Iam back_Euphoria
JF-Expert Member
- Sep 17, 2024
- 356
- 1,071
Ndugu zangu habari za kuwapotea? Naam ni mimi Euphoria mwandishi wa Solo king, mniwie radhi kwa kupotea na kuwa kimya kwa muda mrefu zaidi, kipindi kile nilikuwa nikiumwa, nilikuwa nalala kitanani muda wote, na kuna mambo mengine yalitokea ukijumlisha na matukio ya oct 29, nisiongee sana maana nitaharibu
Ila nilipoteza access ya kuingia JF na kule fasihinet
Nimewaletea simulizi nyingine iitwayo UBORA "THE HIGHEST GOOD" kwa sababu simulizi ya awali nilipoteza research zake hivyo sidhani kama itaendelea hivyo muisamehe
Kuliko kukaa kimya na kuipotezea nimewaletea hii👇
THE HIGHEST GOOD
BY EUPHORIA
CHAPTER 1: Nafasi ya kuishi tena
Anga la bluu lilikuwa limetulia likipendezeshwa na nyota nyingi angani pamoja na mwezi umulikao usiku huo, hali ya hewa ilikuwa tulivu, upepo mwanana ukipuliza maeneo yote ya mji
Usiku huo wa saa nne alionekana mwanaume kijana akitembea hali ya kuwa katika mawazo, muda wote alikuwa akiangalia chini tu, alikuwa amevalia nguo shirt la mikono mirefu rangi damu ya mzee, suruali nyeusi ya kitambaa iliyopauka na viatu vyeusi vilivyoonekana kutumika kwa muda mrefu sana
Haikueleweka mtu huyo alikuwa akiwaza nini kichwani mwake nyakati hiyo ya usiku
Upande wa mbele yake umbali wa kama kilomita mbili kulionekana gari ambalo lilikuwa likija upande wake kwa kasi sana, na bila shaka ilionekana dereva wa gari hilo alikuwa amelewa chakari kutokana na uendeshaji wake wa gari
Mwanaume yule aliyekuwa katika mawazo alionekana kutosikia kabisa wala kuona kutokana na kuzama katika kina cha mawazo na kwa bahati mbaya aligongwa na gari lile na kurushwa na kuanguka na alidhurika vibaya sana, damu nyingi zikimtoka na kumwagikia ardhini
Dereva wa gari kutokana na kuogopa kwa kosa alilolifanya hakusimama wala! bali aliendelea kuendesha gari kuondoka eneo hilo haraka kukimbia dhambi aliyoifanya usiku huo, kibaya zaidi eneo hilo hakukuwa na watu.
Mwanaume yule alikuwa ametulia tuli akiugulia maumivu ardhini kichwa kikiangalia angani na mara muda huohuo mvua ikaanza kunyesha ilikuwa ni mvua ya kawaida sio kubwa sana wala ndogo sana.
"Je huu ndio mwisho wangu? Hivi ndivyo ilivyopangwa nife? Huu ndio mwisho wangu? Mmh?" aliongea akilini mwake mwanaume huyo bila kujua maswali hayo yanamlenga nani au labda pengine alikuwa akijiuliza mwenyewe?
Maskini kijana wa watu alikufa kiholela sana, pengine asingekuwa katika hali ile ya mawazo angeweza kusalimika lakini uzembe siku zote ni uzembe tu, na uzembe huo wa kutokuwa makini ulimgharimu maisha yake na haikuwezekana kurudisha muda nyuma kurekebisha uzembe wake sababu muda siku zote haurudi nyuma kamwe bali unasonga mbele.
Ni jambo la kuhuzunisha sana kwa mtu kufa lakini huo ndio uhalisia wenyewe kwamba kifo ni lazima. Kibaya zaidi kijana huyo alikuwa ndio kwanza amepata ajira baada ya juhudi nyingi na kusota kote kwa lengo la kuishi maisha bora. Lakini unajua nini? Ulimwengu siku zote ni katili sana.
"Sina demu, sina mtoto ndoto yangu ya kuwa baba ndio inakufa hivihivi? Vipi kuhusu ahadi zangu kwa mama na dogo? Kwanini inakuwa hivi? KWANINI?" aliendelea kuongea akilini mwake huku machozi yakimtoka bila sauti
Mvua iliendelea kunyesha juu ya mwili wake uliokuwa umelala barabarani kana kwamba mbingu zenyewe zilikuwa zikilia pamoja naye kimya kimya. Maji yalichanganyika na damu yake, yakasafisha damu yake ardhini taratibu, yakafuta alama za maisha yake kama vile hakuwahi kuwepo.
Dakika zikageuka kuwa saa.
Asubuhi ilipowadia, watu wachache waliokuwa wakielekea makazini walikusanyika kwa mshangao. Simu zikatolewa, picha zikapigwa, vichwa vikatikiswa kwa huzuni, kisha kila mmoja akaendelea na shughuli zake. Hakuna aliyemjua. Hakuna aliyejua jina lake wala sura yake. Alikuwa tu ni “mwili wa kijana asiyejulikana.”
Lakini kwa upande mwingine , katika chumba kidogo cha kupanga kilichojaa unyevunyevu, simu ya mama yake iliita bila kupokelewa. Alikuwa ameamka mapema kuandaa chai, moyo wake ukiwa na furaha kwa sababu jana tu mwanawe alimwambia:
“Mama, nimepata kazi… sasa mambo yatabadilika.”
Alikuwa ameahidi kumpeleka hospitalini kwa matibabu ya muda mrefu aliyokuwa akiahirisha kwa kukosa pesa. Alikuwa ameahidi kumlipia mdogo wake ada ya shule. Alikuwa ameahidi kujenga nyumba ndogo kijijini. Lakini ahadi zake zote zilibaki kuwa historia yaani maneno tupu.
Baadaye, polisi walipogundua kitambulisho mfukoni mwake, simu ile ile ya mama yake ikaita tena safari hii kutoka namba isiyojulikana.
Habari zilipofika, kikombe cha chai kilimdondoka mikononi mwake na kuvunjika sakafuni. Alianguka chini na kufa kwa mshtuko wa moyo familia ile maskini iilivunjika ndani ya siku moja kws uzembe wa mtu mwingine. Kwa uzembe wa dereva aliyekimbia majukumu yake! Ni ulimwengu katili ulioje
*****
"Niko wapi hapa ni wapi" ilikuwa ni sauti ya mwanaume ikiuliza
Mwanaume huyo alikuwa mahali ambapo kulikuwa na nuru nyeupeee asionekane mtu mwingine zaidi ya yeye mwenyewe
"Usiogope mahali hapa ni salama" ilisikika sauti yenye kujirudia rudia kama mwangwi
"Wewe ni nani na mbona sikuoni?" aliuliza tena yule mwanaume
"Mimi? Unauliza kwamba mimi ni nani?"
"Ndio, wewe ni nani?" aliuliza tena
"Sawa nitakujibu kwa uchache wewe mwanadamu, kwakuwa ninyi ni viumbe wenye shauku na kutaka kujua msiyoyafahamu"
"Mimi ndiye, mimi ni MIMI. Mimi ni fahamu ya nafsi yangu. Mimi ni mtu mkuu, mwenye nguvu, niliyeiteka roho yako kabla haijatoweka. Huna haja ya kujua jina langu; unachohitaji kujua ni kwamba nataka kukupa nafasi ya kuishi tena kwa huruma tu lakini kwa masharti kadhaa.”"
"Wewe ni Mungu?"
"Mungu? Hahaha hapana mimi si Mungu, kuhusu mimi ni kiumbe gani hutakiwi kujua"
"Sawa sitakiwi kujua lakini unamaanisha nini kusema kwamba unanipa nafasi ya kuishi kwa mashati kadhaa?"
"Ndivyo nilivyomaanisha kipi kingine unadhani nimemaanisha?"
"Kwanini unanisaidia?"
"Nishasema ni kwasababu ya huruma, lakini juu yako kukubali au kukataa"
"Siwezi kukubali bila kusikia masharti"
"Hahaha usiwe na wasiwasi ninakueleza nilikuwa nikisubiri useme hivyo, sharti la kwanza utafanikisha misheni ambazo nitakuwa nakupatia, of coz zawadi ipo ukifaulu nadhabu pia ukifeli, pili utaishi katika ulimwengu tofauti na huo uliotoka, utakuwa na uhusika mwingine na mwisho kabisa uwe mtiifu"
"Hayo tu?"
"Naam ni hayo tu"
"Unamaanisha nini kuwa mtiifu mi naona unamaanisha itaonekana sitakuwa huru"
"Ni juu yako kuchagua"
"vipi nikikataa?" ,
"Jibu ni rahisi tu ukikataa utakufa roho yako itayeyuka na kupotea"
"Okay nimekuelewa, sharti la kuishi kwingine naweza kukubaliana lakini unamaanisha nini kusema misheni"
"Usijali nitakupa muongozo ambao utajibu majibu hayo mawili ila fanya uamuzi kwanza je unakubali hii nafasi ama unaikataa?"
"Fursa adimu haiji mara mbili na nilikotoka hakunaga kitu cha bure hivyo naweza kukuamini na jibu langu ni Naam" alijibu yule mwanaume na palepale mwanga mkali mweupe ukaongezeka kisha kikatokea duara fulani hivi la bluu kama mpira ueleao na kumsogelea taratibu mwanaume yule
"Usiogope, huo ndio mwongozo wangu na huyo ni msaidizi wangu mruhusu kuungana nawe" ilisikika sauti ya mwangwi na yule mwanaume alitii na kutulia tuli kisha kile kile kimpira kikaungana na roho yake na kuwa umoja(oneness)
*****
Katika ulimwengu ambao ulionekana wa kale sana yaani ulimwengu ambayo teknolojia ilikuwa ni ndogo mno tena mnoo alionekana kijana mtanashati mwenye asili ya ki-asia akiwa amelala ardhini, alikuwa ni mtanashati kweli, alikuwa na mwili wenye afya kama mwanariadha, alikuwa na nywele nyeupe kichwani, yani ieleweke naposema nyeupe, licha ya kuonekana nyeupe alionekana kijana zaidi, alikuwa amevaa mavazi ya kizamani sana, na mavazi yake yalikuwa yamechakaa kwelikweli, alikuwa na umri wa miaka ya ishirini ya mwanzoni
`Kwahiyo huu ndio ulimwengu mwingine nitakaoishi? " alijiuliza
" Naam ndio mdio huu ndio utakaokuwa ukiishi" ilisikika sauti nyingine kutoka katika nafsi yake na kushanga
"Unashangaa nini? Mimi ndiyo muongozo wake ninaitwa" yule mwenye manufaa"
"Jina lako ni yule mwenye manufaa?"
"Naam hilo ndilo jina langu"
"Vipi kuhusu mimi jina langu ni nani?"
"Emiichi, wewe unaitwa Emiichi Shohei" Ilijibu ile sauti kutoka nafsini mwake
"Ooh okay kwakuwa naitwa Emiichi shohei, Basi nawei nikuite Kosei, unaonaje issitoshe kukuita" yule mwenye manufaa" ni kupoteza sauti tu au unasemaje? AliongeaShohei huku akinyanyuka na kukaa kitako ardhini
"Hahaha! sio baya hata hivyo"
"Haya Kosei hapa tupo wapi? na misheni yangu hapa ni ipi na imekuwaje nipo hapa?
"inakubidi nikujibu kwa kirefu Bwana Shohei, kwanza kabisa hapa tupo kwenye himaya la dhehebu fulani au tunaita" sect"" aliongea Kosei na kumfanya Shohei kuangalia huku na huko kwenye eneo walilopo
"Dhehebu hili sio baya lakini, ingawa limekaa kizamani bado pia ni zuri, hewa pia ni Safi kabisa!" aliongea Shohei
"Ni kweli kabisa sasa muanzilishi wa hili dhehebu kiongozi aitwaye Paso Pasio aliwahi kuanguka katika maporomoko marefu na kunusurika hivyo akaunda dhehebu hili na kulipatia jina" mfupa wa chuma" aliendelea kosei na kumfanya Shohei acheke kidogo
"Lengo la kuunda dhehebu hili ni kuwa wenye miili na roho za xhuma ili waje kuisaidia jamii na kufanya yale ya kheri na amani, kiongozi paso pasio alifanya kazi kwa bidii sana kwa zaidi ya miaka kumi na hatimae kufanikisha kuligeuza dhehebu leo ya tisa"
"Levo ya tisa? Ni ukubwa na hadhi gani iliyonayo?" Shohei aliuliza
"Level ya tisa ndio level ya chini kabisa kuliko zote, unapaswa kuelewa zipo leo tisa za hadhi kwa kila dhehebu huku levo ya kwanza ndiyo ya juu zaidi yenye ufalme na heshima iliyoenea" Kosei alimjibu
"Sawa endelea"
"Basi baadae kiongoziPaso Pasii alifungwa jela kwa kufanya kwenye madanguro!"
"Hahaha usinichekeshe bhana, kwamba amefungwa jela kwa kosa la kustarehe kwenye madanguro? Mbona haingii akilini"
"Huu ulimwengu sio kama ule uliotoka kama ilivyokuwa kwenu huko kuwa na sheria zenu huku nako kuna sheria zao, kiongozi wa dhehebu ni kama padre hivyo kufanya uzinzi ni kosa kisheria kwa mujibu wa ulimwengu huu"
"Asee inasikitisha sana, inaonekana huu ulimwengu umekaa kitemi zaidi kuliko ule niliotoka"
**********
CHAPTER 2: Misheni ya kwanza
"Baadae Paso Pasio aliuawa kwa kujaribu kutoka gerezani na wewe Emiichi Shohei namaanishi mmiliki halali wa huo mwili kabla yako alikuwa ni mwanafunzi wa shujaa huyo anayesikitisha" aliendelea kuelezea
"Kwa kifupi Emiichi Shohei halisi, Emiichi wa ulimwengu huu hatuna naye tena, siku tatu baada ya kifo cha mwalimu wake alifariki kwa kudondokewa na ubao mzito usiku wa manena akitaka kwenda chooni, kwahiyo roho yako imeingizwa katika mwili huo na aliyekupa nafasi ya kuishi tena"
"Mpaka hapo umenijibu maswali mawili niliyouliza bado moja la misheni yangu ni ipi?"
"Ooh misheni yako kuu ni kuwa kiongozi wa dhehebu hili na kulifikisha katika kilele cha utukufu unaostahili na unatakiwa utimize misheni hii ndani miaka hamsini ukifeli katika muda huo roho yako itayeyuka na kupotea ni sawa na kusema utakufa"
"Swali langu ni utukufu gani unaostahili hili dhehebu?"
"Swali zuri, utukufu unaostahili dhehebu hili ni kulifanya liwe dhehebu lenye nguvu kuliko madhehebu yote katika ulimwengu huu ikiwa na idadi ya wanafunzi zaidi ya laki moja na katika hilo kutatokea misheni ndogo ndogo na kubwa kubwa"
"Ooh ni hayo tu?" aliuliza Shohei
"Ndio, kwanza unanielewa ninaposema dhehebu?"
"Ndio ndio naelewa unachomaanisha si dini bali dhehebu la kuwafunza watu mbinu za siri na mapigano na kisha kulitumikia kwa jinsi ya sheria zake ni kama wafanyavyo mashaolin"
"Naam inaonekana unafahamu mambo mengi"
"Sana tu"
Mara baada ya mazungumzo hayo marefu kidogo kati ya shohei na kosei basi Shohei alinyanyuka na kusimama na kuanza kutalii eneo lote la himaya hiyo na alikuja kugundua kwamba ni eneo kubwa sana sawa na mita laki tatu za mraba na lilizungukwa na milima mirefu na mabonde kama ngao
Ifahamike kwamba lugha katika mazungumzo ilikuwa ni tofauti kabisa ilikuwa ni lugha ya kale zaidi isijulikane ni lugha gani na Shohei alikuwa akielewa vizuri automatically hata yeye alijishangaa ila hakulitilia maanani jambo hilo
Basi Shohei alitafuta maji akaoga na kubadili nguo safi alizozipata baada ya kuhangaika kuzitafuta kisha kwenda kusimama kwenye eneo la kuingia ndani ya dhehebu hilo yaani langoni kisha kuvuta hewa safi na kuangalia angani
"Sasa kwa kuwa nimekuja katika ulimwengu huu, nitaishi tofauti kama mfalme. Nitakamilisha misheni zote na pia nitawashinda magwiji wote wa ulimwengu huu kwa maarifa yangu yote, ingawa sina uelewa mkubwa na jinsi gani naweza kukamilisha misheni kuu ila ninao muda wa kutosha wa kufikiria na kutafuta njia." aliongea Shohei kisha kunyanyua mikono yake juu kama vile anapokea kitu kutoka angani kisha kusema kwa sauti ya hali ya juu
" Mbinu adimu za uvunaji nishati mbalimbali , maandiko ya siri njooni kwangu!” alinena lakini hakuna kilichotokea zaidi ya upepo kupuliza kisha baada ya kama dakika tatu ukasikika mlio wa ajabu
Ghafla mbele ya macho yako alikuwa akiona mfano kama wa Tv ya hologram, ni kama "touch screen" iliyokuwa na maelezo kuhusu yeye jina lake, umri wake hadhi yake kwa wakati huo na mengi ya maelezo kuhusu dhehebu hilo la mfupa wa chuma
"Oya kosei ni nini hiki naona? Mi nilikuwa nanena to kupoteza sauti" aliuliza
"Huyo unayemuona ni mimi nikijidhihirisha hivyo na hayo maelezo ni kuhusu wewe na dhehebu lako kama unavyoona" aliongea kosei
"Kwamba wwwe ni kama mfumo au robot si ndio?"
"Unaweza sema hivyo ila hapana mimi ni zaidi ya unavyonifikiria utanijua zaidi mbele kwa mbele"
"Maelezo hapo yanaaema natakiwa kutafuta wanafunzi mia moja kukamilisha wanafunzi wanaohitajika kwa dhehebu la hadhi levo ya tisa, na ni misheni nayopaswa kuianza sasahivi nikikaidi napewa adhabu ya kupunguziwa muda kutoka miaka hamsini ya kukamilisha misheni kuu kwenda arobaini seriously!"
"Huu ni unyanyasaji sasa!" aliishia kulalama ila kibishi aliamua tu kuanza mchakato wa kufanikisha misheni ya kutafuta wanafunzi akizingatia lile sharti la utiifu
"Umesahau au unajisahaulisha? hujaja hapa kustarehe kijana, umekuja hapa kutimiza makusudi fulani hivyo changamka kijana muda ni wa thamani sana"
"Nadhani nimesahau kitu unatakiwa kulifanya dhehebu liwe na nguvu kuliko madhehebu yote katika bara hili liitwalo Ardhi ya nyota"
"Nini!? Unasema? Bara zima?"
"Naam" alijibu kosei
"Miaka 50 na unataka nilifanye dhehebu kuwa nguvu namba moja barani? Ni sawa nakuniambia nitumie nusu ya uhai wangu kuhangaikia misheni ya kikuda, laiti ningejua hiki ndicho nachokwenda kufanya nisingekubaliana hata na yale masharti ila kwakuwa nimeyavulia maji nguo sina budi kuyaoga"
"Ding!" ulisikika mlio kwenye nafsi yake na palepale upanga ukatokelezea hewani kimaajabu na kuanguka ukijichomeka ardhini na kumfanya Shohei kushangaa kitendo hiko
"Huo ni upanga wa maafa na kwakuwa unaanza misheni yako ya kwanza siraha hiyo itakufaa sana katika kujilinda unaweza kuuhifashi kwenye stoo iliyoko kwenye mfumo, natumai utautumia vizuri" aliongea kosei na kumuelekeza jinsi ya kutumia mfumo na alifanikiwa kuuhifadhi kwani upanga ule ulipotea kabisa hewani
"Ngoja niucheki huu mfumo kwanza nujue na kupata taarifa" alijisemea na kuanza kubofyabofya kama vile anatumia smartphone
Basi baada ya kuchezeshachezesha vidole hewani kwa dakika kadhaa kuna alivyo elewa na kuna asivyoelewa
"Kuna niliyoelewa hapa ila levo ya ujenzi wa dhehebu na thamani ya mchango wa dhehebu ndio nini hii?"
"Iko hivi dhehebu lako lina sehemu nyingi za kufanyia ujenzi hivyo Kadiri kiwango(level) kinavyokuwa cha juu, ndivyo kazi nyingi zaidi za dhehebu zinavyoweza kufunguliwa."
"Na hapa inaonyesha ni level namba moja je ni kwa namna gani naweza kupandisha levo ya ujenzi?"
"Jibu ni kwa kusajili wanafunzi zaidi"
"Vipi kuhusu thamani ya mchango wa dhehebu"
"Kupitia thamani za mchango unaweza kununua vifaa na vitu vingine kwa lugha nyepesi utanunua kutoka kwangu tutakuwa tunafanya biashara"
"Oh kumbe pia kuna vya kununua kwenye mfumo. Je nikwa namna gani naweza kukuza thamani?"
"Jibu ni lile sajili wanafunzi zaidi"
"Hahaha nishaelewa sasa, iwe ujenzi wa dhehebu, thamani ya mchango wa dhehebu na kufanya dhehebu liwe imara njia ni ileile tu nayo ni kusajili wanafunzi zaidi haya sasa kazi ianze" aliongea Shohei akiwa na dhamira kuu akichukulia ni kazi rahisi sana
Muda mchache mbele alikuwa amekaa nje kwenye benchi na meza ya mbao huku pembeni yake kukiwa na ubao umeandikwa USAJILI WA WANAFUNZI KATIKA DHEHEBU LA MFUPA WA VHUMA kwa lugha ya kale
"Kwa utanashati nilionao nina hakika ndani ya siku tatu nitakuwa nimeshakamilisha idadi mia ya wanafunzi" alijiambia
"Kweli?" kosei alimuuliza
"Tulia ujionee nina uzoefu na hili"
BAADA YA MWEZI MMOJA NA SIKU KADHAA
"Hakuna mtu? Kosei hivi unaweza kuamini kwa mwezi na masiku kadhaa nakosa hata mtu mmoja? Kama sio mikosi ni nini? " aliongea Shohei huku akila viazi vitamu vya kuchemsha akisukumizia na maji
"Pengine huna bahati"
"Sasa tofauti ya mikosi na kutokuwa na bahati ni ipi? Mi naona unanikejeli tu sina hata hamu ya kula" aliongea huku kinishi akila viazi vyake alikuwa amechoka kwelikweli
"Kwa mwezi na masiku nateseka kwa kula viazi na maji na kuketi kwenye mbao kwa masaa nengi nikiumiza makalio yangu halafu hakuna hata mmoja?" Shohei aliongea kwa kukata tamaa na kuinua kichwa juu kuangalia anga la jioni lililopambwa na mawingu pamoja na mwanga wa dhahabu wa jua kuzama
" Hey mkaka nataka kujiunga na dhehebu la mfupa wa chuma" ilisikika sauti nyororo ile ya kumtoa nyoka pangoni
Shohei kusikia sauti hiyo alishusha kichwa kuangalia ni nani
"Hakika ni mrembo! Mimi kama kiongozi wa dhehebu la mfupa wa chuma ninakukaribisha kwa moyo wa dhati kabisa" haikueleweka nguvu alizipata wapi ilihali alikuwa amechoka ile mbaya
"Wewe ndio kiongozi? Basi nimeghairi kujiunga na dhehebu lako"
"Aah tafadhari usiondoke dhehebu langu lina uwezo mkubwa sana, ninaweza kuonekana kijana lakini nitaweza kuleta maendeleo katika dhehebu, kwasasa hivi ni mtu wa kawaida ila ukijiunga utakuwa mtu wa maana mbeleni, mimi nimekuwa kiongozi wa dhehebu hili kws umri mdogo kutokana na juhudi hivyo naimani utafika mahali ukijiunga na dhehebu langu" Shohei alianza kumshawishi kwa maneno ya uongo na kweli na kama dakika hivi alifanikiwa kumshawishi na akajiunga kisha binti yule mrembo akaanza kutalii eneo hilo
"Hatimae nimeweza kumshawishi na maneno hakika mimi ni mtaalamu kwenye sanaa ya kucheza na maneno(art of talking)" alijigamba
"Hongera kwa sasa dhehebu lako lina jumla ya wanachama wawili pia na thamani ya mchango ni moja"
"Unaweza kufanya biashara nami kwa kununua bidhaa katika mfumo" aliendelea kosei
"Kosei" Shohei aliita
"Naam"
"Tangu lini umekuwa tapeli? Unataka kunifilisi eeh yaani nimepata thamani moja na unataka kunipora?
" Tuliza wenge kijana hiyo thamani moja inatosha kabisa kununua bidhaa yenye manufaa nishakwambia mimi ni yule mwenye manufaa"
" Emu nionyeshe bidhaa zilizoko sokoni kwasasa" aliongea Shohei na skrini ya hologram ikajitokeza mbele yake ikiwa na bidhaa nyingi
"Asee mpaka mbinu mbali mbali za uvunaji nishati na mbinu za mapigano wow!, eti kosei kwa thamani moja ni bidhaa gani inayopatikana ikanifaa?" aliuliza maana bidhaa zilikuwa ghali kidogo
"Ngoja tuone" alijibu kosei na kumtafutia
"Naam ni hii Talisman" alimuonyesha kwenye skrini na kuendelea inaitwa Talisman ya uzoefu"
"Itaninufaisha kivipi mimi hiyo Talisman ya uzoefu?"
"Itakusaidia katika hatua za mwanzo za uvunaji nishati ukiipiga makofi kwa mikono yako miwili kwa pamoja kama unaikandamiza itakuvusha levo kadhaa bila juhudi yoyote"
"Sio mbaya nitanunua" aliingea Shohei na kufata maelekezo ya kununua na kuitumia kama alivyoambiwa kwani mara baada ya kuipiga makofi ilibadilika na kuwa moshi mweupe na kumvaa mwilini
Shohei alihisi mwili wake ukiingiwa na nguvu kama umeme hivi na baada ya hilo kuisha na moshi kupotea alijihisi wa tofauti sana mwili mwepesi kuliko mwanzo"
"Hongera Bwana Emiichi shohei kwa kufikia levo ya tano ya ufunguzi wa meridian katika kuvuna nishati"
"Asee nahisi nishati nyingi zikiingia mwilini mwangu" aliongea Shohei kwa bashasha
"Acha kufikiria mbali kijana, levo zote kumi na mbili za ufunguzi wa meridian ni sawa na introduction katika hili bara la ardhi ya nyota kwenye Uwanja wa nishati , levo halisi za uvunaji wa nishata katika ulimwengu wa Martial arts kuanzia chini kwenda juu ziko kama ifuatavyo, baada ya kufungua meridian mpaka levo ya kumi na mbili unaingia kwenye levo ya Mwanafunzi wa mapigano kisha Bwana wa mapigano kisha Bwana mkuu wa mapigano , kisha Mfalme wa mapigano kisha mfalme mkuu wa mapigano kisha mtakatifu wa mapigano kisha Mungu wa mapigano ambayo ndiyo ya juu na katika kila levo kuvuka utapitia stage tisa"
********
CHAPTER 3: kipigo kwa wanafunzi
"Vipi kuhusu hii Talisman ya ufunguzi wa muhuri?" aliuliza kwa shauku
"Hiyo ni kwaajili ya kufungua nguvu za ule upanga wa maafa"
"Damn we kweli ni tapeli, haiwezekani upanga nilioupata bure nao unahitaji kufunguliwa?"
"Ofa ina kikomo kijana pambana hakuna vya bure bure"
******
Ilikuwa ni sehemu yenye mandhari ya kuvutia na asilia zaidi, kukiwa na miti na mimea mingi hali iliyoleta ukijani mwingi
"Kijana! Unaonekana kuwa na kipaji cha asili; wewe ni gwiji wa sanaa za mapigano wa kipekee kati ya mamillion, unaonaje ukijiunga na dhehebu langu la mfupa wa chuma kisha utakuwa hauna ukomo katika uwezo.” aliongea Shohei huku akionekana amemkaja mtu usoni na kiatu chake, alikuwa akimshawishi kimabavu
"Tafadhali Sir unaweza kuondoa mguu wako kwanza?" aliongea kijana huku akijiambia mawazoni gwiji ilihali umenipiga hivi unanikejeli sio?
"Aah uniwie radhi nilikuona ukimsumbua mwanafunzi wangu hivyo nikashindwa kujizuia"
"Nilikuwa tu naongea nae..." kabla hajamaliza alinyanyuliwa juu na kusimama
"Oh kumbe ni hivyo, nisamehe sana inuka sasa!" kisha akamsogelea karibu kabisa na uso wa huyo kijana akiwa na tabasamu la kishetani kisha kumnong'oneza
"Fikiria kwa makini kuhusu kujiunga na dhehebu langu" kwa jinsi alivyonong'ona ni kama vile ilikuwa ni amri na sio ombi
"Vipi kama nitakataa kujiunga!,Tayari nishajiunga na dhehebu la maji ya chemchem" aliongea yule kijana na kumfanya shohei ashushe pumzi nyingi
"Inaonekana huna hatma ya kujiunga na dhehebu langu" aliongea shohei kisha akageuza shingo upande mwingine na kuuliza
"Yaoyao huyu jamaa si alikuwa akikusumbua?"
"Eeh ndio, alikuwa akijaribu kunishika mkono wangu" alijibu Yaoyao kwa sauti tamu na alikuwa ni mwanafunzi wa kwanza kabisa, yule binti aliyemjia, Naam jina lake aliitwa Yaoyao, alikuwa ni kachina karembo
Alikuwa ni binti mrembo kweli tena mrembo kuliko neno lenyewe, alikuwa amevalia mavazi meupe ya kikale na kitamaduni zaidi mkono akishika upanga wake uliochomekwa kwenye ala yake Shohei mara baada ya kusikia jibu lile alimgeukia yule kijana na sura kama ya fisi aliyeona kitoweo
"Umejiletea maafa yako kwa mkono wako mwenyewe" alimaka na kuanza kumshushia kipigo cha mbwa koko kwa mara nyingine
"Lakini sikufanya hivyo.....nilijaribu lakini...jaribio langu likashindwa.....lilikuwa...ni jaribio....tu" alikuwa akiongea kujitetea kijana wa watu huku akishushiwa kipigo
"Yaoyao hawezi kunidanganya namuamini, leo lazima nikushikishe adabu, nyie wahuni ndio mnaotuharibia dada zetu" ilionekana ni kana kwamba kipigo hiko alichompa ni kutolea tu hasira zake za kukataliwa kujiunga na dhehebu lake alikuwa akipooza hasira kutokana na msoto wa kuhangaika kutafuta wanafunzi wapya, aliyekuwa akishushiwa kipigo alikuwa ni kijana mdogo miaka kama kumi na sita hivi!
Aaah....aah....aaaah mkono wanguuu!! "alipiga yowe dogo wa watu."
Baada ya Shohei kuridhika na kipigo alichompa alimuacha kisha akamwambia Yaoyao waendelee na safari yao
"Yaoyao si nimefsanya vizuri eeh?" aliongea shohei na Yaoyao binti mrembo hakumjibu lolote
Huko waendako ilikuwa baada ya shohei kupewa taarifa na koseo ya kwamba kuna usajili unafanyika siku hiyo katika moja ya mji, na kama anataka kufanikisha misheni haraka ni kheri afike mapema, hivyo kukataliwa kwake na yule kijana muhuni hakuona haikumuuma sana
Wakiwa wanatembea kila mmoja akiwa kimya kwa kama nusu saa ghafla walitokea watu tano vijana kabisa wakiruka juu ya miti kama nyani na kutua mbele yao wasijulikane wametokea wapi na walionekana kuwa wanafunzi wa dhehebu fulani kutokana na sare za nguo zao
Mara akaongezeka mtu wa sita akitembea kwa tabu mno
"Kaka mkubwa huyu ndiye aliyenipiga" aliongea kijana yule wa sita akibubujikwa na machozi huku akimnyooshea kidole Shohei
Shohei na Yaoyao walikuwa katika sintofahamu kwa sekunde kadhaa kisha yaoyao akaongea kwa sauti ya kunong'ona
"Kiongozi huyu ni nani?" aliuliza
"Ni yule muhuni aliyekuwa akikusumbua nadhani, kidoho nimsahau" aliongea kwa kunong'ona pia na ilikuwa kweli kwani sura ya yule kijana ilikuwa imevimba na kutoka manundu kadhaa kwenye komwe na kungumu kumtambua
"Wewe mpuuzi unathubutu vipi kumpiga mwanafunzi wa thehebu la maji ya chemchem? Kwanza wewe ni nani? " aliongea mmoja aliyeonekana kuwaongoza
"Emiichi Shohei, kiongozi wa dhehebu la mfupa wa chuma" alimjibu
Yule jamaa baada ys kusikia vile aliwageukia wenzie na kuuliza "Hilo si ni dhehebu ambalo kiongozi wa awali alikamatwa na serikali kwa kustarehe kwenye madanguro? Kisha kuuawa baada ya kujaribu kutoroka gerezani?"
"Naam ndio ndio kaka mkubwa nasikia pia dhehebu lilianguka na kufeli kabisa, nashangaa kusikia yeye ni kiongozi wa dhehebu hilo" mmoja kati yao alijibu
"Madanguro? (kisha kusafisha koo na kuendelea) yaani mmetuziba njia ili udhalilishe dhehebu langu?" Shohei aliongea kwa kupanic mara baada ya yaoyao kusikia "madanguro" alikuwa akihofia pengine kwa sifa hiyo mbaya anaweza kuhama dhehebu
"Kiongozi wa dhehebu la hovyo mchanga usiye na uzoefu, unapata wapi udhubutu wa kumpiga mwanafunzi wetu mpya?" alifoka mmoja kati yao na wote kujiandaa kumshikisha adabu
"Yaoyao kaa pembeni, nataka niwashikishe adabu hawa wapuuzi"
"Sawa ila kabla hujafa ukumbuke pia kunirithisha nafasi yako ya uongozi" aliongea Yaoyao aliyekuwa pembeni akiwaachia uwanja vijana hao
Shohei kusikia kauli hiyo aliishia kunying'onyea na kusikitika, alijiambia yaani ana mwanafunzi mmoja tu na ni siku hiyo hiyo amebahatika kumsajil lakini keshaanza kutamani nafasi yake?
Alimpotezea, kisha kushusha pumzi ndefu na kuchaneli meridian zilizofunguka na ghafla mwili wake ulianza kupitia mabadiliko yasiyo ya kawaida kwani katika mkono wake ilionekana miduara mitatu rangi kama ya chungwa kwenye mikono yote miwili eneo la "wrist" kama vile amevaa bangili
Wale vijana kuona vile waliishia kucheka na kumdharau,
*Yaani miduara mitatu mkononi? Hahaha upo kati levo ya tatu katika ufunguzi wa meridian, wewe ni sawa na kunguni tu usiyejua nafasi yako" kiongozi wao alimdhiklhaki
"Hahaha kiongozi yeyote wa dhehebu angalau anatakiwa awe katika levo ya mwanafunzi wa mapigano hata kama dhehebu ni la hadhi ya chini levo tisa" aliongea mwingine
"Na yeye ndio kwanza yupo kwenye levo ya tatu ya ufunguzi wa meridian! Na bado anapata uthubutu wa kutaka kupigana nasi! Hahaha ni kichekesho kilioje!" alidakia mwingine
"Sikia ewe Emiichi Shohei, kiongozi wa dhehebu la mfupa wa chuma, ukipiga magoti na kuniomba nikuhurumie pengine naweza kukusameha na kusahau makosa yako" aliongea kiongozi wa wale vijana kibabe kisha naye akachannel nguvu zake za kufungua meridian zake na miduara kama bangili mikinoni mwake jumla ikiwa minne ilionekana, rangi ya bluu bahari na wenzake wakafuatia na wote walikuwa levo sawa
Upande wa Yaoyao pembeni alikuwa ametulia tuli akiangalia na kujiambia kwahyo wale wanafunzi wote wapo katika levo ya nne ya ufunguzi wa meridian?
"Piga magoti...." kabla hata hajamaliza kauli yake alishtukia mtu yuko mbele yake na kukung'utwa ngumo ya uso na kurushwa nyuma kidogo
"Unatania au sio? Yaani mimi nipige magoti?" wenzake yule kiongozi walikuwa katika bumbuwazi wasielewe imekuwaje mtu yule aliye dhaifu kuliko wao akawa na nguvu vile na kushambulia pasipo wao kushtuka mapema
"Inawezekana vipi mtu kama wewe aliye katika levo ya tatu ya ufunguzi kuwa na nguvu hivi?" aliuliza kiongozi wa wale vijana baada ya kunyanyuka
"Kwasababu mimi ni kiongozi wa dhehebu" Shohei alimjibu kisha kufumba na kufumbua alikuwa uso kwa uso na yule kiongozi tena na kumtandika teke la tumbo lililomrusha kwa mara nyingine tena
"Ding!" Shohei alisikia mlio kisha sauti ya kosei ikamwambia ""Umepewa misheni, unatakiwa kudili na hao wanafunzi uwashikishe adabu kwa kukudhihaki ili kutunza heshima yako kama kiongozi"
Ifahamke sauti ya Kosei inasikika kwa Shohei pekee na anawasiliana naye kwa namna mbili kwa kuongea kwa sauti na kupitia mawazo/fikra na hapo kosei alinena kupitia fikra
"Usiwaze sana hii misheni ni rahisi kwangu na nimeipenda hivyo nitaikamilisha na matokeo yakuridhisha" Shohei alimjibu kwa fikra pia
Wale wanafunzi wengine kuona vile waliamua kushambulia kwa pamoja na Shohei alipoona hivyo ghafla aliongeza nguvu na kufikia levo ya tano ya ufunguzi ambao ndio ukomo wake wa nguvu ulipofikia
"Levo ya tano ya ufunguzi?" wote walihamaki na kusita kushambulia
"Inaonekana huyu mtu alificha nguvu zake halisi" alidakia kiongozi akinyanyuka kwa mara nyingine safari hii akitokwa na damu puani
Shohei hakutaka kupoteza muda kusikiliza ngojera zao aliona wanamcheleweshea muda hivyo dakika mbili na sekunde kadhaa pekee zilitosha kuwakung'uta na kuwashikisha adabu kisawasawa na walikuwa chini hoi wakiugulia maumivu
"Sikutegemea kama utakuwa unaja kupigana" Ksei aliongea kwa fikra baada ya Shohei kumalizana na wale vijana wasio na adabu
"Unanichukuliaje kwani? Unaniona mzembe sio? Katika maisha yangu ya nyuma nilikuwa nikijifunza mbinu mbalimbali za kujilinda na kupambana japo kwa njia ngumu kutokana na kukosa walimu, naweza nisiwe mtaalamu ila kukinukisha kwa kiasi flani naweza"
"Oh hongera kwa hilo na kwa kukamilisha misheni hii ndogo umepata thamani tano za mchango wa dhehebu kama pongezi kwa kukamilisha misheni" aliongea Kosei na skrini ya mfumo au tuite system ilionekana mbele yake na kuona balance la thamani na kutabasamu kisha skrini ikapotea (Hapa pia ifahamike skrini haionekani kwa yeyote zaidi ya Shohei)
"kwaherini nyote, natumai tukutane tena siku za usoni, Yaoyao tuondoke" aliongea Shohei kisha kuongoza njia
Walipofika mbele kidogo Yaoyao alivunja ukimya na kunena "Tungewaua tu kuepuka usumbufu wa baadae"
Shohei kusikia vile kijasho kilimtoka na kumuangalia Yaoyao kwa sekunde kadhaa na kumwambia
"Kwanini tuwe wakatili hivyo?"
"Ardhi ya nyota ni kama msitu na unatakiwa ufahamu na kufata sheria za msituni hakuna kuonyesha huruma kwa adui" Yaoyao alimjibu kikauzu
"Kama umeshindwa kufahamu hilo basi huna vigezo vya kuwa kiongozi wa dhehebu" aliendelea na kumuacha Shohei katika tafakari
"Yupo sahihi huyo binti, haupo tena kwenye dunia uliyozaliwa uko katika ulimwengu mwingine sasa na huu ulimwengu unaheshimu uwezo wa kupambana pamoja na sheria za msituni huku watu hawatakiwi kuwaonyeshea huruma adui zao" Kosei aliongea fikra akionekana kumuunga mkono binti Yaoyao
"Hata hivyo licha ya kwamba ni ukweli muelimishe binti huyo kutunza heshima na utu wako, na hii ni misheni ndogo uliopatiwa" aliendelea kuongea