Sintofahamu ya alipo makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Ndg. Sosopi


Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,528
Likes
27,499
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,528 27,499 280
TAARIFA KWA UMMA​

KUHUSU SINTOFAHAMU YA ALIPO MAKAMU MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA NDG. SOSOPI

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) taifa, Tanzania Bara, Ndugu Sosopi hajulikani aliko tangu jana Jumapili majira ya saa 3 usiku alipopakiwa ndani ya gari linaloaminika kuwa la Jeshi la Polisi wilayani Iringa kwa ajili ya kupelekwa Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Iringa (OCD) Afande....

Siku ya jana Jumapili, Juni 26, 2016, Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Sosopi baada ya kuhudhuria mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi walio wanachama wa CHADEMA (CHASO) Mkoa wa Iringa ambako yeye alikuwa Mgeni Rasmi akiambatana na Wabunge Peter Msigwa (Iringa mjini) na John Heche (Tarime Vijijini), Mratibu wa Uhamasishaji na Uenezi BAVICHA Taifa, Edward Simbeye na makamanda wengine, aliitikia wito wa Jeshi la Polisi mkoani humo kufika Kituo Kikuu kwa ajili ya mahojiano.

Mkuu wa Kituo Kikuu, Afande Thadei alidai kuwa alikuwa amepewa amri na RPC Sakamba Peter ya kumfikisha Sosopi kituoni hapo kutokana na kosa alilodaiwa kulifanya nje ya Mkoa wa Iringa na kwamba polisi walikuwa wakimtafuta kwa muda mrefu.

Akiwa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani Iringa, RPC aliwaambia kuwa Sosopi anatakiwa kwenda kujibu tuhuma za kauli za uchochezi alizotoa akiwa Dar es Salaam. Hivyo polisi Mkoa wa Iringa wao wanasubiri maagizo tu ya kumsafirisha kwenda huko anakotuhumiwa kufanya kosa ambako angefanyiwa mahojuano.

Viongozi wa chama, wabunge na wanachama wengine walikuwa pamoja nae kituoni, walikuwa tayari kumdhamini ili aondoke kisha arejee leo Jumatatu, Juni 27, kuripoti na kusubiri maelekezo yoyote yatakayokuwepo kuhusu hizo tuhuma.

RPC Kakamba amedaiwa kujibu kuwa yeye hakuwa na tatizo iwapo tu OCD wa Iringa ambaye ndiye mwenye wajibu wa kumshikilia na kumsafirisha Sosopi ataridhia ombi la dhamana hiyo.

Wakati viongozi hao wakijiandaa kuambatana na RPC na OCS kwenda kwa OCD, ilifika gari moja yenye namba za kiraia T 134 CJX RandCruiser, ikiwa na askari 6, wanne wakiwa nyuma ya gari, wawili (pamoja na dereva) wakiwa mbele. Wote 6 walikuwa na silaha.

Sosopi akaamriwa kuingia ndani ya gari hiyo. Tayari kwa safari iliyodhaniwa kuwa ni kwenda ofisini kwa OCD.

Katika hali iliyowashangaza viongozi wenzake aliokuwa nao ambao walikuwa wako kwenye gari jingine, gari ile iliyombeba Sosopi iliondoka kwa kasi ya ajabu ambayo haikutarajiwa hivyo haikuwa hata rahisi kuifuatilia na kujua ilikoelekea.

Hadi taarifa hii inaandikwa muda huu saa 11 jioni ya Jumatatu, Sosopi hajulikani aliko tangu jana saa 3 usiku alipochukuliwa na gari hilo kuelekea kusiokujulikana. Jitihada za Uongozi wa BAVICHA taifa kuwasiliana na Jeshi la Polisi kupitia ZCO kujua kama kiongozi huyo amefikishwa Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na pengine kupelekwa mahakamani hazijazaa matunda ya kujua hasa Sosopi yuko wapi hadi muda huu.

BAVICHA inalitaka Jeshi la Polisi kumleta Dar na kumhoji kwa mujibu wa sheria au kumuachilia huru kwa kuwa ni wazi hakuna sababu ya kuendelea kumshikilia kwa siku ya pili mfululizo.

Kama hadi kesho haitajulikana alipo, mawakili wetu kwa kushirikiana na wale wa chama watapeleka maombi ya Habeas Corpus dhidi ya RPC na RCO Iringa alikokamatiwa na ZPC na ZCO Dar es Salaam, wanaoonekana kufahamu alipo.

Imetolewa leo Jumatatu, Juni 27, 2016

Ofisi ya Katibu Mkuu BAVICHA
 
Shindu Namwaka

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2014
Messages
4,838
Likes
2,960
Points
280
Shindu Namwaka

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2014
4,838 2,960 280
Du sijui kapelekwa wapi?
 
mr gentleman

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Messages
2,700
Likes
2,950
Points
280
Age
34
mr gentleman

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2012
2,700 2,950 280
Huyu ndio alikuwa anahamasisha vijana nchini kote waue polisi, ukatili hauepukiki kwa watu wakorofi.
 
M

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
8,138
Likes
5,191
Points
280
M

Molembe

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
8,138 5,191 280
Kwa matamshi yale jamaa alikosea sana polisi wengi ni makamanda pale wanatumwa hawawezi kukataa.
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,431
Likes
31,659
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,431 31,659 280
Umafia mwingine hauna hata maana!! Sasa hizo kauli zake zingeleta effect gani?
 
L

LOMAYANN

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
1,164
Likes
115
Points
160
L

LOMAYANN

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
1,164 115 160
Kama kweli hiyo imetokea mikononi mwa Polisi its very danger now. Mimi naamini Polisi is a safe place for any innocent person.
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,922
Likes
1,577
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,922 1,577 280
Nendeni Dar mtamkuta anandika maelezo ya uchochezi wake.
 
Sharif

Sharif

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2011
Messages
2,474
Likes
1,660
Points
280
Sharif

Sharif

JF-Expert Member
Joined Mar 13, 2011
2,474 1,660 280
mh !
nilishangaa kijamaa fulani hakijui kizungu lakini kina force kutumia kizungu..
eti jeshi la polisi ni "neutral"
anajua maana ya neutral ?
angejiuliza swali dogo tu..
kuanzia mwaka 2000,jeshi hilo limeshaua CCM wangapi na upinzani wangapi ?
mikusanyiko mingapi ya upinzani ilipigwa mabomu mwaka jana na CCM mingapi ?
namsaidia takwimu..JANUARY 27 2001 pekee waliua wafuasi wa CUF wasiopungua 70 kisiwani Pemba..
 
M

Manosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2012
Messages
4,392
Likes
2,420
Points
280
M

Manosa

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2012
4,392 2,420 280
Siku hizi kukosoa kumebadilika jina kunaitwa uchochezi
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
31,882
Likes
65,438
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
31,882 65,438 280
Niombeenii!!!!
 
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
31,882
Likes
65,438
Points
280
S

Salary Slip

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2012
31,882 65,438 280
mh !
nilishangaa kijamaa fulani hakijui kizungu lakini kina force kutumia kizungu..
eti jeshi la polisi ni "neutral"
anajua maana ya neutral ?
angejiuliza swali dogo tu..
kuanzia mwaka 2000,jeshi hilo limeshaua CCM wangapi na upinzani wangapi ?
mikusanyiko mingapi ya upinzani ilipigwa mabom mwaka jana na CCM mingapi ?
namsaidia takwimu..JANUARY 27 2001 pekee waliua wafuasi wa CUF wasiopungua 70 kisiwani Pemba..
Natamani kumtaja
 
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
13,355
Likes
720
Points
280
M

Molemo

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
13,355 720 280
Hii hali inatia wasiwasi sana.Ni aibu kubwa katika zama hizi za demokrasia.Ee Mungu tusimamie
 

Forum statistics

Threads 1,237,969
Members 475,809
Posts 29,308,205