Simulizi: Nilivyomfumania Mume Wangu Nikaapa Kulipiza

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
153,019
454,035
Sehemu ya 01

Mtunzi Irene Mbowe

Kama kuna vitu wanawake hawaaamini ama hatuamini ni mume kukosa mchepuko. Yanii hii sijui utaniambiaje niamini.

Akili yangu inaamini kabisa mr anachepuka.
Sio kama nimemuona ama najua. Basi tu kuhisi hisi.

Alafu mbaya zaidi saa ya tendo la ndoa ndio naamini kabisa huyu mume ni kahaba, mbwa na malaya.

Nakosa hamu ya tendo, najikuta parfomance inashuka na ninaona sawa.
Maana saa ya tendo nitamsukuma, mara kumkejeli na kumbeza.

Sasa nataka kumshika niwe na uhakika.
Nimechoka kubuni na kuhisi.
Mimi pia nafanya kazi. Na ninasimamia kazi za familia. Miradi ya familia.
Sasa nimechoka kuhisi.
Nitamfumaniaje?

Naanza kupanga mikakati yangu.
Marafiki zangu woote waume zao wanachepuka na michepuko yao naijua.
Huyu wangu ni malaika? Nooo.
Anachepuka lazima.

Nitajuaje?
Nitajua tuuu.
Nimeshaanza kupanga mbinu.
***********

Nitaanza na simu yake. Nitaanza kumfuatilia akitoka tuuu ninaye. Kwa siri sanaa. Yani nataka nijue mchepuko wake. Najua anao.
Akili ikaanza kufuatilia simu. Nitajuaje pass word? Ni ngumu sana.

Dah.
Ngoja nimfuatilie akitoka. Yani siku za jumapili hatufungui ofisi. Hii hiiii.
Sasa nitafanyaje?

Ni jumapili moja nimeipania. Tumetoka kanisani tuu akaniambia anakuja anaenda kuonana na rafiki yake.

Akaondoka. Nikamsubiri aje ale hakuja. Mpaka saa tisa haji. Saa kumi na moja haji. Saa mbili usiku ananiambia sorry mami nilikuwa mbali sana. Pasha chakula nije kula mke wangu.

Mh.. hasira zikanishika hasaaa. Kweli akaja saa mbili. Nikaona hapa hapa nimpime. Akala. Akaoga. Nikasema nifuatilie simu sijaona lolote. Nikasema leo naomba tendo la ndoa. Alinipa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na akili inawaza pesa. Na mwexi ulioisha alikopa bank milioni 50. Kama naamini lakini mhh.. namjua anavyopenda sex.

Namjua.
Akanipa mawazo sana.Nilinuna sana. Asbh nikajisogeza weee ila wapi.
Nikasema"mbwa hiii" jana ilikuwa mahali mpaka haina hamu.
Tukaenda ofisini.
Nikamuita dereva tax. Nikamuomba sanaa anisaidie kumfuatilia mr hii siku. Nikampa laki mbili.

Akafanya . Akaniambiaa hakuna kitu. Nikajua na hii ni mbwa ingine. Zinalindana.
Nikasema nitafanya mwenyewe.

Itaendelea....
Screenshot_20210831-141759_Instagram.jpg
 
Sehemu ya 02

Nilinuna sana. Asbh nikajisogeza weee ila wapi.
Nikasema"mbwa hiii" jana ilikuwa mahali mpaka haina hamu.
Tukaenda ofisini.

Nikamuita dereva tax. Nikamuomba sanaa anisaidie kumfuatilia mr hii siku. Nikampa laki mbili.

Akafanya . Akaniambiaa hakuna kitu. Nikajua na hii ni mbwa ingine. Zinalindana.
Nikasema nitafanya mwenyewe.
Kesho yake nikasema naumwa.

Hivyo niende hospital.Akanipeleka. Akaniacha. Nikasema nabuni kitu . Mpaka nimfumanie. Nililalamika sana tumbo. Daktari alipima kila kitu. Nikalazwa maana si kujinyonga kule na kulalama.

Saa tisa mr akaja kunioona. Akauliza utakula nini nikamwambia uji na keki. Nilitaka asiteseke ili nifanye yangu. Akaniletea chakula cha usiku saa moja uji na keki. Akaondoka saa mbili kamili. Ile anatoka tuu, na mimi nikatoka wodini.

Nikachukua boda boda. Nikamuomba afuate hiyo gari. Nimejifunika hasa.
Mara uwiii,sikuamini nilichoona. Mr akapaki gari. Akaja mwanamke akapanda. Nilitaka kuruka kwenye piki piki. Uwiii.
Haoo wakaondoka.

Wakafika mpaka kwenye nyumba fulani wakaingia geti likafungwa. Nilitaka kufa.
Sasa ndio tumbo likauma hasaaa. Paniki kama loote.

Nimeshajua nyumba. Mwanamke sijamjua.
Uwiiii.
Nirudishe kaka hospital. Nikampa elfu 10 yake.

Niliingia wodini nikapanda kitandani saa nne. Wakati natoka mlinzi nilimwambia nafuata sweta. Nikarudi wala hakuhoji. Nilijilaza nikiwa nawaza hasaaaa.

Presure kama yoote.
Kumbe wanaume ni mmbwa kweli.
Nilipiga simu home, dada hakupokea. Kwa nini?

Nikapiga tena na tena.
Nikakuta simu yake iko busy. Ahaaa. Saa hiyo saa tano. Anaongea na nani?
Nikampigia mr naye yuko busy
Nikahisi dada na mr wanaongea.

Nikaangalia muda nijiridhishe.
Hii siku natamani sasa simu ya dada tuuu. Nilijua nilipomuacha mr. Nikajua dada aliambiwa usipokee simu. Na ndio maana dada na mr wako busy. (Sijui kama mmeelewa)yani naomba Mungu dada asifute calls zake. Uwii.

Mr saa nane ananitext mamii, pole utapona. Nikafyonza kwanza. Sikujibu.
Ila nikasema nikkinuna atahisi kitu. Nikampigia kumsalimia kama saa kumi hivi.
Oo babe wangu pole.

Utapona. Moyoni nasema mbwa ,shetani,lusifa,ibilisi mkubwa.
Akaja asbh sana saa moja. Nikaomba kutoka. Saa nne mr huyu hapa, Tukapita soko kuu .

Itaendelea...
 
Sehemu ya 03

Tukapita soko kuu kanunua vyakula utafikiri nin genge, ooo babe unajua utapona. Yani likiongea naona movie ya jana yoote
Wavyochukuana na yule pepo wake. Mbwa hawa.

Yani nafika tu home mhaho ni simu ya dada.
Mr ndio kwanzaa kavua na suruali kavaa pensi akae na mimi. Nasonyaje.
Kanikatia matunda.
Yani wanaume jamani mh. Kama sio yeye wa jana usiku.

Ni bora nilivyokuwa nahisi sasa nimeona. Ni nani yule mwanamke? Wa wapi? Wa lini? Yani hasira uchungu na mawazo, nikajikuta naanza kulia nawaza mengi. Sijui nimuulize? Lakini nitaharibu. Uchunguzi wangu bado.

Yani hamu, nyege zoote zilikata ghafla mpaka nikatamani kuwa sista. Mr ananihurumia. Eti usilie mamii utapona. Utapona. Unadeka mje wanguu.. natamani kumtukanaje.

Mara akapigiwa simu sijui na nani, moyo ulinipasukaje... hahaha. Nikadhani ni ile pepo yake imempugia.Aliondoka, kabla hata hajatoka getini ndio anawasha gari nilisimama kama jonsina lilichukua simu ya dada na kuangalia sms.

Uwiiii. Mr alimuambia,mama akipiga usipokee. Naye akajibu ndio baba. Alafu akaambiwa akipiga nijulishe. Na ndio ule ule muda jana mr na dada hawapatikani.

Tayari nimepata uthibitisho kuna kitu. Napanikije? Natamani kumzibua dada lakini naanzaje itajulikana.
Wala dada hakujua nimeangalia simu yake. Ba sikufuta chochote.

Mara naona Mr anampigia dada. Uwiii. Nikajikausha mnoo. Namsikia dada anasema hajashika simu yangu. Sijui kufuta. Namsikia tuuu. Na kweli simu ya dada ina sms kibao. Nikajikausha sanaaa.
Jioni mr akaja namfuatilia kisiri siri. Akachukua simu ya dada.

Nikajua atafuta.
Kweli alifuta. Mimi kimya. Ila simpendiii,hamu naye sina.

Nimemkifuuuu.Yani nilimchukia huyu mwanaume sitaki hata anisogelee. Alafu linajidai kama hamna kitu. Rafiki yake akaja. Yani naye namuona tu kama mbwa. Yani mbwa mbili.

Eti Unampenda sana wife. Yani shemeji broo anakupenda sana. Jana kaja home saa tatu hana pa kwenda amelala kwenye kochi.

Unajua nilishindwa kuvumilia nikasema hii mbwa ingine imenitokea wapi. Nilimtizama kwa kejeli.Nawachora tuu. Wal hawajui najua.

Wanaume wanajua kuteteana. Nilikerekwa nikaenda zangu kulala. Plan nijue nani anakaa pale. Yani nijue tuu basi. Nitaenda mpak kwenye ile nyumba. Plan yangu next.

Itaendelea.
 
Sehemu ya 04

Huyu nataka ajue nimeju niwe na vidhibiti. Alafu nilipize kisasi. Ndilo lengo langu. Si anaju kuwala , na mimi ntaliwa. Yani ukimuona mume wangu hutamzania. Akiwa dukani utaskia nguo ya my enjoo, sijui nini nini, yani hawa wanaume jamani.

Huwezi mdhania kabisaaa.Anavyotumia pesa sasa kwa ndugu zangu.yani. hata ukimsema hata wapi bila kidhibiti hutaaminika. Yani unajua smart man. Utaskia hapa mbele mke wangu tuuu anakaa , nyoooo kumbe anakalisha mapepo.

Ila wanawake mnaotoka na waume za watu mnawapaga nini jamani? Maana sio kwa mahaba hayo. Mh. Sasa plan yangu nimjue huyo mwanamke. Naanzia wapi? Kwenye ile nyumba. Asbh mr tukapanda wote ofisini.

Akaniacha ofisini. Jioni kama kawaida tukarudi nyumbani. Akaniacha akatoka. Ile katok na mimi huyoo. Mpaka pale kwenye hiyo nyumba.nikajibanza pembeni. Mara Rav 4 hiyoo nyeusi. Akashuka dada mmoja namjua kabisa wa Bank. Uwiiii.

Namjua. Anaitwa Loi. Sikuamini. Akafungua geti akaingia. Nikiwa naduwaa, V8 ya mr hiyoo. Geti likafunguliwa. Mr akaingiza gari. Aisee hapana. Nilijikuta nalia sana. Mnoo. Yani kiluniuma sanaa. Nilikaa kama lisaa hatoki.

Masaa mawili hatoki. Huwa mr anasemaga yuko na mabest. Na nilikuwa naamini. Akaniambia mamii niko mahali fulani na mabest nitachelewa.

Nikamjibu sawa kabisa. Usijali. Ila moyoni nasema ufe jamani, ukirudi pata ajali ufe na huyo malaya afeee kabisa. Dah. Mpaka saa sita hajatoka. Nikawasha gari huyooo nikarudi home.

Simu ya dada nilikuwa nayo. Niliweka line ingine kwa dada mbovu. Alafu lini y dada nikaichukua nikaiweka kwenye kisimu changu. Lakini mr hakuwasiliana na dada.Ile napanda kitandani mr huyooo.


Nikasema leo namkagua. Huwezi amini, boxer aliyokuja nayo sio ile ya asbh. Na soks sio zile kabisa. Hawa ni magwiji. Nikajiambia. Makusudi nikamuomba unyumba nione.

Akasema oo unaumwa mamii,pona kwanza. Nikamwambi nataka hivyo hivyo. Yani aligoma mbwa mkubwa huyu shetani. Nikajua huyu kalowea.Ukishamjua mwanamke wa mume wako unaanza kujifananisha.

Unajilinganisha. Mimi naendesha carina, yule rav4 , mimi maji ya kunde, yule white, japo kafupi kana tutako twa chini chini lakini ndio tayari mr anadinya. Mpaka najiuliza mr kafuata nini pale jamani?kale kamalaya kamenyoa panki.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 05

Nikakapigia mahesabuu wee, najipa moyo kabaya akili inakataa inasema hata kama kabaya ila mr mpaka anakafata, dah.

Niliumia sana moyo wangu. Asbh nikasema ngoja niende bank yake nikaweke pesa. Tena anihudumie yeye. Nione atareact vipi. Nikaulamba hasaa. Nikajijakamua hasa. Huyooo.

Niliona kwanza rv4 yake maana siku moja tuu ila nilicrem namba hatari. Moyo ukafanya paaa. Nikajikaza nikaingia ndani. Yuleee pale counter 3. Nikaona kaondoka. Mh. Alivyo mpuuzi kaenda kumpigia mr. Maana muda huo huo mr kaniuliza uko wapi? Sikumuaga.

Nikamjibu niko Bank. Mr akanigombeza akaniambia rudi ofisini. Mh, kweli ile namuangalia Loi naona wanacheka na mwenzake huyo mwenzake nilumchukia jamani kuliko Loi. Walinicheka. Hawajui naongeza kisasi. Nilitamani kuwaua.

Nilirudi ofisini , mr alinigombeza sana. Umeenda bank kufanya nini? Maneno kibaoo. Uwiiii. Nililia maana najua kajazwa upepo. Huku kwangu chuki inazidi kujinga. Hapo nina watoto 2 mapacha.

Yani wa miaka 3 mpaka nimewasahau . Ninawenge balaaa. Hivi huyu Loi hana mwanaume zaidi ya mr wangu? Hapo nataka nimsake mwanaume wake nimsemelee hata. Nitamwambia nani? Yani nilijuta kufuatilia. Nikazidiwa. Nikaanza kutafuta ushauri.

Mmoja akaniambia, Irene acha kufuatilia utawehuka. Naachaje? Nitasahauje? Wataachanaje?akaniambia leta picha ya mr na huyo loi tuwafarakanishe.Rafiki yangu Doris alinishauri sanaaa. Nikapose kufuatilia kwanza. Nikatafuta picha ya mr na loi. Nikaanza maombi kwa Nabii Musa yuko Ngaramtoni.

Omba hasaa. Alafu unapaka picha mavi unaziunganisha. Alafu Nabii anakuambia weka na elfu 50 hapo jitakase. Nikafanya hivyo mara 6. Wapi. Laki tatu zikapotelea huko.

Nikaona Doris hana jipya. Nikapata ushauri kwa dada yangu Gilo, akaniambia funga hirizi nyeusi . Yani andika jina lako Irene. Alafu AndikaMimi Loi Muue Irene. Kisha weka hirizi kwenye gari ya mr. Nikafanya hivyo.

Alafu usiku jifanye unanyongwa na mashetani alafu sema Loiii niacheee, loi niacheeee, acha wananguu. Mr akishtuka jifanye hujui kinachoendelea.

Nikajiandaa kwa tukio hili. Hii siku ilikuwa ni lazima nijue wako pamoja.Nilihakikisha namfuatilia hasaa. Nikamuona yuko na Loi. Tena hii siku jamani mpaka wadada wengine wawili wako mahali wanakula

Itaendelea..
 
Sehemu ya 06

Niliumia sana. Ila dada Gilo akaniambia wanaume wanaogopa kulogwa. Cha msingi nisikosee. Nikajikaza hasaa. Hapo mama yangu mzazi ana mashine yake ya kusaga kapewa mashine mpya ya milioni 6.

Namsemeaje? Mama hataamini hii ni mbwa. Hapo kanisani katoa mifuko mia ya kujengea, hivi mchungaji anamsemaje? Mabest zake ndio hao mbwa kama yeye, nimsemeee wapi? Yani dah.

Nikajisemea acha nijaribu hii ya dada Gilo. Hapo naamini kabisa itafaa. Ile ya kupaka mavi picha niliambiwa haijafaa kwa sababu sikumaanisha.

Nilifika nyumbani na hirizi zangu nimezitega vizuri sana. Basi mr akaja. Akaingia ndani najiongelesha kama mwehu. Akiniuliza hivi najibu hivi. Aliniuliza, mamii Ima alikupa zile spare? Nikamjibu ndio, makaburini siendi. Mr akashtuka, akaniambia wewee, nikaitika beee.

Akaniambia umejibuje? Nikamjibu tena kimawenge, Wamevaa nguo nyekundu wote. Yangu iko wapi? Mr akashtuka sana. Akapaniki. Alafu nikajilaza kwenye kochi kidogo nikasema shindwa shetani kwa jina la Yesu.

Namuona anavyoogopa. Akaniambia uko sawa Irene? Nikamwambia kabisa. Kwa nini?Akaniambia Ima alikupa spare? Nikamwambia ndio. Nikamtajia vyema kabisa. Kidogo akatulia. Moyoni nikajisemea subiri mziki wake saa nane usiku mbwa wewe. Tukaenda kulala.

Itaendelea..
 
Sehemu ya 07

Muda wa kulala nilikuwa nausubiri hasa. Bado ile hirizi sijaitupia garini. Nitaiweka saa ngapi? Hilo nalo ni zoezi lingine. Nikasema nitanyongwa usiku alafu nitahakikisha naibeba kwa siri maana watanipeleka hospital kama sio kanisani. Tukapanda kitandani lakini ananifuatilua sana. Huwa hatuna utaratibu sijui wa kuomba wala ibada.

Nikamsikia anasali sala ya baba yetu, mara imani ya mitume, moyoni nacheka nasema lala broo saa nane kuna mziki fulani. Akamalizia eti kwa jina la baba na mwana. Naluangalia tuuu lilivyo lioga na bastola yake.

Tukalala. Kila saa anashtuka kuniangalia. Kama saa saba hivi akaenda kujisaidia. Ile anarudi nikaanza kutingisha mguu sana. Akaanza, mamiii,mamii,mamiiii, nikasema kwa nguvu Subianiiiiiiiiiiiii

Jamani alishtuka mpaka nikapata kucheko. Ila najuaga majini si yanachekaga? Nilionaga bongo movie.

Nikaunganisha hapo hapo ha hahahaha. Sasa napata kicheko kweli ikaletaje uhalisia. Nikaanza kusema, makaburi yapi? Sitaki, sitaki, nikaanza kuvua pete za ndoa nasema usuniue Loi, usiniuue nakuachia. Mchukueee.

Jamani mr anahaha, kukemea pepo hawezi, nikasema naona kama shooo haijamkolea, ngoja nisake kingine. Nikawa naenda kwenye droo tumeweka vyeti vya ndoa nikashika kimoja, niko nampa Mr sasa namwambia chukua Loi chukua niachee.. niacheee..

Weee, mr akaielewa shooo.
Alinishika akanishindilia chini. Maana napigaje kelele. Dada akaamka, Dada ni mtu wa Tanga akamwambia , mr huyo ni kiti. Muulize anataka nini, mshike skio. Basi dada akaingia chumbani akaaanza, kunishika skio ananiuliza .

Anasema umekasirika nini unamtesa kiti wako , mimi nikapiga kelele niacheeeee, nimetumwa kumuuaaa au aachane na huyuu huyuu.. hapo nanyoosha kidole kwa mr.

Dada akasema baba, haya majini sio mazuri. Dada aliposema hivyo nikasema kwanguvu, Tunawaita wengine waje kutoka kaburini. Jeshiiiiiiì.. ile nimesema jeshi niliwachomoka jamani nikaruka wakaanza kunishika. Watoto wakaamka.

Wakaanza kulia, mr akapiga simu namsikia sasa. Anauliza, uko wapiii uko wapi. Naskia kwa mbali darling why? Niko nyumbani. Kwa nini? Mr akasema, Loi umefikia huku? Hapo natetemekaje ili nisikie vizuri. Akamwambia Loi unamloga mke wangu? Nasikia tuuu.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 08

Mr akasema, Loi umefikia huku? Hapo natetemekaje ili nisikie vizuri. Akamwambia Loi unamloga mje wangu? Nasikia tuuu. Mara akakata simu akampigia rafiki yake aje ili twende kwa mchungaji. Hapo ni ile mbwa imepigiwa.

Nilisema tuu, Yani akijja nitajifanya pepo limepanda sijui jini nitavuta kende hataamini. Maana ni malaya wote na wanateteana.

Nikatulia kidogo nivute pumzi ya kulianzisha ile mbwa ikija. Mara dada kaenda kufungua mlango, mr kanishikilia. Ile anaingia weee nilimrukia nasema tokaaa tokaaa, huku nampiga mabao ya hasa. Sujui hata zile nguvu nilitoa wapi.

Nasema tuuu, Subianiiii, makataaaa, makaburinii... mr anamwambia mwenzake, yani wife ameongea vitu vya ajabu hapa, kavua pete, anantaja Loi anasema anataka kumuua. Basi Mike akawa kama anamkonyeza asiseme maana anaogopa.

Mr akamwambia huyo hajui sio yeye ana jini. Mike akamuuliza kwani anamjua Loi? Mr akasema hamjui kabisa huu mwaka wa tatu hamjuu na hatakaa amjue maana nafanya kwa siri sana. Hata gari nilinunua kwa jina langu nataka nikabadilishe liwe kwa jina la Loi ili isiniletee shida.

Uwiii unajua napataje mhaho, kumbe hizi mmbwa zinajua, yani naendesha corola sijui carina Loi anaendesha rv4 kili time, kwelii, nikasema sasa jini linalopanda watajutaaa, nilianza sarakasi moja, nilimng'ata Mike hakuamini, moyoni nasema mbwa wakubwa nyie. Weeee, Mike aliielewa shoo.

Akasema ngoja nimuite wife aje alafu tumpeleke kwa Mchungaji Fredi. Huyo mchubgaji anajuaga kuombea sana hapo mtaani. Basi mke wa Mike akaja , wakaniandaa , hapo nina ile hirizi kwenye brazia. Inabidi niwe mpole ili nisiambiwe vua braa.

Mama Winie, vua brazia vaa dera. Mke wa Mike ananiambia. Niko tuu mmm, mmm, Nguo nyekundu iko pale kwenye zile maiti paleee... Mke wa Mike anaogopaje, maskini analia. Namsikia anasema kwani si kashamchukua mume anamtaka nini mama wa watu? Si aache alee watoto wake? Analiaje. Mimi niko tuu, nataka talaka.

Nataka talaka yangu. Hapo sasa najifanya akili imerudi yoote. Mke wa Mike ananiuliza kwa upole ni nini? Niko tuu mama Cris nataka talaka yangu. Nataka kuondoka. Sitakiiii. Basi ananiambia twende mama Winie. Namuuliza kwani tunaenda wapi? Namuuliza kama sijui kabisa.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 09

Ananiambia kwani mamii unajiskiaje? Namwambia kichwa kinauma sana, alafu baba Winie yuko wapi kwani? Tunaenda wapi? Namuuliza. Maskini mke wa Mike analia tuu.

Niko dadaa watoto wako wapi? Hapo narudi ndani ili nipate pozi la kutoa hirizi nikifika tuu kwenye gari niangushe chini alafu nitoe shoo ya mwisho ya kibabe.

Mara mr akafungua gari mimi niko tuu natembea pole pole mama Cris hanipi nafasi. Nikaona hawa niwachanganye moja wakose muelekeo alafu niingie kwenye gari nitupe hirizi.

Na hivi mama Cris yupo weee itanoga. Nikasema Subianiiiii( hivi Subiani ni nini?) Yani katika kitu kilikuwa kinanibeba ni nikisema Subiani. Alafu nakazanaje sasa. Yani wakanipandisha garini. Nikakaa nyuma na mama Cris. Mike na Mr mbele. Basi haoo kwa pastor.

Ile hapa na pale nikaliamsha nikapata nafasi nikarusha hirizi kwenye kiti cha mbele. Ile tunashuka mchungaji kaja. Akaniona, mama Winie, Bwana Yesu Asifiwe mama. Nikasema Subianiiiiii.. mchungaji akasema, pepo toka nakuamuru kwa Jina la Yesu.

Mhh. Nikasema kimoyo moyo hapa sio pa kuchezea, nisije pata laana bure. Nikasema tuu nipe maji, nipe maji. Mama Mike akafungua mlango achukue waketi yake alimpa Mike amshikie.

Mara akasema. Mamaaaaa, mchungajiiii. Kuna hirizi hii hapa. Moyoni nikasema waoo. Game over. Nimemaliza. Haoo wakaniingiza Sebuleni kwa mchungaji. Nikajifanya akili bado hazijarudi ili wawe huru kuongea. Mara hirizi ikafunguliwa. Kama kawaida, MIMI LOI, MUUE IRENE.

Alafu nikaandika mcharazoo kama sijui kichina kile kiarabu, hahaha. Weeee. Mchungaji akasoma akacheka. Sijui aligundua nini. Akili zikanikaa sawa. Mr katoka nje paniki kama loote. Weeeee. Anagombanaje na Loi. Yanii.. Natamani kumsikia ila mchungaji namuona alivyo makini alafu anatabasamu.

Nikasema kagundua nini? Mh..Nami nikatulia nakunywa tuu maji. Mama Cris anasema hapa kuna nguvu za Mungu. Yani alikuwa na fujo watu wa nne hatumuwezi. Mke wa Mchungaji akatoka naye. Akatazamana na mumewe wakatabasamu.

Nikahisi wamegundua kitu. Ila Mike, mr na mke wa mike mhaho kama wooote. And ofcourse mimi mr ndio akihaha naenjoy zaidi.wee mr yakamshinda akaondoka. Tukabaki 3. Mr alienda kwa Loi. Hasira kama zote. Mimi hapo ninachekeleaje.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 11

Niliona kama yuko serious sana nikasema hapa nikijidai mjinga naumbuka mara aseme najidaisha niakuwa mgeni wa nani? Ile niko naongea na Mchungaji Mike na mke wake wakaaga kwamba wanaaka kuondoka nao. Ni ili waende kazini.

Mchungaji sijui ndio hekima, sijui kuniogopa, Akawaomba naomba mje tuombe pamoja alafu muondoke naye aje jioni.

Hapo nalalamika tuu kichwa kinauma sanaaa. Basi ikapigwa sala moja ya nuvu hatari haooo tukarudi zetu home. Mchungajia akaturudisha na gari yake.

Waooo, nikajisemea kimoyo moyo. Nilishangaa kuona Rv 4 ile ile nilimuona nayo Loi imepaki home asbh ile. Jamani nilitamani kupiga vigelegele.

Yani nikajua mpaka demu kanyang’anywa gari basi mume wangu kamaanisha kumuacha. Jamani nilifurahi. Nikanyamaza kimya. Baada ya kama lisaa hapo Mike na mke wake wameshaodoka, mr akaingia. Yani anathema kabisa na ana hasira. Ila nimejikausha balaa.

Moyoni nawaza nitajuaje wamegombana? Nitamuuliza nani? Yani mpaka natamani yeye mwenyewe anisimulie imekuwaje. Akawa ananiuliza najiskiaje? Namjibu tuu kichwa kizito dadiii, alau naona kama damuu nyingi na mashamba ya miwa.

Sikia mke wangu, usiogope. Akanikumbatia. Kwa mara ya kwanza namsikia analia. Sikuwahi kumuona ananililia. Aliniambia Omba Mungu sana, tuombe sana, uchawi upo lakini tusiamini. Nikamjibu haya.

Tuombe sasa. Akaanza kuomba Sala ya BABA YETU NA IMANI YA MITUME. Yani ndicho anachojua.

Hajui kingine. Akawapigia wafanyakazi wetu wakafungue ofisi.Waje nyumbani kuchukua funguo. Alafu akasema Gerald asiende ofisini , akifika ofisini asiingie mpaka nionane naye, Mh.

Najua biashara zetu. Yani ukiwaacha watu bila mimi ama mr ofisini wataiba mnoo. Kwa sababu ni biashara kubwa sana.

Kwa siku tunafanya mauzo ya milioni tatu mpaka tano.

Hatuuzi chini ya hapo Alafu sasa akasema Gerald asiende ofisini, akili ikafanya tiii taaa… kuna kitu hapa, shenzi taipu, nawaza kuna kituu. Na picha ya kwanza ninavyojua kuunganisha matukio nikajua huyu kaka atakuwa ni ndugu wa Loi, yani niliwaza hivyo nikasema nitaifanyia kazi.

Sasa hawa ukiwaacha wenyewe wataiba sana. Baba Winie, hapana wewe nenda ofisini tu. Yani nikambembeleza sana. Akaniambia nooo, wewe wa muhimu sana mke wangu.


Itaendelea...
 
Sehemu ya 12

Akaniambia nooo, wewe wa muhimu sana kuliko pesa, Nimeogopa sana mama Winie, yani hujui tu ukianza kuumwa unavyokuwa. Moyoni nikasema kumbe kimemuingia eeee.
Mamii, ukijiskia vibaya wewe omba alafu weka biblia chini ya mto Irene. Usilale bila Biblia sawa mami.

Sawa nikamjibu.Yani hapo natamani aondoke nimuite dada yangu Gilo nimsimulie alafu aniamie what next. Nitajuaje wamegombana? Natamani kujua.

Nikajilaza kitandani, na Mr naye kajilaza, basi nikiamka nangalia gari nachekaje, gari mpyaaaa kali balaaa. Nacheka narudi kulala. Na hivi siiongelei ndio anajua kabisa majini subiani yalipanda sikusikia maongezi saa zile akiongea na Yule mmbwa mwenzake. Mfyuuuu.

Tulilala wote, na Kamasaa tatu hivi akapigiwa simu ya kazi, nikaona anawaza, nikamshauri tu aende. Akatoka alafu akaniambia, Mamii, kuna hiyo gari hapo nje ni ya kwetu. Waooo, nikamwambia waooo, Akatabasamu akaniambia ni ya kwako mamii.

Moyoni nasonya nasema mimi sio wa kuendesha kipora, nakuandaia shoo mpya wewe nenda ukirudi utaifrahia.Huyo baba wa watu akaondoka. Nikaoga tena, nikaingia jikoni nikajipikia vitafunwa vyangu safii.

Namuona tu dada anavyoniogopa, ha ha ha. Maana sijui ndio kiti akikasirika hana bahati. Kila saa namsikia akisema, astakafiru lah, toba, yalaah, mimi namcheki tu.

Maana najua atakuwa kaambiwa mchunge mama. Nikapata akili ya kutengeneza hirizi , alafu niandike, MIMI LOI UA MAPACHA UMFANYE MPENZI WANGU NDONDOCHA.

Yani nikasema hii ndio itamfanya asimsogelee kabisa. Mh, Badae nikaogopa nikasema mapacha wangu akuuu, nisiwaingize kwenye hi, Nikasema tuu nitaandika mfanye mpenzi ndondocha mimi Loi. Alafu nikakumbuka kua ile boxer alitoka nayo kwa Loi that night. Nikasema ile nitaifanyia kitu. Yani hizi ndoa jamani.

Mh. Hivi mume anakaa na Malaya (alafu hako ka Loi kabaya jamani, tumatakwo cha chini chini kama wacheza kibisa sijui alimpendea nini, any way) Yani miaka mitatu mimi sijui, ina maana ile nyumba wamepanga, kamjengea au?

Nilirudisha picha nyuma nikasema nooo, hawa watakuwa wamefanya mengi na kuzoeana hasa. Kuna wakati Mr alikuwa anaaga anaenda sijui Dar, sijui Nairobi usikute mbwa hawa walikuwa wanajifungia tuu kule ndani. Yani niliwaza mengi.

Itaendelea....
 
Sehemu ya 13

Yani niliwaza mengi. Nikasonya, hahaha, dada akasikia, Nikaona kafuata simu, Nikamkata jicho aliogopaje.

Ha ha ha. Nikawaza mambo yangu Fulani Fulani. Nyumba yetu ina Camera kila kona. Kasoro chumbani kwangu tuuu.

Na camera zetu huwezi kuziona kabisa, maana ziko sehemu ya decortions, sio rahisi uone.

Na tulizifunga kipindi Yule msichana wa Uganda sijui wapi alipiga mtoto sana. Nikakumbuka Mr anaweza kuwa ananiangalia. Nikakaa kidogo sebuleni huyooo nikaenda chumbani.

Nikampigia dada yangu simu aniletee uzi mwekundu wa kushonea sweta zile nzito. Atanipaje sasa akija? Nikamwambia achukue ndizi mbivu akate uzi mrefuuu alafu amenye ndizi aweke huko alafu aniletee ndizi.

Maana mr si ataona mtu akiingia ndani na kama akinipa kitu si ataona? Ila akileta matunda nitachukua nitaingia na ndizi chumbani game over.

Basi nikamuita sista akaja kama nilivyomuagiza. Hapo lengo ni kuweka hirizi kwenye gari na ile Boxer kuifanya kitu tuu.

Lengo kuwafarakanisha kabisa. Sister akaja, na nimjuzi hatarii. Alielewa mpaka basi. Akaja na shanga kabisa.

Tukaongea akaondoka. Nikaosha ndizi zangu nikaweka kwenye tray huyo nikaingia chumbani kuzila. Nikatoa ule uzi, nikachukua boxer yam r, nikaingiza ule uzi kwa akili sana kwenye belt ya boxer, na tusanga tuchache.

Mimi sivaagi shanga. Sasa ataisoma namba, Pumbavu.
Saa tisa mr akapiga simu, akaniambia unaendeleaje?

Nikamjibu salama ila si sana, akaniambia una kitu anamalizia anakuja. Kweli saa kumi huyu hapa. Anaonekana ana mawazo hasaaa, sana, Akaja kama anataka kuniambia kitu ila anaogopa, namcheki tuu. Hapo lengo langu aoge avae ile boxer. Akaingia bafuni akaoga.

Yani namuona jinsi hana hamu na Loi, ila ananisimuliaje? Ana mawazo balaaa. Kimoyo moyo nasema dadiii kuna ka short show hapo kwa boxer yako jamani Na ilikuwa juu juu tu kwa drooo. Yani kajipaka mafuta kamaliza kachukua boxer kavaaa. Moyoni nikasema haleluyaaaa.

Akavaaa, kale kauzi si kananing’inia alafu kanashanga tatu. Kidogo naona kama anavuta uzi, nikajikausha asinione namuangalia. Mara uzi hauishi anauvuta tuuu, ila ana hofu balaa, na anajua kabisa bila shaka hiyo boxer ni ya kule kwa Yule mpuuzi wake.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 14

Mimi Nikajifanya ndio walaaa simuangaliiiii, Uwiii, baba wa watu akaingia wash room, ha ha ha ha, Huko simuoni ila najua alikutana na kituko. Ha ha ha ha. Alitoka akawa na hofu sana alafu hasemi kitu. Nikaona ngoja nitoke chumbani nimpe uhuru kidogo nshafanya yangu. Nikajidai dada kuna mayai nikaangie, Alafu nikamuuliza, Dadii, nikukaangie mayai? Ndio akajibu nikatoka nikamuacha.

Nilimuacha awe na muda mzuri wa kufanya yake.Ili ajionee vioja vya Loi wake, Yanihii mbinu jamani niliifurahia sana, hapo kunai le hirizi ingine, na hii ya sasa hivi nimekata na kakitambaa kekundu na keupe nikaandika sanda. Yani nilikuwa na hasira sana nahii mbwa. Unaishi miaka mitatu na mume wako hujagundua ana mwanamke wanje?

Ambaye mpaka kuna wanawake wanamuita shemeji? Yani kuna kusanifiana jamani duniani acheni, Natembea najiona mke wa mjanja, naringa natingisha kalio(ila langu sio la chini chini kama la Yule Malaya) Najiona ninapendwa naendesha carina kumbe kuna mwanamke anatembelea rv4, yani nikikumbuka hivyo ndio natamani kabisa kuandika hata sijui nini ili tuu niwakomeshe.

Unajua watu waliopendana kwa miaka mitatu jamani unawaachanishaje? Wana bondi ya hatari, kama ni kuomba kufarakanisha acha kabisa niliomba mpaka nachanganya na matusi kwenye sala kwa hasira, yani hata Mungu hawezi sikia maana Napata hasira kati kati ya aombi nasema Hizi mmbwa zilaaniwe.

Nawajua marafiki zangu ambao hutukana michepuko ya waume zao lakini wapiii, hawajaachana, tena sana sana mchepuko unakuambia , sugua boxer za mumeo, ama msugue mumeo mgongo, yani michepuko jamani ina kashfa uwiii.

Nikasema mimi nikijibiwa hivyo naweza vunja shingo ya mtu bure, nikasema hiyo mbinu ya kumwambia eti mwanamke Malaya wewe achana na mume wangu sitaki maana ni kujidhalilisha, mwingine anakuambia, mbona sijampenda kajileta?

Nakumbuka siku moja rafiki yangu alimtukana Malaya akamwambia mkome mume wangu, Malaya akamwambia Yule ambaye akifika pajani kamaliza game, naye ni mume?

Sasa dharau za hivi za nini jamani? Ila wanaume nao wanaaibisha, hii mmbwa inajua game haiwezi ikafuata nini mwanamke wanje? Yani mke wake kamfchia siri lakini anaenda kujiaibisha huko nje, pooo mbaka.


Itaendelea..
 
Sehemu ya 15

Mimi nikasema hii mbinu ya Subianiii, jeshiiii na hirizi nakomaa nayo.

Nikatoka zangu nikamuacha chumbani. Mara naona mtu anatoka ghafla huyooo anawasha v8 akiwa na pensi ana haraka hatari.

Nikasema waooo, kinaenda kuumana. Baada ya dakika chache nikapiga simu, naona simu yam r iko busy hatari. Yani unajua mume wangu alikuwa sijui ananionaje, alijua kabisa sijajua kitu chochote ujue.

Nikahisi tu anaongea na Loi , Nikaingia chumbani, hamadi, Mr kasahau simu yake nah ii simu hainaga pass word, unajua kushangilia, jamani nilifurahi ile mbaya.

Nilitoka kufunga geti, kisha gril la sebuleni nikaingia chumbani nikajifungia kabisaaa.

Nikasema EE YESU NINAYATAKA MWENYEWE NAOMBA NISAIDIE. Nikakaa kitako, nikafungua jumbe. Uwii sikuamini.
Kwanza nikakutana na ujumbe mmoja mr ndio kaandika.

NI NINI HASA UMENITAKA NKAKUNYIMA MPAKA INAFIKA MAHALI UNATAKA KUMUUA MKE WANGU?

NINI ULITAKA SIKUKUPA LOI? MBONA MIMI UMENIAMBIA UNAPOSWA NA LUKA NA NIMEKUBALI NA TUMEKUBALIANA TUTAFANYA KWA SIRI NIKUACHE UOLEWE? SASA UNATAKA KUMUUA MKE WANGU ILI IKUSAIDIE NINI?

NAOMBA KUANZIA LEO MAZOEA, MAHUSIANO MIMI NA WEWE MWISHO, NAOMBA HATI ZA LILE SHAMBA KULE NDURUMA USIZIFAYE CHOCHOTE NA SITAKI KUMUONA GERALD DUKANI, NA FUNGUO ZA DUKA LA MBAUDA NAZITAKA HARAKA SANA.

Uwiii, nilifanya kupumua kwanza, kumbe mpaka Loi anataka kuolewa, kumbe kuna stoo na duka lingine, kumbe Gerald ni ndugu yake kweli. Nikasema hawa aisee sio tu marafiki huyu ni mke kabisa.

Mr aliniambiaga kanunua shamba Nduruma, na nikaendaga kuliona, mara akaniambia aliliuza akaongeza mtaji wa dukani, kumbe shamba alikuwa kapewa huyu mbwa shetani, lusifa sanbalati mkubwa.

Aisee nilipata hasira moja nikasema mr akirudi hakuna cha majini, mashetani wala subiani, tutakaa tuongee aiseee, Pozi likaniisha, nikajiskia vibaya sana.

Nikapiga tena simu yam r hapokei, bado anaongea na simu. Nikajua tuu atakuwa anaongea na Loi ama Mike, yani nilichukia sana.

Nikajikaza kuendelea kusoma jumbe za Loi, alikuwa analalamika tu kwamba hajui uchawi na hajawahi kuloga na hajui hayo yanatokana na nini. Aliapa nyapo zoote na kumuomba Mr waongee zaidi na asifanye haraka ya kufanya maamuzi ili hali wanapendana.

Itaendelea.....
 
Sehemu ya 16

Loi alibembeleza sana Mr akimhakikishia kabisa hajui kuloga na hajawahi na hatakaa awahi. Na hana chale hata moja kazaliwa katika ukristo.

Kisha akamwambia anamuachaje na mimba yake? Hili nalo likaniumiza sana.

Moyo wangu ukajaa sumu kali. Mr alimjibu tuu, its enough, umekosea sana kugusa familia yangu.

Yani kama kuna msg ya mr ilinishusha hasira nikasema hii mmbwa imegeuka Simba ni aliposema umekosea kugusa familia.

Walau nikaona yuko makini.Uwiii, nikaona sasa jumbe hii ya mimba naihitaji kwa kazi zangu badae itanifaa.

Nikapiga picha kama jumbe nne hivi. Tatu za Loi na moja ya Mr. Nikatulia. Moyoni nimepenga kulipiza kisasi tu.

Sina kingine ninachotaka. Nilipomaliza nikarudisha ile simu pale pale ilipokuwa. Alafu nikarudi kulala. Kwenye kochi. Nikatulia tulii.

Dada huwa anapigiwa simu na ndugu zake na rafiki yake moja msichana wa jirani. Simu ya dada ikaita, akapokea, nikawa namsikiliza kwa makini kwa sababu nilijua tuu muda ule lazima atakuwa ni baba. Nikawa namsikia anaitikia tu ndio, ndio, ndio, ndio.

Na mimi nikajikausha hasa kama simsikiii. Mara nikaona dada huyooo kaingia chumbani kwangu kwa kujiiba. Nikajikausha. Akatoka nikajikausha. Alafu baada ya kama dakika tatu akarudi tena chumbani.

Akili ikaniambia kuna kitu aliambiwa na baba. Nikanyanyuka huyooo nikaenda kwenye meza nikangalia simu nikakuta kadelete msgs zoote na calls zoote alafu kazima simu. Ha ha ha ha, Nikacheka na moyoni nikasema walipolalia mimi niliamkia.

Nikamuuliza dada nani kampigia simu? Akaniambia kwa ujasiri ni mjomba wake. Nikasema ahaaa, ni mjomba wa Lushoto ama Muheza? Akasema wa Muheza.

Nikajifanya hajambo? Hivi anaendeleaje? Akaiambia hajambo. Nikamuomba ampigie nimsalimie. Nikiwa najua tuu Mr atamtuia dada ujumbe nilihisi.

Basi dada akampigia mjomba wake nikamsalimia, mara nasikia jumbe zinaingia. Ha ha ha, Ni Mr, anamuuliza dada kama sijahisi kitu, na akamwambia Nitakununulia zawadi kubwa na nzuri sana mwanangu.

Nikajichekea nikamrudishia dada simu yake wala hajashtuka kitu.Nilijua kumpa mr mhaho.

Alirudi akiwa na hasira sana na kachoka sana. Mimi namuangalia tuu, namuuliza vipi dadiii, akaniambia, Irene wangu akili yangu inazunguka sana, tangu umeumwa.

Itaendelea....
 
Sehemu ya 17

Mimi namuangalia tuu, namuuliza vipi dadiii, akaniambia, Irene wangu akili yangu inazunguka sana, tangu umeumwa sina raha kabisa, mambo sio mambo mamiii.


Nitapona baba Winie, nitapona mume wangu, Umekula hata? Nilimuuliza maana kuna msg kule za nyuma niliona akiitiwa chakula, nikajua atakuwa alimiss kubembelezewa msosi.

Kula mume wangu. Nikamchotea chakula akala. Akaniambia umepona mami mpaka unaweza kunichotea chakula? Nikamwambia ndio. Mungu mwema, yani sasa hivi nalala na Biblia, naomba kila saaa.

Akaniambia tuombe tena, Yani nilikuwa namhurumia, utafikiri sio Yule anayehonga mwanamke rv4, na kumpa sijui duka na shamba.

Ila wanaume jamani sijui wanapewaga nini na michepuko, yani uhonge shamba la heka 5 kisa mdinyo? Michepuko ya tutwako twa chini chini ni hatari. Puuu mbaka. Basi Mr akaniambia tuombe.

Namsikiliza tuuu. Akanza kuomba, Mh,,sala yenyewe sasa uwii. Jamani wanawake tufundishe watoto maombi. Mwanaume wa 40yrs hajui kuombea mgonjwa?

Khaaaa, Basi bwana Akanisomea Zaburi ya 121: NITAYAINUA MACHO YANGU NITAZAME MILIMA. MSAADA WANGU UTATOKA WAPI U KATIKA BWANA.
Nikamuangalia maskini, Nikasema Amen tukaenda kulala.

Usiku kucha hakulala. Anahangaika na meseji.

Mara atoke sebuleni apige simu kwa sauti ya chini. Anagomba hasa, najua kabisa anaongea na Loi mimi kimya, Subiani katulia nayajenga mengine.
Huku kaacha simu kitandani.

KAMA NI KUACHANA TUACHANE LAKINI USIFIKIRI NITAKUPA FUNGUO ZA DUKA LA MBAUDA. KWANZA HATA NA MIMI NIMECHOKA HIZO SHUTUMA, UNIKOME NA USINISUMBUE TENA, ILA IKO SIKU UTAJUA SIJAFANYA HAYO MUNGU YUPO, KILA LA KHERI NAKUBLOKU.

Niliona huo ujumbe nikajikausha nikalala fofofo, mpaka usingizi ukanichukua ukweli kabisa.

Ile msg yani ile msg ya Muache mke wangu niliipenda sana. Sijui alilala sebuleni, yani nilijua kumtesa, naubabe wake, alizima zake.

Mpaka nikamhurumia nikasema hii imefanikiwa kwa asilimia 90. Ila bado nataka kulipiza kisasi. Kwa mr kashanyooka meridhika. Sasa Loi namuachaje achaje bila hasara nikikumbuka walivyonicheka bank aisee hapana.

Na roho ikaniuma zaidi aliyenicheka ni mke wa mtu, hivi anajiskiaje yeye ni mke wa mtu ,hivi anajiskiaje yeye ni mke wa mtu alafu ananicheka mimi ambaye nina mume kama yeye?

Itaendelea...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom