Sina Hamu Ya Tendo La Ndoa.

ibra87

R I P
Jul 22, 2015
5,614
5,351
Wasalaam

wana Jf......

Sijui kama hili ni tatizo ama ni hali ambayo inanitokea kutokana na mengi mabaya niliopitia katika mahusiano yangu.

Ni kweli mimi ni mwanaume lijali na kunawakati huwa nahitaji kuwa na mpenzi. Lakini nina tatizo kubwa. Tatizo lenyewe lilianza kipindi ambacho nilikumbwa na Misukosuko Ya kimahusiano na Kimapenzi. Misukosuko niliyopitia katika Mahusiano Ya kimapenzi niliyopitia nadhani ndio Sababu kubwa Ya Kutokewa na Hali hii ya Kutokutamani Tunda.

Nimejaribu kuingia katika Mahusiano kadhaa wa kadhaa na katika mahusiano hayo nimejikuta nikiwa mkali, mkorofi na Jeuri kwa niliyenae. Inafikia kipindi nashindwa hata kuitawala hasira yangu.. Nakuwa na Majibu ambayo hata wakati mwingine yananishangaza mpaka mimi Mwenyewe.

Naweza Nikawa naingia katika Mahusiano Ya kimapenzi lakini linapofikia Suala la Kugegeda nakuwa mtu tofauti kabisa.. Naonekana kama mtu ambaye sikuwa katika hali hiyo.. Kila msichana ambaye nilifanikiwa kuwa nae katika kipindi ambacho nilitoka kuumizwa nilijikuta nikishindwa kukutana nao kimwili kwa kuwa sikuwa nahisia kabisa juu ya Mapenzi.... Nilikuwa nikiwaonea huruma waliokuwa Wanalia kwa Ajili Yangu. Nilikuwa nikijaribu kwa hali na Mali kuondokana na Hali hii lakini Nimeshindwa...

Nahitaji kuingia katika Mahusiano lakini naogopa kumuumiza mtu

natamani kuwa na mpenzi kwasasa, lakini naogopa kutesa hisia za mtu...

Nimekuwa Ibrah wa Ajabu, nimekuwa Ibrah wakujitenga na Watoto wa kike... Imefikia hatua kuna binti anakuja mpaka kwangu na kuingia ndani. Atafanya kila Aina Ya kitu lakini Bado ibrah nitabaki kumuangalia tu... Atanifanyia kila kitu huku akiliona gegedo likiwa wima lakini kuna Maneno niliyowahi kutamkiwa katika mahusiano niliyopitia nikikumbuka tu basi palepale roho huingia nyongo na Kutamani kumfukuza.

Nateswa na Hali hii, nasumbuliwa na Hali hii. Nahitaji msaada wa kitaalamu au ushauri utakaonifanya niondokane na Hili tatizo kwani kunakipindi natamani kuwa na Mtu lakini maneno ya Kejeli na dharau kwa waliokuwa wapenzi Wangu yananiumiza na Kunitesa sana.

Nahitaji kutoka ndani Ya Minyororo Hii lakini nashindwa. Nashindwa kusimama kwa miguu Yangu naombeni msaada Wenu katika Hili.....

Hasira, dharau, kiburi vinanifanya nionekane ni mwanaume watofauti...

Naombeni Wana Jf wenzangu mnisaidie kunitoa katika hali hii..nahitaji kuwa na mwenza lakini sipo tayari kumuumiza Mwanamke aliyenipenda kwa Moyo Wake Wote...

Ingawa moyo Wangu Unahisia juu Ya Mapenzi lakini Kwenye Suala la Tendo ndio Sina Hamu kabisa

NITATOKAJE KATIKA HALI HII?
 
Wallet inasoma vizuri? maana hamu ya tendo la ndoa ni lazima ubongo na wallet viwe na ushirikiano otherwise huwezi kupata hamu wala kusimamisha. Pesa ndio jibu la yote.
 
Sio lazima ku'do', unaweza kua kwenye mahusiano na mtu bila kufanya hivyo na maisha yakaenda, uzinzi nao sio mzuri
 
Kwanza kujua tatizo ni hatua nzuri ya kutatua tatizo.

Cha kufanya kubali yaliyotokea na yaache yapite usiyaweke moyoni mwako, japo ni muhimu kubaki na funzo ulilolipata ili yasijirudie.

Kama upo tayari kuwa kwenye mahusiano basi kuwa huru acha kufananisha kila mwanamke na yule aliyekutenda hutafanikiwa.

Pia ukimpata unayehisi ni sahihi kwako kuwa muwazi mwambia changamoto ulizopitia katika mahusiano yako, jinsi unavyojisikia baada ya kutendwa, hiyo itasaidia kwake na kwako, anaweza kukuvumilia kwa kipindi cha kwanza na wewe ukiwa unajitahidi kurudi katika hali ya kawaida taratibu (kwa sababu umeshajijua upo vipi).

Jitahidi pia kuonana wa washauri nasaha wakusaidie katika hili.

Jiamini, amini kuwa unaweza kupata mtu atayekupenda na kukuthamini.

Mwisho ukishindwa kabisa kuji control endelea kujipa muda wa kuwa peke yako
 
Yule mpenzi wako wa kwanza hujamwacha aende.Bado hujawa kawaida katika kutulia moyo wako.Subiri kwanza kabla hujaanza uhusiano mpya au kuwa na Mtoto wa kike kwa ajili ya story,, outing na jokes ila umwambie akusaidie usifanye sex wakati ukimtaka.Nenda movie,,pumzika na fanya kazi yako kwa bidii.Usikae mpweke jichanganye baadhi ya mida.
 
Wallet inasoma vizuri? maana hamu ya tendo la ndoa ni lazima ubongo na wallet viwe na ushirikiano otherwise huwezi kupata hamu wala kusimamisha. Pesa ndio jibu la yote.

mkuu kiasi flani hilo sio tatizo kwangu ya mboga inapatikana
 
Unahitaji msaada wa kitaalam zaidi wasiliana na washauri nasaha, kuna mtu anaitwa Chris Mauki he is good mtafute kupitia fb
 
Sio lazima ku'do', unaweza kua kwenye mahusiano na mtu bila kufanya hivyo na maisha yakaenda, uzinzi nao sio mzuri

sijasemea ngono ya tamaa, nasemee kujenga mahusiano thabiti na yasioyumbishwa na hali niliyoisema
 
Kwanza kujua tatizo ni hatua nzuri ya kutatua tatizo.

Cha kufanya kubali yaliyotokea na yaache yapite usiyaweke moyoni mwako, japo ni muhimu kubaki na funzo ulilolipata ili yasijirudie.

Kama upo tayari kuwa kwenye mahusiano basi kuwa huru acha kufananisha kila mwanamke na yule aliyekutenda hutafanikiwa.

Pia ukimpata unayehisi ni sahihi kwako kuwa muwazi mwambia changamoto ulizopitia katika mahusiano yako, jinsi unavyojisikia baada ya kutendwa, hiyo itasaidia kwake na kwako, anaweza kukuvumilia kwa kipindi cha kwanza na wewe ukiwa unajitahidi kurudi katika hali ya kawaida taratibu (kwa sababu umeshajijua upo vipi).

Jitahidi pia kuonana wa washauri nasaha wakusaidie katika hili.

Jiamini, amini kuwa unaweza kupata mtu atayekupenda na kukuthamini.

Mwisho ukishindwa kabisa kuji control endelea kujipa muda wa kuwa peke yako
nashukuru kwa ushauri Wako Luv nadhani umenipa mwanga ambao unaweza kunitoa katika hali niliyonao.... Napambana sana kuondokana na hili lakini inafikia kipindi nakata tamaa na kumuachia Mungu kila kitu
 
Ujaamua nawee kuwa katika mahusiano. Wengine tumetendwa pia miaka inapta tuna move on. Maisha yako ya furaha unayo mwenyewe sasa ni kuamua kuifurahisha nafs yako au kuendelea kuimiza. Mimi yalinikuta yakwako kidogo na nimemoe on nafuraiya dunia yangu. Naomba Mungu anisaidie japo ya nyuma ni kama funzo but siruhusu yaninyime amani ya nafsi.
 
Yule mpenzi wako wa kwanza hujamwacha aende.Bado hujawa kawaida katika kutulia moyo wako.Subiri kwanza kabla hujaanza uhusiano mpya au kuwa na Mtoto wa kike kwa ajili ya story,, outing na jokes ila umwambie akusaidie usifanye sex wakati ukimtaka.Nenda movie,,pumzika na fanya kazi yako kwa bidii.Usikae mpweke jichanganye baadhi ya mida.

nashukuru mkuu wangu, nashukuru kwa ushauri huu.. Huwa nawazaga mengi sana lakini nabaki sina la kufanya
 
Unahitaji msaada wa kitaalam zaidi wasiliana na washauri nasaha, kuna mtu anaitwa Chris Mauki he is good mtafute kupitia fb

nitafanya hivyo mkuu, nahitaji kutoka katika tatizo hili... Nashukuru kwa ushauri wako
 
Ujaamua nawee kuwa katika mahusiano. Wengine tumetendwa pia miaka inapta tuna move on. Maisha yako ya furaha unayo mwenyewe sasa ni kuamua kuifurahisha nafs yako au kuendelea kuimiza. Mimi yalinikuta yakwako kidogo na nimemoe on nafuraiya dunia yangu. Naomba Mungu anisaidie japo ya nyuma ni kama funzo but siruhusu yaninyime amani ya nafsi.

ahsante sana mkuu.. Ulichosema ni kweli na nimejaribu kwa kipindi kirefu bila mafanikio.. Ukiona Chura Analia tambua maji Yamemzidi
 
Pole Sana kijana, Mi pia nmetendwa Lakini nkipata show napiga mzgo kwa nguvu zote kuondoa stress kwa mda
 
Sio lazima ku'do', unaweza kua kwenye mahusiano na mtu bila kufanya hivyo na maisha yakaenda, uzinzi nao sio mzuri

Kwa hawa mabinti wa sasa??? Unamdanganya mwenzio.... binti lazima atagawa kitumbua kwa wajanja.
 
Back
Top Bottom