๐’๐ข๐ฆ๐ฎ๐ฅ๐ข๐ณ๐ข ๐ญ๐š๐ฆ๐ฎ ๐ฒ๐š ๐ค๐ข๐ฃ๐š๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข/๐ค๐ฎ๐ญ๐ข๐ฌ๐ก๐š: ๐Š๐€๐‘๐€๐๐ˆ

๐’๐ข๐ฆ๐ฎ๐ฅ๐ข๐ณ๐ข ๐ญ๐š๐ฆ๐ฎ ๐ฒ๐š ๐ค๐ข๐ฃ๐š๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข/๐ค๐ฎ๐ญ๐ข๐ฌ๐ก๐š: ๐Š๐€๐‘๐€๐๐ˆ

SIMULIZI RIWAYA

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2022
Posts
422
Reaction score
1,314
Simulizi: ๐Š๐€๐‘๐€๐๐ˆ
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
Sehemu ya...........01

๐Œ๐–๐€๐๐™๐Ž
Wingu kubwa jeusi, radi na miungurumo ya hapa na pale ilikuwa imeshika kasi na kufunika mlima mkubwa maarufu kama mliwa wa Zaron. Karibu na kilele cha mlima huo kulikuwa na pango moja kubwa lenye upana na umbali mrefu kuingia ndani mithiri ya zile barabara za chini za treni. Moshi mwingi ulionekana ukifuka kutokea ndani ya pango hilo la kutisha. Ndani kabisa ya pango hilo mzee mmoja aliyevalia mavazi meupe, kofia ya kifalme iliyotengenezwa kwa dhahabu ilikuwa imekipamba kichwa chake chenye mvi, mkononi mwake alikuwa na mkongojo wenye rangi nyeupe pia alionekana akiwa amesimama kwa unyenyekevu mkubwa mbele ya sanamu kubwa lenye muundo wa kichwa cha mnyama wa ajabu mwenye pembe tatu ndefu. Mdomo wa sanamu hilo ndipo ulipokuwa ukitoka ule moshi ulioonekana nje na kusambaa karibu maeneo yote ya mlima wa Zaron.

"Mtihani ulionipa ni mkubwa sana Mungu wangu, kwa nini umeruhusu nipitie haya yote, umeninyang'anya ufalme wangu, ukaruhusu watu wangu waangamizwe na maadui zetu, bado haitoshi ukanitenga mbali na ndugu zangu, nilikuja hapa na kulia mbele zako ukaniahidi ukasema vita ya leo hii ni lazima nitashinda na kurudisha ufalme wangu uliopotea, lakini tazamana kilichotokea mambo ni tofauti kabisa, kwa nini umeruhusu nipitie haya Mungu wa Zaron" Yule mzee mwenye mavazi meupe alikuwa akiongea kwa uchungu wakati huo akiwa amepiga magoti mbele ya lile sanamu kubwa na kuinua mikono yake juu.

Kimya kilitawala kwa muda na mara sauti kubwa nzito na ya kutisha iliyoambatana na mungurumo pamoja na ongezeko kubwa la moshi kutoka kwenye mdomo wa lile sanamu ilisikika ikisema.
"Mfalme Luther, yote unayoyapitia imetokana na uzembe wa kushindwa kuwaongoza watu wako. Makosa yamekuwa ni mengi mno Luther, hebu tazama ni siku chache zimepita ulikuja hapa na kulia mbele zangu nikakuahidi kama hakutakuwa kosa jingine basi utashinda vita yako na kuurejesha ufalme wako mikononi mwako leo lakini unajua nini kimetokea? Umekosa tena Luther"

"Hapana, nimejitahidi sana kulinda heshima na ahadi zangu kwako sijafanya kosa lolo...."

"NYAMAZAAAAAAA!!" Sauti ya kile kiumbe kisichoonekana kutoka kwenye ile sanamu ya kichwa cha mnyama ilisikika ikifoka kiasi cha kusababisha radi na miungurumo mikali kuongezeka na kutetemesha mlima wote wa Zaron.
Binti mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya vita akiwa na mlinzi wake nje pango hilo alionekana kuogopeshwa sana na hali hiyo.

"Baba" alisema yule binti huku akionekana mwenye hofu sana akataka kuingia ndani ya lile pango lakini yule mlinzi alisimama mbele yake kumzuia.
"Lilitha usifanye hivyo, hii ni hali ya kawaida sana huwa inatokea kila wakati baba yako anapokuja kuongea na Mungu wa Zaron usiogope atatoka salama" Alisema yule mlinzi
"Unataka kumaanisha nini? Unafikiri ni mara yangu ya kwanza kuja hapa?" binti Lilitha aliongea kwa kufoka macho yake yakabadilika rangi na kuwa ya bluu, hii ilikuwa ni ishara tosha kuwa watu hawa hawakuwa viumbe wa kawaida.
"Nisamehe Lilitha lakini kumbuka mfalme Luther alisema nisikuruhusu uingie hata iwaje" Yule mlinzi aliendelea kushikilia msimamo wake na hapo Lilitha alikuwa mpole na macho yake yakabadilika na kurudi katika hali ya kawaida.

Hali iliendelea kuwa ni tete ndani ya pango kulipokuwa kukiendelea mazungumzo kati ya Mfalme Luther na Mungu wa Zaron.

"Nimesema NYAMAZAAAAAAA... Watu wako bado wanaendelea kufanya makosa kila siku, kuna mtu wako mmoja hayupo hapa kaenda ulimwengu mwingine anaua viumbe wasio na hatia kinyume kabisa na kanuni na taratibu zetu"
Maneno haya kutoka kwa Mungu wa Zaron yalimfanya mfalme Luther abaki kinywa wazi, zilikuwa ni taarifa zilizomshtua na wala hakutegemea kabisa kusikia kitu kama hicho.
"Kuna mtu wangu yupo ulimwenguni mwingine kivipi!?" Mfalme Luther alijiuliza mwenyewe huku mdomo wake ukiwa wazi, haikuwa rahisi kuamini.

"Hakikisha unamdhibiti huyo mtu wako mapema kabla hajaleta maafa katika ulimwengu wa watu wengine, mambo yanaweza kuwa mazito sana zaidi ya unavyofikiri Luther, haya inuka hapo na uondoke ONDOKAAAAAA" ilifoka ile sauti, kwa mara nyingine tena radi na muungurumo mkali ukatokea.

Kwa mara nyingine tena binti wa mfalme Lilitha alijikuta uvumilivu unamshinda, akaanza kupiga hatua kuingia ndani ya lile pango lakini yule mlinzi alifika haraka na kusimama mbele yake.

" Lilitha tafadhali jaribu kuwa muelewa" alisema yule mlinzi lakini Lilitha hakutaka kupoteza muda alirudisha mkono wake nyuma na kuupeleka mbele kwa nguvu hata kabla hajamgusa yule mlinzi alirushwa umbali mrefu na kwenda kujigonga kwenye ukuta wa lile pango akaanguka chini huku akiwa amejeruhiwa kwenye baadhi ya maneno ya mwili wake, damu yenye rangi ya bluu ikawa inamtoka.
Lilitha aliendelea kwenda mbele lakini ajabu yule mlinzi aliinuka kama radi na kuruka umbali mrefu akatua mbele ya Lilitha. Lilitha alipo jaribu kumsukuma tena kama awali yule mlinzi alimkwepa na kumzunguuka nyuma kwa kasi kama umeme. Wakati huo kila mmoja macho yake yalikuwa yamebadilika na kuwa na mwanga wa bluu sio mlinzi wala sio Lilitha wote walikuwa katika hali hiyo.

"Mnafanya ujinga gani hapo acheniii" Mara sauti kali kutoka ndani ya lile pango ilisikika wote wakageuka kutazama, alikuwa ni Mfalme Luther.

"Baba" Lilitha aliita huku akikimbia na kusimama mbele ya baba yake, alionekana mwenywe shauku ya kujua ni nini kimetokea. Sura yenye huzuni na muonekano wa baba yake vilitosha kumthibitishia kuwa mambo hayakuwa shwari kabisa.
"Binti yangu" Mfalme Luther aliita kwa sauti iliyojaa simanzi.
"Ndio baba, nini kimetokea? Mungu wa Zaron kasemaje?"
"Kuna kosa kubwa tumefanya mwanangu, kosa kubwa sana"
"Kosa gani tena baba? Mbona tulihakikisha kila kitu kinakuwa sawa?"
"Kuna mtu wetu kaondoka ameenda ulimwengu mwingine, anaua watu wasio na hatia. Mungu wa Zaron kakasirika sana kaagiza tumrudishe haraka kama si hivyo basi mambo yatazidi kuwa magumu kwetu na mwisho taifa langu litaangamizwa lote"
Kauli hiyo ilionekana kumshangaza sana Lilitha, taratibu aligeuka nyuma na kumtazama mlinzi wake, wakatazamana kwa sekunde kadhaa mwisho yule mlinzi akainamisha macho yake chini.

"Kuna nini?" Aliuliza Mfalme Luther baada ya kuona kuna kitu hakipo sawa kati ya binti yake Lilitha na mlinzi.
"Baba" Lilitha aliita
"Ndiyo mwanangu"
"Mlinzi aliniambia kuwa kaka Damon hayupo alitoroka tangu usiku wa juzi tulipokuwa tunajiandaa na vita mpaka sasa hajaonekana"
Alisema Lilitha taarifa iliyomfanya Mfalme Luther atoe macho kwa mshangao.
"Eti nini? Kaka yako Damon ametoroka kivipi yani! Si tulimfunga na kuweka ulinzi wa kutosha kivipi tena unasema ametoroka"
"Ilikuwa ni usiku sana, tulishangaa nguvu zake zimerudi ghafula akakata minyororo yote na kisha kuwashambulia walinzi wetu wote baada ya hapo alitoweka" Yule mlinzi alieleza.
Maelezo hayo yalimfanya Mfalme Luther apige hatua na kusimama mbele ya yule mlinzi.
"Kwa nini hamkuniambia? " Mfalme Luther aliuliza kwa hasira huku kidevu chake chenye mvi nyingi kikicheza cheza kwa hasira.

"Mfalme wangu, ulikuwa ukijiandaa na vita ya muhimu sana kwa taifa lako hivyo tuliona tusikusumbue, tulimtuma Raffat afuatilie nina imani atarudi hapa na majibu, tutamrudisha Damon nakuahidi hivyo mtukufu Mfalme" Mlinzi alieleza huku akitetemeka kwa hofu.

Mfalme aliondoka bila kusema chochote, akapiga hatua na kwenda kupanda moja kati ya farasi waliokuwa wamefungwa chini ya mti.

"Mleteni Raffat kwangu mara moja" Alisema Mfalme Luther na hapo akavuta kamba za farasi na kuondoka kwa kasi.

Nusu saa baadae ndani ya hema moja kati ya mengi yaliyokuwa yamejengwa chini na mlima wa Zaron, Mfalme Luther alionekana ameketi katika kiti chake cha kifalme huku akiwa amezunguukwa na walinzi na pembeni yake alikaa binti yake mrembo na mpendwa Lilitha. Mbele yake alikuwepo mwaume mmoja aliyevaa vazi la kivita kiunoni akiwa na upanga mrefu kwenye ara yake. Huyu aliitwa Raffat kiongozi wa ulinzi wa mipaka ya ufalme wa taifa la Mfalme Luther. Raffat alikuwa akitoa taarifa mara baada ya kupewa kazi ya kumfuatilia Damon kaka yake Lilitha ambaye ni mtoto wa kiume wa mfalme Luther.

"Mfalme kama unavyojua Damon aliathirika sana kiakili mara baada ya kuupoteza ufalme wetu na watu wengi kuuwawa kipindi kile hivyo alikuwa ni mtu asiyetulia na aliwaza kisasi mda wote, kama utakumbuka katika vita ile walimuua mpenzi wake Zuzuya hivyo Damon hawezi kutulia anataka kulipa kisasi licha ya kumfungia na kumzuia asitumie nguvu zake lakini Damon amepambana amerudisha nguvu zake na kutoroka" alieleza Raffat
"Acha kueleza mambo ninayoyajua sema Raffat yuko wapi kwa sasa"
Alisema Mfalme Luther baada ya kumsikiliza Raffat kwa muda mrefu.

"Sawa Mfalme, kama utakumbuka watu waliotuvamia na kuua ndugu zetu kipindi kile mpaka sasa hawajulikani ni wa wapi ila walikuwa wamevaa vizibao vya rangi ya KIJANI, Damon amekuwa akihangaika kuzunguuka kila kona ya ulimwengu kuwatafuta kwa bahati mbaya amefika hadi Duniani. Kama tunavyojua akili ya Damon haiko sawa kabisa, kuna nchi moja iko afrika inaitwa Tanzania hivi sasa ipo katika zoezi muhimu la kuhesabu watu wanaita Sensa, watu wanaofanya zoezi hilo wanavaa reflector'/ vizibao vya kijani sawa kabisa na walivyovaa wale watu waliokuja kutuvamia. Tarehe 22 ilikuwa ni siku ya ufunguzi wa Sensa watu wengi sana wanaoitwa Makarani walivaa hivyo vizibao karibu nchi nzima kama ufunguzi wa tukio hilo la muhimu kwa nchi yao. kwa bahati mbaya siku hiyo Damon ndio alikuwa anapita akawaona. Akaweka makazi yake hapo Tanzania akiamini amewapata wabaya wake, Tarehe 23 Damon alianza kuwawinda mmoja baada ya mwingine, kila atakae muona amevaa kile kizibao Damon anamuwinda mwisho anamuua kikatiri na kumnywa damu yake. Mpaka sasa tunavyoongea Damon ameua MAKARANI watatu nchini Tanzania, anafanya kazi hii taratibu sana na kama unavyojua WANADAMU wahawezi kunyamaza kimya watataka kupambana nae na hapo mambo yanaweza kuwa magumu zaidi" Raffat alimaliza kueleza.

Mfalme Luther alisimama kwenye kiti chake mara tu baada ya maelezo hayo.
"Hectoooor" Mfalme Luther aliita na hapo akaingia jamaa mmoja wa miraba minne ambaye yeye alionekana kuwa tofauti kabisa na wengine, macho yake yalikuwa ya bluu wakati wote.
"Nipo hapa Mfalme"
"Kusanya jeshi lako haraka, nenda Dunia hakikisha unamkamata Damon na kumrudisha huku haraka" Alisema Luther lakini mara Lilitha akasimama na kupaza sauti.
"Hapana baba"
Watu wote wakageuka na kumtazama Lilitha
"Baba hatuna haja ya kutuma majeshi kwenda Dunia, tutazua taharuki kubwa na huenda wenzetu wakashindwa kutuelewe, tunaweza kuongeza tatizo ndani ya tatizo na pengine hata kudhuru WANADAMU na viumbe wengine wasio na hatia, kumbuka akili ya kaka Damon haiko sawa na siku hizi za karibu Damon ameonekana kuwa na nguvu ya ziada na hatujuo inatoka wapi, baba nitume mimi niende Duniani nakuahidi nitamrudisha kaka Damon ndani ya siku chache tu, yule ni kaka yangu hawezi kunidhuru" Lilitha aliongea kwa kujiamini sana.
Huu ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa Mfalme Luther, alimpenda sana binti yake hata siku moja alikuwa hataki kuruhusu Lilitha akae mbali naye, zipo sababu zinazomfanya Mfalme Luther kumpenda sana Lilitha sababu zinazobeba siri nzito sana katika taifa lake.

DUNIANI-AFRICA-TANZANIA
MTWARA- MASASI.

Tukio lingine la kushangaza linatokea nchini Tanzania, ukiacha yale matukio ya kufurahisha ya Makarani kuibiwa vishikwambi wengine kujinyonga na wengine kukataa kufanya kazi sasa kulikuwa na matukio mengine ya kutisha ambayo yalishika macho na masikio ya watu wengi. Ilikuwa ni mfuatano wa mtukio ya kutisha ya kuuwawa kwa MAKARANI wa sensa nchini Tanzania. Mpaka sasa kulikuwa na vifo viwili vya kutisha na vyote vinafanana. Leo tena katika hali ile ile na mazingira yale yale KARANI mwingine wa Sensa mkoani Mtwara - Masasi anakutwa ameuwawa kikatiri na mwili wake kutupwa pembezoni kwa barabara.
Hofu,simanzi na sintofahamu inatanda nchini Tanzania. Kila mmoja anakosa majibu ni nini hasa chanzo cha mauaji hayo ya kutisha. Hata serikali yenyewe inajikuta katika mazingira magumu, kabla haijamaliza kupeleleza kifo hiki mara kifo cha KARANI mwingine kinatokea. Hali inakuwa ya kutisha tena ya kutisha sana. Taratibu Makarani wengine wanaanza kuingiwa na hofu ya kufanya kazi yao jambo linalopelekea zoezi muhimu la serikali yaani Sensa ya watu na makazi kuwa gumu.
Je nini kitatokea?
FUATILIA SIMULIZI HII YENYE KISA CHA KUSISIMUA NA LOVE STORY NZURI NDANI YAKE...
Mtunzi: Saul David
Simu: 0756862047....
 
Kipande cha pili kitakuwa hewani hivi punde
20220830_211856-BlendCollage.jpg
 
Simulizi: ๐Š๐€๐‘๐€๐๐ˆ
Mtunzi:๐’๐€๐”๐‹ ๐ƒ๐€๐•๐ˆ๐ƒ
Sehemu ya 02

ILIPOISHIA...
Hofu,simanzi na sintofahamu inatanda nchini Tanzania. Kila mmoja anakosa majibu ni nini hasa chanzo cha mauaji hayo ya kutisha ya MAKARANI wa sensa. Hata serikali yenyewe inajikuta katika mazingira magumu, kabla haijamaliza kupeleleza kifo hiki mara kifo cha KARANI mwingine kinatokea. Hali inakuwa ya kutisha tena ya kutisha sana. Taratibu Makarani wengine wanaanza kuingiwa na hofu ya kufanya kazi yao jambo linalopelekea zoezi muhimu la serikali yaani Sensa ya watu na makazi kuwa gumu.

Je, nini kitafuata?

SONGA NAYO...
(UFALME WA LUTHER)
"Binti yangu" mfalme Luther aliita
"Abeeh Baba" Lilitha aliitika
"Siwezi kukuacha uende Duniani mwanangu, ni hatari sana kwako na kwa taifa letu. Vipi kama utapatwa na jambo baya huko usiweze kurudi tena nini kitatokea? kumbuka taifa letu linakutegemea sasa na baadae Lilitha" alieleza Mfalme Luther
"Baba, hilo taifa la kesho litatoka wapi kama leo nikishindwa kusimama na kulitetea, hata ikitokea nikashindwa kurudi lakini historia itaandika kuwa binti wa mfalme Lilitha alienda kupambana kwa ajili ya taifa lake na hakurudi, hii ni njema kuliko kuendelea kukaa hapa na kushuhudia ufalme wa baba yangu ukiteketea mbele ya macho yangu, hapana baba siwezi" alisema Lilitha.

"Mwanangu najua una nia ya dhati ya kupambania ufalme huu lakini hofu yangu ni kwamba wewe ndio mtu pekee unayetegemewa kuliongoza hili taifa siku zijazo, kuruhusu uondoke ni kama kuipoteza kesho yetu. Acha wengine waende mbona tunao watu wanaoweza kuifanya kazi hii tunae kamanda Hector yupo Raffat na wengine wengi acha waende wao wewe ubaki hapa kwenye taifa lako"

"Baba, kaka Damon hawezi kumuelewa mtu yeyote zaidi yangu. Kama ataenda Hector au Raffat basi tegemea vita kali huko Duniani ambayo itaathiri viumbe wengine wasio na hatia wakiwemo binadamu. Niache niende mimi baba" Lilitha alizidi kushikilia msimamo wake. Mwisho Mfalme Luther alitulia kimya huku akifikiri ajibu nini. Mara wakati huo huo mdogo wake mfalme ambaye ni baba mdogo wa Lilitha alipaza sauti na kuongea, aliitwa Cassius.

"Ewe mtukufu Mfalme tafadhali usihofu, mruhusu binti yako aende mimi nitamsindikiza hadi Duniani nitamlinda dhidi ya maadui na kuhakikisha anarudi hapa salama salmini" alisema Cassius lakini kauli hii haikumfurahisha Lilitha hata kidogo ila Mfalme Luther yeye alifurahi sana.

"Nashukuru sana mdogo wangu Cassius basi bila shaka nawaruhusu wewe na Lilitha muende Duniani hakikisheni mnafanya kila liwezekanalo kumdhibiti Damon kisha mrudi nae hapa mapema, haya kajiandaeni" alisema Mfalme Luther
Lilitha alitamani kupinga maamuzi hayo lakini tayari baba yake alishatoa maamuzi na haikuwa rahisi kumbadilisha.

Cassius alitoka nje ya hema la Mfalme huku akiwa ameachia tabasamu fulani la kinafiki sana, macho yake yalikuwa yakibadirika rangi na kuwa mekundu baadae bluu kisha yanarudi katika hali yake ya kawaida alitembea kwa majigambo na kuingia kwenye hema lake. Cassius alikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa wakiheshimika sana katika ufalme wa Luther licha ya kwamba alikuwa ni mtu mwenye tamaa na mipango yake ya chini chini ikiwa ni pamoja na kutaka kumuangusha kaka yake madarakani.
Alifika akaa kwenye kiti akachukua karatasi fulani chini ya meza akaiweka juu ya meza kisha akasogeza bakuli dogo lililokuwa na wino mweusi. Cassius alichovya kidole chake cha shahada kwenye ule wino kisha akawa anakipitisha juu ya lile karatasi. Cha ajabu licha ya kwamba kidole cha Cassius kilikuwa hakigusi lile karatasi lakini maandishi yalikuwa yakijitokeza yenyewe kwenye lile karatasi. Alichokiandika hewani kilionekana kwenye karatasi, maandishi yalisomeka hivi.

Hatimae tumepata nafasi nyingine ya kuufutilia mbali ufalme wa Luther, amemtoa binti yake mpendwa LILITHA kwenda Duniani...nitaongozana nae tafadhali naomba niandalie watu mahili watakao tufuata hadi Duniani. Kazi yetu itakuwa kuhakikisha Lilitha na kaka yake Damon hawarudi tena huku... Ni mimi CASSIUS.

Cassius alimaliza kuandika barua hiyo ambayo ilijikunja yenyewe na kujipachika kwenye kifaa maalum cha kuhifadhia barua.

"Kijanaaa" Cassius aliita na mara aliingia kijana mmoja ambae pia alikuwa amevalia nguo za kivita.
Cassius alimrushia ile barua ambayo tayari ilishajifunga kwenye kifaa chake, yule kijana akaidaka.

"Unajua kwa kuipeleka kuwa makini hakikisha hakuna anaekufuatilia" alisema Cassius yule kijana akawa anatoka mlangoni akapishana na Lilitha ambae alikuwa ndio kwanza anaingia.

"Mmh! Karibu binti Mfalme" Cassius alimkaribisha kwa tabasamu lile lile lililojaa unafiki.
"Naona bado hujaacha michezo yako michafu baba mdogo, nilishakwambia ipo siku nitathibitisha maovu yako yote mbele ya Mfalme ambae anakuamini sana kwa sababu hajui upande wako wa pili" Lilitha aliongea kwa kujiamini huku akiuma meno yake kwa hasira na macho yake yakabadilika tena na kuwa ya bluu.

"Kuwa mpole binti wewe ni mtoto wa juzi tu hapa, huna unachokijua... Jiandae twende tukamrusmdishe kaka yako asiye na akili"Alisema Cassius.

DUNIANI- TANZANIA
MTWARA- MASASI...
Ndani ya kituo cha polisi wilaya ya masasi KARANI mmoja wa kiume alikuwa akitoa ushuhuda wa kile alichokiona pindi karani mwenzake alipouawa kikatili na kiumbe cha ajabu kisha yeye kunusurika. Alikuwa amezunguukwa na jopo la polisi karibu 12 ambao walikuwa kimya wakimsikiliza.

"Ilikuwa ni saa moja jioni kuelekea saa mbili mimi nilikuwa nimemaliza eneo nililopangiwa siku hiyo nikapitia kwa KARANI mwenzangu ambae nilimkuta anamalizia kuhoji kaya ya mwisho baada ya hapo tukaongozana kurudi makwetu, tukiwa tumefika pale maeneo ya josho kwenye miti mingi mara kwa mbali tulimuona mtu akiwa amesimama katikati ya barabara. Alikuwa ametanua miguu yake na uso wake ulikuwa ukiangalia chini. Eneo alilokuwa amesimama kulikuwa na mwanga ambao hatukuelewa umetoka wapi. Mwanzo tulio kawaida tukahisi labda ni mlevi yupo na tochi lakini kadri tulivyo sogea ndivyo ule mwanga unaomzunguuka ulizidi kuongezeka. Baadae tukasikia sauti kubwa ikisema NITAWAUA WOTE, WOTE NINYI MLIOHUSIKA, NITAWAUA NA KUWANYWA DAMU YENU MMOJA BAADA YA MWINGINE Baada ya kusema hivyo yule mtu linyanyua uso wake na kututazama, macho yake yalikuwa yanatoa mwanga mwekundu mimi na rafiki yangu tuliogopa sana tukageuka haraka na kuanza kukimbia lakini yule kiumbe alikuwa na spidi ya ajabu sana alitupita kwa kasi na kusimama tena mbele yetu, tulikuwa tunapiga kelele kuomba msaada lakini hakuna mtu aliyejitokeza kutusaidia. Tuligeuka tena na kuanza kukimbia lakini yule kiumbe alikuwa ni kama anatuchezea alikuwa nakuja kwa kasi na kusimama mbele yetu tena, akawa anacheka sana kisha akasema na kulitaja jina la rafiki yangu LEO NI ZAMU YAKO JENNIFER baada hapo alikuja kwa kasi na kumkaba shingoni Jennifer kisha akamuinua juu, mimi nilipata nafasi nikakimbia sikuelewa tena kilichoendelea hadi pale nilipopata taarifa kuwa Jennifer amekutwa akiwa ni maiti" Yule karani alimaliza kueleza huku machozi yakimtoka.
Kimya kilitawala kwa muda polisi wote wakawa kimya huku wakijaribu kuyatafakari maelezo hayo. Ilikuwa ni kesi ngumu sana kwao ambayo hawakuwahi kukutana nayo katika kipindi chote cha utendaji wao.
Kwa maelezo yale ya Karani ilikuwa ikionyesha moja kwa moja matukio ya kuuawa kwa Makarani wa sensa yanahusishwa na nguvu za giza.

"Kwa hiyo tablets/vishikwambi mlivitupa wapi?" Askari mmoja ambae kwa muonekano tu alikuwa tayari ametupia chupa ya bia si chini ya tatu aliuliza wote wakageuka na kumtazama
"Afande hebu jitahidi kuwa serious kidogo, watu wanakufa wewe unauliza habari za vishikwambi kweli?"
Askari mwingine akadakia.
"Kwani we huoni Viongozi wanavyotushinikiza tuvipate hivyo vishikwambi kwanza, serikali yenyewe inajali vishikwambi kuliko hata maisha ya Makarani, kwanza mmelipwa hela zenu eti we kijana?" Yule askari aliuliza swali jingine.
"Hebu mtoeni Afande Godfrey hapa, mtoeni upesi, sijui kwa nini sijawahi kutana na God mwenye akili" alifoka askari mmoja ambae alikuwa mkubwa kicheo kuliko wenzake. Baadae afande Godfrey alitolewa huku akiwa bado anaongea maneno yasiyoeleweka.
"Hebu tuambie vizuri, huyo mtu alikuwa anaonekanaje, mfano sura yake uliweza kuiona?"
"Hapana sikuweza kuiona sura yake nachoweza kukumbuka ni kuwa macho yake yalikuwa yanatoa mwanga mwekundu" alieleza Karani
"Na vipi, kipi kingine alisema?"
"Hakuna ni hivyo tu kama nilivyo eleza mara ya kwanza alisema nitawaua wote, na mara ya pili aliongea akisema leo ni zamu yako Jennifer"

Ilikuwa ni kesi iliyoumiza sana vichwa vya polisi hawa ambao mpaka sasa walikuwa wakisubiri kuongezewa nguvu na kikosi kingine cha polisi waliokuwa njiani kuja wakiongozwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Solomoni na wanajeshi kutoka kambi jirani ya Kirungu. Tayari mpaka sasa Makarani watatu wa sensa ya watu na makazi walikuwa wameuwawa kikatili sana. Mbaya zaidi polisi hawakuwa wamefanya jambo lolote ambalo angalau lingeleta matumaini ya kumkamata muuaji. Hakuna aliyekuwa akijua wala kuhisi uwepo wa kiumbe wa ajabu kutoka ulimwengu mwingine Damon.

(UFALME WA LUTHER)...
Farasi zaidi ya 20 walionekana wakikimbia kwa kasi katika njia nyembamba iliyokuwa ikikatisha katikati ya msitu mnene. Msafara huo kutoka kwa Malme Luther ulikuwa ukiongozwa na Lilitha pamoja na baba mdogo wake Cassius. Sasa ulikuwa umewadi mda wa wao kuondoka katika ulimwengu wao kuja Duniani kwa ajili ya kuhakikisha wanamdhibiti Damon na kurudi nae katika ulimwengu wao. Watu wengine waliokuwa katika msafara huo walikuwa ni askari maalumu walioagizwa na Mfalme Luther kuhakikisha wanamsindikiza Lilitha na baba mdogo wake hadi lilipo langu kuu la kutoka ulimwengu mmoja kuingia ulimwengu mwingine.
Farasi walikuwa wakikimbia kwa kasi sana huku bendera zenye nembo ya ufalme wa Luther zikiwa zimeinuliwa juu.

Wakiwa wanendelea na safari hiyo, kwa mbali juu ya mlima mmoja mdogo walionekana watu wengine sita wakiwa juu ya farasi. Walikuwa wamesimama wanautazama msafara wa binti Mfalme Lilitha uliokuwa ukipita kwa kasi kwenye njia iliyokatisha chini ya mlima huo.
Watu hawa walikuwa wa ajabu sana kwanza walivaa mashuka meusi yenye kofia kubwa juu lakini sura zao zilikuwa hazionekani yaani kichwa kilikuwa ni giza tupu. Ndani ya zile kofia hakukuwa kichwa cha mtu lilionekana giza tu lakini viungo vingine vya mwili kama mikono na miguu vilionekana kama kawaida. Hawa ndio wale watu ambao Cassius aliwaandikia barua akiwataka waambatane nae hadi Duniani kuhakikisha wanamuangamiza Lilitha na kaka yake Damon wasiweze kurudi kwenye ufalme wa baba yao Luther.
Baada ya muda msafara wa binti Mfalme Lilitha ulipita wote. Wale watu sita walitazamana kisha mmoja wao akaongea kwa sauti nzito na ya ajabu sana.
"Ni muda muafaka tunaweza kwenda sasa"
Baada ya kusema hivo mara sura za wale watu zilichomoza ghafula zikawa zinaonekana, walikuwa ni watu wa ajabu sana, weusi tii na macho yao yalikuwa ni mekundu. Walianza kuendesha farasi zao wakataremka kwa kasi sana hadi walipoifikia ile njia ulipopita msafara wa binti Mfalme. Nao wakaanza kufuata kuelekea kule Lilitha na watu wake walikoelekea.

Je, nini kitafuata?
ITAENDELEA...
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
Simulizi: ๐Š๐€๐‘๐€๐๐ˆ
Sehemu.........03
Mtinzi: ๐’๐š๐ฎ๐ฅ๐ƒ๐š๐ฏ๐ข๐
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Hali ya sintofahamu inatanda nchini Tanzania kutokana na mfurulizo wa matukio ya kuuawa kwa Makarani wa Sensa. Nchi yote inageuzia macho na masikio yake katika mkoa wa Mtwara ambako ndiko hasa matukio ya kuuawa kwa Makarani watatu yametokea.
Upande wa pili Lilitha Binti Mfalme akiambatana na baba yake mdogo wako njiani kuelekea lango kuu la kutoka na kuingia Dunia nyingine ili kuja kumzuia Damon ambae ndiye kiumbe anaehusika na maauaji ya Makarani hao. Lakini pasipo kujua kuwa lengo la baba mdogo si kumsaidia Lilitha bali anamipango mingine tofuauti ya kuhakikisha Lilitha na kaka yake Damon wanafia Duniani na hawarudi katika tena ulimwengu wao.
Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA...

"Nawaomba watanziania wenzangu tuwe watulivu, serikali imeshaiona changamoto hii tuliyokutana nayo kule Mtwara. Niwatoe hofu Makarani wetu kuwa tayari serikali inalifuatulia na kulitazama jambo hili kwa jicho la tatu. Endeleeni kufanya kazi kama ilivyokuwa awali ili tulimalizie zoezi hili muhimu kwa taifa letu. Tumeimarisha ulinzi hasa kwa Makarani wetu wa Mtwara na tupo kwenye hatua madhubuti za kumkamata muuaji. Makarani endeleeni kufanya kazi yenu, wananchi ambao bado hatujahesabiwa basi tukae majumbani tusubiri kuhesabiwa"
Hii ilikuwa ni tangazo maalum lililoandaliwa na serikali kwa ajili ya kuwatoa hofu Makarani na wananchi wote wakati wao wakiendelea na jitihada za kuhakikisha wanadhibiti mauaji hayo.

Majira ya saa 11 jioni Damon alionekana akizurula zurula nje ya maeneo ya hospitali ya wilaya ya Masasi. Muonekano wake ulikuwa ni sawa kabisa na Binadamu wa kawaida, wala hakuwa na tofauti yoyote na hii ndio sababu iliyowapa ugumu polisi kuweza kumtambua na kumkamata. Licha ya polisi kumwagika kila upande nje na ndani ya mkoa lakini bado jitihada zao hazikuzaa matunda.
Damon alitembea hadi lilipo geti kuu la kuingia ndani ya hospitali hiyo, akaingia. Alikuwa akipishana na watu wengi aliokuwa wakiingia na kutoka ndani ya hospitali hiyo kubwa. Damon alionekana kumfuatilia mtu mmoja ambae aliingia ndani ya hospitali hiyo mda mfupi uliopita. Mtu huyo alivaa kijikoti/ kizibao cha kijani kama ilivyokuwa kwa MAKARANI wa sensa, naam huyu nae alikuwa ni karani vilevile.
Akili ya kiumbe huyu wa ajabu Damon ilimchukia na kutamani kuinywa damu ya mtu yeyote aliyevaa aina hiyo ya kizibao. Alikuwa ameathirika kisaikolojia hasa baada ya kumpoteza mpenzi wake aliyempenda sana Zuzuya katika vita kali ambayo Mfalme Luther alijikuta akishambuliwa vikali na kupoteza watu wengi sana. Kila wakati Damon alipomuona KARANI akiwa na lile vazi la kijana aliikumbuka siku hiyo na kujikuta anatamani kuua.
Damon alikua alifanya mauaji yake usiku mara tu baada ya jua kuzama, hakuwa na uwezo wa kufanya chochote mchana wa jua kali lakini pindi jua linapozama ndipo hapo Damon humfuata mtu aliyedhamilia kumuua siku hiyo.
Leo ilikuwa ni zamu ya KARANI huyu anaeitwa Yohana ambae aliingia hospitali kwa ajili ya kuifanya kazi yake bila kujua kuwa anafuatiliwa na kiumbe wa ajabu Damon tangu mda mrefu sana.

Damon aliendelea kutembea kuzunguuka maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo huku akiwa makini na Karani ambae kwa sasa alikuwa ndani ya ofisi ya mganga mkuu wa hospitali hiyo wakifanya mahojiano.
Mwisho Damon alitembea na akafika hadi wodi ya wazazi, akaingia pasipo kuonekana na mtu yeyote.
Damon aliangaza macho yake huku na huku mbele yake alimuona mtoto mchanga akiwa amelazwa kwenye kitanda chake kidogo maalumu kwa watoto wachanga mara tu baada ya kuzaliwa. Kwa bahati mbaya wakati huo hakukuwa na mtu yeyote, nesi alikuwa chumba kingine akiwa amemsindikiza mama aliyetoka kujifungua dakika chache zilizopita.
Damon alimtazama yule mtoto mchanga kisha akatabasamu. Akasogea karibu kabisa na kile kitanda akawa anayachezea mashavu ya yule mtoto.

Damon alingaza tena macho yake huku na huku, hakuona mtu haraka alijing'ata kidole chake cha mwisho mkono wa kushoto kwa nguvu. Mara damu yenye rangi ya bluu ikawa inamtoka, Damon alielekeza kile kidole chake kwenye mdomo wa yule mtoto mchanga ambae alifungua mdomo wake kisha akanyonya damu kiasi iliyokuwa ikitoka kwenye kidole cha Damon.
Mara hiyo macho ya yule mtoto mchanga yalitoa mwanga wa bluu kisha yakarudi katika hali yake.

"We kaka unafanya nini hapo? Imekuwaje umeingia humu jamani?" Sauti ya nesi ilisikika akifoka kutokeo nyuma ya Damon.
"Hebu toka nje basi humu wanaume huwa hawaingi jaribu kuwa mstaarabu basi naomba unipishe tafadhali" alisema yule nesi na hapo Damon aligeuka na kuanza kupiga hatua kuondoka.
Akapishana na yule nesi bila kuzungumza chochote akafungua mlango na kutoka nje. Yule nesi alimsindikiza kwa macho hadi Damon alipopotea, alibaki na maswali yasiyo na majibu lakini mwisho alisogea kumchungulia mtoto pale kitandani akaona yuko salama.

Nesi aliendelea na kazi nyingine lakini mara ghafula alishtushwa na kilio kikali kutoka kwa yule mtoto, kilichomshtua nesi sio kilio cha mtoto bali ni aina ya sauti aliyoitoa mtoto, ilikuwa ni sauti nzito tofuauti kabisa na sauti ya mtoto mchanga. Mara ghafula kukawa kimya tena.

Nesi alipiga hatua hadi pale alipo yule mtoto, alipomtazama tu nesi alitoa macho na kushika mdomo wake kwa mshangao mkubwa. Yule mtoto alikuwa amebadirika sana, hakuonekana tena kama mtoto mchanga bali mtoto ambae kwa kumtazama alikuwa sawa na mtoto wa mwaka mmoja, hata meno tayari yalishaota.

Nesi akiwa katika hali ya mshangao hapo aliona kitu kingine cha ajabu. Yule mtoto alionyesha ishara fulani kwa kupeleka mkono mdomo huku akimtazama usoni. Ilikuwa ni ishara inayoonyesha kuwa ananjaa nahitaji chakula.

Hapo nesi alipiga kelele iliyopasua anga na kusikika karibu maeneo yote ya hospitali hiyo kisha akatimua mbio na kutoka kwa kasi nje ya wodi ya wazazi.

Dakika chache baadae watu waliozisikia kelele hizo walianza kusogea huku wakitamani kujua ni nini kinaendelea. Yule nesi ambae kwa sasa alikuwa akitetemeka kwa hofu alianza kueleza tukio zima na kuwaacha watu midomo wazi. Haikuwa rahisi kuamini hata kidogo maelezo ya yule nesi. Lakini licha ya kutokuamini lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu kwenda kuhakikisha maneno ya yule nesi.

Dakika chache baadae mganga mfawidhi alionekana anasogea eneo hilo huku nyuma yake akifuatiwa na KARANI Yohana pamoja na wahudumu wengine wa hospitali hiyo.

"Kuna nini?" Aliuliza daktari
"Nesi wako anadai kuna mtoto kazaliwa dakika chache tu lakini kabadili na kukuwa kwa haraka na anatoa sauti kama mtu mzima" alieleza mtu mmoja.

"Yuko wapi?" Aliuliza Daktari
"Wodini, daktari usiende ita polisi kwanza yule mtoto ni wa ajabu sana. Ila kuna kaka mmoja aliingia wodini pengine...." Yule nesi alieleza lakini alishindwa kumalizia sentesi yake kwani tayari daktari alikuwa anaondoka huku akionekana kukasirika sana. Daktari alionekana sio mtu wa mzaha na alikuwa hapendelei kuona matukio ya ajabu kwenye hospitali yake kitendo cha watu kukusanyika kisha kuanza kujadili kitu ambacho aliamini halina uhalisia kilimuuzi sana.

Alipiga hatua kuelekea wodi ya wazazi huku nyuma akifuatiwa na kundi dogo la watu ambao aliwaacha kama hatua tatu hivi nyuma yake. Karani Yohana nae alikuwa ni miongoni mwa watu waliokusanyika kushuhudia tukio hilo na kwa bahati mbaya hakuwa amemaliza mahojiano na mganga mkuu wa hospitali hiyo. Walikatishwa mazungumzo mara tu baada ya kupata taarifa za mtoto wa ajabu wodi ya wazazi.
Wakati hayo yakiendelea kwa mbali Damon alionekana akiwa amesimama nyuma ya mti huku akiwatazama watu walikuwa wamekusanyika eneo hilo kushuhudia tukio la ajabu la mtoto aliyemnywesha damu yake. Damon yeye hakujali hilo macho yake yote yalikuwa kwa Karani Yohana. Ilikuwa imebaki dakika chache sana kabla ya jua kuzama hapo ndipo Damon alipanga kuifanya kazi yake kwa Karani Yohana ambae hadi dakika hiyo alikuwa haelewi hili wala lile.

Daktari akiwa amekaribia kufika ulipo mlango wa kuingia wodi ya wazazi mara ghafula muungurumo mkali na wa ajabu ulisikika kutoka ndani ya wodi hiyo, kufumba na kufumbua mlango ulifungua kwa kasi akatoka mwanamke mmoja akiwa uchi bila nguo yoyote. Akakimbia na kumvaa Daktari akamnyanyua juu na kumtupa pembeni kisha akaendelea kukimbia akipenya katikati ya watu ambao nao walianza kutimua mbio na kutawanyika huku wakipiga kelele.
Mwanamke huyo alikuwa ni yule yule mtoto ambae sasa alikuwa amekuwa na kuwa mtu mzima ndani ya dakika chache sana. Alionekana mwanamke kama wa miaka 18 hivi. Alitisha kwa kumtazama, alikuwa na nywele na kucha ndefu sana. Mdomo mwekundu na macho mekundu pia.
Nguvu zake zilikuwa za ajabu sana, alimnyanyua Daktari na kumtupa pembeni kirahisi sana, kama karatasi.
Mtu huyu alikimbia huku akitoa muungurumo wa ajabu akaruka ukuta na kutokea upande wa pili akatokomea kwenye msitu mdogo ulikokuwa jirani na hospitali hiyo.

Watu waliendelea kukimbia na kupiga kelele za hofu miongoni mwa watu hao alikuwepo Karani Yohana ambae yeye alikimbia kwa kasi sana akatoka nje kabisa ya hospitali hiyo, alikuwa ametupa kishikwambi/tablet chake na wala hakukumbuka kilipo.
Yohana aliogopa sana mara baada ya kumuona mwanamke yule wa ajabu, hofu yake ilikuwa ni kubwa zaidi hasa baada ya kukumbuka kuwa Makarani wenzake watatu wamekufa na inadaiwa kuwa wameuliwa na kiumbe wa ajabu. Aliona kabisa kuna kila dalili ya yeye kuuwawa na kiumbe huyo kwani katika kundi zima la watu waliokuwepo eneo hilo karani alikuwa ni yeye pekee.
Haraka Yohana alivua kizibao chake cha ukarani akiamini pengine inaweza kumsaidia asigundulike na kiumbe huyo wa ajabu. Wakati akifanya hivyo mara ghafula kufumbua na kufumbua akamuona mtu amesimama mbele yake, wala hakujua ni wapi ametokea, naam mtu huyu hakuwa mwingine bali Damon. Na sasa tayari jua lilikuwa limeshazama.

Upande wa pili katika msitu alikokimbilia yule mwanamke wa ajabu kutoka hospitalini njiani alikutana na bibi kizee mmoja ambae alikuwa ametoka bustanini akiwa na jembe lake begani. Ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu usiku bibi kizee alishangaa kukutana na kiumbe huyo wa ajabu akiwa uchi wa mnyama. Bibi aliogopa sana kwa namna kiumbe huyo alivyokuwa akitisha. Alibaki amesimama huku akitetemeka kwa hofu hakuwa na uwezo wa kunyanyua mguu kusogea mbele au kurudi nyuma hata hatua moja, mwili wake wote ulikuwa umeshikwa na ganzi.

Yule mwanamke wa ajabu alianza kupiga hatua taratibu kumsogelea yule bibi kizee huku akijirambaramba midomo ikiwa ni ishara tosha kuwa kiumbe huyu alikuwa na kiu ya damu.
Akiwa amebakiza hatua kama kumi kumfikia yule bibi kizee mara ghafula mbele yake kilitua kitu cha ajabu kikitokea juu na kusababisha mtikisiko mkubwa na vumbi jingi lililopaa angani.
Yule kiumbe alisimama ghafula, nae pia alionekana kushtuka hakujua ni nini hasa kimetokea lakini mara baada ya kutazama kwa umakini aliona watu wawili wakiwa wamesimama mbele yake huku macho yao yakitoa mwanga wa bluu. Watu hawa hawakuwa wengine bali Lilitha na baba yake mdogo Cassius, tayari walikuwa wamevuka na kuingia Duniani.
Yule kiumbe alilia huku kipigapiga kifua chake akatoa muungurumo mkubwa uliosikika karibu kila kona ya mji wa Masasi hofu ikazidi kutanda kwa watu walioisikia sauti hiyo.
Tukio hilo liliwafanya Lilitha na baba yake mdogo watazamane, kawati huo tayari yule bibi kizee alikuwa amedondoka chini na kupoteza fahamu kwa hofu mara tu baada ya Lilitha na Cassius kutua mbele yake.
Sauti na muungurumo wa yule mwanamke wa ajabu ilipenya vizuri kwenye masikio ya Damon ambae aligeuka ghafula na kuangalia upande sauti hiyo ilipotokea, ni kama alihisi kitu ambacho sio cha kawaida. Wakati huo Karani Yohana alikuwa bado amesimama wima akiwa hamuelewi kabisa mtu aliyepo mbele yake, hofu ikazidi kumjaa.

ITAENDELEA...
0756862047
 
shukran mkuu,tuendelee please
 
Simulizi: KARANI
Sehemu.........04
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Sauti na muungurumo wa yule mwanamke wa ajabu ilipenya vizuri kwenye masikio ya Damon ambae aligeuka ghafula na kuangalia upande sauti hiyo ilipotokea, ni kama alihisi kitu ambacho sio cha kawaida. Wakati huo Karani Yohana alikuwa bado amesimama wima akiwa hamuelewi kabisa mtu aliyepo mbele yake, hofu ikazidi kumjaa.

SASA ENDELEA...
Lilitha na baba yake mdogo walitazamana kisha wakageuka tena na kumtazama yule kiumbe wa ajabu.
"Hii ni kazi ya kaka yako Damon ameshaanza kuleta madhara kwa binadamu" Alisema Cassius
"Inabidi tumdhibiti yeye na kila kitu alichoharibu" alijibu Lilitha
"Kwa hiyo tunamfanyaje huyu kiumbe mbele yetu?"
"Tumuue na kumpoteza kwenye uso wa Dunia"
"Sawa twende kazi kuwa makini, bila shaka anazo nguvu za Damon ndani yake" Alisema Cassius na hapo yeye na Lilitha walitawanya mikono yao na mara miale ya ajabu ikatokea kwenye mikono yao. Mkono wa kulia wa Lilitha ilitokea fimbo inayotoa mwanga wa bluu yenye ncha nyekundu wakati huo mkono wa Cassius ulikuwa ukitoa uteute wenye rangi nyekundu uliokuwa ukivuja na kudondoka chini kisha kuzalisha moto.
Bila kuchelewa Cassius na Lilitha wote kwa pamoja walinyoosha mikono yao ya kulia mbele kwa nguvu, mara vikatoka vitu vya ajabu mfano wa vimondo vikimuelekea yule kiumbe wa ajabu mwanamke aliyenyweshwa damu na Damon.
Haikuwa rahisi kama walivyofikiri, yule kiumbe aligeuka kwa namna ya ajabu akavikwepa vile vitu vilivyorushwa kisha kabla havijafika mbali akavigeuza na kuvirudisha tena vilipotoka yaani kwa Lilitha na Cassius ambao walipigwa na kudondoka chini kila mmoja upande wake.
Yule mwanamke wa ajabu alijipiga piga tena kifuani kisha akatoa muungurumo mkubwa kwa mara nyingine, wakati huo meno yake yaliongezeka na kuwa marefu kisasi cha kutokeza hadi nje ya mdomo wake. Baada ya hapo yule kiumbe alikimbia kwa kasi na kutokomea msituni.

"Uko sawa Lilitha?" Aliuliza Cassius huku akijikongoja kuinuka.
"Niko sawa" Lilitha alijibu huku akimtazama baba yake mdogo Cassius kwa macho ya dharau, yeye na baba yake mdogo walikuwa hawaendani kabisa licha ya kuja wote duniani lakini Lilitha alikuwa akimchukia sana Cassius kama sio shinikizo la baba yake Mfalme Luther basi asingekubali kuja nae huku duniani.
Lilitha aliinama na kuikota fimbo yake ambayo ilikuwa imebadilika rangi na kuwa nyeusi mara baada kudondoka chini lakini alipoiokota ikawa tena nyeupe. Bila kupoteza muda Lilitha alianza kukimbia kwa kasi akielekea kule alikokimbilia yule mwanamke wa ajabu.
Muda mfupi baadae yule kiumbe alionekana akikimbia katikati ya barabara ya lami, ilikuwa ni usiku majira ya saa mbili. Mara ghafula pasipo kutegemea, kuna mtu alitokea pembeni ya barabara na kumva yule kiumbe kwa kasi wakaanguka chini kwa pamoja, huyu hakuwa mwingine bali Lilitha binti mfalme.
Sasa alikuwa makini sana kukabiliana na yule kiumbe ambae alionekana kuwa na nguvu kama alivyo kaka yake Damon. Wakiwa katikati ya barabara Lilitha alimgeuza yule kiumbe na kumkalia kwa juu. Kisha bila kuchelewa alichukua fimbo yake na kuiweka shingoni mwa yule kiumbe Kisha akaikandamiza kwa nguvu sana. Yule kiumbe akawa anatapatapa huku akirusharusha miguu yake, sasa hakuwa na ujanja tena Lilitha alikuwa amembana vilivyo.

Haukupita muda yule kiumbe alilegea na kuishiwa nguvu kabisa. Mara ghafula taa za basi lililokuwa likija kwa kasi liliwamulika Lilitha na yule kiumbe waliokuwa katikati ya barabara. Hili lilikuwa ni basi Super Feo kutoka songea kuja Mtwara. Dereva pamoja na baadhi ya abilia walipigwa na butwaa baada ya kuona viumbe wa ajabu wakiwa wamelaliana katikati ya barabara.
Kwa kasi aliyekuwanayo dereva wa basi hilo ilikuwa ni ngumu sana kuwakwepa au kufunga breki kabla hajawafikia Lilitha na kile kiumbe pale walipo. Hali ilitisha mno.

Upande wa pili ndani ya kituo cha polisi cha wilaya ya Masasi. Walionekana polisi watatu wakiwa wamekaa huku kila mmoja akiwa mwenye mawazo sana. Walikuwa wakisubiri taarifa kwa hamu kubwa kutoka hospitali ya wilaya Mkomaindo ambako ilidaiwa kuna kiumbe cha ajabu kimeonekana huko ndani ya wodi ya wazazi. Polisi karibu wote walikuwa wameondoka kuelekea eneo hilo sasa alibaki mkuu wa kituo Inspekta Onyango akiwa na polisi wengine wawili ambao wao walikuwa wakisubiri taarifa kwa hamu kutoka kwa wenzao walioondoka.

"Kijana mbona unaniangalia sana vipi?" Aliuliza Inspekta Onyango huku akimuangalia askari mmoja ambae ni kijana mdogo aliyekuwa hapo kwa ajili ya mafunzo na si mfanyakazi(field)
"Aah! Ha hakuna shida mkuu" Alijibu kijana huyo huku akionekana kuwa na kigugumizi kiasi, aliitwa Pater.
"Sema tu unajua kila mtu kachoka hapa, haya matukio yanatuchanganya sana mawazo yako yanaweza kutusaidia kuwa na amani Pater" Onyango alisisitiza
Kauli hiyo ilimfanya Pater ajisikie amani kidogo kuzungumza, akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake simu janja(smartphone) akaibonyeza mara kadhaa kisha akasogea hadi alipo mkuu wa kituo Inspekta Onyango akakaa pembeni yake na kumpa ile simu.

"Ona mkuu, hii ni Simulizi ambayo niliwahi kuisoma miaka mitatu iliyopita kipindi niko nasoma sekondari. Hii hadithi iliandikwa na jamaa mmoja anaitwa Alex Millazo na hii ni Page yake inaitwa Hadithi za KING Wamillazo lakini cha ajabu ni kwamba hadithi hii inafanana kabisa na matukio yanayoteka sasa ya kuuawa kwa Makarani wa sensa" Alieleza Pater huku akiendelea kuperuzi kwenye mtandao wa Facebook.

"Unamaana gani Pater" aliuliza Onyango huku akiwa hajamuelewa kabisa Pater.
"Ni ngumu kuamini mkuu lakini kuna mambo yameandikwa kwenye hii hadithi yanafanana sana na haya matukio ya hapa mjini Masasi. Hii stori inaitwa MSIMAMIZI inaelezea kiumbe cha ajabu kilichokuja Duniani na kuaanza kuua wasimamizi wa zoezi la UCHAGUZI hapa nchini, yaani hadithi hii inavyoelezea namna wasimamizi walivyokuwa wanauawa ni sawa kabisa na hawa MAKARANI wa sensa sasa hivi" Pater aliendelea kueleza.

"Hahahah! We kijana kweli umevurugwa kwa hiyo unataka kusemaje?" Inspekta Onyango alicheka na kisha akauliza swali.
"Yaani unataka kusema mtu anaeuwa huenda akawa ni huyo Alex Wamillazo au?" Yule askari mwingine aliuliza huku nae akimuangalia Pater usoni na kutabasamu. Ni kweli maelezo ya Pater hayakuwaingia akilini hata kidogo lakini ajabu ni kwamba Pater alionyesha kumaanisha anachokisema.

"Mkuu hebu sikia, kwenye hii hadithi hata majina ya watu waliouawa ni sawa kabisa na hawa wa sasa hivi. Mfano Msimamizi wa kwanza kufa kwenye simulizi anaitwa Anitha, hata sasa hivi Karani wa kwanza kufa anaitwa Anitha, Wa pili aliitwa Abdullah hata huku ni hivo hivo pamoja na Karani wa tatu kufa anaitwa Jennifer hata kwenye hii simulizi Msimamizi wa tatu kufa anaitwa Jennifer. Mkuu huoni kama kuna kitu hakipo sawa hapa?" Maneno haya ya Pater kidogo yalionyesha kumuingia Inspekta Onyango japo kwa kiasi.
"Lakini Pater huwezi kuhusianisha matukio ya sasa hivi na hizo stori zako za mtandaoni hebu achana na hayo mambo ya kufikirika mdogo wangu"
"Mkuu lakini hata haya matukio yanayotokea hivi sasa ni mambo ya kufikirika pia, nani anajua huyo kiumbe alivyo ni mtu au ni jini?" Aliuliza Pater
Kimya kilitawala kwa muda kisha Onyango akauliza.
"Enhe mtu wa nne kufa kwenye hii stori yako ni nani?"
"Anaitwa Yohana, Yohana kutoka mbeya" alijibu Pater na mara hiyo simu ya Inspekta Onyango iliita haraka akamrudishia Pater simu kisha akapokea yakwake na kuiweka sauti kubwa(loudspeaker)

"Ee nambie afande Charles nini kinaendelea huko hospitali"
"Mkuu mambo ni magumu sana, kuna KARANI mwingine ameuawa mda mfupi uliopita kisha mwili wake kutupwa barabara na aina ya mauaji ni ile ile, tumempoteza Karani mwingine wa nne mkuu" Sautu hii kutoka upande wa pili wa simu ilionekana kumnyong'onyesha Inspekta Onyango.
"Nini kingine mmepata afande"Aliuliza inspekta Onyango kwa sauti isiyo na matumaini
"Hakuna mkuu, lakini jirani na ulipotupwa mwili wa huyu karani ndipo ilipo hospitali ambako inasemekana kuna kiumbe wa ajabu alionekana huko, nilitaka nikupe kwanza taarifa hii mkuu nitakupigia tena kwa wakati mwingine" alieleza yule askari. Inspekta Onyango alitaka kukata simu lakini alitazamana na Pater usoni hapo akakumbuka jambo.

"Hebu usikate kwanza simu afande" alisema Onyango
"Ndio nakupata mkuu, kuna maagizo zaidi"
"Hapana, nataka kujua jina la huyo Karani aliyekufa anaitwa nani jina la kwanza"
"Mmh hebu subiri sekunde chache...mmmh anaitwa...anaitwa YOHANA"
Kauli hii ilimfanya Pater, Inspekta Onyango na yule askari mwingine watazamane. Kulikuwa na kila dalili ya kile alichokisema Pater kuhusu simulizi aliyosoma mtandaoni ni ukweli mtupu

Je, nini kitatokea?
Kuna siri gani nyingine hapa?
Damon yuko wapi?
Vipi kuhusu vita ya Lilitha na yule kiumbe wa ajabu?

ITAENDELEA...
0756862047
 
USIACHE KUFUATILIA SIMULIZI ZANGU ZINAZOENDELEA HUKU JAMII FORAM

1. DO NOT SHOUT - usipige kelele
2. THE MODERN WAR- Vita ya kisasa
3. STAY WITH ME- baki na mimi
4. KARANI
 
Simulizi: KARANI
Sehemu yaโ€ฆโ€ฆ.05
Mtunzi: Saul David
whatsApp: 0756862047

ILIPOISHIAโ€ฆ
Pater anatoa maelezo ya ajabu yanayoonekana kuwashangaza polisi wenzake kuhusu mfanano wa matukio aliyosoma kwenye simulizi moja mtandaoni na matukio yanayoendelea hivi sasa kuhusu kuuawa kwa MAKARANI wa sensa. Jambo la ajabu zaidi ni kwamba hata majina ya watu waliokuwa wakiuawa kwenye simulizi hiyo ni sawa kabisa na wanao uawa hivi sasa.
Upande wa pili Lilitha binti mfalme anapambana vikali na mwanamke ambae ni kiumbe wa ajabu aliyepatikana mara baada ya kunywa damu ya Damon..

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEAโ€ฆ
Baada ya kuona kuna basi linakuja kwa kasi na wao wako katikati ya barabara haraka Lilitha alimshika yule kiumbe wa ajabu wakaviringita wote kwa pamoja hadi pembeni ya barabara na mara hio basi likapita kwa kasi, alimanusra wagongwe wote wawili. Kutokana na mshtuko aliokuwa nao dereva wa basi hilo alijikuta anashindwa kustahimili kuendelea kuushikilia usukani hasa baada ya kujaribu kufunga breki ghafula na kuwakwepa viumbe wale wa ajabu barabarani. Hili lilikuwa ni kosa kubwa kwani basi iliacha barabara na kuingia msituni, mbaya zaidi kulikuwa na korongo kubwa kule ambako basi lilikuwa likielekea. Abilia walipiga kelele kwa hofu na wengine kuanza kuomba kila mmoja kwa imani yake kwani ilikuwa ni wazi kuwa kilichokuwa kinakwenda kutokea ni ajari mbaya sana ya gari na kwa namna korongo lilivyokuwa refu ama kwa hakika hakuna hata mmoja anaweza kupona.

Dereva alijitahidi kufunga breki lakini wapi hakuna kilichobadilika. Lilitha akiwa bado pembeni ya barabara aliiona hatari kubwa ya kupoteza maisha iliyokuwa ikiwanyemerea binadamu waliokuwa ndani ya basi hilo. Haraka bila kupoteza muda Lilitha aliachana na yule kiumbe wa ajabu akakimbia kwa kasi, kufumba na kufumbua tayari alikuwa mbele ya lile basi akawa anajaribu kulizuia kwa nguvu zake zote. Dereva pamoja na baadhi ya abilia waliokuwa siti za mbele walishuhudia tukio hilo la mwanamke mrembo na wa ajabu aliyekuja ghafula na kusimama mbele ya basi kisha kuanza kulizuia lisiingie kwenye korongo.

Nguvu aliyoitumia Lilitha ilikuwa ni nguvu ya ajabu mno kiasi cha kumfanya macho yake yawe mekundu huku mwili wake ukionekana kama unawaka moto.
Baada ya muda kidogo mwisho basi lilisimama huku likiwa limebakiza hatua kama mbili kuingia kwenye lile korongo refu.
Baada ya kutoa msaada huo kwa binadamu Lilitha alipotea ghafula mbele ya lile basi hakuna aliyemuona tena, alitoweka.
****
Upande wa pili yule kiumbe mwanamke wa ajabu alionekana akitembea kwa kujivuta vuta akiwa katikati ya ile barabara ya lami, tayari Lilitha alikuwa amemjeruhi vibaya sana hakuwa na nguvu zozote za kumbia ama kwenda mbali. Alipopata mwanya baada ya Lilitha kumuacha na kwenda kusaidia binadamu waliopo ndani ya lile basi yeye aliinuka kwa kujikongoja na kuanza kuondoka.

Baada ya mwendo kama wa dakika saba hivi ghafula bila kutegemea Lilitha alitokea tena mbele yake akivuma kwa kasi kama upepo, alikuwa na ile fimbo nyeupe mkononi mwake. Lilitha hakuwa na muda wa kujiuliza mara mbilimbili haraka aliinyosha ile fimbo yake kumuelekea yule mwanamke. Mwanga kama radi ulitoka kwenye ile fimbo na kwenda kumchoma yule kiumbe kwenye kifua chake. Lilitha aliishikilia fimbo yake kwa nguvu wakati ule mwanga ukiendelea kumuunguza yule kiumbe ambae alipiga kelele kutokana na maumivu makali aliyoyapata na baada ya dakika tatu yule kiumbe alipasuka vipande vipande na baadae akapotea na huu ndio ukawa mwisho wake.

Lilitha alivuta mpumzi ndefu na kuitoa taratibu, kisha akawa anaifutafuta ile fimbo yake. Wakati akifanya hivyo mara akasikia vishindo mbele yake, kuna mtu alikuwa anakuja akitembea taratibu katikati ya barabara. Lilitha aliinua macho yake na kumtazama.

โ€œkaka!!โ€ Lilitha aliita kwa mshangao, aliyekuwepo mbele yake hakuwa mwingine bali Damon kaka yake
โ€œLilithaโ€Damon nae aliita kwa mshangao baada ya kumuona mdogo wake, haikuwa rahisi hata kidogo kuamini kuwa Lilitha amekuja duniani pia.
โ€œUmefikaje huku na kwa nini?โ€ aliuliza Damon
โ€œNimekufuata wewe kaka, baba amenituma nije nikuchukueโ€
โ€œah! Tangu lini mfalme Luther akanijali mimi?โ€
โ€œsikiliza kaka Damon tangu uje huku duniani umekuwa ni kama laana kwenye ufalme wa baba, mambo hayaendi, mungu wa zoran amekasirika sana na ameahidi kama utaendelea kubaki huku na kuua wanadamu wasio na hatia basi ufalme wetu utasambaratika wote na kupotea โ€
โ€œWasio na hatia? Umesema wasio na hatia?โ€
โ€œndio hawa binadamu hawana hatia yoyote kaka Damon, umekosea sana kuja kwenye dunia yaoโ€
โ€œLilitha hivi umewaona? Hawa ni wale waliokuja kutuvamia wakawaua ndugu zetu pamoja na mpenzi wangu zuzuya wewe unasemaje hawana hatia, najua sio wote lakini wapo wale ambao wanavaa koti la kijani subiri kesho nitakuonyeshaโ€
โ€œkaka Damon nielewe tafadhali hao unaowaua kila siku sioโ€
โ€œsio kivipi? Mbona wanavaa nguo sawa na wale waliokuja kutuvamiaโ€
โ€œni sawa lakini wachunguze kwa makini, zile nguo ni tofauti kabisa hizi ni maalumu kwa ajili ya zoezi la nchi yao zoezi la kuhesabu watu wao wanaita sensaโ€
โ€œLilitha hivyo ndivyo baba alivyokutuma si ndio, uje unipotoshe ili nirudi nyumbaniโ€
โ€œHapana siโ€ฆ.โ€
โ€œkumbuka hata nikirudi nyumbani bado mnanikamata na kuniweka gerezani kama mfungwa hivi hata ungekuwa wewe ungekubali, hebu niacheni na maisha yanguโ€
โ€œtunakufungia kwa sababu akili yako haiku sawa kaka sio kwamba hatukupendi, ona sasa umekuja huku unaua binadamu wasio na hatiaโ€

โ€œNyamazaaaโ€ฆโ€ฆ!!โ€Damon alifoka
โ€œKaka Damon heโ€ฆ.โ€
โ€œLilitha naomba uondoke sasa hiviโ€ Damon alizidi kufoka huku taratibu macho yake yakianza kubadilika rangi.

Wakati mazungumzo haya yakiendelea kwa mbali alionekana baba mdogo wao Cassius akiwa amejificha nyuma ya mti mmoja mkubwa huku akishuhudia na kusikiliza kila kitu.
***

Upande wa pili ndani ya kituo cha polisi wilaya ya masasi tayari mkuu wa kituo inspekta Onyango aliwasiliana na makao makuu ya kituo cha polisi jijini Dar es salaam akiomba msaada wa kumpata kijana Alex wa millazo ambae ni muandishi wa simulizi inayoitwa MSIMAMIZI katika ukurasa wa facebook simulizi ambayo inaendana kabisa na matukio ya vifo vya makarani hivi sasa. Hata majina ya watu waliouawa na kiumbe cha ajabu katika simulizi hiyo ni sawa kabisa na majina ya makarani waliouawa mpaka hivi sasa.

Je, nini kitafuta?
ITAENDELEAโ€ฆ.

We jamaa nimekuvulia kofia
 
Back
Top Bottom