Nashauri route za safari ndefu ziwe na ukaguzi maalam madereva huwa wanachoka wanataka kuwahi ndio matokeo yake hayo safari ya zaidi ya saa 15 dereva anasinzia tu.Mabasi ya dar to mwanza,mbeya to mwanza,dar to manyara,dar to shinyanga,dar to songea,mbeya to arusha huo mfano tu.
Kuna siku niko kwenye basi la hood toka dar to moro ilikuja basi nyuma yetu ya dar to manyara sikumbuki eneo ile basi ilikuwa inatuovateki sasa bahati mbaya mbele kulikuwa na semi trela inakuja ilibidi dereva wetu wa hood asaidie kwa kula pembeni ya barabara ili jamaa aweze kupenya pia jamaa wa semi trela nae ikabidi ale pembeni kwake ili jamaa wa basi apenye na ndio kilichosaidia vinginevyo ingekuwa ajali mbaya.