Hapo kabla mliishi nchi ambayo haikuwa ikiwabana, ukaja uchaguzi mkuu mkashindwa kufanya uchaguzi sahihi, mkakaa mkisubiri maisha mazuri bila kufanya kazi sasa imeshindikana. Mnaishi ugenini, yaani zama mpya, huku mkisahau kwamba nyie ndio mlifanya uchaguzi. Na sasa hamuwezi kurudi nyuma kwa kuwa mliyataka wenyewe. Mnaota na mnataka kupiga kelele dhidi ya utawala wakati ni zao lenu, kaeni kimya mtashughulikiwa. Mwenye masikio na asikie.
Pangu Pakavu