tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,932
- 29,484
Unapoitazama Tanzania katika kipindi hiki, haikupi taabu kubaini uwepo wa mabadiliko ya kijamii katika ngazi na kada tofauti.
Zile sifa zilizoimbwa kuanzia kwa mkulima kijijini hadi ngazi ya taifa, kisha zikapenya na kuvuka mipaka kuifikia jumuiya za kimataifa, zinazidi kufifia na ikizembewa, zitatoweka.
Tulishiriki kuimba, Tanzania itajengwa na akina nani, kama si mimi na wewe lengo lilikuwa kuhamasisha ushiriki wa kila raia katika kuifanya nchi iwe mahali salama na rafiki kwa Mtanzania.
Ni wangapi leo hii wakiwa kijijini ama mjini, wanaweza kuthubutu, wakafungua vinywa vyao na kuuimba wimbo huo?
Kwamba umshawishi Yule, njoo tuijenge nchi? Inawezekana lakini kwa mazingira ya sasa, inakuwa ngumu.
Kwa maana kuijenga nchi kunahitaji kujitolea muda, kutoa sehemu ya pato ama mali inayotokana na jasho lako, iwekezwe kwenye shughuli za kijamii na kitaifa.
Yaani kama wakati ule wa vita vya Uganda na Tanzania, jinsi Watanzania walivyoshiriki kuchanga mbuzi, muhogo, ngombe, kuku, bata, visu, uwele, mtama na vinginevyo, vikapelekwa kwa wapiganaji kule Kagera.
Leo hii, ikitokea hali inayofafana ile, kwamba ikatoa mwanya kwa raia kujitolea vitu kama hivyo, kuna uhakika gani kwamba vitafikishwa salama? Bila shaka ni ngumu kuamini kwamba hilo linawezekana.
Kwa maana walio kwenye dhamana za kuyafanya hayo, kuchagiza urejeshwaji wa imani ya raia kwa nchi na viongozi wao, wanaipeleka nchi kusikostahili.
Hata kama ni wachache kwa idadi yao, lakini wana nguvu kubwa hasa za kiuchumi zinazowafanya wapenye kwenye kila kona, wakiiacha jamii umbali mrefu ili wayafikie maslahi binafsi.
Hapo ndipo unapoibuka mfumo wa kikandamizaji, dhuluma na hujuma dhidi ya binadamu na ubinadamu.
Matukio kama ya kuibuka na kushamiri kwa asasi ndogo zinazojificha chini ya mwamvuli wa dini, na kuifanya nchi isitawalike, ili mradi wakidhi matakwa binafsi.
Kwa kada ya utawala iliyokabidhiwa dhamana ya kuwaongoza Watanzania katika idadi yoyote watakayokuwapo baada ya `kuzaliana, inawezekana vipi wakashindwa kuidhibiti hali hiyo, ama ni hisia potofu kudhani kwamba miongoni mwao wanashirikiana na asasi hizo!
Watu wanatekwa, wanapigwa, wanajeruhiwa na hata kuuawa. Jitihada gani zinazonekana kuchukuliwa, ili Tanzania iendelee kuwa eneo huru za nyimbo za kitovu cha amani na utulivu.
Zipo nyimbo nyingi zilizoimbwa miongo kadhaa iliyopita, ambazo hivi sasa zinahitaji ujasiri wa kipumbavu kuzirejea, pale mazingira yanapoonekana si rafiki kwa nyimbo hizo. Pia yapo matukio mengi ya machukizo yanayotokea, kiasi kwamba si rahisi kuyaainisha hapa, yakatosha. Lakini yanajulikana na mengine hayajulikani.
Katikati ya hali hiyo, wenye dhamana ya kuiondoa jamii kutoka katika kadhia hiyo, hawaoneshi nia njema ya kulitimiza hilo.
Ni kama wameingia katika sanaa ya kuonyesha `sinema ya jamii inayotegemea ubunifu wa matukio ya kijamii.
Mfumo wa sinema za aina hiyo unazidi kukua, lengo likiwa ni kuuhamisha umma katika kujadili mambo ya msingi kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa watu, wabaki kuyafanya yaliyo ya kipuuzi.
Miongoni mwa watawala wakishirikiana na taasisi kadhaa wameingia katika sanaa hiyo, wakitunga na kutoa taarifa ama kutekeleza jambo ambalo hata kwa akili ya kawaida, halikubaliki.
Lakini si kwamba wanafanya hivyo kwa kukosea, la hasha. Kwa maana uwezo wa wanaohusika katika hayo unajulikana, ujuzi na maarifa yao ni jambo lisilotiliwa shaka.
Kwamba kama wakiamua kuvitumia vipawa hivyo kwa nia njema, basi ni rahisi Tanzania ikapiga hatua za kasi katika kuyafikia maendeleo endelevu, huku watu wake wakipata ustawi bora.
Lakini kupitia sanaa ya sinema za jamii, zile ambazo zimejipenyeza kuanzia vijijini, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi taifani, hakuna mwanga wa matumaini ya kufika huko.
Labda kuendelea kushuhudia mifumo ya sekta muhimu kama elimu, afya, ulinzi na usalama, japo kuitaja kwa uchache, ikidorora. Nani anayejali?
Kwa vile wanaohusika na usanii huo ni baba zetu, mama zetu, kaka zetu, dada zetu na zaidi ya yote, Watanzania wenzatu, ambao pamoja na kuwapo mwanya wa kuwawajibishwa, hawawajibishwi, sinema zao zinakuwa sinema zetu.
Zinaendelezwa sinema za jamii kwa mfumo unaoiharibu na kuiathiri nchi yetu. Lakini kwa upana wake, ni kama watu walio ndani ya blanketi jeusi ndani ya chumba, wakati wa giza nene, wasione.
Mambo yanaiharibikia nchi kwa uzembe unaochochewa na sinema za jamii, walio katika jamii ni kama wamewekewa vifaa vilivyotoboa ngome za masikio yao, wasisikie.