britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 15,636
- 30,004
Kila anapokufa mtu yeyote ndipo sifa zake uanza kuenea kwamba amefanya haya na yale, mara huyu mtu amekuwa nguzo katika suala fulani au amewezesha kitu fulani,
Hii ni tabia ya unafiki iliyojaa kwenye waafrika walio wengi , ni ama saa nyingine kuogopa kumuongelea mtu aliyekufa vibaya , ama kufuata mkumbo kuongezea sifa kwa marehemu ionekane naye anamjua,
Meseji hii ni moja kwa moja kwa wale mliopewa dhamana ya kuongoza nchi hii, ni kwa wale walio na nafasi ya kuweza kuwaongoza walio chini mfano wachungaji, wafanya biashara wakubwa, makasisi na mashehe bila kusahau wachungaji,
We kama kiongozi wa nchi uliwahi kujiuliza hivi ikitokea leo nikaondoka nitasemwa vipi au nitasemwaje? na wanaoweza kuusema ukweli ni wachache , je umewahi jiuliza kwamba pamoja na kwamba tuna tabia ya kusifia marehem je we watakusifia kwa kutoka moyoni au watakusifia tu kwa kufuata mkumbo na kuogopa ile laana ya kumsema marehem vibaya?
Kama kiongozi unayo nafasi ya kukumbukwa kwa mengi Mfano kukumbukwa kwa uongozi shupavu usioegemea upande, usio na chembe chembe za upendeleo, isiyo na aina yoyote ya unyang'anyi na kuwatishia unaowaongoza,
Kama kiongozi unayo nafasi ya kutengeneza mazingira ya kukumbukwa kwa kutowafanya wananchi kuishi kwa dukuduku na wasiwasi mpaka wengine kufika hatua ya kujipendekeza kwako ionekane unafanya sahihi kumbe ni uoga uliotawala mioyo yao,
Kama kiongozi unayo nafasi ya kuwakumbatia wote walio wako na wasio wako na kuweka tofauti zao pembeni na kuwaleta pamoja,
Kama kiongozi hutakiwa kuwa na ubaguzi wowote kati kuwateua wasaidizi wako ama watu wa kupata nafasi mbali mbali,
Tunajua viongozi wengi uacha alama kubwa nazo zaweza kuwa zina athari chanya ay hasi ndani ya jamii wanayoishi,
Ni auala la muhimu sana kuziepuka athari hasi kama vile kuua, kufilisi, kusingizia wasio na hatia, kula rushwa , kuweka mifumo ya ki imla ndani ya uongozi ulioukuta imara , kupandikiza chuki kwa unaowaongoza dhidi ya viongozi waliopita kwenye nafasi kama uliyonayo sasa na ambao wako juu yako au chini
Tujitathmini je
1.Umewahi kutuma mtu akamuue mwenzake ?
2.Umewahi hamasisha utekaji wa watu ili wanyang'anywe mali?
3.Umewahi kuwahadaa wananchi na kuwaahidi usiyoweza kutimiza?
4.Umewahi leta mgawanyo baina ya wanajamii uliowakuta wamoja kabla ya kupewa dhamana?
5.Umewahi kuamua kwa jazba mpaka kuepelekea ugumu wa maisha kwa uliowaamulia?
6.Umewahi zuia haki za watu ambazo ni za msingi?
kama ni hivyo jua siku ukifa wanayasemea moyoni japo magazeti yanaweza kupamba na kuonesha mazuri machache tu
WITO KWA WATUMISHI WA UMMA PIA NANYI ACHENI ALAMA CHANYA MNAPOFARIKI MUONGELEWE VIZURI SI KWA UNAFIKI ,BALI KWA UKWELI KWELI KABISA
Britanicca