Robbykan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2015
- 509
- 470
Wakuu habarini za mida hii,
Poleni kwa majukumu ya kila siku ya kukabiliana na changamoto za maisha. Nina hoja nataka mnipe ushauri ndugu zangu.
Nimejikuta nakosa hamu kabisa ya kuwa na msichana. Hii hali imenitokea karibia mwezi unaisha. Ninaye mpenzi ila saivi namchukia sana na nataka niachane naye. Yaani nimetokea kumchukia sana sijui kwanini hadi najishangaa mwenyewe sina msichana mwingine pembeni ila nimejikuta tuu na hii hali.
Yaani akili yangu inanituma niishi peke yangu bila mwanamke. Nimekuwa navumilia tuu kujikaza ili huyu mpenzi wangu asijue lolote ila kiukweli sina hamu kabisa na mahusiano na mwanamke. Ifahamike kuwa sina tatizo na wanawake ila hii hali imenitawala kwenye ubongo wangu yaani hadi sijielewi.
Naombeni ushauri wenu hasa wataalam wa saikolojia kwanini nakuwa hivi.