Singasinga wa PAP aelekea Dodoma kuzima wabunge dhidi ya wizi wa 200 Bilion

Singasinga wa PAP aelekea Dodoma kuzima wabunge dhidi ya wizi wa 200 Bilion

Tatizo kubwa la Tz mpaka sasa linasababishwa na kupata Uhuru bila kutwangana.."Hatukuingia vitani kupata Uhuru"..

Imefanya tumekosa Uzalendo ..Wanaoiba na wanaoibiwa Wote Haiwaumi..

Billion 200 !?!! Tunastahili kuingia kwenye Maajabu ya Dunia..
Mahesabu Uwanja wa Ndege kutokuwa na taa hiyo ni kesi nyingine..Baada ya miaka 50..Mji mkuu wa Tanzania.. Dodoma Kiwanja hakina taa asee!!!!

Ni muda wa kujuta na kujifunza..Wakati Nchi nyingine zinachagua viongozi...Sisi tunachagua Watalii kutuongoza..
 
Last edited by a moderator:
Kweli Kuna watu ni vichwa maji,mnapewa taarifa nyie mnaanza kujifanya wajuaji, visa visa upuuzi gani?

Hii PAP ni kampuni ya nini, huyo Singasinga ni nani, anaitwaje?
 
Hii PAP ni kampuni ya nini, huyo Singasinga ni nani, anaitwaje?

Mkuu unataka utafuniwe kila kitu?

Au wewe siyo M-Tanzania? Kuwa Mzalendo Umeshapewa tetesi hangaika kutafuta ukweli..

Hoja hapa ni 200 B.....Siyo Singasinga..
 
unaonekana unae stress sana kwa kichwa chako maana unaongoza kwa kubuni story za kijingajinga na za kichochezi ili kupandikiza chuki kati ya wananchi na serikali Yericko Nyerere

Habari za uhakika ni kuwa singasinga wa kampuni ya kifisadi ya PAP na wasaidizi wake wamelekea Dodoma kwa ndege ya kukodi usiku huu kwa lengo la kazi maalumu ya kulainisha wabunge kuhusu ufisadi wa bilioni 200.

Wakati huo taarifa kutoka idara ya ujasusi wa UK East Africa, zinasema mkwe wa JK kakimbilia UK kwa hofu kuhojiwa na TAKUKURU. Alikuwa middle men issue ya escrow.
 
Last edited by a moderator:
unaonekana unae stress sana kwa kichwa chako maana unaongoza kwa kubuni story za kijingajinga na za kichochezi ili kupandikiza chuki kati ya wananchi na serikali Yericko Nyerere
Na kama kweli anachochea hiyo serikali inakubaliana na.uchochezi wake????!!!
Wananchi hawachuji yaani kila wanaloambiwa na.huyo mleta mada wanakubali tuuuu!!!!?????

Tulia kwanza uzi ndio kwanza uzi uko na 60's ngoja ukomae kitaeleweka tu!!!!
 
Last edited by a moderator:
Billion 200! Wananchi kijijini hata hawajui hizi ni pesa kiasi gani na zinaweza kufanya nini. Maelezo ya zekomedi juu ya hili yangesaidia kuwaelewesha lakini zekomedi wako wapi na tbccm yao! Kafulira amelianzisha, cdm lichukulieni kwa uzito unaostaili, ukawa juisheni jambo hilo ktk mpango wa katiba mpya.

Ninamashaka na takukuru kulitendea haki taifa ili kwani ilishakiri kutokuweza kesi zinazohusu vigogo wakubwa.

Ningependekeza kamati maalum ya Bunge ikiwausisha wapinzani na wazalendo wachache kutoka ccm (kama wapo).

Nasikitishwa na jf member wasiotoa mchango chanya ktk uzi huu juu ya nini kifanyike kuwajibisha wanaojihusisha na wizi mkubwa wa fedha hizi.

Toka scandal za richmond....tanesco imekuwa mkondo wa kutoroshea mabilioni kuingia mikono ovu.....imediriki kupandisha umeme mara kadhaaa na kulazimishwa kulipa madeni kumbe ni mbinu fisadi.

Hivi kweli tunahitaji shirika ili kuendelea kuwa chini ya serikali?,,,,inaweza kuwa vigumu kwa sababu ' za ukiusalama' lakini tuthubutu kulihoji hilo.

Huu wizi unatisha....!!!
 
Jana nilisoma maoni ya mwananchi mmoja wa kawaida katika gazeti ambayo yanafikirisha akili. Mwananchi huo alisema hivi "Siku hizi wizi unapotokea serikalini (akijaribu kurejea mishahara hewa na huo wizi 200B) serikali badala ya kujiuliza ni kwa vipi wizi huo umetokea? lakini serikali ndio inakuwa mstari wa mbele kutetea wizi huo"
 
Habari za uhakika ni kuwa singasinga wa kampuni ya kifisadi ya PAP na wasaidizi wake wamelekea Dodoma kwa ndege ya kukodi usiku huu kwa lengo la kazi maalumu ya kulainisha wabunge kuhusu ufisadi wa bilioni 200.

Wakati huo taarifa kutoka idara ya ujasusi wa UK East Africa, zinasema mkwe wa JK kakimbilia UK kwa hofu kuhojiwa na TAKUKURU. Alikuwa middle men issue ya escrow.

....................................

Taarifa zinasema kampuni ya PAP iliweka dola 40m kuhonga wanasiasa na media na watendaji serikalini kuzima wizi huo, ambapo taarifa zinazidi kusema mwenye jamhuri "ana hisa" kwenye kampuni hiyo, na Mwanasheria Mkuu Fredrick Werema kalamba 2m dola.

NB

Singasinga na wapambe wake walitua salama salmini uwanja wa ndege Dodoma majira ya saa nane na dakika 16 usiku, hii ni kwamjibu wa maafisa wa kiwanja hicho,

Ndege inaweza kutua wakati wowote. Emergency night landing lights zinawekwa pembezoni ya uwanja na ndege inatua kama kawaida!!
Aliyekula ni PAP au VIP ya mzee wa Heineken Rugemalira?Singa katapeliwa na VIP akauziwa hisa feki kwa kuwa muda wa IPTL kurejesha mitambo Tanesco umeshafika.Tanesco nayo bado inadaiwa na Wamalaysia wenye mitambo na deni hilo kuwakabidhi Standard Chart Bank iidai Tanesco.In Short kuna mkanganyo mkubwa juu ya IPTL
 
Hili la uwanja wa ndege Dodoma kutokuwa na taa linapaswa kumfanya @Yericko Nyeree aje kuweka mambo sawa hapa. Au jamaa amepitia MZA au KIA kwanza ili kukipambazuka ndo warudi Dar?

Jiulize kidogo tu...Hivi ndege za ISOS toka S/A zinapofuata mgonjwa usiku saa nane wanatuaje kule Geita or Buzwagi? ukishajua hilo basi tongotongo zitakuwa zimetoka
 
Mkuu unataka utafuniwe kila kitu?

Au wewe siyo M-Tanzania? Kuwa Mzalendo Umeshapewa tetesi hangaika kutafuta ukweli..

Hoja hapa ni 200 B.....Siyo Singasinga..

Mkuu, nilidhani kwa kuwa hapa ni Where we DARE to talk OPENLY kila kitu kitawekwa hadharani, kwani pamoja na ukweli kuwa mimi ni Mtanzania, sijui kila jambo na kila mtu aishie Tz. Nikadhani kwa wenzangu na mie ambao hatujui, angalau ugumu wa hii puzzle ingepunguzwa, ikatajwa karibu na uhalisia. Hadi sasa ni PUZZLE kwangu, sina idea ya PAP wala Singx2, bado cjajua hata kwa fununu ni nani! Anyway hata kwenye google ambalo ndo kimbilio langu sidhani kama nitaambulia majibu.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Ukiona watu/mtu anatetea sana hii chama yao ya kifisadi ujue ana maslahi ndani yake kila kukicha ni skendo za ajabu ajabu alafu bado ziko mtu zinashadidia ufisadi wa namna hii.
 
Mkuu unataka utafuniwe kila kitu?

Au wewe siyo M-Tanzania? Kuwa Mzalendo Umeshapewa tetesi hangaika kutafuta ukweli..

Hoja hapa ni 200 B.....Siyo Singasinga..
Mkuu, nashukuru kwa challenges, kule google nimesearch heading tofautitofauti kwa bahati nilipoandika PAP Tanzania daah, detail zote zipo! Ahsante mkuu kwa changamoto uliyonipa!
 
  • Thanks
Reactions: prs
Ndege kuruka DAR saa mbili usiku kuelekea DODOMA
Propaganda inakosa mashiko, hakuna usafiri wa ndege kuelekea dodoma unaoruhusiwa kutua kuanzia saa kumi na mbili jioni
UWANJA HAUNA TAA.....
Ni sawa leo mtu akwambie mechi kuchezwa saa tatu usiku uwanja wa KINESI.... halafu na wewe upige makofi na kushangilia
Great thinkers always think outside the box......
acha ujinga wewe tulikwenda kuchukua mgonjwa Lindi kwenye makampuni ya uchimbaji gas na tukaruka usiku na ndege kwa kupanga chemli kwenye njia ya kurukia ili mgonjwa akatibiwe Nairobi, this is JF usichokijua mie nakijua na usichokifanya mie nakifanya and vice versa!
 
Jiulize kidogo tu...Hivi ndege za ISOS toka S/A zinapofuata mgonjwa usiku saa nane wanatuaje kule Geita or Buzwagi? ukishajua hilo basi tongotongo zitakuwa zimetoka
acha nao hao hawajawahi kufanya kazi kwenye mazingira magumu ndo hao wanaoshindwa kutataua matatizo yetu kisa wanahisi tu haviwezekani. ------- ZAO.
 
mi naona kulalamika na kukimbilia kupost hapa jf bado haisaidii. Make hili la kuchota mijihela ya umma lilishazoeleka sana make tunajua fika kuwa ccm ni ukoo wa panya kwanini tusichukue hatua stahiki? Wanasiasa pekee kamwe msitegemee watageuza njano kuwa nyekundu bali utashi wa kizalendo na kujitoa mhanga nje ya ulingo wa kisiasa ndio utang'oa uongozi dharmu. Vinginevyo tutaishia kutoa povu jingi hapa huku wezi ccm wakitung'ong'a na kuendelea kufanya yao ya utafunaji wa mema ya nchi.

Vijana tuamkeni, acheni uoga na ujinga wa kuthubutu.

trf

trf
 
Ndege kuruka DAR saa mbili usiku kuelekea DODOMA
Propaganda inakosa mashiko, hakuna usafiri wa ndege kuelekea dodoma unaoruhusiwa kutua kuanzia saa kumi na mbili jioni
UWANJA HAUNA TAA.....
Ni sawa leo mtu akwambie mechi kuchezwa saa tatu usiku uwanja wa KINESI.... halafu na wewe upige makofi na kushangilia
Great thinkers always think outside the box......

Inawezekena. ....Uliza watu wanaofahamu. ...
Sio jambo la ajabu, ku request landing usiku..
Huwa taa zinawekwa (hata za magari) ndege hutua bila shida kabisa. ...
 
Back
Top Bottom