Singida yafanya maombi kushukuru ahueni ya covid-19

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
491
763
Na Godwin
Myovela, Singida

KAIMU Afisa
Vijana wa Mkoa wa Singida, Mwalimu Frederick Ndahani ameongoza waumini wa Kanisa
Katoliki ambao ni marafiki wakubwa wa Mtakatifu ‘Rita wa Kashia’ mkoani hapa
kwenye maombi maalumu ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea
kuwalinda na kuwaepusha watanzania dhidi ya madhara yatokanayo na janga la
Covid- 19
Ndahani,
ambaye alimwakilisha Mkuu wa , Dkt. Rehema Nchimbi kwenye kusanyiko la maombi hayo
yaliyofanyika jana eneo la Sukamahela, wilaya ya Manyoni mkoani hapa,
linalosadikiwa kuwa kati kati ya Tanzania, eneo ambalo Kanisa Katoliki limejenga
kituo cha hija kwa heshima ya Bikira Maria
“Tumekuja hapa
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa namna anavyoendelea kulipigania taifa letu kupitia
maombezi ya Bikira Maria dhidi ya janga la corona. Na tumeamua kufanya maombi yetu
eneo hili kwa sababu lipo katikati ya nchi na ndio kitovu…lakini zaidi mama huyu
yupo hapa na kwa maombezi yake anaendelea kuimarisha ulinzi wa taifa letu,”
alisema Ndahani
Ndahani ambaye ni miongoni mwa vijana walioshiriki kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2017, katika hotuba yake amemfananisha Rais John Magufuli na Nabii Musa kwa namna anavyoongoza taifa kwa unyenyekevu na maono ya kimungu huku nchi ikishuhudia miujiza mikubwa katika
kipindi hiki kigumu.

Kijana huyo ambaye amekuwa na juhudi kubwa za kuhamasisha umoja wa kitaifa kupitia vijana wa mkoa wote wa Singida, amewataka watanzania walionusurika na ugonjwa wa Corona na wale waliopona kuendelea kuchukua tahadhari zinazoelekezwa na wataalamu na Rais, ili kuepuka maambukizi mapya.

“Kwa wakristu mkifatilia kitabu kile cha ‘Kutoka’ mtakumbuka namna Mungu alivyomuongoza Musa
katika kuwavusha wana wa Israeli kwenye bahari ya Shamu kwa kutumia ile fimbo…na ndivyo baba yetu Magufuli anachokifanya kwa sasa,” alisema Ndahani huku akishangiliwa Kupitia maombi hayo ya shukrani, Sista wa Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Katoliki la Singida, Maria Subi, alisema anamshukuru Mungu kwa namna ya kipekee hasa anavyojidhihirisha katikati ya kiongozi mkuu wa Tanzania Rais Magufuli, kwa namna anavyoonesha hekima na utulivu mkubwa… wakati wote anaposhughulikia suala la corona “Kwa nguvu yake Mwenyezi Mungu furaha na amani ya watanzania imeanza kurejea tena, na tayari tumeanza kuungana na wageni mbalimbali kwa kuwakaribisha.

Naamini sasa tutaendelea
kufanya kazi zetu kama kawaida na nchi itachangamka kama mwanzo, tunapaswa kumshukuru
Mungu” alisema Subi.

Screenshot_20200523-122048.jpeg
Screenshot_20200523-122102.jpeg
Screenshot_20200523-122116.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha waombe kesho zamu yetu kusindikiza pasaka ya maombi

It is never too late to begin. Start now
 
View attachment 1457383View attachment 1457384View attachment 1457385

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti mzigo wa corona umepungua, kwani walikuwa na visa vingapi na sasa wanavyo visa vingapi?
 
Back
Top Bottom