuzima Intaneti kuanzia leo Januari 13 ili kupisha Uchaguzi Mkuu
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha taifa (UBC), Waziri huyo alibainisha kuwa awali Kamisheni ya Mawasiliano ya Uganda (UCC) ilitangaza kuzima mtandao kwa kile kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiusalama, lakini akashangaza wengi kwa kuongeza madai mapya kuwa hitilafu hiyo inatokana na sababu za kiufundi. Waziri alidai kuwa amepata taarifa kuwa meli iliyokuwa ikipita katika pwani ya Mombasa nchini Kenya ilikata kebo kuu ya mtandao vipande viwili, na hivyo kusababisha nchi nzima kukaa gizani kidijitali.
Licha ya mwandishi wa habari kuhoji kuhusu uhalali wa taarifa hizo na uhusiano wake na mchakato wa uchaguzi, Waziri alisisitiza kuwa mafundi wako kazini usiku na mchana kujaribu kuunganisha kebo hiyo, akitabiri kuwa huduma hiyo inaweza kurejea ndani ya wiki moja au mbili.
Katika kile kilichoonekana kama dongo kwa vijana, Waziri aliwataka raia kuwa na subira na kumwamini Rais, akidai kuwa kiongozi huyo ndiye aliyeleta teknolojia hiyo nchini na ndiye atakayeirejesha. Alimalizia kwa kuwakosoa vijana kwa kutumia muda mwingi kwenye mtandao wa TikTok badala ya kusikiliza jumbe za kiongozi wa nchi, huku akiwakumbusha kuwa enzi za nyuma nchi ilikuwa ikijiendesha bila mtandao, hivyo hali ya sasa isichukuliwe kama jambo la ajabu.