Simulizi: 'Sauti ilimuitikia'

Simulizi: 'Sauti ilimuitikia'

Kaguo alikuwa tajiri mkubwa zaidi katika mji wa Masoko na aliyependa kujitolea.

Siku moja kwa furaha alidamka kuwahi kwenye msikiti wake mkubwa aliokuwa akiujenga ili kutumika na wakazi wa mji wake huo alioupenda.

Alipofika na kuingia ndani ya msikiti, alijikuta akiangaza macho kotekote mjengoni humo, huku akikubali uzuri na ukubwa wake.

Rangi ya kidhahabu iliyopakwa msikitini ilirandana na kanzu yake aliyovalia.

Kwa furaha, bila sababu alijikuta akipanua mdomo wake na kuongea, "Assalaam aleykum", kinywani salamu ilimtoka.

Kwa wakati huo hakukuwa na mtu mwengine zaidi yake kwenye msikiti huo mkubwa.

Ila mara, kaupepo kenye nguvu kakavuma, na kanzu yake aliyovalia kuanza kupepeswa na huku madirisha ya msikiti yakaanza kujibamiza.

Mara sauti kubwa na nzito ya kiume ikasikika, ikimuitikia, "wa aleykum salaam".

Kaguo akawa kashtuka na kubaki kaduwaa, mara ghafla upepo uliovuma ukapotea na madirisha yakaacha kujibamiza na kutulia.

Macho yakamtoka Kaguo, asielewe nini hasa mbele ya macho yake kilitokea, kwa haraka na mbio nje akatimkia.
Endelea ndugu
 
Ishaisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom