Simulizi: Nilivyomfumania Mume Wangu Nikaapa Kulipiza

Sehemu ya 18

Nilisema hajui yuko na mbwa tuu? Niliumia sana. Mimi aisee nikishajua unatembea na mume wa mtu hata kama mke wa huyo jamaa sio ndugu yangu siwezi kukupenda kabisa.

Nakumbuka siku moja nilishawahi kumnyima baba mmoja spare ya gari kisa alikuwa anamnunulia hawara yake hiyo spare.

Nikamwambia zimeisha. Mara kibao nimeacha vikoba kisa najua tuu kuna wanawake wanadanga na waume za watu ,alafu niko nao vikoba, yani nikisikia ile mibebisho yao na waume za watu uwii, nasikia kuumia sana..

Yani mimi ni team mke hasa, na sio team mchepuko kabisa. Yani hii ilinipa hasira nikasema kwa Mr nimemaliza, nanza na Loi, alafu shoga yake aliyenicheka….

Yani nalala nawaza what next. Hapo bado nina lile hirizi. Nikaona sasa hapa nimefanikiwa kitu kimoja, nataka sasa nimalizie hirizi alafu nijue mume anaongea nini juu ya hili sakata na je atakuwa na mausiano mengine?

Maana nilishaona mwanaume ni mmbwa tuuu, yani unajua kuchukia, ila sasa ile msg ya kumwambia Loi kuhusu kuudhika Loi kutaka kunidhuru jamani ilinipa afya mpaka nikaanza kuhisi hamu na mume wangu baada ya muda sana, maana hata tendo ni kama nilikuwa nabakwa tuu. Nilikuwa namuangalia Mume wangu namhurumiaje,naona aliyo na mawazo.

Usiku nikajigeuza nikamkumbatia, naye akaonyesha ushirikiano, sasa nna uhakika kabisa jamaa hajadinya kama wiki hivi, maana Subiani si mchezo. Akanikumbatia akaniambia mamii uko sawa? Nikamjibu ndio mume wangu. Akaniambia call me darling.

Ha ha ha, Uwiii, Makubwa Iren, Na mimi nikajidai Darlie,wala sio darling tena, hapo najua jamaa mpyaaaa, hajadinya kitambo, Asikwambie mtu, nilipewa shoo moja hatari, ilikuwa nzuri sanaa, Huku naongeleswa ki boys two men, ile Baby ur the one and the only, Nakupenda mke wangu. Na mimi najidai nakupenda sana, nauona upendo wako kwangu, unanijali sana Darlie, si nimeshaambiwa niite Darlie.

Yani mimi kuhisi mume ni Malaya kulinifanya hata kitandani nikawa mzembe na sina hata hamu ya masham sham, yani unajua kubweteka, nilibweteka sana, Hivi unahudumiaje mtu kabisa unajua ni Malaya ama unahisi ni Malaya? Uwiii.

Asbh Nkasema hembu hili jini liniache nihudumie mume wangu mie Nikaamka, nikaandaa chai nzuri sana. Akamaliza kuoga, akaja akakuta chai mezani...

Itaendelea...
 
Sehemu ya 19

Nikaamka, nikaandaa chai nzuri sana. Akamaliza kuoga, akaja akakuta chai mezani, akanikumbatia, akaniambia Irene I love you mamiii.

Nikamshukuru sana. Akaniangalia Akaniambia Irene una Mungu, tena Mungu wako ni mkubwa sana. Nikasema tu amina darlie.

Hapo najisemea moyoni sijui ndio nitaombewa tena, maana sala zake ni Zaburi, nikahisi akiomba sabh hii ataomba sijui Mithali, Ha ha ha. Akaniaga, Nikamwambia darlie naomba kwenda salon, Akasimama kidogo, Akaniambia utaendaje?

Nikamwambia nitadrive, Akaniambia , ngoja nikuachie V8, mimi niondoke na RV4, Yani hakutaka kabisa nitumie RV4. Alihisi jini atapanda. Ha ha ha ha.Nitatumia njia gani nisikie mazungumzo ya Mr? Yani nilikuwa nawaza sana.

Mh, Akili ikaniambia hivi mwanaume ukimtendea mema, mfano kumjali, kumsikiliza, kumheshimu, kumpa mapenzi inasaidia yeye kutulia au ndio ile hata umfanyie nini hatulii?

Nawaza maana kusema ukweli sikuwa na mahaba hata kidogo kwa mume kwa kile nilichokuwa naamini hizi ni mbwa tuuu, maana kila mwanaume hata kama ana mwanamke mrembo kiasi gani anadanga tuu. Nikakaa kitandani nikajtasmini, yani mimi ni Yule mwanamke, ili mradi life lisonge.

Kweli tuna pesa namaisha lakini hata manjonjo sina, Ndani nimejaza magauni ya lesi utafikiri sijui nini, yani manguo ya vitenge yamejaa kabatini mpaka basi, nikasema au mr alikuwa anapenda uvaaji wa Loi? Maana Loi uvaaji wake vinguo Fulani hivi, mh, niliwaza mengi, Mapenzi ndio jamani sijui zaidi ya kulala chali nimenyoosha miguu kama gogo la mkaratusi pale Mafinga linasubiri ku tritiwa, nikijitahidi sana nimekunja miguu kama niko leba napush, yani hapo ndio nimemeliza.

Sijawahi kulala na Mr akarudia game, maana namkeraje, maana si nina hasira? Nikasema sasa hapa nijaribu mbinu ingine sasa, kwanza nijue anaongea na nani? Pili binafsi nirekebike, maana kaachana na Loi, maana yake hana mahali pengine mpaka aanzishe tena. Lakini nina wazo langu moja Kubwaaa la kulipiza kisasi bado sijasahau. Mh.. kazi ninayo.

Nikaoga, nikavaa kagauni kangu Fulani hivi, kadogodogo hapo naanza kumuiga Loi. Ha ha ha, Huyoo nikaondoka naelekea salon, Nikampigia Mr, tena naita Darlie, naenda salon, ndio natoka nyumbani . Akaniambia sawa mke wangu.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 20

Nikamwambia Siku njema Mungu akutangulie. Akaniambia amina mpenzi, nakupenda. Kwanza nikapaki gari pembeni, Nilipataje kulia machozi mengiii.

Nikasema kumbe ndoa yangu nilikuwa naiharibu mwenyewe, kumbe mapenzi yapo? Kumbe mume wangu ananipenda? Nilimaiza kulia, nikafuta machozi, nikaeleea salon.

Nikatengeneza nywele, Nikasema EE Mungu nipe mbinu nyingine niponye ndoa yangu. Uwiii, Nikapata Mbinu mpya. Nikacheka kwanza, alafu nikasema Kama ilivofanikiwa ya kwanza nah ii ikafanikiwe.


Alafu nikasema nasaka kungwi wa Kiswahili hasaaa mwenye kujua manjonjo yoote ya mapenzi anifundishe, mpaka nijue kweli mwanaume ukimhangaikia haridhiki? Niliamua hasaaa. Natamani kufanya huyu mwanaume asitoke kabisa.

Kama hii nimefanikiwa, tutaenda kwa style hii hii. Niliwahi kusikia Mbauda kuna mwanamke Mtanzania wa Kisomali anafundisha wanawake kukatika na mahaba. Mh, nitampataje?Nitamuuliza nani? Ninawaza tu sasa ili nione kama itahuisha ndoa yangu. Nikaona wacha kwanza nianze na kimoja kimoja.

Wazo la ile Hirizi ya kiporo ninayotembea nayo. Alafu sasa nina wazo jipya. Nikasema ninunue simu mbili za kitochi. Na nisajili laini zangu 2 za siri sana. Lengo ni kumrekodi mr. Namrekodije? Yani nachaji kisimu alafu nakipiga mwenyewe.

Alafu nakipokea nakiweka nyuma ya head rest ya kiti cha gari. Imeisha hiyoo. Nataka tuu kujua anaongea na nani nini. Najua hili nitafanikiwa. Leo niko na v8. Nikaanza kufanya kazi hiyo. Nikanunua simu.

Nikanunua line zangu. Nikaweka vocha ya elfu 40. Hakukuwa na hivu vifurushi. Huyoo nikaenda home. Nikachaji kisimu kimoja fasta. Maana nilisema hiki kingine kitakaa kweny chaja.


Nikafanikiwa. Mpaka saa moja kasoro mr hajaja. Mara nikatoka kwenda kuweka simu nyuma ya head rest. Tena ilibidi niende supermarket as nje kuna camera zinaface car parking. Uwiii. Natetemeka ila sina namna. Hapo ni saa moja nimepiga nimepokea.

Huyoo nikarudisha gari.
Mara mr huyoo. Kama bahati kafika, tumesalimiana akakaa kama dakika kumi akaniomba funguo atoke.

Nilimpa haraka sanaa. Huyoo akaishia. Yani unajua akapanda kwenye gari tuu akampigia Mike. Hajui nyuma kuna ka simu. Namsikia akisema na Mike wakutane mahali.

Itaendelea Kesho....
 
Sehemu ya 21


Bado nilikwa nasikiliza maongezi yak na Mike, na nilijiambia sitaki kabisakujipapresha, na sitapanikikwa chochote ambacho nitakisikia no mata what. Kama nimejua kuna Loin a nimenyamaza, nimejua mambo yoote na nimenyamaza, kipi kipya? Nilikuwa tayari najiona mshindi.

Kuna saa nilikuwa nakaana kujitafakari alafu najiambia haloo hivi ni Mimi Irene ama ni nani?

Nawezaje kujua mambo makubwa hivi lakini nanyamaza? Ila nimekaa na wanawake wengi, na mimi kuwa mpole ndani ya sakata hili sio kwa sababu siwezi kuleta valangati, nooo, sio kwa sababu siwezi kupigana na Loi nooo, kwanza kafupi kadogo nakamudu kabisa, viao kadhaa tuu nakamaliza, Lakini nilikuwa naona wenzangu wanaopigana na hawaachani na waume za nikujiabisha tuu, yani watoto uiowazaa wanakuja kuona mama yetu ni mhuni anapigana hovyo na wanawake.

Lakinihata wanawake ambao waume zao wanachepuka hata wakitukana michepuko a wanaume bado hawaachani, yani hakuna kuachana, nikajiabia mimi nataka kujua huyu mtu ana mwanamke? If yesnni kitu gani kitawaachanisha? Ndio nikapata wazo la mashetani siji majini.

Ni mara chache sana nimekutana na wanawakw Waombaji ambao wanaamua kudeal na maombi ili waume zao watulie. Na hii aina ya Wanawake waombaji dah, Sio waombaji tu, ni Mwanamke ambaye ukimuangalia haloo mpaka unasma huyu kweli Muombaji, Yani tabia zake, mwenendo wake na kila kitu chake kimekaa Kiungu. Kimungu kabisa.

Si oleo uaomba saa ne, saa saba umeshakunywa mibia, mara unaomba usiku, asbh umshatukana, yani Utangoja sana Kujibiwa, tna ukiwa hivyo ndio unakuwa kama umechochea Moto hasaaa, mume ndio anakuwa kiberenge. Nikakumbuka namna nilikuwa naomba alafu katikati najikuta nawatukana hatari.

Na ukiamua kuwa Muombaji hasa, uamue kuwa na Mausiano mazuri na Mungu kwanza, kwa sababu swala la komba Mungu kisa unataka mume abadilike ni lingine na swala la Kumuomba Mungu kama umpendaye ni kitu kingine, alafu kumpenda Mungu na kuomba mum abadilike ni kitu kingine.

Nilikuwa napiga mahesabu namna wanawake wengi wanakimbilia makanisani ili waume wabadilike na sio Maisha yao yabadilike nikawa najichekea maana ni kama wanajaza maji kwenye gunia. Any way hiyo nayo ni stori ingine nitawasimulia siku nyingine.

Itaendelea....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom