Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Mnamo tarehe 6 Agosti 2018 tulipokeaa simu toka Mpwapwa, kuhusu binti wa miaka 16 aitwaye Dora (sio jina halisi) aliyekatishwa masomo ili aolewe.
Mama na kaka yake walikuwa tayari wamempatia mume kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na haki za watoto. Kitendo hiki kilimsukuma msamaria mwema kutupigia simu bila malipo kupitia nambari 116 kutueleza madhila hayo.
Mara moja tulimtafuta Afisa Ustawi wa Jamii Mpwapwa ili afanyie uchunguzi suala hilo ili kusudi Dora aweze kupatiwa msaada. Afisa huyo alifika mpaka nyumbani alipokua akiishi binti huyo na kugundua kuwa taarifa ile ilikua ya kweli.
Kwa kushirikisha na Serikali za mitaa pamoja na Jeshi la Polisi, Mama na kaka yake Dora walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi na kuwafungulia mashtaka ya kukiuka Sheria na haki za watoto kwa kumlazimisha Dora aolewe huku wakimkatisha masomo yake.
Kwa wastani, wasichana wawili kati ya watano hutarajiwa kuolewa kabla ya kutimiza miaka 18 hapa Tanzania, (TDHS 2012). Kuwa na uwezo wa kusema uolewe wakati gani na nani akuoe ni haki ya msingi kwa kila binti. Tusikae kimya tukijua mipango hii inaendelea mtaani na vitongojini mwetu.
Wasiliana nasi kupitia nambari 116 bila malipo ili tuzungumze.