Sehemu ya 21
Siku iliyofuata ilikuwa ni ya kutembea katika mbuga hiyo wakipiga picha vya kutosha na kuwaangalia wanyama. Ilikuwa ni safari ya kawaida lakini kila mmoja alionekana kufurahia safari hiyo.
Baada ya kukaa hapo kwa siku mbili, wakaambiwa kuhusu Mbuga ya Wanyama ya Ngorongoro, hawakutaka kusubiri, iliwavutia na hivyo kupanga safari ya kuelekea huko kwa gari maalumu la mbugani.
Safari haikuchosha, kila mtu aliifurahia na baada ya muda fulani, wakafika huko na kuendelea kukatalii kama kawaida.
“Kwa saa hivi hakuna wanyama wengi sana, twendeni tukapumzike halafu baadaye turudi,” alisema mwanaume aliyekuwa na kazi ya kuwatembeza, wakakubaliana naye na kwenda kuchukua chumba katika hoteli iliyokuwa hapo Ngorongoro.
Walikaa humo kwa saa tatu ndipo wakatoka, wakachukuliwa na kupelekwa katika gari jingine pamoja na watu wengine, wakaingia ndani na kutulia katika kiti cha pamoja wao wawili huku walinzi wao wakiwa wameambatana nao.
Wakati gari likitaka kuondoka, sauti ya msichana mmoja ikasikika ikimtaka dereva kutokuondoka, akafanya hivyo, msichana huyo akaanza kupiga hatua huku akikimbia, alipolifikia, akaingia ndani.
Kila mtu aliyemuona aliguna, alikuwa msichana mrefu, mweusi, aliyekuwa na figa namba nane iliyojichora vilivyo, kichwani alikuwa na nywele za wastani huku akiwa ametoboa pua na kuvaa kisketi kilichoyaacha mapaja yake wazi.
Alipendeza, sketi ile laini aliyoivaa iliifanya hata nguo yake ya ndani kuonekana kitu kilichomtamanisha kila mwanaume aliyemwangalia.
Kifuani hakuvaa kitu chochote kile, kilikuwa kimesimama kana kwamba ncha za misumali, kwa juu alivalia fulana ndogo ya kike ambayo iliifanya hata shanga aliyoivaa kiunoni kuonekana wazi, msichana huyo alikuwa Catherine.
|
|
|
Je, nini kitaendelea?