Kuna mtu namfahamu anadai Tshs Mil. 380, ameachishwa kazi baada ya ya kampuni aliyokuwa anafanyia kazi kuyumba kiuchumi, alikuwa ni mtu mwenye hali nzuri sana, lakini anavyoteseka sasa inatia huruma.
Amefuatilia madai yake bila mafanikio. Anaambiwa mpaka afikishe miaka 55! Mtu ana familia, anasomesha, ana majukumu mengine kibao, hakutarajia kuachishwa kazi wala sio kwamba yeye alitaka. Tufanye kuachishwa kazi sio tatizo, lakini je, hela yake halali aliyoikusanya kwa mfumo wa kuweka akiba kwa nini asipewe? Hiyo hela anaomba akopeshwe au ni haki yake? Kwa nini anyimwe?
Inaingia akilini kuwa wabunge walisoma kabisa hiyo sheria na kuunga mkono? Mtu aachishwe kazi halafu anyimwe mafao mpaka afikishe miaka 55, kwa maisha haya ya Tanzania ya leo ambapo maisha ya watu ni magumu sijawahi kuona?
RODRIGUEZ NORIEGA DUERTET hebu niambie ingelikuwa wewe ungalifanyaje?