Simulizi ya January Makamba:- Fuko lililojaa tembo

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,698
2,000
Simulizi Hii imesimuliwa Na January Makamba kwenye ukuta wake wa Facebook.


Kule kwenye kilele cha mlima ndio kijijini kwetu, panaitwa Mahezangulu, Bumbuli. Kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima unapita kwenye shamba la mkonge, ambapo ndipo nimesimama kupiga picha.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mzee Makamba na wazee wengine, miaka 60 iliyopita hapa hakukuwa na shamba la mkonge, bali palikuwa na msitu na mlima huo unaoonekana ulikuwa umefunikwa na msitu. Moja ya "legacies" za uchumi wa kikoloni (ambao ulijikita kwenye monoculture plantations) ni uharibifu mkubwa wa mazingira na kuteketeza uoto wa asili.

Mzee Makamba ananiambia kwamba mwaka 1953, wakati sehemu hii niliyopiga picha palikuwa na msitu, watu walikuta tembo amekufa porini. Wanakijiji wengi wakashuka mlimani kuja kujikatia nyama. Mmojawapo aliyeshuka kufuata nyama alikuwa mdogo wake Babu yangu (yaani babake mdogo Mzee Makamba) anaitwa Bakari Makamba (maarufu kama Baba Komweta). Akarudi nyumbani na fuko kubwa la nyama nyingi sana. Wakati anaingia tu nyumbani, Babu akamwambia hiyo nyama huwezi kuingia nayo hapa ndani...sisi ni Waislamu na Uislam hauruhusu kula vibudu (mizoga) wala tembo. Babu yangu alikuwa mtu wa msimamo mkali sana kwenye mambo yake. Kwahiyo yule Babu Mdogo (Babu Bakari) akaambiwa akaitupe ile nyama.

Hakwenda kuitupa. Baada ya muda mfupi, akarudi ndani kwa Babu akiwa na fuko la ile nyama na akatangaza rasmi kwamba ameingia rasmi Ukristo. Akageuka akaondoka zake na fuko lake la nyama kwenda kukaa kwa rafiki zake kwenye kitongoji kingine.

Baada ya kuhama, akaenda tena mara ya pili bondeni kuchukua nyama nyingine na akawa anagawa kwa wana-kitongoji wengine. Alikuwa kama shujaa wa kile kitongoji. Akatungiwa hadi wimbo wa kisambaa uliokuwa unasema "Sheja Komweta auye tihomoe mazama" (yaani Baba Komweta arudi tutafune manyama). Baada ya nyama kuisha akarudi na kumwambia Babu kwamba mambo yaishe na kwamba karejea tena Uislam.

 

charty

JF-Expert Member
Oct 28, 2013
7,395
2,000
Nimekumbuka vile vikatuni vyake baada ya uchaguzi..January yuko vizuri kwenye haya mambo.hahaha
 

Hossam

JF-Expert Member
Feb 10, 2011
3,386
2,000
Yaani iko hivi, kwa muda huu huko ccm huwezi kuleta wazo kwa kuwa aliyepo hawezi kukupa nafasi. Kubadili dini ni kuhama chama ambako utafurahiwa kwa inputs zako lakini kwa kuwa huko si asili yako jamaa wa ccm akimaliza muda utarejea.

Makamba acha wazo hili.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,698
2,000
Yaani iko hivi, kwa muda huu huko ccm huwezi kuleta wazo kwa kuwa aliyepo hawezi kukupa nafasi. Kubadili dini ni kuhama chama ambako utafurahiwa kwa inputs zako lakini kwa kuwa huko si asili yako jamaa wa ccm akimaliza muda utarejea.

Makamba acha wazo hili.
Duh
 

MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
3,710
2,000
Sasa hivi CCM kuna nyama wote wameukataa Upinzani nyama ikiisha wanatamani upinzani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom