Singida: Askari polisi atekwa, akutwa kichakani hajitambui

ASKARI POLISI ATEKWA NA WASIOJULIKANA

ASKARI wa Jeshi Polisi aliyetambulika kwa jina moja la PC Ali, ametekwa kisha akapigwa na kuumizwa vibaya na watu wasiojulikana kabla ya kutupwa kwenye vichaka, mkoani Singinda.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA kutoka vyanzo vyake vya habari mkoani Singida zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi ya Mei 10, mwaka huu.

Mmoja wa marafiki wa karibu wa PC Ali, ambaye pia ni askari polisi aliyezungumza na MTANZANIA kwa sharti ya jina lake kutotajwa gazetini, alisema kabla ya tukio, PC Ali ambaye ni dereva wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mkalama (OCD), alikuwa ameegesha gari baa ambako alikunywa pombe nyingi mpaka akalala usingizi.

“Ali ni rafiki yangu wa karibu alipolazwa hospitali alisema kuwa baada ya kulewa alikutwa na watu ambao inasemekana ni askari wa usalama, walimpiga picha na kuondoka.

“Baadaye aliamshwa na kupewa taarifa za kupigwa picha, akawatafuta na kuwauliza kwanini wamempiga picha bila ridhaa yake.

“Ali aliniambia kuwa walipatanishwa na mkuu wao lakini baadaye alipigiwa simu usiku huo aende ofisini ndipo akakamatwa na kupigwa sana kwa kutumia waya hadi akapoteza fahamu na baadaye kutupwa vichakani.

“Aliniambia baada ya kupata fahamu alijikongoja hadi Kituo cha Polisi Nduguti ndipo akachukuliwa na kulazwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida,” alisema.

Jitihada za kumtafuta Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ziligonga mwamba lakini mwandishi wa habari hizi kufika katika wodi namba nne alipolazwa PC Ali na kupewa ushuhuda na baadhi ya wagonjwa kuwa ni kweli askari huyo alikuwa amelazwa.

Gazeti la Mtanzania
Je ni kidume?anakula wake za watu hapo nduguti?maana hapo nduguti ni kamji kadogo sana ila kuna vitoto vya kiarabu vzr ile mby na kuna mganga wa kienyeji hapo ni soooooooo anaagua huyo ile mbayaaaaa
 
Hi ni dharau kwa jeshi la polisi,
kwakuwa anawafahamu,ilitakiwa wawe likapu,regardless ni watu wasiojulikana ama lah,

jeshi la polisi lina mandate ya kuarrest hata hao wasiojulikana,labda wayamalize kiundugu
Sio kiurahi mzee baba
 
Watoto wa baba mmoja wamepigana na kutekana!

Naomba episodes ziendelee tu za wao kwa wao.
 
Hi ni dharau kwa jeshi la polisi,
kwakuwa anawafahamu,ilitakiwa wawe likapu,regardless ni watu wasiojulikana ama lah,

jeshi la polisi lina mandate ya kuarrest hata hao wasiojulikana,labda wayamalize kiundugu
Tena dreva wa OCD! Wakikaa vibaya uhasama unaanzia hapo. Hapo waliweke sawa lisibakishe mtima nyongo...
 
Huyo aliyetekwa amekaguliwa kila idara? Maana watekaji wengine wanaharibu na visivyoharibika...
Jicho!!
 
Mmoja wa marafiki wa karibu wa PC Ali, ambaye pia ni askari polisi aliyezungumza na MTANZANIA kwa sharti ya jina lake kutotajwa gazetini, alisema kabla ya tukio, PC Ali ambaye ni dereva wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mkalama (OCD), alikuwa ameegesha gari baa ambako alikunywa pombe nyingi mpaka akalala usingizi.

Bahati yake kama hawakutoboa suruali kwa nyuma wakashinda
 
sijui nina tatizo gani siku hizi..nikisikia habari hizi za kuumizwa polisi wa Tunisia roho yangu inakuwa kwatuu
 
Ukiona hivyo fahamu kuna shida mahala fulani.. Haiwezi kuwa bure hivi hivi
 
Huyo afande ninamfahamu na nilimpiga picha,aache ulevi.Huyu hapa jamani
tapatalk_1524417551505.jpeg
 
ASKARI POLISI ATEKWA NA WASIOJULIKANA

ASKARI wa Jeshi Polisi aliyetambulika kwa jina moja la PC Ali, ametekwa kisha akapigwa na kuumizwa vibaya na watu wasiojulikana kabla ya kutupwa kwenye vichaka, mkoani Singinda.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA kutoka vyanzo vyake vya habari mkoani Singida zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi ya Mei 10, mwaka huu.

Mmoja wa marafiki wa karibu wa PC Ali, ambaye pia ni askari polisi aliyezungumza na MTANZANIA kwa sharti ya jina lake kutotajwa gazetini, alisema kabla ya tukio, PC Ali ambaye ni dereva wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mkalama (OCD), alikuwa ameegesha gari baa ambako alikunywa pombe nyingi mpaka akalala usingizi.

“Ali ni rafiki yangu wa karibu alipolazwa hospitali alisema kuwa baada ya kulewa alikutwa na watu ambao inasemekana ni askari wa usalama, walimpiga picha na kuondoka.

“Baadaye aliamshwa na kupewa taarifa za kupigwa picha, akawatafuta na kuwauliza kwanini wamempiga picha bila ridhaa yake.

“Ali aliniambia kuwa walipatanishwa na mkuu wao lakini baadaye alipigiwa simu usiku huo aende ofisini ndipo akakamatwa na kupigwa sana kwa kutumia waya hadi akapoteza fahamu na baadaye kutupwa vichakani.

“Aliniambia baada ya kupata fahamu alijikongoja hadi Kituo cha Polisi Nduguti ndipo akachukuliwa na kulazwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida,” alisema.

Jitihada za kumtafuta Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo ziligonga mwamba lakini mwandishi wa habari hizi kufika katika wodi namba nne alipolazwa PC Ali na kupewa ushuhuda na baadhi ya wagonjwa kuwa ni kweli askari huyo alikuwa amelazwa.

Gazeti la Mtanzania
Mkuu fuatilia vizuri vyanzo vya habari zako na utueleza kama hakuna dalili yoyote ya kujiteka mwenyewe>
 
Hao ndo watu wasiojulikana?
 
Back
Top Bottom