Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
Ni shehe anayeendesha kipindi cha ARISALAH kwenye kituo cha Channel 10.
Jana nilibahatika kumsikiliza kwenye redio fulani ambapo pamoja na yeye alialikwa Askofu Gamanywa. Ndugu zetu hawa muhimu katika maswala ya kiimani pamoja na mambo mengi waliyoyajadili ni suala la viongozi wa dini kuingilia mambo ya kisiasa.
Shehe huyu mbali na kutotaja jina lakini alionekana wazi akimpiga vijembe Kakobe na kumlaumu kwa kitendo chake cha "kuwaelimisha waumini wake elimu ya URAIA" Lakini pia hakuacha kumwagia sifa kemekem mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa ni jasiri, anafuata utawala wa sheria, ametuongoza vizuri na wezi wote wa fedha za umma wamefikishwa mahakamani. Hakusita kuonyesha kukubali kwake uamuzi wa JK kuwasifia na kuwapigia debe hadharani wale wenye kesi mahakamani za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. Kwake yeye na alikuwa anataka kutulazimisha tuamini kuwa watu wale watakuwa na hatia pindi tu mahakama itakaposema watu wale ni wevi kweli. (hatujui ni baada ya miaka mingapi uamuzi utatolewa na watu wale wataendelea kula kuku tu)
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa:
1. Katika kipindi chake cha ARISALA aliwahi kusema Endapo CCM isingeleta mahakama ya Kadhi basi yeye angezunguka Tanzania nzima ikiwezekana kwa mguu kupiga mbiu ya wananchi kutoichagua CCM.
2. Aliwahi kusema kuwa si busara kumchagua Rais ambaye hana ndoa na kwamba akiapa atakuwa anaapa kwa kutumia kitabu gani cha dini maana biblia inakataa uzinzi na Rais huyo akichaguliwa akiwa hana ndoa tafsiri ni hiyo kuwa tutakuwa na rais mzinzi.
3. Kupitia Radio Kheri aliwahi kusikika kuwa waislam wasiwe na waswasi na CCM kwakuwa JK hakuhusika kuandaa ilani iliyowekwa ahadi ya mahakama ya Kadhia na aliyeweka ni BWM, Maleccella pamoja na Mangula so wakristo wanaunga mkono mahakama hiyo.
Wakati yeye ni kinara wa kumkoromea kakobe kuwa anachanganya dini na siasa yeye, pamoja na Magazeti yake ya ALHUDA pamoja na ANNUUR wanashabikia Udini kwa asilimia 100%.
Mfano, Alhuda ya Jana ilikuwa na habari ya kuwachonganisha waislamu wema na Dokta slaa. Kichwa Cha habari kilisema Mpangoi wa Dkt Slaa wakwama. Eti kwa research waliyofanya Alhuda, Wakatoliki wapo Milioni 8 ambao wote wangempigia kura Slaa. Kwakuwa hesabu za Slaa na Chama Chake ni kuwa Wapigakura ni milioni16 kabla tume "haijachomekea" wapigakura milioni3 maana yake Slaa alikuwa na uhakika na nusu ya kura za wapigakura wooote (uchochezi wa uongo). Eti tume imeharibu mkakati wa Slaa.
Wanajamvi, viongozi wa dini wa namna hii tuwafanyeje?