Tien corrector
Member
- Dec 11, 2020
- 60
- 157
Wandugu, Salam ziwafikie popote mlipo.
Miaka iliyopita, tulizaliwa Mimi na pacha wangu(Kurwa na Dotto) na kukufanya familia yetu iwe maarufu Sana maana enzi hizo kupata watoto mapacha ilionekana ni bahati ya Hali ya juu Sana.
Enzi hizo Mimi ni mpole Sana lakini pacha wangu (Dotto) alikuwa Hana hata punje ya upole. Ukorofi yeye, ugomvi yeye, yaani kila kitu alikuwa amenizidi ingawa na Mimi nilimzidi kidogo akili.
Sijui Kuna mechanism gani ..?Mana mapacha utakuta Dotto ana mwili mkubwa na Afya ya maana lakini Kurwa anakuwa simple tu. ndivyo ilivyokuwa hata kwa pacha wangu alikuwa na mwili as if amekula hamira imemvimbisha.
Professional ya baba. Civil Engineer na Professional ya mama lawyer.(kwa bahati mbaya wote ni marehemu)
Enzi za uhai wao wakati sisi ni wadogo ndio tunaanza shule za vidudu BABA alitaka tusome tuwe ENGINEERS na MAMA alitaka tusome tuwe LAWYERS
Tulikuwa tunaambiwa hayo hata hatujui nini wanamaaisha maana bado tulikuwa na akili za kutokujitambua. Basi kutapelekwa shule kwa Mara ya kwanza tumefika huko Mara tunaambiwa nyoosha mkono shika sikio.
Tukaanza na Mimi shika sikio halishikiki, akaja Dotto shika sikio akaweza kulishika, ghafla nikasikia "Engineer" hapa Dotto ataanza shule lakini Kurwa ataanza mwakani arefuke kidogo.
Nilivyokuwa na kimuemue Cha kuanza kusoma nikihisi homa ghafla. Ashukuriwe MUNGU Mzee baba akajiongeza akatoa note za mia mbili 2 na kumwambia mwl.hawa hawajawahi kutengana waandikishe wote. kweli Mambo yakatiki.
Tukaanza kusoma lakini Kuna Jambo ambalo lilikuwa linatokea mpk Leo sijapata jibu sahihi..Dotto alikuwa ni mtundu Sana japo walimjua yuko hivyo lakini adhabu Kama kawaida zilimfikia lakini Cha ajabu ilikuwa akichapwa yeye maumivu nilikuwa napata hata Mimi
(watalaam hapa naomba ufafanuzi tafadhali.....)
Miaka ikasogea tulivyofika kidato Cha pili wiki ya mitihani siku ya jumanne ambayo kesho yake ilikuwa siku ya kumalizia mitihani ya taifa ya form two kwenda form three.
(Ndio siku za wazazi wetu ku-Rest in peace zilifika wakapata ajari mbaya Sana ya Gari iliyopelekea wote wapoteze maisha yao)
Aisee kufiwa wazazi wako kwa mkupuo inauma sana usiombe kusimuliwa. Mbaya zaidi mkuu wa shule alikuwa katiri Sana Sijui alikuwa na moyo wa chuma yule mwl, alitulazimisha tufanye mitihani wa form two wakati tumefiwa na wazazi wote.
Tulifanya mtihani huku roho zinauma Sana unaandika kwenye pepa machozi yanadondoka... aisee sitosahau. Basi matokeo yakatoka tulifeli kabsa enzi hizo kulikuwa na mchujo mkali Sana.
Ikabidi turudie kidato Tena, nguzo la familia zime-rest in peace. Maisha yetu ghafla yakaanza kuwa magumu as if sio watoto wa watumishi.
Hakuna ndugu mwaminifu mbele ya pesa hata ndugu waliopewa kusimamia mirathi ya wazazi wakatuzunguka na kuona wamepata mzinga wa Asali ( MUNGU anawaona aisee)
Ghafla tulivyofika form 3 mwezi wa 5. Tukahamishwa shule na kupelekwa government school kwa kisingizio kuwa private school Ada ni kubwa. Sincerely waliendelea kutudidimiza kisaikolojia ndipo niliamini kuwa kweli...
uchungu wa mwana anaujua mzazi.
Basi maisha yakaendelea Sasa tulipo ingia form four nikamuuliza pacha wangu(Dotto)
"Unasoma ili uwe nani? Alinijibu, kaka Mimi sitofaulu mtihani wa mwisho form four" vipi wewe unasoma uje kuwa nani? Kwa jibu alilonipa liliniumiza Sana mpk namie nikashindwa kumjibu vizuri.
Kweli wakati uliwadia tukafanya mitihani tukawa tunasubiri matokeo. Enzi zetu matokeo yalikuwa yanachelewa Sana kutoka. Nikamwita Tena Dotto tunafanyaje kipindi hiki tunasubiri matokeo. Akanijibu Sina Wazo lolote kaka.
Ghafla nikapata Wazo la kwenda kuomba kufanya kazi ya ulinzi mahali Fulani, nikaenda kukutana na bosi wa hapo akaniambia hatuajiri wanafunzi, niliumia Sana.(japo sikuwa na sifa yeyote sikupita mgambo Wala nini, ujasiri tu ulinipeleka)
Nikarudi nyumbani kila nikifikiria maisha tuliyokuwa tunaishi enzi wazazi wetu wapo machozi yakawa yananilenga. Nikakaa sebuleni mbele yangu kulikuwa na TV kubwa Wazo likanijia uza hiyo TV.
Nikamuita Dotto na kumwambia Mdogo wangu nataka tuuze hii TV tupate pesa uende veta ukasome hata shot course wakati tunaendelea kusubiri matokeo.
Dotto alikataa kabsa anasema kaka unatafuta laana za wazazi Mali za wazazi haziuzwi hata waliotudhurumu mirathi ya wazazi wameshalaaniwa.
Maneno ya Dotto yaliniumiza Sana binafsi niliogopa Sana.
Kuangalia upande wa ndugu kwanza ndio wameuza maeneo yote ya mzee hata Nyumba wanatamani kuuza.walikuwa ni zaidi ya viumbe wakatili Sana mpaka ikafika hatua Dotto alipanic na kusema nyie sio wazazi Wala sio ndugu zangu, bila Shaka alifika mbali Sana lakini maumivu ndio yaliyokuwa yanaongea pale.
Baada ya siku tatu nikakaa sebuleni naandalia TV Wazo likanijia Tena uza hiyo TV. Nikashindwa kujizuia moyo wangu ukajawa na amani kupita kiasi, faster bila hata kumwambia Dotto nikaenda kwa ofisi ya fundi Tv na kumwambia. Ashukuriwe MUNGU yule fundi akanielewa.
Basi pesa iliyopatikana nikaenda veta kumuombea Dotto nafasi ya kusoma short course, bila hiana nafasi nilipata nikarudi nyumbani na kumjulisha Dotto Mimi nimeuza TV ili usome short course veta Kama ni laana za wazazi haziwezi kutufikia maana tunafanya vitu vizuri hatujui vitatusaidia vipi maisha ya mbeleni .
Basi akanielewa na kwenda kuanza masomo yake pale chuoni. Siku zikasonga matokeo yakatoka ikawa Kama alivyosema matokeo yake hayakuwa mazuri kabsa japo na Mimi hayakuwa mazuri lakini yalinipa nafasi ya kwenda mbele.
Nikifikiria nasomaje nguvu zinaisha na kukosa matumaini kosa kubwa mbele yangu naona kabati kubwa la vyombo na kabati kubwa la nguo. Nikawaza moyoni hivi ndivyo vitanisogeza mbele.
Dotto akasoma na kumaliza akarudi nyumbani maisha magumu ni hakuna mfano. Nikamshauri aende tanesco kuomba kazi ya kujitolea Basi akafanya Kama nilivyomshauri
Alifanya kazi kwa hasira Sana mithili ya mtu aliyeajiriwa kwa mshahara mkubwa kumbe anajitolea tu hakuna anacholipwa.
Kulitokea fursa za ajira pale tanesco ile kuomba tu kikwazo kikaibuka walitaka Cheti Cha form four, mwenzangu na Mimi hana. Na nyakati hizo kupata ajira ilikuwa ni kwa kujuana Sana plus rushwa. Kitendo Cha kukosa sifa kilimvunja Dotto Hali ya kuendelea kujitolea.
Akaamua kuacha, sikuchoka nikamshauri Tena usife moyo endelea kupata uzoefu utakuja kukusaidia baadaye alishindwa kunielewa kabsa akaondoka kwa hasira mbele yangu.
Kesho yake, nikamshauri Tena aendelee kuenda kujitolea bila kuchoka. Wakati huo huo Mimi nasoma kwa Shida Sana nilipata sehemu kaka mmoja alikuwa anauza chips na nyama nilimuomba niwe namsaidia kazi kila jioni alikuwa ananipa kiasi Fulani.
Basi Dotto akanielewa akaanza kwenda kazini kwa kujitolea. Kazi mtiti mtiti ngumu kinoma anarudi amechoka mbaya. Siku zikasonga akazoea kazi Mara akaanza kulipwa ya maji maisha yakaendelea.
Na Mimi yule kaka wa chips akawa ananipa nagawa pesa Moja kwenye kibubu nyingine tunanunua mikate Ile ya ngano inayopikwa kienyeji tunakula na kunywa maji maisha yanasonga.
Basi siku Moja baada ya muda kwenda nikaamua kufungua kibubu changu
shikamoooo kibubu .......mliopitia masuala ya vibubu mnaelewa Sana hapo ni pagumu Sana yahitaji usiwe na tamaa maana unaweza kuvunja siku ambayo hata hukupanga kukivunja.
Baada ya kuvunja nikaona Kuna pesa kiasi. Nikamwita Dotto mwenzangu una kiasi gani ulichotunza. Masikini Hana hata Mia pamoja na pesa ya maji aliyokuwa anapewa, nikakumbuka Kuna binti mmoja yupo karibu naye ikakuwa Mdogo wangu ameshakuwa in love.
Kweli ujana maji ya Moto mawazo yangu yakawa sahihi ikawa hivyo kweli. Nikamkalisha na kumsema, Dotto maisha yetu ni magumu Sana Mdogo wangu bila kutumia akili haya maisha tutateseka sana, fikiria huyo binti amepata ujauzito tutaishije pia Kuna magonjwa "stop" hiyo tabia.
Alinijibu sawa nimekuelewa lakini hakumaanisha. Basi kile kiasi nilichokikuta kwenye kibubu nikaenda kumlipia Ada veta ili aendelee na level nyingine. Maisha yakaendelea full changamoto mpaka unatamani dunia isimame ushuke lakin wapiiii.
Akamaliza level zote kwa kozi aliyochukua kurudi kazini shavu Hilo akapata kazi pale pale kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi na kujituma sana mshahara mzuri tu na form four yake failure maisha yakasonga.
Huku Mimi niliyejiona Nina akili Sana nimeenda nimefika mahali graduate na nasubiri ajira tu, Mara paa ajira hiyo porini vijijini ndani kweli hakuna mtandao kabsa simu iligeuka calculator.
ushirikina mwanzo mwisho, sijakaa sawa Matatizo ya macho, mara umelala usiku unachapwa fimbo anayekuchapa humuoni. (Vikao vikafanywa wenye hizo tabia waache ni Kama waliwachochea walizidi Mara 3)
Nikarudi nyumbani kitaa kuanza upya nikamkumbuka yule kaka wa chips na nyama alikuwa anaingiza pesa Sana. Pia kabla siacha kumsaidia mtaani wakaanza kunisifia bwana misosi unapika vizuri vyepeee.(True mpaka leo nimekuwa mpishi mzuri Sana Ila sijasomea)
Nikakutana na yule kaka na kuomba mwongozo. MUNGU ambariki Sana huyo alikuwa anaitwa "peter David Zambi" bila choyo akaniambia tips zote.
Faster nikampigia cm pacha wangu, tukaongea hakuamini nilipomwambia niameacha kazi,
lakini nilimaanisha ndipo nikawaza kufungua ofisi yangu ya kuchoma chps japo ilikuwa ngumu sana na watu walisema Sana lakini sikujali Wala kuogopa. nikatafuta mahali na kufungua kiofisi.
MUNGU si athumani kupitia hiyo kazi nimefanya mengi ambayo hata kupitia Ile ajira nisingeweza kufanya. Ila bado napambana mpaka kieleweke
USHAURI WANGU KWA GRADUATE
1. Tusichague kazi kwa kisingizio Cha elimu zetu.mimi nasema cheti ni makalatasi tu uwezo wa mtu huthihirishwa kwa matendo na matokeo chanya katika kila suala alifanyalo.
2. Kujitolea ni njia rahisi kwako kwa kupata ajira ya kudumu kikubwa uwe na juhudi. pia unapata experience ambayo ndio hutazamwa Sana kwenye ajira mahali popote.
3. Changamkieni kozi zinazotolewa na vyuo vya veta na SIDO Kuna kozi zinafanya vizuri Sani sokoni na hazipatikaniki vyuo vikuu.
4. Hakuna ndugu mwaminifu kwenye Mali/pesa tuwe makini Sana na ndugu wengi wao sio ndugu Bali ni donda ndugu.
5. Unaweza kuzaliwa kwenye familia ya kitajiri lakini ukaishi maisha ya kimasikini Sana. Pia kuzaliwa kwenye familia maskini sio dhambi, dhambi kufa ukiwa masikini. Hakuna mafaniko rahisi tupambane bila kuchoka no matter tunapitia yepi na mangapi
6. MAOMBI, IMANI NA UJASIRI
vizingatie katika maisha yako.
7.Wazazi tuache kuwachagulia watoto fani za kusomea, Tuwachunguze na kuwasikiliza wao wanasema nini. Unakuta mtoto anasema Mimi nataka kuwa fundi magari, lakini wazazi wanamwambia soma uje kuwa doctor.
Huo ni ukatili wa kimaamuzi sio sawa.
Nawatakia Usiku mwema.