nusuhela
JF-Expert Member
- Jan 26, 2014
- 6,274
- 7,774
Baada ya kurudi Mbeya nyumbani, kuna mradi wa familia niliuona kuwa potential hasa kwa mazingira ya vijijini. Mradi huu unaingiza faida ya sh 10000 kwa siku. Ni mradi ambao hakika ukisimamiwa vizuri, unaweza leta mabadiliko.
Nikapiga mahesabu ya tangu kuwa na huu mradi familia ina akiba ya sh ngapi? Nikakuta ni zero. Yaani wanautumia huu mradi kama sehemu ya kutatulia shida zao huku mradi huu ukiwa hauna back up.
Hakika iliniuma nilipoona zaidi ya miaka 5 ya mradi huu bado fimilia haina hata balance.
Nikaamua niweke mikakati ya kuweka akiba kwaajili ya back up ili hata mashine zikisumbua, tusianze kuhangaika. Basi bwana kuna ka account kangu ka nmb nilikua nako na kapo active, nikaona sio mbaya nikiwa naweka huko hela wakati nafanya mpango wa kufungua account maalum kwaajili ya huu mradi. Nikaweka kama sh 80,000 hivi. Kwakua nina NMB MKONONI app, nikataka kuangalia salio. Eeeebwana eehh!! Nilichokikuta huko nilipagawa. Badala ya sh kukuta 80,000, nikakuta kuna 70,880. Ikabidi nichoke. Nikaona acha niombe statement ili nijiridhishe. Kunitumia statement kwenye email yangu wakakata sh 1,000 ikabaki sh 69,880. Nikasema hapa usinitanie, kesho lazima nikatoe balance hii. Basi leo ilipofika asubuhi na mapema nikaenda ATM ya pale Mbalizi tawi la NMB USONGWE. Kila nikijaribu kutoa sh 60,00, naambiwa huduma haijakamilika. Ikabidi niingie ndani ili nitolee dirishani. Kilichonikuta ndicho kilichofanya niandike hapa. Nikachukua fomu ya kutolea ha na nikaijaza vizuri ili niweze kutoa japo sh 68,000. Kwenda dirishani nikaambiwa siwezi kutoa kiwango hicho kwakua salio halitoshi. Nikashtuka. Nikamwambia teller kuwa mbona acc yangu ina sh 69,880? Akanijibu kwa ukali kuwa "bro kutoa hapa ni sh 6,500 kwahiyo inatakiwa utoa sh 60,000" nikahamaki huku nikijisonya kwanini nilidumbukiza hela bank.
Nikiwa na uchungu wa hela yote ninayoipa NMB pasipo wao kutoa jasho, nikajaza fomu ya kutoa sh 60,000
Hakika ni bora kuchimbia hela chini kuliko kuweka hela NMB