Simuogopi yeyote, nina msimamo - Werema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simuogopi yeyote, nina msimamo - Werema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Oct 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Frederick Werema (55), amesema ana msimamo na haogopi shinikizo la yeyote.

  Werema amesema, Rais Jakaya Kikwete, anafahamu kuwa ana msimamo na pia waliowahi kufanya kazi na yeye wanatambua kuwa hafanyi uamuzi kwa kushinikizwa.

  “Bila shinikizo hakuna kazi, mimi ni mtu wa msimamo, aliyeniteua anajua msimamo wangu na hata waliowahi kufanya kazi nami wananijua sishinikizwi na mtu” amesema Werema jana muda mfupi baada ya Rais Kikwete kumuapisha Ikulu, Dar es Salaam.

  Werema anafahamu kuwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu inatuhumiwa kwa rushwa katika kuingia mikataba ya Serikali lakini yeye amesema “ninaporidhika ndipo mikataba itatekelezwa sitaki kushinikizwa”.

  Amesema, hana taarifa rasmi kwamba, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inahusika kuingia katika mikataba mibovu.

  “Mimi sifahamu taarifa hizo nasoma kwenye magazeti hivyo nahitaji kufanya utafiti wa kutosha na kuwasiliana na taasisi nyingine za Serikali kupata taarifa kamili ndipo nijue kama nachukua hatua” amesema.

  Werema ana taaluma ya sheria ya biashara, namna ya kujadiliana katika mikataba na namna ya kufanya biashara ya umeme katika kubinafsisha nishati hiyo.

  Amesema, ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali haina uhaba wa wataalamu wa mikataba na amebainisha kwamba, mikataba mingine wanalazimika kuingia bila kuwa na uwezo wa kujadili ikiwemo ya Benki ya Dunia.

  Jaji Werema amewahi kuwa wakili wa Serikali kwa miaka 23 kuanzia mwaka 1984,na Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu kuanzia mwaka 2007.

  Anachukua nafasi ialiyoiacha Johnson Mwanyika,yupo kwenye likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Mwanyika aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Desemba, mwaka 2005.

  Rais Kikwete pia amemuapisha George Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Werema na Masaju waliteuliwa Jumanne, kabla ya uteuzi huo, Masaju alikuwa Mshauri wa Sheria wa Rais,Ikulu.

  Rais Kikwete pia amewaapisha Makatibu wakuu wa Wizara za Serikali na maofisa wawili waandamizi wa Serikali. Rais aliwateua Jumatatu wiki hii.

  Rais amemuapisha David Jairo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbarak M. Abdulwakil kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Amemuapisha pia Christopher Sayi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, na Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais.

  “Nakwenda kujifunza kwa nitakaowakuta na kushirikiana na wanasekta za habari, michezo na utamaduni” amesema Kamuhanda.

  Mbena, amesema, atamsaidia Rais Kikwete katika mambo mbalimbali yanayomkabili likiwemo tatizo la umeme, kuyumba kwa uchumi, usafirishaji, na uchaguzi mkuu mwakani.


  Chanzo:
  Gazeti la HabariLeo
   
 2. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watamsaidia kuiba !!
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mwanasheria Mkuu mpya aanza kazi kwa mkwara

  [​IMG]

  Na Exuper Kachenje

  SIKU moja baada ya kuteuliwa na kisha kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, Jaji Frederick Mwita Werema alisema atahakikisha kuwa taifa haliingii mikataba mibovu.

  Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kuapishwa Ikulu jana, Werema alisema kwa msisitizo: "Rais aliyeniteua ndio anaujua msimamo wangu."

  Werema aliyemrithi Johnson Mwanyika aliyestaafu kwa mujibu wa sheria, alisema kuwa atafanya kazi na kutekeleza wadhifa wake mpya kulingana na kiapo alichokula mbele ya Rais na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kuapishwa, mwanasheria mkuu huyo alisema katika kutekeleza wajibu wake mpya hataki mashinikizo ya wanasiasa au mtu yeyote.

  "Mashinikizo… Hayo yapo huwezi kufanya kazi bila hayo kuwepo; lakini aliyeniteua anajua msimamo wangu. ..Sitaki mashinikizo na sipendi kuhukumu bila ushahidi. Mnataka nirudie kiapo changu? Nawahakikishieni kuwa nitafanya kazi kufuatana na kiapo changu," alisema Jaji Werema.

  Alipoulizwa kuhusu kashfa ya Kampuni ya Richmond (LLC) ambayo mtangulizi wake (Mwanyika) amehusishwa, Jaji Werema ambaye pia ni mtaalamu wa sheria za mikataba na biashara, alikataa kulisemea hilo. Hata hivyo alisema hilo linafanyiwa kazi na wahusika.

  "..Richmond, kwa kweli siijui mimi nasoma tu katika magazeti kwamba, lipo katika 'arbitration' (usuluhishi), hivyo siwezi kulisemea," alijitetea Jaji Werema.

  Kuhusu mikataba mibovu ya madini inayodaiwa kuingiwa na watangulizi wake pamoja na tuhuma za ufisadi na rushwa, Jaji Werema alisema: "Kuhusu hilo; unapozungumzia watuhumiwa lazima uwe mwangalifu, usihukumu, usije ukahukumiwa. Kwa sasa sina lolote jamani, mpaka nikiingia ofisini na kusoma majalada. Nitalizungumzia hilo nikishaingia ofisini, bado sijakabidhiwa ofisi."

  Aliongeza: " Katika hilo; ndugu waandishi nimefanya kazi na ninyi na nitafanya kazi na ninyi. Lazima muwe waangalifu, mnapoandika tuhuma msihukumu, nimeshuhudia hukumu nyingi zinaathiriwa na magazeti".

  Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu uwepo wa sheria ya adhabu ya kifo na sheria zilizopo kwa muda mrefu alisema: " Sina maoni kuhusu sheria ya kifo. Unapoangalia umuhimu wa sheria si lazima uonyeshe sheria za zamani kuwa hazifai, kwani pengine zinatoa manufaa zaidi kwa jamii. Uzee si kashfa wala ujana si sifa, lakini nitazifanyia kazi sheria zote kwa kutumia Ibara ya 59 ya Katiba ya Tanzania".

  Ibara ya 59 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbali na kueleza nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atateuliwa na Rais, Ibara ya tatu ya kifungu hicho inafafanua wajibu wake kwa serikali kuhusu sheria.

  Tukio hilo la kuapishwa Mwanasheria mkuu lilienda sambamba na kuapishwa kwa Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju, makatibu wakuu wanne wa wizara pamoja na katibu wa rais walioteuliwa hivi karibuni.

  Makatibu wakuu walioapishwa ni pamoja na David Jairo Katibu Mkuu (Wizara ya Nishati na Madini), Sazi Salula (Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Seth Kamuhanda (Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo) na Christopher Sayi (Wizara ya Maji na Umwagiliaji).

  Hata hivyo ukumbi palipofanyika hafla hiyo ulifurika watu wakiwemo ndugu na jamaa wa wateule hao.

  Kutokana na ukumbi huo kujaa watu, muda mfupi baada ya kuanza shughuli ya kuapisha wateule wake, Rais Jakaya Kikwete alisikika akimwita na kumwagiza mmoja wa wasaidizi wake, kuwa hakuna hewa ya kutosha hivyo madirisha yaliyofungwa yafunguliwe.

  "Ebu mkafungue madirisha yale, hakuna hewa kabisa hapa," alisikika rais akisema na msaidizi huyo alikwenda haraka kuleta wahudumu watano waliovalia nadhifu na kuyafungua madirisha.

  Awali, baada ya Jaji Werema kumaliza kusoma kiapo, kabla ya kupeana mkono na Rais na kukabidhiwa hati ya kiapo chake, aligeuka na kuanza kurejea alipoketi, lakini alishtuka na kurudi kuendelea na utaratibu. Kitendo hicho kilizusha miguno ya chinichini ndani ya ukumbi huo.

  Katika tukio jingine baada ya Rais Kikwete kumwapisha Katibu wake mpya, Prosper Mbena na watu kushangilia, akamweleza mteule huyo kwa sauti kwamba, aanze kazi wakati huo huo na kusababisha umati uliokuwepo kuangua kicheko.

  "Prosper, anza kazi sasa hivi," Rais Kikwete alisema.

  Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Makammu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Wakati huohuo, akitoa maoni yake kuhusu uteuzi wa Jaji Werema, Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Dk Fauz Twalib alisema Rais amefanya uchaguzi mzuri.

  Akizungumza na Mwnanchi jana, Dk Twalib alisema ni imani yake kuwa Mwanasheria Mkuu huyo mpya atafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kuwa ni mchapa kazi.

  "..Ni uchaguzi mzuri, namfahamu siku nyingi Jaji Werema, ni mchapa kazi, amefanya kazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa siku nyingi, ndio ofisi iliyomkuza tangu alipotoka chuo kikuu," alisema Dk Twalib.

  Kauli hiyo iliungwa mkono na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema aliyesema Rais amefanya uamuzi mzuri.

  "Rais amefanya uamuzi mzuri, yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, sasa amri imeshatoka sisi ni kufanya kazi, lazima tuhakikishe amefanikiwa, tutashirikiana naye, tutampa ushirikiano na wengine pia wampe ushirikiano," alisema Mwema

  Jaji Frederick Mwita Werema alizaliwa Oktoba 10, 1954 na amafanya kazi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali tangu mwaka 1984 na mwaka 2007 aliteuliwa kuwa Jaji.

  Amewahi kuwa Wakili wa Serikali na Mkurugenzi wa Katiba na haki za binadamu ambapo elimu yake aliipata pia katika nchi za Uingereza, Marekani, Bolivia aliposomea masuala ya mikatabaa ya umeme.


  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15481
   
 4. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  atadanganyika tu, hayo ni maneno tu lakini kwenye vitendo je?
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Angelijua ukubwa wa mambo yanayomkabili mbele yake, asingelisema sana.
   
 6. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hivi na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima alikuwepo kwenye press conference hiyo hiyo au yeye aliandaa mkutano wake tofauti?..Au ndio mambo ya mtazamo wa mwandishi? Maana ukiisoma habari hii hii kwenye TD picha unayopata ni tofauti kabisa na hii ya kwenye Mwananchi na Habari Leo.

  Vita ya Ufisadi: Mrithi wa Mwanyika aonya

  • Asema hatashitaki mtu kwa rushwa kwa shinikizo la wanahabari
  na Sauli Giliard

  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali mpya, Jaji Fredrick Mwita Werema, aliapishwa jana na kutoa mkwara mzito kwa kueleza kukerwa na tabia ya watu na vyombo vya habari kuwahukumu watu kwa kuwaita mafisadi.

  Mbali ya hilo, Jaji Werema alisema wakati atakapokuwa kazini, hatakubali kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa rushwa kubwa kwa shinikizo la vyombo vya habari wala mtu yeyote.

  Akizungumza na wanahabari kwa kujiamini, muda mfupi baada ya Rais Kikwete kumuapisha kushika wadhifa huo akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Johnson Mwanyika aliyestaafu, Werema alisema kwa msimamo wake huo hata Rais Jakaya Kikwete anamfahamu vema.

  “Sipendi mtu ahukumiwe kabla. Suala la rushwa, vyombo husika vitashughulikia…nikijiridhisha na kesi hakuna wa kunizuia. Sipendi mashinikizo,” alisema mrithi huyo wa Mwanyika.

  Alisema anaamini kwamba, kutokana na kuwa na msimamo huo katika utendaji wake wa kazi, ndiyo ameteuliwa kushika wadhifa huo nyeti serikalini na ambao unamfanya aingie bungeni kwa wadhifa wake huo.

  Wengine walioapishwa katika hafla hiyo ni pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju ambaye awali alikuwa Mshauri wa Sheria wa Rais, Ikulu na makatibu wakuu wapya wa wizara.

  Werema alitoa msimamo huo mzito baada ya kuulizwa na mmoja wa waandishi wa habari walioshuhudia hafla hiyo, kwamba amejiandaa vipi kukabiliana na hali ya sasa ya mapambano dhidi ya ufisadi.

  Katika hilo aliongeza kuwa, baada ya kuridhika na aina ya kesi inayotakiwa kupelekwa mahakamani, hakuna mtu yeyote atakayemzuia.

  Jaji Werema, aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, alivionya vyombo vya habari kutoandika habari zinazoweza kuathiri mwenendo wa kesi za rushwa kubwa.

  Katika hilo, aliwataka waandike habari zilizofanyiwa utafiti wa kina kwani zikiandikwa kwa ushabiki, zinamweka jaji njia panda wakati wa kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na anayetuhumiwa anaonekana kutotendewa haki.

  “Tuwe waangalifu, waandishi zingatieni maadili ya uandishi, hasa juu ya tuhuma juu ya watu. Kama jaji ataamua kumwachia mtu kutokana na aina ya tuhuma kinyume na watu walivyotarajia, nadhani uhuru wa mahakama unaingiliwa,” alionya Werema, aliyekuwa jaji katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.

  Alipoulizwa namna atakavyoshughulikia sheria mbovu kama ile ya madini inayolalamikiwa na wanasiasa, wasomi na wanaharakati, alisema si wakati wote sheria zinakuwa zimepitwa na wakati, bali mashinikizo kutoka mashirika ya kimataifa ndiyo yanayotoa msukumo wa kukubali na kusaini baadhi ya mikataba.

  Alisema, si mambo ya kisheria pekee yanayosababisha taifa kuingia katika mikataba mibovu kwani kuna wanasheria wengi ni wazuri nchini wanaofahamu sheria, hasa za mikataba ya kimataifa ila tatizo ni kwamba mashinikizo kutoka mashirika ya kimataifa yanachangia.

  Hata hivyo, mtaalam huyo wa mikataba alisema, hawezi kujibu ovyo ovyo juu ya mikataba mibovu inayolalamikiwa kwa sasa, kwa kuwa bado hajaingia ofisini na kuanza kazi rasmi.

  Mwanasheria huyo alipata elimu ya taaluma ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nchini Marekani.

  Wakili huyo wa serikali kwa miaka mingi, alishawahi kwenda nchini Italia kusomea masuala ya sheria katika mikataba, Uingereza na Bolivia alikoenda kusomea mchakato mzima wa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa nishati.

  Hata hivyo, Werema anachukua nafasi hiyo huku mtangulizi wake, Mwanyika akiwa ni mmojawapo wa vigogo waliochunguzwa kwenye kashfa ya kuipa mkataba wa ufuaji wa umeme wa dharura Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC.

  Mwanyika (60), alitajwa kwenye taarifa ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harison Mwakyembe kuchunguza kashfa hiyo.

  Mbali ya Werema, na Naibu wake, Rais Kikwete pia aliwaapisha makatibu wa wizara.

  Makatibu hao na wizara zao kwenye mabano ni David Jairo (Wizara ya Nishati na Madini), Sazi Salula (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na Mbarak Abdulwakil (Mambo ya Ndani ya Nchi).

  Wengine ni Christopher Sayi (Wizara ya Maji na Umwagiliaji), Sethi Kamuhanda (Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo) na Prosper Mbena (Katibu wa Rais).

  Akizungumza katika viwanja vya Ikulu, mara baada ya kuapishwa, Katibu wa Rais alimshukuru Kikwete kwa kumpa wadhifa huo na kuahidi kwamba atasaidiana na kiongozi huyo kuhakikisha kuwa yale yote yaliyoahidiwa yanatekelezwa.

  Naye Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe aliwaambia waandishi wa habari kwamba, mipango iliyopo katika wizara yake ni kuhakikisha kwamba kesi haiendeshwi kwa zaidi ya miaka miwili.

  Mbali na Chikawe, viongozi wengine waliohudhuria tukio hilo nyeti ni pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Shein.
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tunahitaji majaji shupavu na wanaojiamini kiutendaji na walioiva kisheria kama huyu! Mungu akuongezee hekima katika utendaji wako na maarifa zaidi katika kutoa maamuzi sahihi! MUNGU ibariki Tanzania
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Oct 22, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii ndio inaitwa Hatari ya Kusikiliza Hadithi Moja (The Danger of a Single Story). Someni na vyanzo vingine. Na msome katikati ya mistari (Read between the Lines).

  Kwa mfano, gazeti la The Citizen linamnukuu AG mpya akisema hivi: "The new AG came to the defence of his predecessors, saying they should not be accused of failing to properly advise the Government on legal matters, for doing so without evidence was an attack on the judicial process. 'Judge others not, before you are judged. When you are trying to link these people (his predecessors) with mishandling major contracts you must first have sufficient evidence. 'You cannot say whether or not they were involved in the allegations before you have strong evidence in hand. I urge you, journalists, to observe ethics and not condemn people unfairly".

  Kwa hiyo wanaotumia evidence ya SFO wanamhukumu Mzee wa Vijisenti? Na wanaotumia Ripoti ya Kamati teule ya Bunge ya kuchunguza Richmond wanamhukumu Mwana wa Nyika unfairly?
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mwanzoni kila mtu anasema hivyo hivyo, mwansheria mkuu atakuwa judged kwa matendo yake na wala sio alichosema wakati anaapishwa.

  Mara nyingi ni rahisi mno kusema lakini inapokuja kutenda Watanzania hapo ndipo tunajikanyaga mno.

  Mimi namtakia mafanikio mema katika kazi yake. Huu mkwara bora asingeusema na kuacha sisi wananchi tuujue through matendo yake kwenye kazi yake mpya.
   
 10. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Ndo watanzania tulivyo kuona kila kitu in a negative way au kuto appreciate...kwahiyo mlitaka aseme kazi ya AG ni ngum ili muanze kumkosoa?
   
 11. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Inaonekana hili pia ilikuwa pia ni criteria?
   
 12. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #12
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mtani marwa unataka kusema kuwa aliye kutangulia mwanyika alikuwa anafanya kazi kwa kushindikizwa? au unawambia wa TZ kuwa mwanyika alikuwa hajui kazi yake?
   
 13. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #13
  Oct 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa mkwara mzee warema. Lakini isije ikawa nguvu za sakafuni............
   
 14. M

  Mchili JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Huyu dingi anaweza akafaa, tatizo ni siasa za TZ. Asishangae akigusa pengine kipenga kinalia au yellow card.

  Kila la kheri mh. Werema
   
 15. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kwa kweli tumezidi, yani woote tumeshaikubali hali hadi hatuoni opportunities za mabadiliko. kwa nini lakini,is true we cant change the situation? acheni kumkatisha tamaa wala kumpigia ramli, wacha afanye anavyoamini yeye. nijuavyo mimi wakurya huwa wana msimamo na hawapendi dharau, he can make it happen, just give the support guys.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Judge Werema, I know the guy one of my sister amekuwa assistant wake Sheria for a longtime, na I have spend a lot of quality time arround him nilipokuwa NY alikuwa mara kwa mara akija kwenye kuiwakilisha Serikali UN wakati wa GA, good man, strong, very serious, na siku zote straight on the line, na intelligent with a sound vision na ni kiongozi pia.

  - Hapa tatizo lake ni moja tu nalo ni kwamba serikali ya sasa na zote zilizowahi kupita, hazina a strong record on kuheshimu utawala wa sheria na thew worst of all nafasi yake haitokani na kuchaguliwa na wananchi, amechaguliwa na Rais ili aonyeshe royalty yake kwa Rais kwanza na sio sheria, ndio maana hiyo nafasi inaweza kushikwa na mtu yoyote yule sio lazima awe amesoma sheria.

  - Otherwise, ninamtakia hongera na kazi njema ni mfano biora sana wa kufanya kazi kwa bidii, hata kama wakubwa hawakuoni lakini Mungu anakuona na utalipwa tu tena hapa hapa, Werema deserves this promotion.

  Respect.

  FMEs!
   
Loading...