😟pole sana,mi niko poa,, naendelea kusubiri ufungue PMNiko mzima mm kidogo tu flue imenibana sana mobutu hofu kwako tu
AhsanteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeCc Norshad Tumosa bobefu zoefu PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk, marybaby, nipo2, Bishop Hiluka ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, dumejeuri kuku mweus, Thad, hearly, moneytalk, Kinondoni Sweetheart Mine eyes, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, boga la kiangazi, Richard @irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, SUPER EMILY, WISDOM SEEDS MWINDAJI @HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa SUPER EMILY iron2012 popie Albinoomweusi SPYMATE Rubawa Tieli Kingsharon92 Jane Msowoya ADK babu na mjukuu the_legend
😍haya nakuletea dhawadiAsante babe pm sikumbuki hata inavyofunguliwa
Sehemu ya 09.
|
|
“Samahani mama! Mwenye simu amepata ajali!” nilimwambia bila hata salamu.
“Uwiiiiii...unasemaje?” aliniuliza huku akionekana kupaniki.
“Ameumia kidogo! Nilimsaidia! Yupo Mwanyamala anapatiwa matibabu, hakuumia sana mama usijali,” nilimwambia mama yake, hata kabla hajaniambia kitu kingine, simu ikaishiwa chaji hapohapo, ikazima.
Nilichanganyikiwa ila sikuwa na jinsi, nilichokifanya ni kuondoka na kurudi hospitalini, ilikuwa ni lazima nifanye hivyo kwa sababu ni utu kumsaidia mtu na hata kumjulia hali kutokana na kile kilichokuwa kimetokea lakini pia ilikuwa ni lazima nimpelekee simu yake.
Nilipofika, niliulizia na kuambiwa mahali alipokuwa na hivyo kwenda kule. Aliponiona tu, kwa mbali akaanza kutoa tabasamu, nilishindwa kugundua kama huyo msichana ndiye aliyepata ajali kwani alionekana kuwa mzuri kupita kawaida.
Kama nitaambiwa nimzungumzie sifa zake, zilikuwa nyingi sana, alikuwa mweupe, kama Mpemba fulani hivi, mwembamba kidogo, miguu ya kawaida, alikuwa na vishimo viwili mashavuni ambavyo vilionekana kila alipokuwa akitabsamu, alikuwa na nywele ndefu, yaani kwa jinsi alivyokuwa ilikuwa ni kama nilikutana na jini katika daraja la Salenda.
Nikabaki nikiushangaa uzuri wake. Msichana huyo aliitwa Scaila John ambaye ninataka nianze kukupa stori yake hii ndefu na ya kusisimua mno ambayo itaweza kukufundisha mambo mengi katika maisha yako.
|
|
Je, nini kitaendelea?
Cc Norshad Tumosa bobefu zoefu PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk, marybaby, nipo2, Bishop Hiluka ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, dumejeuri kuku mweus, Thad, hearly, moneytalk, Kinondoni Sweetheart Mine eyes, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, boga la kiangazi, Richard @irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, SUPER EMILY, WISDOM SEEDS MWINDAJI @HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa SUPER EMILY iron2012 popie Albinoomweusi SPYMATE Rubawa Tieli Kingsharon92 Jane Msowoya ADK babu na mjukuu the_legend
SEHEMU YA 19.
Tukaachiana na kuanza kuwasalimia marafiki zake. Sikutaka kuleta macho ya tamaa. Wanaume huwa tunakuwa na matatizo, tunapokutana na marafiki wa wapenzi wetu akili zetu huwa zinaruka, yaani ni kama tunachanganyikiwa na mwisho wa siku unatamani uwe na hao wote.
“Mungu nisaidie! Huu mtihani mgumu sana,” nilijisemea kimoyomoyo huku nikiendelea kuwasalimia kwa kuwashika mikono yao laini iliyoniachia harufu mbalimbali za manukato yao.
“Jamani huyu ndiye aliyenisaidia,” alisema Scaila huku akiwaangalia wenzake.
“Jamani kumbe ni kaka mzuri hivi,” alisema msichana mmoja, alikuwa mweupe, ana mwanya na nywele zake alizinyoa kwa staili ya panki, alivalia skin tight nyeusi, japokuwa alikuwa amekaa, lakini kwa jinsi bastola zilivyoonekana, niligundua alikuwa na mzigo wa haja.
“We Janeti! Koma,” alisema Scaila huku akijifanya kukasirika, hapohapo akaanza kucheka kwa kicheko cha taratibu.
“Oh! Anaitwa Janeth! Mungu endelea kunipigania kijana wako, napata tabu sana, yaani nateseka,” niliendelea kujisemea moyoni mwangu, hakukuwa na kipindi kilichokuwa kigumu kama hicho.
Tuliongea mambo mengi mahali hapo, Scaila hakuisha kunisifia, alizungumza maneno yote mazuri kuhusu mimi kiasi kwamba marafiki zake walihisi walikutana na malaika kwa jinsi nilivyoonekana kuwa mwema.
Baada ya nusu saa, marafiki zake wakaaga, wakasimama na kuanza kuondoka. Hapo ndipo nilipomfaidi huyo Janeth. Alikuwa si mchezo, yaani kila nilipokuwa nikimwangalia kwa kuibia, nilijikuta nikimsifu Mungu kwa uumbaji wake maridhawa.
“Mungu nisaidie! Mungu nisaidie! Bila wewe mimi siwezi!” niliendelea kujisemea.
Nilikuwa nikikutana na ugumu mkubwa sana mbele yangu, kulikuwa na mapambano mazito ambayo nilitakiwa kuyashinda kwa nguvu zote.
Huyo Janeth na wale wengine walionekana kudhamiria kabisa kuniingiza kwenye matatizo na Scaila kwani hata walivyokuwa wakiondoka, walikuwa wakiondoka kimitego sana.
Kwa kawaida mpaka muda huo ilikuwa ni lazima ugundue kuwa siku zote rafiki wa mwizi lazima awe mwizi lakini kwangu sikuhisi hilo kabla.