Simulizi ya Kifaransa: Ubora "THE HIGHEST GOOD"

Simulizi ya Kifaransa: Ubora "THE HIGHEST GOOD"

THE HIGHEST GOOD

BY EUPHORIA

CHAPTER 14: Chui wa milia


"Kiongozi wa dhehebu la mfupa wa chuma nadhani unanichukulia kama fala mwenzio sio?" aliongea na kunyanyua mkono wa kulia kisha kugusanisha kidole gumba na cha shahada kisha ku-snap na kutoa sauti


Kwenye moja ya pango la himaya hiyo ulisikika mburuzo na sauti ya mtu kulalama maumivu na palepale kwenye lango la pango alionekana mtu mwenye sura mbovu kama nyanya iliyooza


Alikuwa ameshika mguu wa mtu huku akimburuza bila huruma, mtu aliyekuwa akiburuzwa alikuwa kijana mdogo mwenye umri wa miaka kumi na sita aliyefungwa kamba mwilini asifurukute


"Kiongozi...kiongozi... nisaidie, niokoe jamani!" alikuwa akilia sana kiasi cha kutia huruma


Yule kijana alitupwa karibu na mkuu wa himaya hiyo kisha yule mkuu alisimama na kumuinua kichwa kwa kushika nywele zake


"Kiongozi Shohei nitamuua mwanafunzi wako mmoja halafu tuone kama utaendelea kuleta kiburi" aliongea


"Tafadhali usiniue, nipo tayari kuwa mmoja wa wafuasi wako, nipo tayari kuwa mtumwa wako, tafadhali usiniue!" alilia akiomba kuonewa huruma


"Huyu kijana bila shaka woga umemzidia, ona mpaka ana jikojolea na kuinajisi madhabahu ya mkuu wetu" aliongea mmoja wa wahalifu waliomzunguka shohei


Shohei aliishia kujiambia ni mwanafunzi wa aina gani amemsajili? Hana uaminifu kabisa, hata kama ni muoga ndio kulisaliti dhehebu na kutaka kuwa miongoni mwa maadui? Hata hivyo alielewa alikuwa bado kijana mdogo mwenye ndoto nyingi za kutaka kutimiza ndio maana hakutaka kufa mapema


"Kiongozi Shohei, kwa mwanafunzi muoga kama huyu na msaliti sidhani kama utahoji nikimuua?" aliongea na palepale bila kupoteza muda alizungusha shingo ya kijana yule, na kupoteza maisha papohapo


Shohei moyo ulimdunda paah! akiwa na uso usioelezeka, na palepale mlio wa ding! ulisikika akilini mwake kisha kosei kwa njia ya kifikra alimtaarifu


"Umepoteza mwanafunzi mmoja na kwasababu hiyo umepatiwa misheni ya dharula, waue wote walioko hapo asibaki hai hata mmoja, ili roho ya mwanafunzi huyo ipate amani huko iliko"


"Hehehe! Inaonekana huyu mwanaharamu amekasirika" aliongea kibaraka yule aliyehusika kumburuza kijana aliyesimama karibu na jukwaa alipo mkuu wake mara baada ya kumuona Shohei yupo kimya kana kwamba alikuwa kwenye maombolezo ya kimya kimya


"Unapaswa kushukuru we mwanaharamu, mkuu wetu amekusaidia kushugulika na mwanafunzi wako msaliti" aliendelea kuongea na ile anamaliza sentensi yake tu alishtukia kutobolewa kifuani upande wa moyo kiasi cha upanga kutokelezea mbele


Na nyuma yake alionekana Shohei ambaye alitimiza azma hiyo, haikueleweka upanga ameutoa saa ngapi


"Kibaraka wako alikuwa anapiga domo hovyo, hakuwa na adabu hivyo na imani pia hutonioji kwa kukusaidia kumshughulikia sio?" aliongea Shohei


"Umethubutu kumuua ndugu yangu? Unapaswa kulipia kwa uhai wako!" alimaka mmoja wa wahalifu kwa hasira na kumsogelea Shohei kwa spidi akilenga kumpiga ngumi ya utosi akidhamiria kupasua kichwa chake kwa nguvu za nishati ya mbingu na ardhi


Hata hivyo Shohei alionekana kuwa makini mno kwani alikwepa ngumi ile na kwa wakati huohuo akichannel nguvu za nishati kwenda mguuni mwake na kumsindilia teke lililomrudisha nyuma mita kadhaa, licha ya kuvaa joho, kurusha teke haikuwa tabu kutokana joho kuwa pana


"Acheni kupigana!" ilisikika sauti ya mamlaka na msisimko wa nguvu kusambaa eneo llote kiasi kwamba Shohei alihisi ubaridi kwenye uti wake wa mgongo


“Hakika ustadi wako wa sanaa za mapigano ni wa kipekee sana, nakubali kwa kumuua kibaraka wangu na mimi huwa sipendi kukuza jambo dogo kuwa kubwa. Umebakiwa na wanafunzi arobaini na sita walio mikononi mwangu


Kabidhi shekeli elfu arobaini na sita kwa wote kisha kila mmoja ashike njia yake” aliongea mkuu yule


Shohei alijiambia inaonekana huyu mkuu ana shida sana na pesa, kwani alikuwa tayari kupoteza kibaraka wake kwa ajili ya pesa Hata hivyo haikumshangaza sana


"Nimeshasema na narudia tena kusema, Shekeli moja kama ada ya malezi hakuna maridhiano"


"We mshenzi..!" alikunja ndita huku akijizuia hasira


"Mkuu niachie mimi hii kazi, nitamuua kisha tunamsachi tu nguo zake na kama tukikosa bila shaka ndani ya dhehebu lake kutakuwa na za kutosha" aliongea yule mtu aliyedhamiria kumpasua kichwa mwanzo


"kuwa makini, inaonekana huyu kijana ana kasi kubwa" mkuu yule alimruhusu


"Usiwaze sana mkuu wangu hawezi kunizidi kasi" alimjibu mkuu wake


"Usimuonyeshee huruma, mpatie kifo chenye maumivu kulipiza kisasi kwa wenzetu waliotangulizwa kwa mkono wake!" aliongea mmoja wa wahalifu akionekana kuwa chawa na asiye na mafunzo ya kinishati


"Mvunje mifupa huyo ya kila mwili aone ya maumivu!" aliongea chawa mwingine


Upande wa Shohei hakujisumbua hata kuwasikiliza zaidi ya kutulia tuli akitazamana na yule mtu, alijiambia kwa muonekano wake wa kibaunsa bila shaka atakuwa ni aina ya wale wanaotumia uzito wa miili kushambulia hivyo kudili naye ni suala la kufumba na kufumbua tu


Lile baunsa alikuwa akitumia mafunzo ya nishati, alikaa mkao wa kuwa tayari kwa pambano kisha alichannel nishati za mbingu na ardhi katika mishipa yake kuongeza kasi ya msukumo wa damu na kwa uwepesi wa hali ya juu kama unyoya wa kuku alimsogelea Shohei akimtandika ngumi ya kifua iliyomrusha mita kadhaa na kujibamiza mgongo kwenye moja ya nguzo za mbao eneo hilo na kuanguka chini


"Sh*t anaspidi kali" aliongea huku akitema damu mdomoni kisha kwa msaada wa upanga alioushika alijinyanyua na kusimama wima


Alionekana kumchukulia poa sana mshindani wake na palepale alikumbuka sheria ya kwanza kwenye pambano aliyowahi kujifunza kwa njia ngumu.


Kwamba usimdharau adui yako hata kama anaonekana mdhaifu mbele yako, kwani hata chui wa milia awindapo hadharau kitoweo chake hata kama ni sungura mdogo


Alijiambia anapaswa kuwa kama Chui wa milia na palepale alikaa mkao wa utayari wa kupambana awamu hio akiwa na sura ya kazi kwelikweli kuliko mwanzo


Kufumba na kufumbua Shohei kwa spidi ya hali ya juu baada ya kuamsha nguvu zake za nishati alimsogelea


"Shwaah! Shwiih! Swiiih! Shwuush!" ilikuwa ni milio ya upanga kukata hewa, kwani mshindani wake alionekana kuwa na spidi kubwa kumzidi bado hivyo alikwepa mashambulizi ya Shohei bila tabu


"Una spidi ndogo sana, ngoja nikuonyeshe maana halisi ya kuwa na spidi kali" aliongea mtu yule na palepale alianza kumzunguka Shohei kws kasi ya ajabu na kuonekana kana kwamba anazungukwa na kimbunga


"Inaonekana ameimarika karltika mbinu ya hatua saba za kimbunga kuliko mwanzo" aliongea mkuu wa himaya akiangalia pambano kwa namna ya kuridhika


"Ni kweli hata mimi pia kwa spidi yake ya sasa inanipa wakati mgumu kidogo kuendana naye" alimuunga mkono mmoja wa kibaraka wake aliyesimama nyuma yake upande wa kushoto


"Haijalishi huyo kiongozi ana utaalamu gani ila mbele ya spidi kubwa ni bure tu!" aliendelea


Upande wa Shohei aliyekuwa akizungukwa kwa spidi aliishia tu kutabasamu na kuushika upanga ule wa maafa imara kisha kwa spidi alifanya shambulizi kama anajaribu kuchoma upepo


Na palepale kichwa cha yule nmtu kilitenganishwa na shingo yake huku damu nyingi zikiruka kwa kasi kama bomba lililofunguliwa maji


"Spidi yako ni kubwa sana kiasi kwamba unashindwa hata kuicontrol, kwani hujui kukata kona? Kulikuwa na ulazima wa kulivamia psnga langu? ona sasa ulivyokufa kizembe!" aliongea bila hatia yoyote


Ukweli alichofanya ni kuegesha tu upanga usawa wa shingo kwenye mzunguko wa yule mtu na kutokana na kazi asingeweza kuepuka kulivamia panga lake, ni kama alikuwa akiwaonyeshea udhaifu wa hiyo mbinu yao


Yule mtu aliyepoteza uhai alikuwa ni miongoni mwa wale watu nane waliosimama nyuma ya mkuu wao, hivyo idadi kupungua na kubaki saba


Hivyo baada ya kuona mwenzao ameuawa kirahisi hivyo walikasirika na kumuona Shohei kuwa tishio na wote kwa pamoja waliamua kumshambulia wakimzunguka pande zote


Shohei alionekana kushtukia hilo mapema na palepale alisafirisha nguvu za nishati kwenda miguuni mwake na kuruka juu urefu wa kama mita thelathini na ushee na wakati akiwa hewani aliachia mashambulizi ya mawimbi yenye makali kama upanga hivyo hawakuwa na jinsi zaidi ya kujikinga na mashambulizi hayo na kurudi nyuma


"Kwahiyo mmeona mnishambulie kwa pamoja baada ya kuona kila mmoja haniwezi?, inaonekana sina jinsi zaidi ya kutumia ile mvinu" aliongea Shohei baada ya kutua ardhini


Kisha palepale baada ya kuchezesha mkono hewani ilitokea karatasi nyeupe yenye michoro na maneno ya ajabu, ilikuwa ni ile talasimu ya ufunguzi wa muhuri kwa upanga huo wa maafa


Na bila kupoteza muda aliipigisha ile talasimu kwenye upanga wake na ile talasimu kugeuka moshi na moshi ule kuuvamia upanga huo


Kilikuwa ni kitendo cha sekunde tano kwa kutoa talasimu kwenye mfumo na kuigusanisha na upaga ule, kisha sekunde tatu zingine upanga ule ulianza kutoa mwanga mkali kiasi cha kufunika eneo lote wasipate kuona vizuri


"Inaonekana alikuwa amebeba siraha ya kimiujiza" alijiwazia mkuu wa himaya hiyo huku akikinga macho yake kwa mkono kutokana na mwanga kuwa mkali


Sekunde ambayo mwanga ule mkali unapotea mkuu huyo alishtukia ncha ya upanga ule kuwa karibu na uso wake


Kilichomshangaza ni umbali uliopo kati Shohei na yeye, umbali wa mita arobaini, kilichomvchangaza zaidi ni msisimko uliokuwa ukitoa, na ule ni msisimko ulimfanya kutetemeka bila kupenda, kupumua nako kulikuwa ni kwa tabu sana kutokana na mkandamizo wa hewa


Hisia alizokuwa akizipata ni kana kwamba upanga huo una uhai ndani yake, na upanga kuwa ni kiumbe cha kutisha


Mara aligundua kitu kingine tena kilichozidi kumuogopesha zaidi, ni kuwa watu wake wote walikuwa wamekufa miili yao ikiwa chini imetenganishwa kwa kukatwa viuno. Damu nyingi zilikuwa zimetapakaa ardhini


"Kwahiyo hii ndio nguvu iliyojificha ya huu upaga wa maafa? Lakini urefu wa mita arobaini ni mrefu kishenzi" alijiongelesha, ilioneka upanga ule uliongezeka urefu na makali






**********
 
THE HIGHEST GOOD

BY EUPHORIA (SAMUEL JK)

CHAPTER 15: Pumzika kwa amani


Shohei alionekana kushangazwa na upanga huo kwa jinsi ulivyorefuka.
Hata hivyo urefu ule ulimrahisishia mambo, kutokana na mwanga kuwa mkali alichukua faida hiyo kuwashambulia wale wahalifu waliomzunguka wote Kwa kufyeka tu mara chache, upanga ulikuwa na makali mno


Mkuu wa himaya hiyo alimeza mate kwa tabu sana huku jasho likimtoka kwenye paji la uso, ni kana kwamba amekutana uso kwa uso na bwana shetani aliyekuja kumchukua waende kuzimu


"Kiongozi Shohei, tunaweza kuliongea hili kiungwana, haukuwa na haja ya kwenda mbali hivi" aliongea mkuu wa himaya hiyo ambaye muda huo hakuwa mkuu tena, kutokana na presha kubwa ya upanga wa maafa alishindwa hata kusimama kwenye kiti chake, ni kama kuna nguvu ya maajabu ilikuwa ikimkandamiza


"Oh wataka kuzungumza kiungwana? Basi sawa, nina swalila kuuliza kwanza." aliongea


"Nina shauku kwanini ukalenga dhehebu langu na wanafunzi wangu?" alimuuliza


"Ni kwasababu..nime.... ni..." aliongea kwa kusitasita


"Unataka kuongea kiungwana ama hutaki?" alimuuliza akimuangalia na sura isiyotaka utani akimwekea upanga shingoni


"Ni dhehebu la maji ya chemchem! Walinilipa na kunitaka kuwateka wanafunzi wako na kuwatesa! Kisha kuwatumia wanafunzi kukuleta hapa na kukuua" alimjibu kwa sauti akihofia kukatwa shingo


"Ooh kumbe iko hivyo, basi maongezi ya kiungwana kati yangu mimi na wewe yanaishia hapa"


"Tafadhali usiniue, nionyeshee rehema!"


"Rehema? nimekuwa mungu mpaka nikuonyeshee rehema? Kwa udhalimu mliofanya sasa na hapo kabla unadhani unastahili huruma? Vipi roho zisizo na hatia za watu mliowaua na kuwadhulumu, je uliwaonyeshea huruma? Unadhani watakubali uonyeshewe huruma?" alimuuliza lakini mkuu yule aliendelea kuomba kuhurumiwa hata kupiga magoti, japo kwa tabu kutokana na mkandamizo


"Leo acha niwe shujaa kuwasaidia watu wa mji huu kusafisha takataka kama nyinyi na kuwalipia kisasi wale waliokufa kwa mikono yenu." aliendelea kuongea


"Tafadhali ni...."


"Leo nitakuwa shujaa ambaye atakusindikiza kuzimu, kwaheri ya kuonana kamanda!" alimkatisha na palepale kufyeka kichwa chake


Mara baada ya kitendo kile upanga wa maafa ulirudi katika hali yake ya kawaida ni kama ulikuwa na uelewa wake binafsi kwamba kazi imeisha, mara ghafla Shohei akaanza kuhisi uchovu na nguvu zikimuishia papohapo na kuanguka chini mzobemzobe kama furushi ingawa hakuzimia ila hakuwa na nguvu hata ya kunyanyua kidole


"Kosei nini kinaendelea? Kwanini niko hivi?" aliuliza kifikira maana kufungua mdomo tu ilikuwa ni tabu


"Ni kwasababu upanga wa maafa unanyonya nguvu za nishagi na kiroho kwa mtumiaji endapo akafungua muhuri" alimjibu


"Lakini mbona sikuhisi nguvu kunyonywa? Iweje tu baada ya kumaliza kuutimia ndio nione madhara?


"Hivi unajua kwa nini unaitwa upanga wa maafa? Si tu kwamba unaleta maafa kwa maadui bali kwa mtumiaji pia, ukiwa unautumia hutoweza kuhisi nguvu zako zikinyonywa mpaka pale utakaponyonywa nguvu zote ndipo madhara yataonekana, na endapo ikanyonya nguvu zako zote na bado adui yuko hai nadhani unajua nini kitatokea si ndio?"


"Asee mbona hukuniambia mapema, nilikuwa nikibisha hodi mlango wa kifo ni bahati tu nimewaua wote kwasababu walikusanyika pamoja vinginevyo ingekuwa ni habari nyingine"


"Sababu hukuuliza eniwei umekamilisha misheni yako kwa kuwaua wahalifu wote wa mlima mweusi, umepatsa thamani hamsini za mchango wa dhehebu" alimtaarifu


"Pia utabaki katika hiyo hali kwa nusu saa mpaka kurudiwa na nguvu zako, na muda huo hutoweza kufanya chochote endapo adui atatokezea mbele yako, hivyo hata kama ni katoto ka miaka mitatu kukuua ni dakika sifuri tu" aliendelea


"Tutumaini kwamba hakuna kitakachotokea kwa muda huo" aliongea Shohei kisha kutulia kimya


Baada ya zaidi ya nusu saa Shohei alionekana kufukia kaburi eneo fulani la bonde kwenye himaya hiyo, alikuwa amemzika mwanafunzi wake aliyeuliwa kwa kuvunjwa shingo


Mara baada ya kumaliza kufukia kaburi hilo alisimama pale na kulitazama kaburi hilo kwa muda


"Nitawaambia nini wazazi wake mmh?" aliongea Shohei kwa huzuni


"Kuna muda kwenye maisha kuna mambo lazima yatokee na inatupasakukubali matokeo hata kama ni ngumu kukubali isitoshe ulikuja kwa nia ya kuwaokoa mikononi mwa maadui ingawa kwake imeshindikana, huwezi kuokoa kila mtu ulimwenguni, wewe ni binadamu sio mungu!


Kwenye ulimwengu wa Ardhi ya nyota kifo ni kitu kinachotokea kila siku, kifo ni sehemu.... "


"Kosei sijakwambia unifariji na maneno, nimeulisa nitawaambia nini wazazi wake?" alimkatisha na kumuuliza lakini hakujibiwa ilionekana hata yeye kosei hakujua na cha kusema


Shohei alivuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha kuongea kwa sauti hafifu


"Pumzika kwa amani kijana, ingawa sijabahatika kulifahamu jina lako, mimi kama kiongozi ni wajibu wangu kuwalinda wanafunzi wangu lakini nimeshindwa kutimiza wajibu huu kwako, naomba unisamehe kwa hilo, nisamehe sana" aliongea huku akianza kububujikwa na machozi


"Ulijiunga na dhehebu langu ukiwa na ndoto.... Ulifika ukiwa na matumaini ya kuwa mwenye nguvu, ingawa sijui kusudi la wewe kutaka kuwa mwenye nguvu ila nina hakika miongoni mwa sababu ni kutaka kuilinda familia yako na wale uwapendao, na kuandika hatima yako mwenyewe katika ulimwengu huu, lakini kuna washenzi wamekatiza ndoto zako


Sijui nitawaambia nini wazazi wako, lakini sitakuwa na budi kuwaambia


Nitawaambia kijana wao alikuwa jasiri, jasiri vya kutosha kuweza kuondoka nyumbani akiiacha familia yake kwa lengo la kuwa mwenye nguvu na kuwalinda hapo baadae


Jasiri vya kutosha kuweza kustahimili mateso ya adui, Jasiri vya kutosha kuingia katika dhehebu langu na hata kama alikufa siku yake ya kwanza… alikufa akiwa mwanafunzi wa dhehebu langu na nitamkumbuka ndani ya moyo wangu" aliongea kwa hisia sana kisha kufuta machozi na kuondoka eneo hilo


*********


Upande wa dhehebu la mfupa wa chuma alionekana Yeri Su ameketi kwenye ngazi fupi karibu na mlango wa kuingilia dhehebu hilo, alionekana kuwa na wasiwasi sana kiasi cha kutotulia


Pembeni yake alionekana yaoyao amesimama akiegemea ukutani akikunja mikono yake


"Tutafanye kama ikitokea kiongozi wetu ameuawa?" aliongea kwa wasiwasi Yeri Su


"Ni rahisi tu, nitakuwa kiongozi wa dhehebu kisha wewe utakuwa mwanafunzi wa kwanza wa dhehebu" alijibu Yaoyao kiwepesi sana


"Angalau unapaswa kuonyesha wasiwasi hata kidogo, mbona una roho ngumu hivyo?" aliongea Yeri Su akijiambia ikitokea nikifa ataomboleza kwaajili yangu kweli huyu?


"Usiwe na wasiwasi, japokuwa ni mzembe na asiye na aibu ila si mjinga kivile, bila shaka kuna njia ya kulifanikisha anaijua" aliongea Yaoyao na mara macho yake yalichanua baada ya kumuona mtu umbali wa mita kadhaa akija uelekeo wao


Naam Emiichi Shohei, kiongozi wao, alionekana kutembea kwa mwendo wa taratibu, akiwa amevalia kibegi cha kale upande wa mkono mmoja


"Kiongozi, umefanikiwa kulitatua? Hivi unajua ni hatari kiasi gani wewe kwenda peke yako? Tunatakiwa..."


"Yeri Su" Shohei alimkatisha kwa kumuita kisha kuendelea "Kuna wanafunzi wenzako zaidi ya arobaini walioko nyuma wakitembea kwa tabu, kusanya wanafunzi ksdhaa waliowasili mkawasaidie"


Aliongea kisha kumpita kuingia ndani ya dhehebu lakini alisita baada ya kukumbuka kitu


"Oh si umesema maboresho hayajakamilika bado?" aliongea huku akivua kibegi na kumkabidhi kisha kuelekea zake ndani


Yeri Su kutokatana na uzito wa begi ilimbidi aangalie kuna nini humo. Macho yalimtoka mara baada ya kugundua ni majiwe ya madini, dhahabu na almasi


"Kiongozi, himaya ya mlima mwe...."


"Himaya ya mlima mweusi imefutika katika uso wa ulimwengu huu" alimjibu bila kugeuka akielekea zake ndani


******


Siku kadhaa mbele walionekana watu wawili wakiwa katika eneo la himaya ya mlima mweusi ambayo ilikuwa haitaminiki hata kidogo kwa kubomolewa


"Bwana wangu, baada ya kuchunguza inaonekana majeraha ya hawa wahalifu yamesababishwa na silaha moja na mtu mmoja kuhusika" aliongea mmoja aliyeonekana kupiga goti kwa heshima


"Mtu mmoja ty? Inaonekana kwenye mji huu tuna mtu mwenye nguvu" aliongea mtu aliyetambulika kama bwana wangu akitabasamu


********


Upande wa dhehebu la mfupa wa chuma alionekana Shohei amesimama kwenye uwanja mkubwa wa mafunzo, mbele yake kukiwa na wanafunzi tisini na tisa wakimtazama


"Najua mnanifahamu kwa jina langu Emiichi Shohei na ni kiongozi wa dhehebu hili" aliongea kwa sauti ya kusikika vyema na wote


"Lakini bado mna mnajiuliza mimi ni nani na ni mtu wa aina gani si ndio?" aliendelea


"Mimi ni nani? Mimi ni mimi, niliyesimama mbele yenu. Ni mtu niliyekufa hapo kabla na kufufuka. Mimi ni kama enzi iliyovikwa mwili, Master wa mbinu zisizokuwa na idadi. Mtawala wa njia yangu mwenyewe.


Wanafunzi wangu wanapaswa kunifuata kwa uaminifu kwa sababu kwa uwepo wangu, hofu inageuka kuwa ujasiri, shaka hugeuka imani, na udhaifu unapata kusudi la kuwa imara.


Mimi si mtakatifu wala dhalimu. Mimi ni Kiongozi wa ddhehebu aliyeokoa baadhi ya mliosimama maisha yenu, mimi ni kiongozi sio kwa sababu nilirithi cheo, bali kwa sababu mbingu yenyewe ilinichagua


Kwangu mimi dhehebu hili ni kama himaya iliyojificha, hivyo kando na kuwa kiongozi wa dhehebu mimi ni kama mfalme wenu Na ninyi wanafunzi wangu ni kama upanga nyuma ya kivuli changu, Na chini ya amri yangu, mtapata kutambulika na kuheshhimika, mtapata kuwa wataalamu miongoni mwa wataalamu na hata mkifa mtapata kukumbukwa katika historia


Sina haja ya taji, kwa maana mbingu yenyewe ni dari yangu. Sihitaji kiti cha enzi, kwa maana ardhi yenyewe ulimwenguni kote ipo chini ya miguu na hatua zangu


Mimi ni yule atakayechonga majina yenu na jina la dhehebu hili katika bara zima la Ardhi ya nyota" alitoa hotuba ndefu kidogo akijitambulisha kwa kirefu


Wanafunzi walimsikiliza kiongozi wao kwa makini na walipatwa na motisha kwa hotuba hiyo fupi iliyowatia ujasiri ingawa hawakumuelewa alichomaanisha mtu aliyekufa hapo kabla ila hawakufikiria sana





**********
 
THE HIGHEST GOOD

BY EUPHORIA (SAMUEL JK)

CHAPTER 15: Pumzika kwa amani


Shohei alionekana kushangazwa na upanga huo kwa jinsi ulivyorefuka.
Hata hivyo urefu ule ulimrahisishia mambo, kutokana na mwanga kuwa mkali alichukua faida hiyo kuwashambulia wale wahalifu waliomzunguka wote Kwa kufyeka tu mara chache, upanga ulikuwa na makali mno


Mkuu wa himaya hiyo alimeza mate kwa tabu sana huku jasho likimtoka kwenye paji la uso, ni kana kwamba amekutana uso kwa uso na bwana shetani aliyekuja kumchukua waende kuzimu


"Kiongozi Shohei, tunaweza kuliongea hili kiungwana, haukuwa na haja ya kwenda mbali hivi" aliongea mkuu wa himaya hiyo ambaye muda huo hakuwa mkuu tena, kutokana na presha kubwa ya upanga wa maafa alishindwa hata kusimama kwenye kiti chake, ni kama kuna nguvu ya maajabu ilikuwa ikimkanda Mwamba huyu hapa asante kwa chai
 
THE HIGHEST GOOD

BY EUPHORIA (SAMUEL JK)

CHAPTER 16: Andiko takatifu la mabadiliko


JANA YAKE


Shohei kabla ya siku hiyo ambayo alikuwa mbele ya wanafunzi wake uwanjani alikuwa akifanya mipango na harakati za kuanza kuliongoza dhehebu la mfupa wa chuma


"Kosei, kwakuwa wanafunzi tayari na dhehebu limekamilika sasa ni muda wa kupata muongozo wa mbinu za uvunaji nishati wa mbingu na ardhi, shida ni kwamba mbinu ni nyingi kiasi kwamba sijui hata ipi ina ubora kuliko zingine" aliongea huku akiangalia skrini ya mfumo wa hologram iliyoko mbele ya macho yake


"Usiumize kichwa kwa kitu kidogo kama hicho, mimi nitakushauri utumie mbinu hii, ni nzuri kwa wanaoanza mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi hasa katika hatua ya ufunguzi" aliongea kosei akimuonyeshea mbinu yenyewe kupitia mfumo


"Andiko takatifu la mabadiliko?" Shohei alisema


"Ndio inaitwa andiko takatifu la mabadiliko, ni muongozo wa uvunaji nishati ambao huimarisha mifupa ya mwili pamoja na meridian"


"Ni nzuri kwa wanafunzi wako katika hatua ya ufunguzi wa meridian na wale ambao hawajaanza kuvuna bado"


"Lakini mbona wataka kunitapeli kwa thamani hamsini za mchango? Nipunguzie gharama basi!"


"Kwa ubora wa mbinu hiyo sidhani napaswa kupunguza gharama, utaelewa baada ya kuitumia" alimjibu


"Okay, kuna suala jingine muhimu pia, ni kuhusu sare za wanafunzi wa dhehebu"


"Ni kweli hilo nalo ni la muhimu, vipi una design yoyote na rangi ya sare? Unachopaswa ni kunipa maelekezo tu ya hizo sare!"


"Hata mavazi pia ni bidhaa ulizonazo? nilidhani ni mbinu na siraha tu"


"Hivi Kosei wewe ni nani? Na yule kiumbe aliyenipa nafasi ya kuishi ni nani haswa?" aliuliza, akiweka sura yenye shauku


"Kwasasa huna kibali cha kunijua mimi wala yule aliyekupa nafasi ya kuishi tena" aliongea kosei


"Kibali? Kwanini unanificha? Kuna haja ya vibali?"


"Kijana nishasema huna kibali hivyo tafadhali elewa, usinipe wakati mgumu subiri mpaka utakapopata kibali ila jua tu ya kwamba yule aliyekupa nafasi ya kuishi tena ni mkuu sana" aliongea kosei


"Kama hutaki kunijibu potezea, kupewa nafasi ya kuishi tena ni jambo lenye thamani kubwa hivyo sitahoji sana ilimradi nafsi yangu inaniambia nyinyi si wabaya" aliongea kisha kubadili mada


"Unaweza nielezea zaidi uspesho wa hiyo mbinu?"


"Mbinu ya andiko takatifu la mabadiliko ni kwaajili ya dhehebu lako pekee, ni wewe kiongozi wa dhehebu na wanafunzi wako mnaweza kuvuna, ikitokea mwanafunzi awaye yote akalisaliti Dhehebu au kutaka kuvujisha taarifa kuhusu mbinu hiyo kwa maadui au ikatokea akafukuzwa kwenye dhehebu atapoteza kumbukumbu zote kuhusu mbinu hiyo" alielezea


"Duuh! ni ulinzi mkali wa mbinu ulioje! Kwa stahili hiyo sitohofia siri za dhehebu kuvujishwa" aliongea Shohei



PRESENT DAY


Shohei alikuwa amesimama uwanjani akitazamana na wanafunzi wake, chini ardhini kukiwa na vitabu vilivyofanana jumla ya idadi vikiwa tisini na tisa


"Nimebuni mbinu ya uvunaji nishati itakayowawezesha kuvuna nishati kwa urahisi" aliongea huku akichukua kitabu kimoja


"Amebuni mbinu ya uvunaji nishati? Au nimesikia vibaya?" Yeri Su alijiuliza


"Yaoyao tafadhali njoo uchukue vitabu uvikabidhi kwa wanafunzi wenzako" Shohei alimwambia, kisha binti huyo bila ubishi alianza kugawa vitabu kwa wanafunzi wote


Mara baada ya kukabidhiwa vitabu walivifunua na kuanza kusoma, yalikuwa ni maelezo rahisi na mepesi kuyafuata


"Haina haja ya mimi kujisumbua kuwaelekeza kwakuwa kils kitu kipo kitabuni, japo inaonekana maelezo ni rahisi ila si rahisi kama mnavyofikiri, hivyo ni juhudi zenu ndizo zitakazowavusha katika hatua za juu" aliongea Shohei


Kwenye vitabu vile kulikuwa na michoro mbalimbali ya mikao tofauti tofauti na maelezo ya kutosha


"Kiongozi, hii mbinu itatusaidia kweli? Mimi naona ni staili mbalimbali tu za kukaa kwa muda maalum" aliuliza mmoja wa wanafunzi


"Ooh ndivyo unavyodhani? hiyo ni mbinu inayoimarisha miili yenu na meridian ili iwe rahisi kwa kuvuna nishati, kuhusu itakusaidia au lah ni juhudi zako, sitaki maswali mengine" alimjibu


"Vipi kama mbinu uliyobuni kama haitokuwa na manudaa yoyote, je naweza kuitelekeza?" aliuliza Yaoyao


Shohei alimsogelea binti huyo mpaka karibu kabisa, uso wake ukiwa inchi kadhaa na uso wa binti huyo kisha kutabasamu na kumuangalia machoni


"Yaoyao, labda kama una mbinu yako binafsi unayotumia kuvuna nishati na unahisi ni bora kuliko yangu, jibu ni ndio" alimwambia kwa sauti ndogo kamaya kunong'ona


Kutokana na binti huyo kukutanisha macho na mwanaume huyo kwa sekunde kadhaa palepale uso wake ulibadilika na kuwa mwekundu kwa kuhisi aibu na alikwepesha macho yake na mwanaume huyo


"Nitajaribu" aliongea na kuondoka eneo hilo kwa kukimbia mbio za kike isieleweke anaenda wapi


Shohei aliishia kutabasamu tu na kujiambia kumbe binti anaona aibu licha ya kuwa kauzu?


"Haya nataka muanze mafunzo, nina mambo ya kushughulikia, pia Yeri Su usisahau kuniletea vipimo kwaajili ya sare" aliongea akiondoka eneo hilo


Muda mchache mbele Shohei alionekana akiwa ndani ya chumba chake akiwa amekaa mkao fulani hivi isieleweke ni mkao wa aina gani, ni kama alikuwa akifanya yoga


"Kosei, nimekuwa nikihangaika na hiyo mbinu yako kwa masaa zaidi ya tatu lakini mbona sihisi mabadiliko yoyote?"


"Shohei, hata kama mbinu ya andiko la mabadiliko ni rahisi kuelewa itakuwa ngumu kwako kupiga hatua kuliko wengine kwasababu ya kutokuwa na kipaji cha uvunaji nishati"


"Si unamaanisha kwamba bila wewe mimi si kitu?"


"Aah.. Nadhani upo sahihi kijana"


"Hata kama ni ukweli huoni maneno yako yanaumiza? Yananivunja moyo mno!" aliongea Shohei akiwa na sura ya kama amekosewa


"Hata kama itanichukua mwaka, lazima nifanye bidii na kupiga hatua, sitaki kuamini kwamba siwezi kupanda levo bil6 wewe" aliendelea kuongea huku akiongeza bidii na kuendelea kufanyia mazoezi andiko lile


BAADA YA SIKU MBILI


Siku mbili zikapita na Shohei alikuwa akifanya mazoezi kwa siku mbili mfululizo akijifungia ndani kwake





"Haha kosei, futa yale maneno yako ya kwamba sina kipaji, baada ya siku mbili nimeweza kufanikisha mzunguko wa kinishati wa ndani ya mwili" aliongea kwa furaha


Shohei aliweza kuhisi nishati nyepesi yenye joto ikikusanyika taratibu katika kitovu chake cha ndani, eneo lililojulikana kama kitovu cha nishati. Kutoka hapo nishati hiyo ilianza kusonga polepole kama mkondo mdogo wa maji ukipita katika kila meridian mwilini mwake


Kadri mzunguko huo ulivyoendelea, Shohei alihisi mwili wake ukizidi kuwa mwepesi, akili yake ikipata utulivu, na hata uchovu wa siku mbili za majaribio ulitoweka, alijihisi mpya


Mzunguko wa ndani wa kinishati "Qi circulation" au kwa lugha nyingine nishati ya uhai, ni nishati isiyoonekana iliyopo ndani ya mwili wa binadamu na pia katika mazingira ya asili.


Ni kuzungusha nishati ya ndani, ndani ya mwili kwa njia iliyodhibitiwa. Ni mzunguko endelevu usiosimama ni kama mfano wa damu kusafiri kwenye mishipa ya damu au umeme kusafiri kwenye waya n.k


Sasa Shohei alikuwa amefanikisha hili na alikuwa akifurahi sana, basi akiwa katika ya furaha Yeri Susn aliingia ndani humo naye akiwa na furaha pia


"Kiongozi, inaonekana mbinu yako ni ya kitaalamu mno! Ndani ya siku mbili pekee nimeweza kufanikisha mzunguko wa nishati ya ndani, nadhani hivi karibuni nitapanda levo na kuingia hatua ya kumi na moja ya ufunguzi"


Shohei ambaye alikuwa akidhani ana kipaji kikubwa kuliko wengine ghafla alifuta mawazo yale na kujiambia kwa staili hii itabidi aongeze bidii maradufu vinginevyo ni suala la muda mwanafunzi wake kumuacha mbali kwenye kuvuna nishati


Upande mwingine ndani ya chumba alionekana binti Yaoyao akiwa ameketi mkao wa tahajudi, mwili wake ulionekana kufuka moshi kama mvuke wa barafu


Alifumbua macho yake huku akijiwazia akilini mwake "Ni kama alivyosema, ni rahisi kuelewa lakini si rahisi kwenye kutenda"


"Bila shaka mbinu hii ni yenye ufanisi wa hali ya juu, ni ngumu kuamini mtu aliye katika hatua ya ufunguzi kutengeneza mbinu hii, pengine huenda dhehebu hili lina historia ndefu ya kale


Nimeweza kufanikisha mzunguko wa ndani wa kinishati na unaendana vyema na mbinu yangu ya uvunaji element ya barafu


Nikiongeza bidii na kuyafanyia mazoezi pamoja, ni suala la muda tu kuweza kulipiza kisasi changu, inaonekana nimemdharau sana kiongozi wa dhehebu hili" aliwaza


*********


SIKU ISHRINI BAADAYE





Kukiwa asubuhi eneo la bweni la wanafunzi wa kiume wa dhehebu la mfupa wa chuma, ndani ya chumba kimoja wapo alionekana kijana akiwa katika mkao wa tahajudi akipumua kwa mapafu


Ghafla alifumbua macho yake na kuanza kupayuka kwa sauti


"haha nimefanikiwa kufikia hatua ya kwanza ya ufunguzi!" aliongea na ile anamaliza sentensi yake alishtkua mto ukimpiga usoni


"Unatupigia makelele asubuhi asubuhi, kwanza kuna haja gani ya kujivunia ikiwa wewe ndiye mtu wa levo ya chini kwenye bweni?" aliongea mwanafunzi aliyempiga na mto, ilionekana walikuwa wakishea chumba


"Haya nipe mto wangu, nataka nilale" aliendelea kuongea lakini kijana aliisjia kumuangalia na sura iliyokuwa ikisema "F*ck off!"


Upande wa nje wa bweni hilo alionekana Shohei akipalilia bustani nyuma yake alisimama Yeri Su


"Siku kumi tangu tuanze kufuata muongozo wa andiko la mabadiliko ni wanafunzi tisa walioweza kufikia hatua ya tatu ya ufunguzi, tano katika hatua ya nne ya ufunguzi na mmoja katika hatua ya tano ya ufunguzi


Siku ya ishiriki wanafunzi wote tumeweza kupanda levo hatua moja, hakika inafurahisha sana kwa wanafunzi kupiga hatua kwa siku chache" aliongea Yeri Su kwa furaha kubwa huku akionyesha kuikubali mbinu ya kiongozi wake


Kwenye ulimwengu wa uvunaji nishati ni ngumu mno kupiga hatua kwa siku chache kama, labda asili imekupendelea vinginevyo utasota mno hata kwa miaka kuweza kupiga hatua


Alijiambia kama ni kweli kiongozi huyo ndiye aliyebuni kama alivyosema basi anastahili heshima yake.


"Yeri Su siku za mbeleni litakuwa ni jambo la kawaida kwa wanafunzi kupanda levo haraka, na kama mwanafunzi wa pili na kiranja itakupasa uwasimamie vizuri"


"Sawa kiongozi, nimekuelewa nitahakikisha kuwaongoza ipasavyo" aliongea








**********
 
THE HIGHEST GOOD

BY EUPHORIA (SAMUEL JK)

CHAPTER 17: Zensu Zuji


"Bwana mdogo!" waliita tena watu wake huku wakimkimbilia, hawakuthubutu kumshambulia Kiongozi aliyempiga boss wao isitoshe hawakuwa na nguvu zozote za kinishati wala uwezo wa kupigana, kifupi walikuwa ni kama vijakazi tu


"Tuondoke! Tutarudi kulipiza kisasi" aliongea kwa jazba yule kijana na wale watu wake walimbeba boss wao na kuondoka mahali hapo


Mara baada ya kuondoka mahali hapo Shohei alimegeukia Yeri Su na sura yenye kutaka kububujikwa na machozi


"Eti Yeri Su si naonekana kama kiongozi eeh? Kwanini wanashindwa kunielewa? wanadharau vijana kuwa viongozi, wamenivunja sana moyo" aliongea


"Kaza moyo kijana" ilisikika sauti ya Kosei kwenye fikra zake





"Unajua nini wewe? Nyamanza!" aliongea Shohei kifikra





*********


Muda mchache mbele ndani ya eneo la makutano ya dhehebu yaani eneo la kufanyia mkutano walionekana watu watatu, nao hawakuwa wengine zaidi ya Shohei, Yeri Su na Yaoyao


Sababu ya Yeri Su na Yaoyao kuwa wao pekee na si wanafunzi wengine ni kwa wao kuwa viranja wa dhehebu hilo, hivyo walikuwa na kibali cha kuwepo mahali hapo


Chini sakafuni alikuwa amelala yule kijana aliyekuwa akipigwa kwa kosa la wizi akilala kwenye godoro dogo la futon. Yeri Su mara baada ya kumfanyia uchunguzi alimgeukia kiongozi wake na kumwambia


"Kiongozi anaonekana kuvunjika mifupa nane ya mbavu na kuna ishara ya kuvuja damu kwa viungo vya ndani" aliongea


"Kwa sana anaweza kuvumilia kwa masaa manne kabla ya kupoteza uhai ila kwa hali yake hakuna daktari anayeweza kumtibu, isipokuwa...."


"Isipokuwa akitumia kidonge cha uponyaji atapona si ndio?" Shohei alimaliza sentensi yake


"Ndio, maana ndiyo njia pekee ya kuokoa maisha yake" alijibu


""Unadhani kidonge ni kama pipi? Kwamba utaweza kuwa nacho muda wowote utakakao?" aliongea Yaoyao akimlenga Yeri Su


"Ukweli kidonge cha uponyaji ninacho, ishu ni je nimuokoe maisha yake au nimuache afe?" Shohei aliwauliza


"Muokoe" Yeri Su alijibu


"Hapana, muache afe" alijibu Yaoyao


Shohei aliishia kujiambia, interesting.. mmoja malaika mwenye huruma huku mwingine akiwa ni israel mtoa roho asiye na huruma na uhai wa mtu


"Kuuokoa maisha ya watu ni maadili mema!" aliongea Yeri Su akimwambia Yaoyao


"Watu wengi wanakufa kila siku kwenye ardhi ya nyota, je utaweza kuwaokoa wote?" Yaoyao aliweka hoja mezani akimuuliza Yeri Su


Yeri Su aliishia kubaki kimya tu, alijua ni kweli hawezi kuokoa maisha ya watu wote ulimwenguni isitoshe yeye ni binadamu hakuna malaika wala mungu


"Yeri Su.... inaonekana wewe ni kijana mwenye moyo wa huruma, na kwa hilo nimekupenda lakini muda mwingine ukweli huwa ni mchungu sana, ulimwengu ni katili..." aliongea Shohei huku akisimama kutoka kwenye kiti alichoketi


"Kipindi nakusaidia kule msituni, sikudhani kama kitakuwa na nguvu na matokeo ya haraka, ila kwasababu nishajua nguvu halisi ya kidonge siwezi kugawa tu hovyo kwa watu nisiowajua" aliendelea kuongea akimkaribia Yeri Su aliyesimama pembeni ya mgonjwa


"Je unajutia kuniokoa?" Yeri Su aliuliza na kumfanya kiongozi kutabasamu


"Umejiunga na dhehebu langu la mfupa wa chuma na kuwa mwanafunzi wa pili kwasababu ya mimi kukuokoa, kama nisingekuokoa yangekuwa ni majuto makubwa kwangu" alimjibu


Yeri Su baada ya kusikia hivyo alibadili mtazamo wake palepale, mwanzoni alidhani kiongozi huyo alimsaidia kutokana na moyo wa huruma kumbe ilikuwa ni kwaajili ya faida, hata hivyo bado alikuwa na shukrani kwani licha ya dhamira kuwa ni kupata faida ni dhamira hiyo hiyo iliyookoa maisha yake


"Kidonge hiki chenye thamani kimeweza kuniletea mwanafunzi mwenye kipaji" aliongea huku palepale Kidonge cha kijani kikitokezea hewani kimaajabu na kutua kwenye kiganja cha Shohei, ilionekana alikwisha kinunua mda tu


Aliinama na kupiga magoti chini kisha akamnyanyua yule kijana akitaka kumlisha kile kidonge huku akisema


"Natumai kidonge hiki kwa mara nyingine tena kikaniletea mwanafunzi mwenye kipaji"


"Kwahiyo unamuokoa? Unadhani vijana wote ni wenye vipaji kama Yeri Su?" aliongea Yaoyao


"Pengine nitapata bahati" Shohei alimjibu binti huyo kisha kummezesha Kidonge kijana yule


Mara baada ya kumezeshwa kidonge hazikupita hata sekunde kumi kijana yule alianza kupitia mabadiliko ya mwili ya haraka na baada ya nusu dakika alishtuka huku akihema kwa nguvu


Kisha alianza kuwatazama waliokuwa mbele yake na mara baada ya macho yake kutua kwa Shohei aliita


"Mr Shohei?" alionekana kumjua kiongozi huyo


"Kijana, hivi unajua nimetumia Kidonge cha thamani sana ku...."


"Kiongozi Shohei, tafadhali naomba unichukue, nataka kuwa mwanafunzi wa dhehebu lako" aliongea yule kijana akimkatisha huku akinyanyuka na kupiga magoti kuomba


"Eeh... nilikuwa nataka nianze kuzunguka zunguka kukushawishi ila umeenda moja kwa moja kwenye point? Kwanza unaitwa nani kijana?" aliuliza Shohei


"Naitwa Zensu Zuji, mzaliwa kutoka familia ya Zuji kwenye mji wa mashariki" alijibu yule kijana


"Wewe ni Zensu zuji? Kiongozi Inaonekana bahati imekuangukia, inasemekana aliamsha nguvu za kiroho hatua ya mwangaza mkuu angali akiwa mdogo" aliongea Yeri Su akionekana kumfahamu na kumfanya Shohei atabssamu kana kwamba ameokota hazina kubwa


Kwa mujibu wa Yeri Su anasema kwamba Zensu Zuji ni mzaliwa wa kwanza wa kizazi hiko kutoka katika familia ya Zuji ambayo ni yenye nguvu na ushawishi ndani ya mji wa mashariki


Alifanikiwa kuamsha nguvu zake za kiroho mpaka hatua ya mwangaza mkuu, hata hivyo kwa namna fulani nguvu zake za kiroho zilishuka na kuzimika na kurudi katika hatua ya kivuli ya mwamko wa nguvu za kiroho na meridian zake kujifungua hali iliyopelekea kupoteza uwezo wake wa kinishati


Na kwasababu hiyo mchumba wake alivunja uhusiano wao na kumdhalilisha mbele ya wanafamilia wa ukoo wa Zuji


"Na kwasababu ya udhalilishaji walioupata walimfukuza katika ukoo ili kuepuka hadhi yao kushuka, kwa maelezo zaidi...." alimalizia maelezo lakini alikatwa na Shohei


"Yeri Su inaonekana umezaliwa kuwa mwanahabari, unaongea sana" aliongea Shohei huku lile tabasamu la kuokota hazina likiwa limeshapotea usoni mwake kitambo tu


Alijiambia kwahiyo nimeokota mzigo? Kama ni hivyo nitambadilisha kwa namna yoyote ile ilimradi atakuwa mwanafunzi wangu nitajua namna tu


"Kiongozi Shohei, je utanipokea kama mwanafunzi wa dhehebu lako?" aliuliza akiwa na sura yenye kutia huruma


"Bila shaka hapana" Shohei alimjibu kimtego


"Oh, nilitegemea hili, najua sistahili kuwa mwanafunzi wa dhehebu la mfupa wa chuma hivyo samahani kwa usumbufu nitaondoka" aliongea kwa huzuni na hali ya kukata tamaa kisha kunyanyuka na kuanza kupiga hatua kuondoka eneo hilo


"Zensu Zuji usiondoke, hata kama hutokuwa mwanafunzi wa dhehebu lakini kwa muongozo wa kiongozi wetu utaweza ku...." aliongea Yeri Su lakini aliishia njiani baada ya kukatishwa na Shohei kwa ishara


"Kama una huzuni nyingi kiasi na kukata tamaa kiasi cha kutamani kufa. Ukitoka nje ya lango la kuingilia chukua uelekeo wa kushoto, kuna maporomoko marefu unaweza jirusha hapo, pengine usipokufa utapata fursa" aliongea Shohei na kumfanya Zensu asimame bila kugeuka na kumjibu


"Tangia nipoteze uwezo wangu wa kinishati basi fursa nazo nilipoteza, hakuna fursa itakayojitokeza hata nifanye nini"


"Unakosea, Fursa hujitokeza kwa wale waliojindaa, hakuna mtu kwenye huu ulimwengu anazaliwa akiwa mwenye nguvu, ni juhudi zake pekee zitakazomfikisha huko anakotaka


Acha kukata tamaa kirahisi hivyo, sio kosa kukata tamaa ila pale utakapojaribu kwa uwezo wako wote, moyo wako wote na akili zako zote na bado ukashindwa kupata ukitacho basi ni sawa kwako kukata tamaa


Lakini je, umejaribu vya kutosha? Ni sawa umeweza kuvumilia mchumba wako kukuvunja moyo na kukudhalilisha, umeweza kuvumilia kukataliwa na familia yako.


Je, hutaki kusimama imara mbele ya mchumba wako kipofu? Je hutaki kusimama imara mbele ya wanafamilia waliokukataa na kuwaonyesha kwamba watu hubadilika" aliongea Shohei akiwa tayari amemkaribia kijana huyo akimshikka bega


Zensu uso wake ulikuwa ukibubujikwa na machozi, ilionekana amepitia mateso mengi mno na kuvumilia vya kutosha lakini maneno ya Shohei yalikuwa ni kama bomba lifungulialo maji kwani alishindwa kuvumilia na kulia kwelikweli kiasi cha kukaa chini hadi udenda ukimtoka


Shohei alisimama na kumuangalia kijana huyo kisha kuchuchumaa nakumpiga mgongo kwa kumsugua, alikuwa akimfariji kwa kiasi fulani


"Ukweli hakuna mtu kwenye ulimwengu huu anayeweza kujua kwa undani ni maumivu kiasi gani mwingine anahisi moyoni, haiwezekani.
Utaweza kuelewa kwa undani kile unachojisi wewe mwenyewe, nachoweza kukwambia nikwamba binadamu hulia pale wanapoumizwa, hivyo lia, toa sumu lakini hakikisha huwezi kulia kwa mambo yaleyale uliyotendewa" aliendelea kumfariji


Shohei ni kama alikuwa akiweka mafuta ya petroli kwenye moto kwani kijana huyo alizidisha kulia


Upande wa Yeri Su na Yaoyao walikuwa kimya na kwa namna fulani walimuhurumia kijana huyo


Basi baada ya Zensu kulia vya kutosha hatimae aliweza kunyamanza na kufuta machozi yake


"kama unataka kuondoka unaweza kuondoka, ukiamua baki ni chaguo lako" aliongea Shohei


"Hapana, nitabaki, nitajiunga na dhehebu la mfupa wa chuma, nataka kurudisha kile nilichopoteza" aliongea Zensu huku akipiga magoti kuonyesha shukrani


"Umeishi katika majonzi kwa muda mrefu mno, sasa ni wakati wa kurejesha utukufu wako uliopotea" aliongea Shohei na kumfanya Zensu kububujikwa na machozi ya furaha kwa kukubaliwa kujiunga na dhehebu hilo


Kisha Yeri Su alimchukua kwaajili ya usajili na mengineyo zaidi, isitoshe alikuwa kiranja upande wa wanaume, Yaoyao hakuwa na sababu ya kuendelea kubaki hapo hivyo naye aliondoka


Shohei alishusha pumzi na kuketi zake kwenye kiti huku akijiambia, kazi ya kulea vijana ni kubwa mno








*********

ITAENDELEA KESHO KUTWA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom