Simulizi Za 116: Ulawiti katika kituo cha kulelea watoto

Simulizi Za 116: Ulawiti katika kituo cha kulelea watoto

Sema Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2016
Posts
251
Reaction score
466
Jirani msamaria mwema alipiga simu namba 116 Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto baada ya kushuhudia tendo la ulawiti katika kituo cha kulelea watoto kilichopo jirani na makazi yake. Aliendelea kusimulia kuwa, mwanaume mtu mzima aliekadiriwa kuwa na umri wa miaka takriban 40 ama zaidi ambaye kimsingi ni mlezi wa watoto katika kituo hicho alimlawiti mtoto wa miaka 13 kituoni hapo. Kitendo hicho cha kidhalimu kiliteka hisia za jirani huyo na kushindwa kuvumilia na ndipo alipoamua kupiga simu namba 116 kupata msaada.

Tulipokea taarifa hizo na kuzifikisha kwa Afisa Ustawi wa Jamii Temeke ambaye mara moja alianza uchunguzi wa kina juu ya swala hili akishirikiana na Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi. Uchunguzi ulibaini kuwa matukio ya kulawiti watoto kituoni hapo yamekithiri na hivyo jalada lilifunguliwa kumshitaki mtuhumiwa.

Mpaka sasa, afya ya mtoto imeimarika vyema ingawa kwa bahati mbaya, mhusika wa tukio hilo alitoroka na hivyo hajafikishawa mahakamani. Hata hivyo, polisi wanaendelea kufanya jitahada kubwa kila iitwapo leo ili waweze kumtia nguvuni mtuhumiwa. Aidha, kituo cha huduma ya simu kwa mtoto kinaendelea kusuburi taarifa za mara kwa mara juu ya muendelezo wa kesi hiyo kutoka kwa Afisa-Ustawi pamoja na Dawati la Jinsia la Polisi kwa madhumuni ya kupatikana kwa haki za watoto wa kituo hicho.

Tusikae kimya tukijua matukio kama haya yanaendelea mitaani na vitongojini mwetu. Wasiliana nasi kupitia nambari 116 bila malipo tuzungumze.
 
Sio mawe tu hata kunyonga hadharani sielew dunia inakoelekea vitendo vimekua vingi vya kutisha sana watoto wanaharibiwa na mijitu mizima sijui watoto wetu tutawaweka wapi Mungu atunusuru na haya majanga maana ukilisikia kwa mwenzio utaona la kawaida ila ni mambo yakutisha sana jaman
 
Shingo idondoshwe tu, ili yule mwenye kujifanya anajua kusimamisha Saaaanaaaa, akiona tu jongoo anaywea akikumbuka kitu kitakachofuata...
 
mimi nikiwaona wabakaji walawiti watoto majambazi na wezi mahakamani wamevunjwa taya wakiwa hawawez kuongea nafurahi sana askari kwenye interrogation huwa wanawafinya vilivyo afu na kuwandikisha maelezo yasiyo ya kweli ili wakafungwe... unaacha malaya wamejazana mtaani uko unalawiti mtoto dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee wakati naanza kusoma nilidhani kwamba imetokea huko Ulaya " kumbe ni hapa hapa .....

Yaani hilo lijamaa likikamatwa na lenyewe lilawitiwe kwanza ", ili liweze kuyatambua maumivu ya kuingizwa ukuni yalivyo ...period

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee wakati naanza kusoma nilidhani kwamba imetokea huko Ulaya " kumbe ni hapa hapa .....

Yaani hilo lijamaa likikamatwa na lenyewe lilawitiwe kwanza ", ili liweze kuyatambua maumivu ya kuingizwa ukuni yalivyo ...period

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao watakao mfanya mwenzao na wao watatafuta pakupumulia baadae.

Hiyo Sio Tiba.
 
Back
Top Bottom