Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Tarehe 25 Oktoba tulipokea taarifa toka Geita ambapo jirani alituarifu juu ya usafirishaji haramu wa watoto unaofanywa na mama jirani yake. Kwamba mama huyo tayari mabinti zake Esta mwenye umri wa miaka 14, Naumi miaka 12 na Tere mwenye miaka 10 wako Dar es salaam kama wafanyakazi za nyumbani.
Tulimpigia Mwenyekiti wa Kijiji (VEO) ambaye aliahidi kwenda kuhakiki ukweli wa taarifa zile na kuzifanyia kazi. Baada ya siku moja Mwenyekiti wa Kijiji alitupigia kueleza kuwa taarifa zile ni za kweli na tayari mama mzazi wa watoto hao amekwisha wasiliana na waajiri wao kuwarudisha nyumbani hasa Naumi na Tere ambao sheria hairuhusu wao kuajiliwa.
Baada ya mwezi mmoja tulipata wasaa kumpigia mama huyo ambaye alikiri kuwarudisha watoto hao wawili shuleni na akatoa shukurani kwa kupewa elimu juu ya ajira kwa watoto
Ewe ndugu, jamaa, rafiki ama jirani, Usisite kutupigia namba 116 bila malipo unapoona au kuhisi watoto wanahitaji msaada mahali popote nchini. IT'S POSSIBLE|INAWEZEKANA!