Hyungnim
JF-Expert Member
- Sep 25, 2016
- 301
- 482
Hafijawa Matata alidamka asubuhi na mapema kwani usiku wote kwake ulikuwa kiza cha kuogofya!naaam kaka hafijawa hakupata hata lepe la usingizi.
Aliposikia milio ya jogoo kuashiria kuwa kiza kimefurushwa mbali na nuru,aliruka toka kwenye kitanda duni cha mianzi na kwa pupa akaanza kutatinga yake masulupwete.shati pana la mikono mifupi kuukuu lililopambizwa na picha za ndege tausi licha ya ukuukuu wake alilithamini na kulivaa vivyohivyo.Licha ya ukuukuu wake lakini pindi alipolitia maji,kipande cha sabuni ya mshindi na kulifikichafikicha lilimfanya aonekane kijana bora.Suruali yake njiwa rangi ya njano na kiatu cheusi kilichoisha upande vilitosha kumfanya aonekane mtanashati na hivyo kupapatikiwa na warembo wa kijijini Vugwa!.Kina sayona binti mateyo,husna binti milanzi,Mona mahewa,na Chelina binti kiuno.yeye kila alipotembea alinesanesa kwa madaha,akizungusha rasilimali makalio taratibu lakini kwa mbwembwe ya aina yake.
Chelina hakuwa binti wa mchezomchezo.Aliishia darasa la 7 tu lakini alikuwa mjuvi wa mengi hasa mambo ta mahaba.Shule iliyohusisha daftari,kalamu na kukariri hesabu za magazijuto ilimkana!akaikana,lakini akawa na kipaji ajabu kilichowaliza madume wakware,wakatamani kumnasa lakini ukata wa kiuchumi ulioikumba jamhuri ya Pandeo miaka ya themanini uliwakosesha utamu.Chelina hakuwa na choyo bwana,lakini kama walivopata kunena wahenga mkono mtupu si tu haubarikiwi wala hauendi kinywani bali pia haulambwi.chelina hakuwa mkulima wa uwele, kunde,korosho wala mhogo.Hivyo alihitaji mwanaume mkarimu asiye mbanizi ndio sababu kina shomari na musa walilalama chelina hana utu!hana upendo kama misingi ya siasa ya ujamaa ilivosisitiza Bali chelina wa watu aliishi ktk tanuru la ubepari,nalo likamlazimisha agengeneze fwaida ooh faida kupitia rasilimali kiuno!Akalazimika kuwa mbanizi kwa waliozificha senti zao kibindoni na akawatunuku pendo na huduma maridhawa ya mahaba kwa wanaume wakarimu waliokenua meno pindi chelina alipogusa kipochi cha akiba ya fedha kibindoni ilopatikana kwa mauzo ya nafaka.ujamaa uliokumbatiwa na shomari ukamnyima bashasha la chelina na vinono vingine.
Licha ya ujanja na maisha yake hayo chelina alimpenda sana Hafijawa.Alimtunuku Zawadi murua ya penzi isiyohitaji malipo.Hivyo aliezua vizuizi vya kiuchumi kwa hafijawa.Ikawa ubepari huria.
Wakati hayo yakijiri serikali ya vugwa ikikuwa ikijiandaa Ku.......
Itaendelea
(Hyungnim).