Ninahisi kama vile baadhi yetu ni wepesi wa kusahau mambo,hujenga hoja kutokana na kauli za vyombo vya habari visivyo na maadili, huiangalia timu yao peke yake kama vile ndiyo pekee inayocheza ligi na kutaka kila kocha apange timu vile tunavyoona sisi.
Angalia:
1. Baada ya kocha wa msimu uliopita kukatiza mkataba wake, nani alihoji usahihi wa Maximo kuwa mbadala wake?
2. Baaada ya mechi saba za ligi kocha mpya aliyekuta timu imeshasajiliwa 90% kuifikisha timu aliyoikuta kwenye nafasi sawa na kocha wa klabu inayotetea ubingwa aliyehusika na usajili 100%, anastahili lawama au pongezi?
3. Kwa hoja za mtoa mada, ni kocha yupi kati ya wawili hao ndiye hafai zaidi?
4. Kama kutofaa kwa kocha ni kwa mchezaji aliyemsajili kutofanya vizuri, Mourinho anafaa kwa kumsajili Ballak, Shevchenko, n.k? Au hapa nyumbani, mabingwa watetezi wamesajili wageni wawili ambao hawajafanya la maana kiasi cha mmoja kuvunjiwa mkataba, je na kocha huyo hafai?
5. Nani ana uhakika kwamba Niyonzima amekataa kusaini kwa sababu hafurahii maisha? Hata huyo aliyeripoti hivyo hana uhakika, asingesema 'habari kutoka kwa watu wa karibu na mchezaji'.
6. Kadhalika habari kuhusu Maximo kusema Kiiza aachwe, huku vyombo hivyohivyo vikisema kwamba Maximo ameagiza usajili usifanyike mpaka atapokuja. Usahihi ni upi? Hizo ndiyo habari au fununu? Tangu lini mtu akhukumiwa kwa fununu?
7. Wanaohoji ubadilishwaji wa wachezaji, mbona wanashindwa kubaini kwamba mara mbili wachezaji wanaoingizwa wamefunga mabao mawili? Huo si ushahidi kwamba mabadiliko hayo ni sahihi? Kwamba ramani yake ya mchezo (game plan) ni sahihi?
8. Wanaohoji kutochezeshwa Kaseja wamesahau alivyoboronga msimu uliopita mpaka baadhi wanabaki kuamini kwamba kufungwa kwake 'kwa bahati mbaya' ndiyo kumeikosesha Yanga ubingwa? Au tu wanaweweseka baada ya kusikia anatakiwa Simba? Mbona hawamtetei Barthez ambaye kabla ya kuja Kaseja alikuwa ndiye chaguo la kwanza? Si kwa sababu naye alisawazishiwa mabao matatu yanayodhaniwa kuwa baadhi ni ya Kizembe?
9. Wanaohoji uwezo wa Jaja, mbona hawavinukuu vyombo hivyohivyo wanavyomlaumia Maximo vinapowanukuu makocha kadhaa wanaomwona mchezaji huyo ni bora kiasi cha kutamani kuwa naye kwenye timu zao?
Kila mtu, akiwemo mwanzisha mada, ana haki ya kutoa maoni yake humu jamvini. Ushauri wangu ni kuwa tuwe tunawatendea haki wana JF kwa kujenga hoja sahihi, elimishi, chokonozi na changamshi.