nashukuru kwa ushauri Wako Luv nadhani umenipa mwanga ambao unaweza kunitoa katika hali niliyonao.... Napambana sana kuondokana na hili lakini inafikia kipindi nakata tamaa na kumuachia Mungu kila kituKwanza kujua tatizo ni hatua nzuri ya kutatua tatizo.
Cha kufanya kubali yaliyotokea na yaache yapite usiyaweke moyoni mwako, japo ni muhimu kubaki na funzo ulilolipata ili yasijirudie.
Kama upo tayari kuwa kwenye mahusiano basi kuwa huru acha kufananisha kila mwanamke na yule aliyekutenda hutafanikiwa.
Pia ukimpata unayehisi ni sahihi kwako kuwa muwazi mwambia changamoto ulizopitia katika mahusiano yako, jinsi unavyojisikia baada ya kutendwa, hiyo itasaidia kwake na kwako, anaweza kukuvumilia kwa kipindi cha kwanza na wewe ukiwa unajitahidi kurudi katika hali ya kawaida taratibu (kwa sababu umeshajijua upo vipi).
Jitahidi pia kuonana wa washauri nasaha wakusaidie katika hili.
Jiamini, amini kuwa unaweza kupata mtu atayekupenda na kukuthamini.
Mwisho ukishindwa kabisa kuji control endelea kujipa muda wa kuwa peke yako
Yule mpenzi wako wa kwanza hujamwacha aende.Bado hujawa kawaida katika kutulia moyo wako.Subiri kwanza kabla hujaanza uhusiano mpya au kuwa na Mtoto wa kike kwa ajili ya story,, outing na jokes ila umwambie akusaidie usifanye sex wakati ukimtaka.Nenda movie,,pumzika na fanya kazi yako kwa bidii.Usikae mpweke jichanganye baadhi ya mida.
Ujaamua nawee kuwa katika mahusiano. Wengine tumetendwa pia miaka inapta tuna move on. Maisha yako ya furaha unayo mwenyewe sasa ni kuamua kuifurahisha nafs yako au kuendelea kuimiza. Mimi yalinikuta yakwako kidogo na nimemoe on nafuraiya dunia yangu. Naomba Mungu anisaidie japo ya nyuma ni kama funzo but siruhusu yaninyime amani ya nafsi.
Sio lazima ku'do', unaweza kua kwenye mahusiano na mtu bila kufanya hivyo na maisha yakaenda, uzinzi nao sio mzuri