Simulizi ya Kweli: Jinsi Nilivyoacha Uzinifu

Simulizi ya Kweli: Jinsi Nilivyoacha Uzinifu

Sunbae

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2015
Posts
254
Reaction score
176
Safari yangu ya maisha na mapenzi na uhusiano ilianza mwaka 2008 baada ya kufika chuo na hii ilisababishwa na ukweli kwamba sikuona haja ya kujihusisha na mapenzi kabla sijafika level hiyo. Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2008 nilipata mpenzi ambaye tulikuwa tunasoma nae hapo chuoni.

Mwaka 2009 nilishiriki tendo la ngono kwa mara ya kwanza na sababu iliyopelekea kufanya hivyo ni kwasababu marafiki waliniambia nilikuwa na mwanamke mzuri sana hivyo kama nisipofanya nae mapenzi itakuwa rahisi yeye kuniacha.

Baada ya tendo nilitopea katika mapenzi na msichana wangu, maisha ya mapenzi yalikuwa mazuri kwa kiasi fulani na mabaya kwa kiasi chake. Tulikuwa na furaha na mara nyingi tulikula chakula maeneo ya Posta Mpya ( Kuna ule Mghawa upo Kituo cha Mafuta) na wakati mwingine tulikuwa Chef Uhindini kwasababu nilifanikiwa kupata kazi nikiwa mwaka wa pili.

Kwa kiasi fulani ilikuwa ni changamoto kuwa na mrembo yule kwasababu vishawishi vya wanaume vilikuwa ni vingi sana na kuna wakati nilihisi sipo peke yangu. Lakini hadi kufikia mwisho wa masomo yetu tulikuwa pamoja na lengo hasa lilikuwa kuja kuishi pamoja, familia ya binti ya karibu ilifahamu nia yetu isipokuwa baba wa binti tu.

Kipindi hiki kulikuwa na binti wa kitanga akinisumbua tangu mwaka 2011 akihitaji mahusiano nami, lakini kwa penzi nililokuwa nalo kwa mrembo wangu sikumsikiliza abadani.

Sekeseke la lilianza Novemba mwaka 2012 mwaka mmoja baada ya kumaliza chuo wakati huo mimi naendelea na kazi yangu na binti alipata kazi ya kujishikiza katika moja ya makampuni ya Umma. Baada ya ugomvi na confrontation binti aliomba tupeane muda wa miezi 6 kila mmoja ajitafakari kuhusu mahusiano yetu.

Nilikubali kwa shingo upande na nakumbuka siku ile nazungumza nae akiniambia kuhusu jambo hili nilikuwa nimeshika wallet natoka dukani, nusu saa baadae sikuwa na wallet mfukoni na sikujua niliangusha wapi. Baada ya taarifa hiyo akilini mwangu nilitambua kwamba sasa niko mwenyewe na ilibidi kuishi hivyo.

Nilianza maisha ya upweke mwaka 2013 kwa hali ya uchungu na majuto wa hali ya juu, kaka yangu alifahamu mapenzi niliyokuwa nayo kwa binti yule na alinisihi nisije kufanya maamuzi ya kurudiana nae maana lile sekeseke lililotokea Novemba 2012 alilifahamu “ Ole wako nikuone unarudiana na Z” kauli hii aliitoa kaka yangu.

Itaendelea......
 
Aiseeeee pole sana ila ushauri wa kaka yako ufuate kwani maji yakishamwagika hayazoleki na matapishi........ kwa hiyo si jambo la busara kumrudia hasa ukiwa hujui alivyoishi toka muachane 2012 ametembea na akina nani yawezekana marafiki zako wamo kwani kuna msemo unasema ukisusa twala
 
Haa nikajua legend kumbe mjukuu, Sema bado kabisa hujaanza wala hujaingia kwenye mapenzi,
 
Inaendelea;


Baada ya hapo niliamua kuwa na yule binti aliyekuwa akinifuatilia kwa muda mrefu ambaye kwa wakati huo alikuwa amehamia Dar kutoka mkoani. Niliendelea na binti huyu mpya lakini nilikuwa nachepuka na wasichana wengine tofauti tofauti kwa wakati fulani na frequeny ilikuwa kubwa. Siku moja niliamka nikajiandaa kwa ajili ya kwenda kazini, usiku wa kuamkia siku hiyo nilifanya mapenzi na mtanga wangu. Nilitoka nikakamata njia ambayo ingenipeleka hadi kituoni kupanda Daladala. Nilitembea umbali wa takribani mita 50 tu alikuja Kunguru (ndege) akanikwangua kichwani na kuondoka. Jambo hili lilinishtua kidogo lakini nikajitoa wasiwasi kuwa huyu Kunguru atakuwa alikosea tu njia.


Maisha yakaendelea na kabla ya mwezi huo kuisha nikatembea tena ( Nikafanya mapenzi), kesho yake nikajiandaa kama kawaida ili niende nikatumike nipate mkate wa kila siku lakini kuna jambo lilinishangaza mno na kuniogopesha, at the very same location, very same style kunguru alikuja tena akanikwangua kichwani. Nilipata mashaka kuhusu suala hili lakini lilinipa nafasi ya kujifakari upya, nilikuja kugundua kwamba niliyokuwa nayafanya hayakuwa sahihi na hii pengine ilikuwa ni namna ya kukumbushwa kwamba nafanya jambo baya hivyo nilikata shauri la kuacha kuzini.


...................................................................Mwisho................................................................................
 
Aiseeeee pole sana ila ushauri wa kaka yako ufuate kwani maji yakishamwagika hayazoleki na matapishi........ kwa hiyo si jambo la busara kumrudia hasa ukiwa hujui alivyoishi toka muachane 2012 ametembea na akina nani yawezekana marafiki zako wamo kwani kuna msemo unasema ukisusa twala
Nilifuata ushauri wa kaka.
 
Back
Top Bottom