Sehemu ya 33.
“Nakupenda sana,” aliandika msichana huyo.
“Nakupenda pia! Wewe ni msichana wa tofauti sana kwenye maisha yangu. Unajua kupenda, unanukia vizuri, unapendeza mno, ni msichana ambaye kama kuna siku nitampoteza, nina uhakika nitalia maisha yangu yote,” aliandika Gibson, Shadya alipousoma ujumbe huo, tabasamu pana likachukua nafasi yake.
“Kweli?”
“Niamini mpenzi! Kwa kipindi kirefu sana nilitamani kumpata msichana kama wewe, mwisho wa siku umetokea katika maisha yangu, kipindi ambacho nilionekana kukata tamaa,” aliandika Gibson.
“Nashukuru kwa kunipenda!”
“Na wewe nakushukuru kwa kukubali kuwa mpenzi wangu! Utapenda nikupeleke wapi ukale leo?” aliuliza Gibson.
“Popote upendapo!”
“Basi nakuja kukuchukua! Jiandae, vaa ile nguo nzuri kipenzi!” aliandika.
“Sawa!”
Shadya akasimama kutoka kitandani, moyo wake ulibadilika na kuwa mtu mwenye furaha kubwa, akaelekea bafuni, akaoga na alipomaliza akarudi na kuanza kuvaa nguo zake huku tayari ikiwa ni saa saba mchana.
Akaichukua simu yake na kuangalia, kulikuwa na missed calls tatu kutoka kwa Ngwali, alimtafuta alipokuwa akioga. Kwa mara ya kwanza akahisi kumdharau mwanaume huyo, hakuwa na hamu ya kumpigia kwa sababu tayari moyo wake ulianza kuchukuliwa na mwanaume mwingine.
“Missed calls tatu utadhani ananidai figo yake...mxiiiiuuuuu...” alisema msichana huyo na kusonya, huo msonyo wake si wa nchi hii, halafu akaifunika simu.
Penzi jipya liliuchanganya moyo wake na hakutaka kusikia la yeyote yule.
Alipomaliza kujiandaa, akampigia simu Gibson ambaye alimfuata na gari chuo na kumchukua kuondoka nay kuelekea katika Mgahawa wa Samaki Samaki kwa ajili ya kula.
Muda wote Shadya alionekana kuwa na furaha tele, alitokea kumpenda Gibson na kuhisi angekuwa naye muda wote katika maisha yake.
Walikula na kunywa na walipomaliza, wakachukuana na kuelekea nyumbani kwa kijana huyo. Hapakuwa na ugumu wowote ule, alivuliwa nguo, akaanza kuguswa hapa na pale na mwisho wa siku kuanza kufanya mapenzi kama ilivyokuwa siku iliyopita.