Sintofahamu kifo cha kijana Kigamboni

Sintofahamu kifo cha kijana Kigamboni

CCM ni adui wa nchi hii, sote tulitambue na kulikubali hilo, hakutakua na uhuru wala haki kama tutaendelea kuwa chini ya huyu adui wa nchi.
 
Hivi askari hawana ndugu wala jamaa zao...?
 
Albadiri moja tu mama utusafishie watu na vizazi vyao..upanga kwa upanga,jicho kwa jicho,jino kwa jino....
Hakuna kitu kinauma kama mzazi kumpoteza mtoto wake tena kupitia sehemu aliyokuwa akidhani ni salama.
Hali hiyo imemkuta Edna Clement, mama wa watoto wanne ambaye kwa sasa yupo katika kipindi kigumu cha kumpoteza mwanaye wa kwanza, Innocent Vitus kutokana na kile kinachodaiwa alishambuliwa na wananchi wenye hasira.

Edna na watoto wake wanaishi eneo la Kibugumo, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Ilikuwa Alhamisi saa 2:00 usiku nilisikia kijana wangu wa pili akaniita mama kaka kakamatwa na polisi, nilikimbia hadi kwenye lile gari na kuwauliza wanakompeleka mwanangu usiku wakaniambia mwanangu hayumo,” alisimulia Edna na kuongeza: “Nikamuuliza mdogo wake mbona simuoni akasema mama yupo huwezi kuona vioo ni vyeusi basi gari ikaondoka, kwa mbele kidogo ili igeuze nikasimama katikati ya barabara nikawaambia sitoki hadi mniambie mnakompeleka, wakasema kituo cha polisi.”

Alisema wakati ya gari linaondoka aliwasiliana na baadhi ya ndugu zake waliomsihi kutulia ili wafuatilie.
Hata hivyo, Edna alisema usiku huohuo aliamua kwenda kituo cha polisi na saa 4:00 usiku alishuhudia kijana wake akiingizwa mahabusu ya kituoni hapo.

Alisema alirudi nyumbani na Agosti 30 saa 4:00 asubuhi alimpelekea chai lakini alishangaa kusikia kuwa hawezi kutembea. “Alipoitwa mmoja wa mahabusu aliniambia ‘mama huyu kaumia mguu hawezi kutembea’, hivyo akaingiza chai na kumpatia, niliomba RB nijue ni nani aliyemkamata na kosa lake,” alisema.

Alisema aliandikiwa jina la mpelelezi alipoingia ofisini kwake alimuuliza jina la mtuhumiwa, lakini alimwambia hana taarifa zake wala hajakabidhiwa jalada la kesi hiyo.
Alisema Agosti 31, alipeleka tena chai lakini kijana wake alipoitwa na askari wa zamu hakuiti, jambo hilo lilimfanya na yeye (Edna) kuanza kuita bila mafanikio huku mahabusu mmoja akijibu tena kuwa alitolewa tangu Alhamisi saa 10:00 jioni na hakurudishwa.

Alisema aliombe namba ya mpelelezi alipompigia alimweleza kuwa kesi ngumu hawezi kuisimamia kwa sababu haina jalada na kwamba, baada ya kufuatilia walimwambia walimtoa mahabusu akataka kukimbia.

Polisi watupiana mpira

Septemba 2, gazeti hili lilimtafuta kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuthibitisha tukio hilo lakini alijibu: “Nipo likizo wasiliana na mtu niliyemuachia madaraka.”

Baada ya kuwasiliana na ofisi ya Mambosasa, walimwelekeza mwandishi kuwasiliana na kamanda wa polisi mkoa wa Temeke ambaye naye alidai hana taarifa hizo. “Naomba niwatafute eneo husika ambao ni Kigamboni niweze...uwe mvumilivu na kesho unipigie,” alisema Amon Kakwale ambaye ni kamanda wa polisi Temeke.

Septemba 3, simu yake ilipopigwa ilipokewa na msaidizi wake ambaye alidai kamanda yuko kikaoni huku akimtumia mwandishi namba ya simu ya mkuu wa kituo cha polisi Kigamboni kurahisisha upatikanaji taarifa. Hata hivyo, mkuu huyo wa kituo alisema: “Anayeweza kuzungumzia hayo ni RPC Temeke naomba umtafute kwa sababu ndiyo nasikia kutoka kwako, wasiliana naye ila mimi kwa kweli sijui.”

DC akataa kuzungumzia
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri alipopigiwa simu alisema msibani mkoani Mwanza. “Mambo ya kesi nendeni kwa OCD niko msibani Mwanza,” alisema Sarah.

Mazishi utata

Awali, Edna alikataa kuzika mwili wa kijana wake hadi atakapojua sababu za kifo na kukamatwa kwake. Hata hivyo, mjomba wa marehemu Jackson Vincent alisema wameamua kuzika kwa sababu waliambiwa kufanya hivyo na polisi waliowasindikiza kufanya uchunguzi.

“Tulikuwa na askari sita tulipoenda kufanya uchunguzi, tulipofika hata daktari mwenyewe hakupata nafasi ya kufanyia uchunguzi ule mwili bali askari ndiyo walitoa maelezo ya kuwa ni jambazi aliuawa akijaribu kukimbia mikononi mwa polisi, maneno hayo yalifanya tuanze kulumbana na wao kunipa kibali cha kuzika kwa lazima na kuambiwa fanyeni mazishiView attachment 1198673
 
wazazi mnapoona watoto wenu ni majambazi wameshindikana msiwaonee huruma huko nje wamewadhuru wananchi wengi na kuwa choma visu na kuwaibia na nyinyi wazazi mnajua sana sasa wakikamatwa mnajifanya polisi wanaonea

Hata kama ni jambazi ndo utaratibu wa kushughulika nao kisheria uko hivyo, umeandika nini mkuu!, fikiri na kuandika kama mtu mwenye "UTASHI". Siku yakiwa upande wako ndo utaelewa!
 
Huyo anko naye anayedai polisi waliwalazimisha wazike ni jipu, hakuna mtu wa kukulazimisha kuzika ikiwa bado unahisi kuna utata. Angekuea ndugu yangu hapo polisi kituo kizima wangeomba likizo maana sio kwa vurugu ambalo lingeanzishwa hapo.
 
Mungu pekee wa kututetea kwa hapa tulipofika sasa maana dah!!
Yan mtoto wa watu ndio kauawa kirahis rahis namna hiyo aisee!!!!no maelez ya kueleweka.

Kwnn nao ndugu wasingetia mgomo kuzika.???

Walichofanya nagikiri ni kitu sahihi zaidi.
Ni kama wamemwachia Mungu ahukumu, wangeweza kutokumzika ndugu yao na wala wasipate chochote cha maana.
 
Aisee..inatia uchungu sana mkuu.Kwel no one is safe.Kama wanatujia hata sisi wakina "no body" huku mtaani.
 
Tunapopataka kufika tutafika na hakutakua na nafasi ya kurekebisha Bali kutibu majeraha na makovu tuliyoyaruhusu yatokee tukidhani hayatuhusu.
 
Aisee..inatia uchungu sana mkuu.Kwel no one is safe.Kama wanatujia hata sisi wakina "no body" huku mtaani.

Nilivyokua nasoma maelezo nilikua na maamuzi kama yako kwamba wangegomea kuzika bila taarifa ya kueleweka ya kifo cha ndugu yao.

Lakini mwishoni nimewaza, hakuna ambacho wangefaidika nacho, bora waendelee na mambo mengine.
 
nmeumia sana pumzika kwa amani kijana pole kwa wafiwa
 
Tumesoma upande wa Mama, Polisi na mjomba.

Ila hatujapata chochote hadi kijana anakamatwa, chanzo kilikua nini (hata tetesi tu)
 
wazazi mnapoona watoto wenu ni majambazi wameshindikana msiwaonee huruma huko nje wamewadhuru wananchi wengi na kuwa choma visu na kuwaibia na nyinyi wazazi mnajua sana sasa wakikamatwa mnajifanya polisi wanaonea
Utii wa sheria bila shuruti ni kwa wote hata polisi inawahusu, mwenye mamlaka ya kuthibitisha kuwa ni mualifu ni mahakama na si polisi na ndio wenye kutoa hukumu, najua unaongea coz hujui uchungu wa kufanyiwa kitendo kama hiko au angekuwa ni ndugu yako. Ila najua ni utoto ukikua utaacha.
 
Hakuna kitu kinauma kama mzazi kumpoteza mtoto wake tena kupitia sehemu aliyokuwa akidhani ni salama.
Hali hiyo imemkuta Edna Clement, mama wa watoto wanne ambaye kwa sasa yupo katika kipindi kigumu cha kumpoteza mwanaye wa kwanza, Innocent Vitus kutokana na kile kinachodaiwa alishambuliwa na wananchi wenye hasira.

Edna na watoto wake wanaishi eneo la Kibugumo, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Ilikuwa Alhamisi saa 2:00 usiku nilisikia kijana wangu wa pili akaniita mama kaka kakamatwa na polisi, nilikimbia hadi kwenye lile gari na kuwauliza wanakompeleka mwanangu usiku wakaniambia mwanangu hayumo,” alisimulia Edna na kuongeza: “Nikamuuliza mdogo wake mbona simuoni akasema mama yupo huwezi kuona vioo ni vyeusi basi gari ikaondoka, kwa mbele kidogo ili igeuze nikasimama katikati ya barabara nikawaambia sitoki hadi mniambie mnakompeleka, wakasema kituo cha polisi.”

Alisema wakati ya gari linaondoka aliwasiliana na baadhi ya ndugu zake waliomsihi kutulia ili wafuatilie.
Hata hivyo, Edna alisema usiku huohuo aliamua kwenda kituo cha polisi na saa 4:00 usiku alishuhudia kijana wake akiingizwa mahabusu ya kituoni hapo.

Alisema alirudi nyumbani na Agosti 30 saa 4:00 asubuhi alimpelekea chai lakini alishangaa kusikia kuwa hawezi kutembea. “Alipoitwa mmoja wa mahabusu aliniambia ‘mama huyu kaumia mguu hawezi kutembea’, hivyo akaingiza chai na kumpatia, niliomba RB nijue ni nani aliyemkamata na kosa lake,” alisema.

Alisema aliandikiwa jina la mpelelezi alipoingia ofisini kwake alimuuliza jina la mtuhumiwa, lakini alimwambia hana taarifa zake wala hajakabidhiwa jalada la kesi hiyo.
Alisema Agosti 31, alipeleka tena chai lakini kijana wake alipoitwa na askari wa zamu hakuiti, jambo hilo lilimfanya na yeye (Edna) kuanza kuita bila mafanikio huku mahabusu mmoja akijibu tena kuwa alitolewa tangu Alhamisi saa 10:00 jioni na hakurudishwa.

Alisema aliombe namba ya mpelelezi alipompigia alimweleza kuwa kesi ngumu hawezi kuisimamia kwa sababu haina jalada na kwamba, baada ya kufuatilia walimwambia walimtoa mahabusu akataka kukimbia.

Polisi watupiana mpira

Septemba 2, gazeti hili lilimtafuta kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuthibitisha tukio hilo lakini alijibu: “Nipo likizo wasiliana na mtu niliyemuachia madaraka.”

Baada ya kuwasiliana na ofisi ya Mambosasa, walimwelekeza mwandishi kuwasiliana na kamanda wa polisi mkoa wa Temeke ambaye naye alidai hana taarifa hizo. “Naomba niwatafute eneo husika ambao ni Kigamboni niweze...uwe mvumilivu na kesho unipigie,” alisema Amon Kakwale ambaye ni kamanda wa polisi Temeke.

Septemba 3, simu yake ilipopigwa ilipokewa na msaidizi wake ambaye alidai kamanda yuko kikaoni huku akimtumia mwandishi namba ya simu ya mkuu wa kituo cha polisi Kigamboni kurahisisha upatikanaji taarifa. Hata hivyo, mkuu huyo wa kituo alisema: “Anayeweza kuzungumzia hayo ni RPC Temeke naomba umtafute kwa sababu ndiyo nasikia kutoka kwako, wasiliana naye ila mimi kwa kweli sijui.”

DC akataa kuzungumzia
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri alipopigiwa simu alisema msibani mkoani Mwanza. “Mambo ya kesi nendeni kwa OCD niko msibani Mwanza,” alisema Sarah.

Mazishi utata

Awali, Edna alikataa kuzika mwili wa kijana wake hadi atakapojua sababu za kifo na kukamatwa kwake. Hata hivyo, mjomba wa marehemu Jackson Vincent alisema wameamua kuzika kwa sababu waliambiwa kufanya hivyo na polisi waliowasindikiza kufanya uchunguzi.

“Tulikuwa na askari sita tulipoenda kufanya uchunguzi, tulipofika hata daktari mwenyewe hakupata nafasi ya kufanyia uchunguzi ule mwili bali askari ndiyo walitoa maelezo ya kuwa ni jambazi aliuawa akijaribu kukimbia mikononi mwa polisi, maneno hayo yalifanya tuanze kulumbana na wao kunipa kibali cha kuzika kwa lazima na kuambiwa fanyeni mazishiView attachment 1198673

Inauma, lakini wajue tu kuwa sote tutapita.
Aliyetoa amri ya kuuwa, na aliyepokea amri hiyo na kuitekeleza wajue damu hiyo itawafuatilia.

Mungu tu ndiye mwenye mamlaka ya kuutoa uhai wa mtu, sasa hao wanachukua nafasi ya Mungu, wajue yatawapata makubwa
 
Back
Top Bottom