Sindumuja - Ukweli kuhusu burundi 2



hahahaha....naona foot soldiers wa hii JF interahamwe wanaongezeka. karibu sana. alianza na akina rushasha lakini sijui jamaa alitokomea wapi. unajua uongo una short life span. walianza na "facts" nyingi lakini kadiri siku zinavyoendelea wanaishiwa.
 
Last edited by a moderator:
hahahaha....naona foot soldiers wa hii JF interahamwe wanaongezeka. karibu sana. alianza na akina rushasha lakini sijui jamaa alitokomea wapi. unajua uongo una short life span. walianza na "facts" nyingi lakini kadiri siku zinavyoendelea wanaishiwa.

Ndio tatizo lenu ninyi banyamulenge/m23,MTU yeyote anaesema ukweli anakuwa ni FD RL kwenu.Refer kikwete alipomshauri kagame kuzungumza na wapinzani wake aliropoka majina mbalimbali ya kimtukana kikwete.The same to you, mwisho wa propaganda zenu umefika, I am telling you!
 
Last edited by a moderator:

Jmali, hawa kina murutongole kwa asili yao huwezi kuwatifaitisha na kagame au karake. Wamekuwa wakikuita majina mbalimbali labda ni mabaya kwatazamo wao, usikate tamaa, endelea kuwaumbua na kuweka wazi mipango yao. Nimekuwa nikisoma mada zako mbalimbali, kwa hakika hakuna unapodanganya. Kagame na museveni wamekuwa mstari wa mbele kuvuruga amani ya DRC na Burundi kwa kusaidiwa na marekani. Ukiwaambia tu ukweli huu, hawachelewi kukuunganisha na mauaji ya kimbari au kukuita majina ya hovyohovyo.Kuhusu siasa za maziwa makuu hujawahi kudanganya!
 

Hadi sasa, nkurunziza ni rais halali wa Burundi, hao unaodhani watatawala milele wameshashindwa!
 
Wewe "mtanzania". Usiingize rwanda kwenye masuala ya burundi. Nenda kamsaidie Nkurunziza manake naona the Hague inamuandalia one way ticket.
aah acha kunivunja mbavu! Mtanzania? hata kama keshanunua uraia, ideology haijabadilika... they say, if you see a bird that walks like a duck, swims like a duck and quacks like a duck then it's what? na kwa kasi aliyo nayo, hata huko Bongo wakimkenulia tu, basi we juwa hata radio kama RTLM iko njiani kufunguliwa.
 
Ukweli inaelekea unafuatilia kweli yanayotokea nchi ya Burundi, na kwenu Rwanda:
1:Unasema mgogoro wa kisiasa ulimalizwa kisheria baada ya mahakama mbili kuamua kuwa Nkurunziza anaruhusiwa kuongoza:
Kwa hili you are very WRONG,japo kweli mahakama iliamua hivyo lakini what about the coup attempt?? unaongeleaje mgawanyiko jeshini baada ya failed coup serikali ilianza kuwinda wale wote waliokuwa wanasapoti coup d`etat.
Kwahiyo kusema uamuzi wa mahakama ulimaliza mgogoro hapo unatudanganya.
Leo hii nina uhakika Maalim Seif akienda mahakamani akidai uchaguzi usirudiwe atashindwa tu..lakini hii haitakuwa mwisho wa mgogoro uliopo Zanzibar.
2:Unasema Wapinzani walisusia uchaguzi kwasababu wanazozijua wao...hapa tayari unaonesha upande wako, wapinzani walikuwa hawakubaliani na kitendo cha Nkurunziza kutaka kuendelea kuongoza.
3.Mwenyewe unakubali kwamba Nkurunziza alipigiwa kura na wanachama wa chama chake tuu.. mpaka hapa unakubali kwamba issue sio kabila kwani kuna zaidi ya vyama kumi ambavyo viko active kati ya hivyo very few are owned by Tutsi, as such Wahutu wengi pia hawakumpigia Nkurunziza kura.
4:Hivi unaweza kutujuza ni kwanini International Media/Community imefumbia macho mauaji yanayo fanywa na waasi?? international media inachuki gani na Nkurunziza na kwa sababu gani.. kumbuka all was well kwa mda wote aliokuwa madarakani kabla ya kutangaza kugombea tena.
5. Sindumuja movement... hii umeifanya title ya post yako, nimejaribu kuisearch kumbe ni twitter hashtag ambayo ina tweets 124 kati ya hizo mwenye account kapost more than 80 posts, hashtag yenye 80 followers na 4 likes!!!
Is this a big deal for a country?? hastag with last tweet done in May?? Cmon!
6:Issue ya history ya Ufalme huwa unapenda kuileta sana, yes it happened lakini kumbuka this was everywhere in Africa,Tanzania inclusive: Ufalme ulikuwa hereditary na Familia za kifalme lived as dictators...issue ni current leaders.
Nyerere angekuwa na idelogies kama zako Tanzania ya sasa isingekuwepo kungekuwepo na ukabila..angeanza kukumbusha wananchi jinsi walivyonyanyaswa na wafalme.
7:Reference uliyotoa juu ya Rwanda is irrelevant to the topic you started though wengi tunakujua huwezi kumalizia bila ya kuongelea Kagama au kabila la Kitutsi in a negative way lakini please, Rwanda ni Rwanda na Burundi ni Burundi:
8:Unasema Watutsi wanataka kuwachokoza wa Hutu ili in turn wahutu waue wa Tutsi, so that Nkurunziza can be removed by International community??? really??? hivi watu wanachukua mda wa kuanalyse statements zako??
Sasa nani atachukua madaraka kama watakuwa tayari wameuawa, kwa msemo wako nikama vile wanajitoa mhanga..
Hapo sikuelewi eti UTENGENEZAJI WA GENOCIDE DHIDI YAKO KWA KUKUSUDIA is it ???????
Ukweli ni kwamba mauaji yanayoendelea Burundi yanafanywa na pande zote it is tit for tat... in this case as long as Nkurunziza ndiye Rais wa nchi he is answerable.
Yeye hajitofautishi na waasi wa serikali yake, wakiua na yeye anaua, huo sio uongozi kashindwa.
 
Ndugu Talkandtalk , nafurahi leo unazungumza kiungwana. Baadhi ya majibu kwa maswali yako:

1. Unasema mgogoro wa kisiasa ulimalizwa kisheria baada ya mahakama mbili kuamua kuwa Nkurunziza anaruhusiwa kuongoza:
Kwa hili you are very WRONG,japo kweli mahakama iliamua hivyo lakini what about the coup attempt?? unaongeleaje mgawanyiko jeshini baada ya failed coup serikali ilianza kuwinda wale wote waliokuwa wanasapoti coup d`etat.



JIBU: Hapa ni wewe ndie unayekosea, mgogoro ulikuwa tafsiri sahihi ya mkataba wa Arusha kisheria. Sasa kama mahakama zimeamua kuwa hakuna tatizo, hao wenye matatizo na Nkurunzinza msingi wa hoja zao ni nini? Maana kama kungekuwa na any ruling inayokubaliana na tafsiri yao halafu Nkurunzinza akakataa hapo sawa, otherwise ni magaidi tu.

Kama wangekuwa wanapinga uchaguzi uliompa Nkurunzinza madaraka, maybe wangeeleweka, but they chose to boycott the elections AFTER mahakama ya EAC allowed it! Kama wana msingi wowote ule please tuelezee sisi tusiojua.

Kuhusu the coup, naona wewe umegeuza maneno. Wanaowindwa sio walio support coup, actually wanaowindwa ni wale waliomrejesha Nkurunziza madarakani! Aliyepambana na Niyombere na kumrudisha Nkurunziza madarakani Lt. Gen. Adolphe Nshimirimana amepigwa roketi na kuuawa, MKUU WA MAJESHI Gen Prime Niyongabo naye kaponea chupu chupu kuuwawa last month katika tukio ambalo walinzi wake 7 waliuawa! What are you talking about kuhusu walio support coup kulengwa. Jeshi lote sasa hivi liko chini ya Nkurunziza, maafisa wote wanamtii Nkurunzinza. Niyombere na wenzie walisha surrender na wako chini ya Nkurunziza. Hao wanajeshi wanaompinga Nkurunzinza wanaolengwa ni kina nani? You should be asking who is behind these targeted assassinations against government officials ikiwa Niyombere is no longer in the picture.

Mfano wako kuhusu Zanzibar ni irrelevant. Maalim Seif hawezi kuchukua silaha na kuanza kuua maafisa polisi na jeshi wa serikali ya Zanzibar, hawezi kuchukua mabomu na kurusha hovyo mashuleni na masokoni ili kuleta vita vya kikabila. Na hata akiandamana, ataandamana kwa sababu za msingi na zinazoeleweka, hataandamana kwa kutumia slogans alizokuwa anatumia anatumia sultani aliyepinduliwa na karume zisizo na kichwa wala miguu!

2. Unasema Wapinzani walisusia uchaguzi kwasababu wanazozijua wao...hapa tayari unaonesha upande wako, wapinzani walikuwa hawakubaliani na kitendo cha Nkurunziza kutaka kuendelea kuongoza.
3.Mwenyewe unakubali kwamba Nkurunziza alipigiwa kura na wanachama wa chama chake tuu.. mpaka hapa unakubali kwamba issue sio kabila kwani kuna zaidi ya vyama kumi ambavyo viko active kati ya hivyo very few are owned by Tutsi, as such Wahutu wengi pia hawakumpigia Nkurunziza kura.



JIBU: Sababu zao zilishapingwa na mahakama, kwa hiyo tendo la kufanya uchaguzi lilikuwa halali. Vinginevyo toa sababu zingine tofauti na zile ambazo wapinzani walikuwa nazo zilizowafanya kususia uchaguzi. Na zaidi ya hapo tafadhali tupe hypothesis yako juu ya nani aliyekuwa anaua raia wasio na hatia kwa kutupa mabomu vituo vya kura, kwa kupiga risasi wapiga kura etc, ikiwa wapinzani walisusa uchaguzi.


Sindumuja movement... hii umeifanya title ya post yako, nimejaribu kuisearch kumbe ni twitter hashtag ambayo ina tweets 124 kati ya hizo mwenye account kapost more than 80 posts, hashtag yenye 80 followers na 4 likes!!!
Is this a big deal for a country?? hastag with last tweet done in May?? Cmon!



JIBU: Mimi nazungumzia sindumuja yenye link hii: https://twitter.com/hashtag/sindumuja hiyo ya mwezi mei ni ya kwako mkuu.



Issue ya history ya Ufalme huwa unapenda kuileta sana, yes it happened lakini kumbuka this was everywhere in Africa,Tanzania inclusive: Ufalme ulikuwa hereditary na Familia za kifalme lived as dictators...issue ni current leaders.
Nyerere angekuwa na idelogies kama zako Tanzania ya sasa isingekuwepo kungekuwepo na

ukabila..angeanza kukumbusha wananchi jinsi walivyonyanyaswa na wafalme.



JIBU: Usemayo ni kweli kabisa. Naona umekubaliana na mimi kuwa hata Nyerere ?angeanza kukumbusha?? tungekuwa na matatizo. Sasa je kuna haja gani ya wapinzani ambao ni watutsi kuanzisha slogan ya #sindumuja fully knowing its implications kwa wahutu regardless of how ?positive? YOU tutsis define it? Huu sio uchokozi wa wazi wazi kukumbushia historia kama ulivyosema? Burundi was more advanced in tribal reconciliantion than Rwanda, look at what this #sindumuja is doing now. How would a Tutsi feel if a political party, majority composed of Hutus use #SinduInyenzi? Halafu wadai wanamlenga Kagame because he has extended his rule? Where is the relationship here?
Zingatia kuwa wahutu wa Burundi wamekandamizwa na watutsi toka uhuru, kila rais aliyechaguliwa toka uhuru aliuawa na jeshi la watutsi kuchukua madaraka kwa mtutu. Nkurunzinza ana uhalali unaothibitishwa na mahakama halafu watutsi wanatumia #sindumuja kutaka atoke bila sababu za kisheria?




Sasa nani atachukua madaraka kama watakuwa tayari wameuawa, kwa msemo wako nikama vile wanajitoa mhanga..
Hapo sikuelewi eti UTENGENEZAJI WA GENOCIDE DHIDI YAKO KWA KUKUSUDIA is it ???????



JIBU: Watutsi wa kawaida sio wanaojitoa mhanga, wao ndio wahanga, wanaowatoa mhanga ni the elite behind #sindumuja. Kama ambavyo when the dust settled ndio ikajulikana kumbe Interahamwe iliyokuwa inafanya genocide against the Tutsis, ilikuwa inaongozwa na MTUTSI afterall! Kwa hiyo sio ajabu kabisa kuwa when its all over ukagundua kumbe ?Imbonerakure? wanaofanya unyanyasaji wa watutsi kiongozi wake ni mtutsi! Right now ripoti zote zinadai wanaofanya mauaji wamevaa nguo za polisi. Lakini polisi wenyewe hawana rekodi zozote za hao watu, na hata mauaji yenyewe ni senseless. Why would a police officer atumwe na Nkurunzinza kwenda kurusha mabomu kwenye neighbourhood ambayo ni stronghold ya CNDD??? Huu ndio ule uongo wa Kagame enzi zile za kudai miili inayoelea mto Kagera ni watutsi waliouawa na interahamwe, mpaka pale watu wetu walipomtolea uvivu na kumkumbusha kuwa jeshi lake la RPA lilikuwa limeshikilia hayo maeneo for a whole year!


Ukweli ni kwamba mauaji yanayoendelea Burundi yanafanywa na pande zote it is tit for tat... in this case as long as Nkurunziza ndiye Rais wa nchi he is answerable.
Yeye hajitofautishi na waasi wa serikali yake, wakiua na yeye anaua, huo sio uongozi kashindwa.



JIBU: Yes majeshi ya Nkurunziza kill, lakini why do they kill? Hilo ndio swali. What reason do these sindumuja have for killing innoncent civilians? Why don?t they target the army only kama vikundi halali vya uasi vinavyofanya? Did ANC kill innoncent white people during the struggle? Here you have tutsi opposition thugs, killing hutu innocent civilians while shouting #sindumuja, what do you expect if not revenge killings? Do they have to burn buildings and destroy properties? Sasa hapo kuna kosa gani kwa polisi wa Nkurunzinza kutumia risasi kupambana na hawa watu?

Mwisho kabisa labda nikuulize wewe, given the situation, what would you have done if you were Nkurunzinza? Na kwa sababu ipi?
 
nilishakuambia ideology yenu itaharibu sana, iwapo watu wataendelea kuwakenulia... mlianza kwa Mobutu mkatia kimavi, hivi sasa mshatia kimavi mshikaji wenu Nkurunziza... nafikiri huu ndio unaenda kuwa mwisho wenu wa kuwaponza viongozi wa nchi za watu,anyway yetu macho...
 

I will not go into the detail nadhani jibu langu kwa swali lako, includes everything:
Ningekuwa Nkurunziza 1:Nisingegombea , hii ni kwasababu tayari wananchi wake walikuwa wamemuonyesha kuwa hawamtaki..rejea maandamo yaliyokuwa yakifanyika kabla hata ya coup attempt:
Maandamo yalikuwa yamakabila yote, hii issue ya ukabila Nkurunziza ndiye aliingiza ili kupata support ya upande mmoja.Kwanza kugombea kwenyewe kulikuwa na utata, kama anaipenda nchi yake kwanini asingemwachia mwingine kutoka chama chake agombee?:
2:Ningekuwa Nkurunziza wale wanaonipinga ningetumia vyombo vyangu vya dola, kuwasaka, niwakamate, niwafungulie mashtaka...sio kuuwa mtaa kwa mtaa, kila unaye msasuspect unatuma polisi kuuwa, then unatofauti gani nahao unao waita waasi?
Umeongelea watu wa upande wa Nkurunziza waliouawa, lakini nani alimuua kiongozi wa upinzani..Zedi Feruzi?nani kamuua Charlotte Umugwaneza kiongozi wa chama cha MSD? who burned down RPA Radio? list is endless na hii yote imefanywa na utawala wa Nkurunziza, sasa Raisi akianza ku act kama waasi, then he has lost control of the state.
 
Watu wanakufa kwa sababu gani? Yeye ndie anayewaua ili atawale? Nani anawaua na kwa nini? tuanzie hapo.

Watu wanakufa kwa sababu hataki kuachia madaraka , askari watiifu kwake ndio wanauwa wapinzani na . Kwani ni lazima awe raisi? Acheni upumbavu mnaivuruga nchi kwa tamaa za kishenzi mnaniudhi sana nyie warundi basi tu hamjuwi.
 
Aisee na wewe ni mtusi nini? Dunia kuna kazi ya kufanya hapa hili tatizo ni zaidi ya nijuavyo.
 
Post nzuri umegusia maeneo yote na sababu za chokochoko za Kagame na vibaraka wake.Ni vyema tukajadili hoja za msingi.


 

1. Nkurunzinza hatakiwi na watu wachache sana kwenye baadhi ya wilaya za Bujumbura. With the exception of hizo wilaya (ambazo hutaki kukubali sababu zake), the rest of Bujumbura and the rest of Burundi is calm and peaceful. Hivyo sio kweli kwamba 'WATU' hawamtaki, hatakiwi na 'watu' kwa herufi ndogo. Nini maandamano? Hakujawahi kuwa na maandamano dhidi ya Nyerere lakini Nyerere amenusurika coup attempts zaidi ya tatu kama sikosei! Je maana yake WATANZANIA tulikuwa hamtutaki?
Lakini personally nakubaliana kuwa Nkurunzinza hakutumia busara kugombea tena even though kisheria yuko sahihi. Just like Kagame na Museveni hawatakiwi kugombea tena no matter how legally feasible it is.

2. Ni kweli mwanzoni maandamano hayakuwa na ukabila. Msingi wake ulikuwa wa tafsiri ya kisheria. Baada ya mahakama kukubali, walio wengi wakaachana nayo. Waliobaki hivi sasa wanaandamana kwa nini? Na kwanini watumie "sindumuja"? Hiyo "sindumuja" ina wahutu wangapi?
Vile vile kama hakuna ukabila, mbona hao "sindumuja" wanalia kwamba kunataka kufanyike genocide? Je hiyo genocide itakuwa against nani? Unachoongea kinapishana na hata hao sindumuja wenyewe unaowatetea.

3. Kupambana na magaidi ni vigumu. Waasi wa Burundi wanavamia vituo vya polisi na kijeshi na kufanya ambush, wanaua raia kwa mabomu, wanavamia kwa risasi na kuua indiscriminately. Hivyo huwezi kutumia mbinu za kawaida za kijeshi kwa sababu hupambani na jeshi la kawaida. That being said, mauaji mengi yanayofanywa na upande wa serikali yanafanywa dhidi ya watu walio na silaha na wanauawa katika mapambano. Hayo mauaji dhidi ya watu wa upinzani hayafanywi na serikali ya Nkurunziza kama serikali, kwa sababu politically haina sababu. Nkurunzinza hata akijiuzulu leo atakayeshinda ni mtu wake tu. There is no threat politically upande wa upinzani kiasi cha serikali kuwaua. It doesn't make any sense. Hata hivyo nakubali kuwa wanaoua wapinzani ni watu wanao support serikali ya Nkurunziza.
 
J mali you seem to know mach about RwandaURUNDI history! I believe on you!
 
wewe ni muhutu na ni mwanachama wa fdlr nachochote kile utakacho kijadili hapa jukwaani ni lazima utaje mabaya ya kagame na watutsi,
hivi nikuulize kitu kwani huwezi kuandika bila kutaja watusti na kagame? wenzio wako wanajenga nchi wewe unapiga kelele mitandaoni mwisho unaonekana chizi tu!
 

Hahahaha. Wewe ungekuwa mtanzania mwenzangu ungeandika "mhutu" sio "muhutu". Hapo umejianika maana hivyo ndivyo mnavyoongea. Wewe ndio uache propaganda za FDLR na uungane na wahutu wenzio mjenge nchi yenu ikiwa na umoja.
 
Hahahaha. Wewe ungekuwa mtanzania mwenzangu ungeandika "mhutu" sio "muhutu". Hapo umejianika maana hivyo ndivyo mnavyoongea. Wewe ndio uache propaganda za FDLR na uungane na wahutu wenzio mjenge nchi yenu ikiwa na umoja.
hivi unaona raha gani kujipakazia utanzania na kuficha nationality yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…