Sina amani naye japo nampenda huyu binti

Bwana wetu Yesu asifiwe wapendwa, Asalaam naalykum kwa waisilam wote natumaini mu wazima wote.

Moja kwa moja nizame ndani ya maada wapendwa. Mimi ni kijana ambaye natarajia kuingia kunako ndoa ikimpendeza Mungu wangu,
Umri wangu miaka 25

Kuna binti ambae tulikutana kwa mazingira fulani tukazoeana na tunaishi naye mitaa ya karibu japo kuna umbali kidogo, baadae alichukua namba yangu bila mi kujua, baadae ndo kuanza kuchati pamoja na mazungumzo kwa njia ya simu na ana kwa ana hadi kufikia binti kunitamkia kuwa anahitaji me niwe mme wake wa ndoa na ananipenda ,, basi sikumpa jibu la kumaanisha nikamwambia poa ikimpendeza Mungu tutakuwa pamoja.

Nimekaa naye hivo huku nikiendelea kumchunguza basi nami moyo wangu ukazidi kumpenda kila kukicha na nipo radhi kumuoa japo hapa katikati ilitokea changamoto fulani ambayo nikawa najiuliza saana, kuna kuna jamaa ambae tunasali nae kanisa moja naye akawa anamtaka kwamba anahitaji kumuoa na binti akawa ananitumia zile chating za jamaa akimuomba anahitaji kuwa naye.

Binti akanithibitishia kuwa anipenda mie na akamtumia jamaa sms kuwa mi ndo ntakuwa mumewe au baba watoto wake,, lakini sijajua kama jamaa bado wanaendelea naye katika harakati hizo.

Changamoto ya huyu binti:
Au niseme asili yake ambayo nishaiona kwake ni mtu ambae anapenda kuongea na kila mtu halafu ni mwongeaji sana halafu marafiki wengi wa kiume na kuchati anachat sana kila wakati yaani chaji yake huwa inaisha mara nyingi kwa kuchat hata nikiwa nae sms mara kwa mara zinaingia kwake, hiyo hali inanitia shaka je atakuwa mwaminifu kweli kama mimi nilivyo mwaminifu kwake?

Je, ntaiweza kweli hii hali maana mpaka tusha elewana me nikipata mahari nimchukue mtoto niweke ndani,,

Wadau kwa hili limekaaje?
Hauna haja ya kutoa hizo salamu,salamu ni moja tu,nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano ya Tanzania!!
 
Asa mtu kama huyu niwa kuombea ushauri?
Afu inaonekana kwenye haya mambo ya mahusiano pia hauna uzoefu nayo

Kaa ujifunze game ukikomaa ndo uoe
Daaah! Ni kweli sina uzoefu saana lakini kwa mahusiano nilo pitia na kujifunza kupitia makala mbali mbali ninao uzoefu, ndo maana nipo na mashaka.
 
Vp mkuu kuna ulazima wa kumwambia kuwa sipendezwi na tabia yake?

Maana nakumbuka siku moja tupo tunaongea kwa njia ya simu kumbe kaongeza round speaker ananiskilz huku anachat,nikaskia vibatan vinasikika ndo nikamwambia harafu upo unachati?

Ndo kuomba msamaha nimsamehe basi nikamwambia haina shida tukaendelea na mazungumzo yetu.
Mkanye hiyo tabia mimi wangu ashawahi kuwa anachati huku tunaongea akawa hatusikilizani maana anaitika tu nikakata simu alipiga sana sikupokea siku nzima, nikamtext ukimaliza kuchat utaniambia aliomba samahani balaa nikakaza na bahati yake alikua anachat na mdogo wangu kumbe mda huo nikamsamehe baada ya siku 3.
Mpaka leo hata nikiwa nae anatumiwa text anasoma anaeka simu pembeni.
 
Mkanye hiyo tabia mimi wangu ashawahi kuwa anachati huku tunaongea akawa hatusikilizani maana anaitika tu nikakata simu alipiga sana sikupokea siku nzima, nikamtext ukimaliza kuchat utaniambia aliomba samahani balaa nikakaza na bahati yake alikua anachat na mdogo wangu kumbe mda huo nikamsamehe baada ya siku 3.
Mpaka leo hata nikiwa nae anatumiwa text anasoma anaeka simu pembeni.
Inakera sana hali hiyo mkuu yaani unaweza hata kuvunja maagano mlio wekeana. Me ntamkanya aisee asipo nielewa basi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom