Sina amani naye japo nampenda huyu binti

Hauna haja ya kutoa hizo salamu,salamu ni moja tu,nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano ya Tanzania!!
 
Asa mtu kama huyu niwa kuombea ushauri?
Afu inaonekana kwenye haya mambo ya mahusiano pia hauna uzoefu nayo

Kaa ujifunze game ukikomaa ndo uoe
Daaah! Ni kweli sina uzoefu saana lakini kwa mahusiano nilo pitia na kujifunza kupitia makala mbali mbali ninao uzoefu, ndo maana nipo na mashaka.
 
Mkanye hiyo tabia mimi wangu ashawahi kuwa anachati huku tunaongea akawa hatusikilizani maana anaitika tu nikakata simu alipiga sana sikupokea siku nzima, nikamtext ukimaliza kuchat utaniambia aliomba samahani balaa nikakaza na bahati yake alikua anachat na mdogo wangu kumbe mda huo nikamsamehe baada ya siku 3.
Mpaka leo hata nikiwa nae anatumiwa text anasoma anaeka simu pembeni.
 
Inakera sana hali hiyo mkuu yaani unaweza hata kuvunja maagano mlio wekeana. Me ntamkanya aisee asipo nielewa basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…