Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi amewaagiza watumishi wa Halmashauri za wilaya na Manispaa katika Mkoa huo kuhakikisha wanakuwa na mizinga miwili ya nyuki na kwamba Halmashauri zina wajibu wa kutafuta mahali pa kwenda kutundika watumishi hao mizinga hiyo.
Dk.Nchimbi alitoa agizo hilo kwenye Kambi ya ufugaji nyuki kibiashara yanayofanyika katika Kijiji cha Kisaki,Tarafa ya Mungumaji,Manispaa ya Singida alipokuwa akifungua mafunzo kwa vitendo ya ufugaji nyuki yanayoendeshwa kwa muda wa siku 28 yanayoendeshwa na Chama cha ushirika cha Vijana (SYECCOS) kilichopo Manispaa ya Singida.
“Nilivyokuwa nazunguka kwenye Halmashauri kuongea na watumishi,watendaji na viongozi wa Halmashauri nimeagiza kwani hizi fikra ndizo fikra zilizopo kwa watumishi na watendaji wa Halmashauri
Fikra hizi hizi hatuna uwezo,hatuna uwezo sasa nimeagiza sijali uwezo watautoa wapi nimesema ndani ya msimu huu kila mtumishi wa Halmashauri lazima awe na mizinga miwili”alisisitiza huku akiwakazia macho watumishi waliokuwepo.