Sintofahamu kuhusu kuchukua mafao mifuko ya jamii

Joined
Mar 26, 2018
Posts
72
Reaction score
59
Habarini wana jamvi,

Kuna kitu sijaelewa kuhusu mifuko ya jamii na suala zima la kuunganisha mifuko ya jamii, kwa update nilizoona kuna mfumo uko indicated by picture ukionyesha SSRA(Regulatory Authority),ndo mfuko mama ukiwa na watoto wawili PSSF(Public Sector) na NSSF(Private Sector), PSSF na NSSF na wana watoto watatu kila mmoja ikiwa na maana PSSSF watoto wake ni PPF/LAPF/GEPF na NSSF watoto wake ni PPF/LAPF/GEPF.

Kuhusu mchanganu wa stucture yake haina shida sana, ila nimejaribu kuchimba sheria zipi zinaaply wakati mtu ukiwa unataka kupata mafao yako baada ya kuacha, kusimamishwa au kufukuzwa bado sijapata clear information ila nna case study mbili.

1.Dada yangu alikuwa anafanya kazi NMB alikuwa akitumia mfuko wa NSSF, baadae akaona maslahi ni madogo hivyo akaamua kuachana na kazi na kutafuta njia mpya ya kutafuta riziki yake,alifuatilia mafao yako NSSF akaambiwa mpaka afikishe umri wa miaka 55.Akaendelea kufuatilia maslahi yake kiasi cha kwenda kwa mkuu wa mkoa Mh. Makonda lakini at the end majibu yakawa ni yaleyale.

2.Rafiki yangu alikuwa akifanya kazi katika kampuni changa ya simu hapa Tanzania alikuwa LAPF, kutokana na msongo wa maisha na kutokuelewana na mabosi zake akaamua kubwaga manyanga lakini last month alifuatilia mafao yake kiasi cha Tsh. 5,000,000 na kufanikiwa kupata ela zake bila tatizo lolote.

Kwa kutumia hizo casy study hizo mbili nimeshindwa kuelewa je ile sheria ya kuchukua mafao ni mpaka miaka 55 imeshasainiwa na Mh. Rais wa wanyonge au bado? Pia napenda kujua kwanini treatment kwenye mifuko zinakuwa tofauti? Wengine kama NSSF/PSPF wanakwambia mpaka ufikishe miaka 55, wengine wanatoa?

Kwa ambaye anafahamu ili suala kiundani naomba ufafanuzi ili niweze kujua au mwenye document zinazoonyesha sheria na taratibu za kuchukua mafao za sasa naomba atume hapa japo nipate uhakika kuhusu ili suala.

MWISHO.
Hivi Watanzania tumelogwa na nani? Wabunge wetu ni wasomi kweli au zuga? Unapomwambia mtu kuchukua mafao yake ni mpaka akifikishe miaka 55, je sisi tuliofanya kazi mwaka mmoja na mikataba yetu kukatishwa na kwenye mifuko yetu ya jamii tuna 1.5 milioni, Je milion 1.5 ya mwaka wa 2018 itakuwa na uwiano gani na 1.5 ya mwaka 2045 wakati nitapofikisha umri wa miaka 55.

Mpaka mwaka 2045 milioni 1.5 itakuwa ni ela ya kuendea sokoni kutafuta vitu vya kupika au kuendea kunywa bia mbili na kongoro, kwanini wasinipe wakati ambao inaweza kununua Bodaboda au kufungua genge la nyanya na vitunguu.
Akili zetu huwa tunaziweka wapi wakati tunatunga sheria za nchi hii
 
Mkuu hili ni janga kubwa mno. Sheria kandamizi zinaua ndoto za watanzania. Kwa nia njema kabisa niombe washauri wa Rais watumie busara zao katika kuwasilisha uhalisia wa maisha ya mtanzania wa hali ya chini na sio kuwasilisha vitu vya kusadikika.
 
wanaelewa kabisa ni sheria kandamizi lakini wanafanya makusudi tu.
 
Wasikuzingue sana hao NSSF, wakikuambia mafao mpaka kustaafu waambie waanze kukulipa fao lako la kutokuwa na ajira, watakuzungushia hapo na wakikuona n muelewa wa hayo mafao watakupa chako mapema
 
Serikali dhalimu kila siku Ina angalia namna ya kumkandamiza mwananchi badala ya kumpunguzia kero na kumletea unafuu wa maisha!!!!!

Wanasiasa wanajilipa mishahara mikubwa na malupu lupu ya kutisha!!!! Huku wakiwa acha wananchi wakiangamia kwa ahadi tamu za uongo!!!!!

Kero na mabalaa kwenye nchi hii kamwe hayatakwisha mpaka pale ambapo sisi wananchi ambao ndio wahanga wa kwanza wa madhila ya hii serikali dhalimu na wanasiasa kwa ujumla tutakapo sema kuwa imetosha!!!!!......

HAKI HAIOMBWI BALI HUPIGANIWA
 
Habarini wana jamvi,

Kuna kitu sijaelewa kuhusu mifuko ya jamii na suala zima la kuunganisha mifuko ya jamii, kwa update nilizoona kuna mfumo uko indicated by picture ukionyesha SSRA(Regulatory Authority),ndo mfuko mama ukiwa na watoto wawili PSSF(Public Sector) na NSSF(Private Sector), PSSF na NSSF na wana watoto watatu kila mmoja ikiwa na maana PSSSF watoto wake ni PPF/LAPF/GEPF na NSSF watoto wake ni PPF/LAPF/GEPF.

Kuhusu mchanganu wa stucture yake haina shida sana, ila nimejaribu kuchimba sheria zipi zinaaply wakati mtu ukiwa unataka kupata mafao yako baada ya kuacha, kusimamishwa au kufukuzwa bado sijapata clear information ila nna case study mbili.

1.Dada yangu alikuwa anafanya kazi NMB alikuwa akitumia mfuko wa NSSF, baadae akaona maslahi ni madogo hivyo akaamua kuachana na kazi na kutafuta njia mpya ya kutafuta riziki yake,alifuatilia mafao yako NSSF akaambiwa mpaka afikishe umri wa miaka 55.Akaendelea kufuatilia maslahi yake kiasi cha kwenda kwa mkuu wa mkoa Mh. Makonda lakini at the end majibu yakawa ni yaleyale.

2.Rafiki yangu alikuwa akifanya kazi katika kampuni changa ya simu hapa Tanzania alikuwa LAPF, kutokana na msongo wa maisha na kutokuelewana na mabosi zake akaamua kubwaga manyanga lakini last month alifuatilia mafao yake kiasi cha Tsh. 5,000,000 na kufanikiwa kupata ela zake bila tatizo lolote.

Kwa kutumia hizo casy study hizo mbili nimeshindwa kuelewa je ile sheria ya kuchukua mafao ni mpaka miaka 55 imeshasainiwa na Mh. Rais wa wanyonge au bado? Pia napenda kujua kwanini treatment kwenye mifuko zinakuwa tofauti? Wengine kama NSSF/PSPF wanakwambia mpaka ufikishe miaka 55, wengine wanatoa?

Kwa ambaye anafahamu ili suala kiundani naomba ufafanuzi ili niweze kujua au mwenye document zinazoonyesha sheria na taratibu za kuchukua mafao za sasa naomba atume hapa japo nipate uhakika kuhusu ili suala.

MWISHO.
Hivi Watanzania tumelogwa na nani? Wabunge wetu ni wasomi kweli au zuga? Unapomwambia mtu kuchukua mafao yake ni mpaka akifikishe miaka 55, je sisi tuliofanya kazi mwaka mmoja na mikataba yetu kukatishwa na kwenye mifuko yetu ya jamii tuna 1.5 milioni, Je milion 1.5 ya mwaka wa 2018 itakuwa na uwiano gani na 1.5 ya mwaka 2045 wakati nitapofikisha umri wa miaka 55.

Mpaka mwaka 2045 milioni 1.5 itakuwa ni ela ya kuendea sokoni kutafuta vitu vya kupika au kuendea kunywa bia mbili na kongoro, kwanini wasinipe wakati ambao inaweza kununua Bodaboda au kufungua genge la nyanya na vitunguu.
Akili zetu huwa tunaziweka wapi wakati tunatunga sheria za nchi hii
Aliekwambia SSRA ni mfuko wa pensheni ni nani?

Mifuko minne imeunganishwa na kuwa mfuko mmoja. Hayo matawi sijui umeyatoa wapi. Mifuko iliyounganishwa(iliyofutwa) ni PPF,PSPF,LAPF na GEPF na hivyo kuunda PSSSF mbayo itakua ikishughulika na watumishi wa uma na agency zake.
NSSF itakua ikishughulika na wafanyakazi wa sekta binafsi.

Huyo alieambiwa mpaka miaka 55 ndio alipwe mafao(kama ni kweli) mwambie aende akashtaki SSRA na sio kwa mkuu wa mkoa.
 
Bado kuna sintofahamu kubwa miongoni mwa wafanyakazi juu ya hii mifuko!
 
Aliekwambia SSRA ni mfuko wa pensheni ni nani?

Mifuko minne imeunganishwa na kuwa mfuko mmoja. Hayo matawi sijui umeyatoa wapi. Mifuko iliyounganishwa(iliyofutwa) ni PPF,PSPF,LAPF na GEPF na hivyo kuunda PSSSF mbayo itakua ikishughulika na watumishi wa uma na agency zake.
NSSF itakua ikishughulika na wafanyakazi wa sekta binafsi.

Huyo alieambiwa mpaka miaka 55 ndio alipwe mafao(kama ni kweli) mwambie aende akashtaki SSRA na sio kwa mkuu wa mkoa.
brother SSRA ni Regulatory authority na mchanganuo nlioutoa ni current updated
 
Hivi wabunge waliotunga (au kukubali kutungwa) hizo sheria nao wanangoja mpaka wafikishe miaka 55 ndio wapate mafao yao au zao wanachukua baada ya miaka mitano (lakini za wengine zingoje mpaka wastaafu) ? Kama kuna anayefahamu naomba atueleweshe
 
Mkuu hili ni janga kubwa mno. Sheria kandamizi zinaua ndoto za watanzania. Kwa nia njema kabisa niombe washauri wa Rais watumie busara zao katika kuwasilisha uhalisia wa maisha ya mtanzania wa hali ya chini na sio kuwasilisha vitu vya kusadikika.
Sheria huwa zipo kuwakandamiza wanyonge watungapo huwa udhani haziwahusu wakishatoka kwenye system uanza tena kujutia Sheria hizo.Hakuna sehemu yeyote duniani mafao yako upewe ukifika miaka 55,kionekanacho ni kwamba hawana hela walizani no zitasomwa na wa chini ni hadi juu.Wafanye mifuko iwe ni hiari kujiunga na sio lazima. Miaka 55 atafika nani,hata ukifika unapewa hela bila riba tena unakatwa tena kodi hali wameizungushia hela yangu wakati ningewekeza ningewezapata mara kumi ya hio.
 
Nchi hii imejaa mambumbu sana, wasomi na wasio wasomi karibia wote uelewa wao wa mambo ni mdogo sana.
Hivi kama huyo mdada anayekwenda kwa Makonda kuishitaki NSSF anajitambua kweli?
Kila siku nasema kuwa somo la sheria lifundishwe kuanzia Primary.
Na umbumbumbu wa watu wanasiasa hugeuza fursa.
 
Kuna mtu namfahamu anadai Tshs Mil. 380, ameachishwa kazi baada ya ya kampuni aliyokuwa anafanyia kazi kuyumba kiuchumi, alikuwa ni mtu mwenye hali nzuri sana, lakini anavyoteseka sasa inatia huruma.

Amefuatilia madai yake bila mafanikio. Anaambiwa mpaka afikishe miaka 55! Mtu ana familia, anasomesha, ana majukumu mengine kibao, hakutarajia kuachishwa kazi wala sio kwamba yeye alitaka. Tufanye kuachishwa kazi sio tatizo, lakini je, hela yake halali aliyoikusanya kwa mfumo wa kuweka akiba kwa nini asipewe? Hiyo hela anaomba akopeshwe au ni haki yake? Kwa nini anyimwe?

Inaingia akilini kuwa wabunge walisoma kabisa hiyo sheria na kuunga mkono? Mtu aachishwe kazi halafu anyimwe mafao mpaka afikishe miaka 55, kwa maisha haya ya Tanzania ya leo ambapo maisha ya watu ni magumu sijawahi kuona?

RODRIGUEZ NORIEGA DUERTET hebu niambie ingelikuwa wewe ungalifanyaje?
 
Serikali imechezea pesa ss haina za kuwalipa watu wanakuja na miaka 55,.hatutokubali
Hio sheria ifanyiwe ammendment
 
Itabd wafanyakazi kusign petition ya kutaka mabadiliko ktk hio sheria...ss sijui nani aanzishe ila acha watu waisome namba watajiorganize tu
 
Serikali inakopa hii mifuko Trillions of money hairejeshi watawalipa nini mkidai?.,

Sidhani kama kuweka miaka 55 ndo suluhu,unaahirisha tu tatizo binafsi sikubaliani abadani na huo utaratibu
Esp kwa wale wenye kazi za mikataba inawaumiza mno
 
Back
Top Bottom