Simulizi: Ndoa Yangu

lotto3

Member
Dec 23, 2017
63
35
NDOA YANGU

EPISODE -01

Baada ya kufuta meza ya chakula na kuosha vyombo, nilienda chumbani, sikujisumbua kusema usiku mwema kwa Antony ambae alikuwa sebuleni akiangalia fainali ya ligi ya mpira wa kikapu (NBA) kati ya Golden Warriors na Cleveland Cavaliers.

Nikijua lazima atakuja chumbani si muda mrefu, hivyo nlitaka akifika tu afikiri mimi nimeshalala muda mrefu. Haraka haraka nikaingia bafuni na kuoga kabla sijapanda kitandani. Nikahakikisha navaa suruali ndefu ili kusiwe na namna yeyote ya yeye ku-'access' mwili wangu.

Baada ya saa moja nikamsikia akipanda juu ya kitanda na kugeukia upande mwingine, kidogo nikashusha pumzi nliyoibana kwa muda mrefu. Nikafurahi kwa kuwa niliweza kukwepa kufanya tendo la ndoa usiku ule.

Asubuhi ile nilijua lazima tutakuwa na ugomvi tena, nikamuomba Mungu kimya kimya aniepushe na ugomvi. Mara nikahisi mikono yake ikinipapasa papasa mwili wangu. Nikawa sina shaka kabisa nini kinachohitajika na ni kipi kitatokea.

Nikafungua macho yangu na kutizama saa iliyopo ukutani. Ilikuwa saa kumi na mbili kasoro robo asubuhi. Nikageuka na kuondoa mikono yake na kujaribu kuamka lakini akanivuta nisiamke. Kama mara tatu kila nikitaka kuamka ananivuta nibaki kitandani.

Mwishowe akasema; "Baby leo unayo sababu gani ya kuninyima haki yangu ya ndoa? Ni wiki mbili sasa for Christ sake. Unafikiri mimi nitakuwa na furaha kivipi kama unaninyima haki yangu ya ndoa?" Akasema hayo huku akionekana ameghafirika mno!!

"Unataka kuniambia furaha yako ni kufanya mapenzi tu? Kwa hiyo bado hujanielewa mwenzako? Nafanya hivi kwa ajili yetu. Kwa ajili ya ndoa yetu na kwa ajili ya kesho yetu.

Nilikwambia kabla sijaanza hivi kwamba haya yatakuja kutokea na tukakubaliana hutafanya hivyo na sasa hivi umenigeuka nionekane nina hatia. Seriously mimi unanichanganya!!" Nikamweleza hayo huku nami nikiwa nimekasirika!

Victoria, mimi sipingi wewe kufunga na kuomba. Nampenda Mungu pia na ninaenda kanisani lakini hauwezi ukategemea mimi nikae siku 100 bila haki yangu ya ndoa eti kwa vile upo kwenye maombi ya kufunga, hiyo haipo!!" Tony aliongea.

Nilikasirika mno baada ya kunieleza hayo, "seriously Tony? Unanitania? Hauwezi kujizuia? Hii inaonesha ni jinsi gani mume wangu umeanguka kiimani.

Sio wewe uliyekuwa ukifunga na kuomba na mimi kila mara kabla hatujaoana? Kwahiyo kipindi kile ulikua ukijifanyisha tu! Sio sisi tuliokaa kwenye uchumba miaka miwili bila ya kufanya ngono? Kwaio inamaanisha ulikua unanisaliti?

Nini? Unawezaje kusema hayo? Umechanganyikiwa ee? Unaweza vipi kufananisha kipindi kile na sasa hivi? Kipindi kile nilikuwa single sasa hivo nimeoa. Kuna maana gani ya mimi kuoa kama siwezi kupata haki yangu ya ndoa?

"Ahaa kwaio mimi ni sex machine? Ulinioa kwa sababu ya sex?" Nilimuuliza.

"Unajua nini, siwezi kupoteza muda wangu katika maongezi na wewe yasiyo na tija. Ninakuonya mara ya mwisho. Sitaki kusikia mambo yako ya kufunga na you will learn to respect me katika hii nyumba. Kama huu ndio upuuzi mnaofundishana huko kanisani, nitakuzuia kwenda tena shabàash"

"You wont dare Tony, usijaribu nakwambia. Kama ningeambiwa kuchagua wewe na Mungu wangu, wewe ungepoteza. Mungu kwanza wewe unafuata. Huyo shetani anaejaribu kukutumia..hatanikamata na mimi"

"Try me Vicky, nijaribu uone Vicky" akaongea huku akielekea bafuni na kufunga mlango. Nikatoka chumbani na kuelekea jikoni nikiwa nimeumia mno moyoni. Nikiwa ninaandaa kifungua kinywa nilikuwa nimejawa na huzuni mno, sikuelewa kwanini Tony alikuwa na hasira juu ya uhusiano wangu na Mungu. Sikutarajia kama mambo kama haya yangetokea ndani ya miezi 6 tu ya ndoa yetu.

Anafahamu fika ni jinsi gani ninavyompenda Mungu na ni kiasi gani uhusiano na Mungu una maana kwangu lakini hakuwa akinielewa. Na tuliongea haya wakati wa uchumba na alikuwa akiniambia ni kwa namna gani ananipenda kutokana na nilivyojitoa kumpenda Mungu.

Tumejaribu kutafuta mtoto kwa kwa miezi mitano sasa, na hakuna lolote lililotokea. Na ninafahamu fika inanibidi nikazane kumuomba Mungu kabla hiyo miezi mitano bila ya ujauzito isije kuwa miaka 15 bila ya mtoto. Na nikamwambia kabisa nataka kujiunga na maombi ya kufunga ya siku 100.

Mwanzoni alikubali kujiunga na mimi kwenye maombi ila baada ya siku tatu akaacha. Sikuhisi amenitenga mimi niliendelea mwenyewe, sikufikiri kama atakuwa mchungu kwangu katika jambo jema kama hili.

Baada ya kumaliza kuandaa kifungua kinywa ikiwa ni kama nusu saa tokea tuzozane alitoka chumbani akiwa ameshavaa vizuri suti iliyompendeza na akapitiliza moja kwa moja nje huju akinipita bila kunisemesha lolote.

Nikamkimbilia na kumshika mkono, kabla hajaingia kwenye gari yake. " Haujala kifungua kinywa nilichokuandalia" Nikamwambia..

"Nitolee upuuzi wako hapa, kifungua kinywa my foot!! Sitaki chakula chako sasa na mpaka utakapojifunza kuniheshimu kama mume wako na kichwa cha nyumba na pale utakapoona kipi ni cha muhimu kwako" akasema hayo huku akiingia ndani ya gari na kufunga mlango kwa nguvu, akawasha gari na kuondoka haraka, nikasimama pale huku nimepigwa na butwaa.

Tumekuwa na kutoelewana juu ya tendo la ndoa wiki ya pili sasa ila sijawahi kumuona Tony akiwa amekasirika kama leo hii. Nilijua kabisa nipo kwenye jaribio kubwa sana la ndoa yangu, nilitakiwa kuomba sana juu ya mume wangu...labda sikujua ni nini natakiwa kufanya kama mke! kwa kweli nilichoka..........

ITAENDELEA...
 
NDOA YANGU

EPISODE (2)

Baada ya Tony kuondoka, niliazimia hili jambo nilifikishe kwa Mungu wangu kupitia maombi. Niliingia ndani na kuanza kusali. Nilisali kwa takribani masaa mawili nikimlilia Mungu juu ya ndoa yangu.
.
"Baba nilinde juu ya ndoa yangu, ondoa kila aina ya ushetani unaomnyemelea mume wangu. Mithali 21:1 inasema, "Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; Kama mifereji ya maji huugeuza popote aendapo."
.
Oh Mungu wangu geuza moyo wa mume wangu Tony asipende Sex mpaka siku hizi 100 za kufunga ziishe..Amen. Baada ya sala ya muda mrefu nikajihisi kupata moyo upya na nikapata namna ya kufanya.
.
Nilikuwa sina sababu yeyote tena ya kuweza kumshawishi Tony asifanye mapenzi na mimi, hivyo nilitakiwa nitumie busara tu kuzuia kwa kufanya mambo ambayo yatamfanya Tony asitamani kufanya tendo la ndoa na mimi.
.
Hivyo nikaamua nisioge siku nzima. Nilifahamu fika ni jinsi gani Tony alivyokua akipenda kuniona nikiwa naoga na kuwa msafi nikinukia muda wote.
.
Alirudi nyumbani mishale ya saa moja jioni, nilihakikisha chakula cha usiku nimeshakiandaa. Nilijua tu lazima malumbano yataanza tena. Na kwa kweli sikukosea maana baada tu ya kuingia ndani akaanza;
.
"Madam, umeshaweka mambo yako sawa?"
"Mambo gani Tony?" Njoo ule chakula nilichokuandalia"
"Ulifikiri ninakutania? Unafikiri kwa kutokuoga kwako kutasaidia kunibadilisha maamuzi yangu? Au unafikiri mimi ni mpumbavu nisijue kwamba kutokuoga kwako leo ni trick ya kujaribu kunizuia nisishiriki na wewe sex?"
.
Kwa kweli nilipata mshtuko na kigugumizi nisijue niongee nini baada ya yeye kugundua plan yangu ilikua ni nini. "Tony please naomba unielewe. Natakiwa nijikite kwa Mungu." Nikaanza kumuomba Tony.
.
.
"Vicky, get it straight, mimi sikulazimishi usifunge. Kuna ubaya gani kama tukishiriki tendo kati ya saa kumi na mbili jioni unapofungua funga yako mpaka saa sita usiku unapoanza funga yako tena? Hicho ndicho ninachokuomba Vicky mke wangu."
.
"Samahani Tony, siamini kama hivyo ndio vizuri zaid. Natakiwa niwe msafi bila kushiriki tendo siku zote 100. Kushiriki tendo katikati ya hizo siku nitajisikia si msafi." Nikamuelezea hayo Tony.
.
"Upi si usafi katika tendo la ndoa kati ya mume na mke waliohalalishwa? Tunaruhusiwa kabisa!!"
.
"Nisikilize Tony, unatakiwa uwe mvumilivu. Nimebakiwa na siku 85 tu baada ya hapo tutafanya mpaka mwenyewe uchoke"
.
"Ngoja nikwambie kitu Vicky, hii ni mara ya mwisho kwangu kuongelea hili suala. Kama umeshindwa namna ya ku-balance ndoa yako na kufunga, basi utakua huna tena hiyo ndoa baada ya kumaliza hizo siku zako 100 za kufunga_
.
"Nini unamaanisha Tony? Mungu aingilie kati kuzuia hayo maneno mabaya ya mkosi yatokayo kinywani mwako."
.
Tony akaniacha nimesimama pale na akaelekea chumbani. Nikapata mshangao baadae usiku pale Tony alipoanza kuhamishia vitu vyake chumba cha kulala wageni. Nilitaka niende nikamuombe asifanye vile lakini baadae nikaamua ni bora akae huko kwa hizo siku 85 zilizobaki.
.
Labda huu ulikua mpango wa Mungu kunitafutia ufumbuzi. Nikamshukuru Mungu kwa kunipa ile njia ya kukaa chumba tofauti na Tony na hivyo kutosumbuliwa tena juu ya tendo la ndoa.
.
.
Siku ya 60 ya kufunga na kuomba, nikazidi kuchangangikiwa. Furaha na amani ya kufunga na kuomba ikapotea. Tony na mimi tukawa kama wageni ndani ya nyumba.
.
Hakula chakula nilichompikia kwa takribani wiki 6 sasa, nikajawa na hofu na uoga. Akawa ameanza kurudi nyumbani kwa kuchelewa na tukawa hatuongei tena. Kila nilipojaribu kumuongelesha aliniambia nifunge mdomo wangu hataki kunisikia.
.
Wote tulikuwa tukienda kazini na kurudi nyumbani lakini kila mtu alielekea chumbani kwake. Nilikuwa sijui hata nianzie wapi. Nilifahamu fika hakuna jambo baya nililolifanya, nilichokua nafanya ni chema kwa ajili ya ndoa yetu na nikashangaa kwanini Tony halioni hilo.
.
.
Siku moja jioni nikiwa nimetangulia kufika nyumbani mida ya saa moja usiku nilipata text toka kwa Tony iliyoniumiza sana, text hiyo ilisema "Usinisubiri mimi, sitarudi nyumbani leo"

Sikuamini macho yangu, na haraka haraka nikamjibu text iliyosema "Uko wapi? Kwanini hutarudi nyumbani?"
.
.
Jibu lake lilinifanya nilie kilio kikubwa na uchungu mwingi.....oh ndoa yangu, masikini mimi kumbe sikujua!!!!...

ITAENDELEA...
 
Kuna mtu mwingine humu kaipost tumeshasoma karibia tunamaliza
 
NDOA YANGU

EPISODE -O3

Alinitumia text ikisema, "please muulize roho mtakatifu atakwambia nilipo na kwa nini sirudi nyumbani."

Nikasema sasa imetosha, nimechoka na tabia ya Tony nikajiambia kwamba sasa tunahitaji councelling. Nilimsubiri asubuhi yake arudi lakini hakuonekana. Nikampigia simu mchana baada ya kujawa na wasiwasi mwingi lakini hakupokea simu yangu.

Baadae kidogo nikapata text yake aliyoiandika kwa kingereza akisema; ”I am quite surprised you are looking for me. Don’t worry, I am fine. Don’t let me distract you from God”.

Akimaanisha anashangaa kwanini ninamtafuta, kwamba yuko mzima hataki anisumbue juu ya suala langu la kufunga na kuomba. Nikaamua ni muda sasa wa kuomba ushauri kwa mama mchungaji.

Jioni ike nikaenda nyumbani kwa mama mchungaji na baada ya sala ya jioni tukaanza kuongea kuhusiana na changamoto za kufunga tokea tuanze mfungo.

Nikamuelezea kuhusiana na uhusiano wangu na Tony ulivyo kua na matatizo. Nilijua nitapata ushauri wa namna ya kufanya kutoka kwa mama mchungaji.

Mama mchungaji akasikitika sana kwa kutingisha kichwa nilipomuonesha texts za Tony.

Dada Vicky, Biblia inasema nini juu ya kuheshimu wazazi wako?"

"Waheshimu baba na mama yako, ili siku zako za kuishi zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA" nikamjibu haraka huku nikimshangaa kwanini anaongelewa wazazi wakati mimi nahitaji ndoa yangu iponywe.

"Unakumbuka kipindi ulipokuja kwangu na kuniambia umeamua uolewe na huyo kijana Tony ambae ndio kwanza alikuwa mbichi katika imani? Nilikuasa uolewe na waliobobea katika imani. Kama ungeyasikiliza maneno yangu huenda haya yasingetokea" aliongea huku akionekana amekasirika.

"Samahaniama, nampenda mume wangu na ninafikiri anampenda Mungu pia"

"Anampenda Mungu?, Bado unatetea matendo yake? Mume ambae hataki kukubaliana na wewe katika maombi atawezaje kumruhusu roho mtakatifu aingie mwilini mwake? Aliniuliza!

"Samahani mama" mama alikuwa akijulikana kwa hasira na sikutaka kuendelea kumuudhi.

"Hata hivyo agano limeshafanyika, ni mume wako. Inabidi tutafute way forward. Unaona shetani hapumziki. Yupo kazini kuharibu ndoa yako.

Kumbuka maandiko Waraka wa paulo mtume kwa Waefeso 6:12 inasema, "kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho"

"Hii vita sio dhidi ya mume wako bali ni vita dhidi ya roho na pepo wabaya"

"Sawa mama" nikajibu.

"Shetani anafahamu kabisa kwamba mfungo huu utaiokoa ndoa yako na anataka kuhakikisha anazuia hilo. Endelea kuhakikisha unasugua goti kwa Mungu"

"Sawa mama. Nifanye nini sasa kuhusu Tony kukataa kurudi nyumbani?"
"Usijali Vicky, Tony atarudi nyumbani, ni kama mtoto wa Prodigal kwenye kile kisa cha wana wawili wa baba tajiri katika kitabu cha Luka 15:11-32. Ninao uhakika utarudi. Tumuombe Mungu mpendwa".

Niliondoka nyumbani kwa mchungaji baada ya masaa mawili ya kuomba. Nilijihisi nina nguvu mpya. Nilitakiwa nijikite katka kuomba na nisiache imani yangu iyumbishwe.

Nilipofika nyumbani nilimkuta Tony akiwa ame-relax sebuleni, nilithibitisba kauli ya mama mchungaji kwamba Tony atarudi tu nyumbani kama alivyotabiri.

Siku zilivyozidi kwenda na ndivyo mambo yalivyozidi kuparanganyika. Tony akaacha kwenda kanisani kwetu na kunitaka nihamie kanisa alilohamia yeye.

Nilipingana nae idea yake. Sikutaka kukubaliana na uamuzi wake. Nikawa napokea text za kunipa moyo na kunifariji kutoka kwa mama mchungaji.

Mwishowe siku 100 ziliisha. Ikatangazwa kanisani kuwa wanandoa tuhudhurie pamoja katika mkesha wa ibada ya maombi. Nikambembeleza kweli Tony twende pamoja lakini akanikatalia kata kata.

Sikuwa na jinsi nikaenda kwenye maombi peke yangu. Usiku ule niliomba kila aina ya maombi. Furaha yangu ilikua juu ya kwamba sasa ugomvi na Tony utakua umeisha. Nilijihakikishia tutafanya tendo la ndoa kadiri atakavyotaka yeye.

Kumbe nilikua najiongopea.....

ITAENDELEA....
 
NDOA YANGU

EPISODE -04

Ni wiki moja imepita tokea nimalize mfungo, Tony hajawahi kulala hata usiku mmoja nyumbani. Ilikuwa akirudi asubuhi sana anabadili nguo na kwenda kazini.

Kila asubuhi nilikuwa nikimuomba arudi nyumbani lakini sikufanikiwa. Alikuwa akirudi tu anapitiliza moja kwa moja chumba cha wageni anabadili nguo na kuondoka asiniongeleshe hata neno moja.

Nilianza kufikiri kwanini nisingemkubalia tu kipindi kile. Sikufikiri kama ingefikia hatua hii. Na sikufahamu nitumie njia gani kumaliza hili tatizo.

Nilifahamu Sex ni jambo la muhimu kwa wanaume, lakini kwangu sijui ni nini sikuwahi kufurahia hata siku moja. Siku ambapo Tony aliondoa bikira yangu nilifikiri maumivu yataishia siku ile ile kwamba siku nyingine nitakuwa nikifurahia tendo.

Lakini ile miezi mitano kabla sijaanza mfungo, kila tulipokua tukifanya tendo la ndoa yale maumivu niliendelea kuyapata. Ukweli ni kwamba nilitamani tuishi tu bila ya kufanya tendo la ndoa. Ila kwa kuwa ni ndoa sikua na jinsi.

Mwishoe nikaona labda nahitaji ufumbuzi wa kimwili zaidi kwani ufumbuzi wa Kiroho haukuwa ukileta matunda yeyote kwa Tony.

Nilichukua simu yangu mchana ule baada ya kutoka kazini nikaingia 'google' na kutafuta "jinsi gani ya kuzuia maumivu wakati wa tendo la ndoa?". Yalikuja majibu mbalimbali nikasoma baadhi na baada ya kumaliza kusoma mikao mbalimbali ya tendo la ndoa ili kutoumia wakati wa tendo, nikaazimia kufanya maamuzi ambayo yatanifanya nifurahie tendo.

Baada ya hapo nikatafuta tena katika 'google' "Jinsi gani ya kumshawishi mumeo ashiriki tendo na wewe" yakaja mambo ambayo kwangu niliyaona hayana upako. Ila nikaamua kuyasoma baadhi ili niweze kuyatumia kuhakikisha Tony analala na mimi.

Nikapata texts kadhaa kutoka 'google' na kuamua kuzi-copy na kumtumia Tony kwa interval ya lisaa limoja. Text ya kwanza nikamtumia ikisema;

"Nakuhitaji mme wangu, mwili wangu unakutamani mno"

Baada ya saa moja bila kupata jibu lolote, nikamtumia text nyingine ya kingereza niliyoipata hukohuko 'google' iliyokua ikisema; "I can’t focus, all I can think about is what you will do to me if you were here with me"

Ila napo sikupata majibu yoyote, baada ya dakika 39 za ukimya nikaamua kumtumia text nyingine ya kiingereza niliyotunga mwenyewe iliyosema; "You taught me how to make love, tonight I will show you how much I have learnt"

Nikapata majibu text yake ikisema, "please niko kwenye kikao na bodi"

Nilifurahi mno, nikaruka juu kwa furaha kutoka kwenye kochi nililokuwa nimekaa. Nilifurahi kwa kuwa ndio maneno pekee Tony aliyoongea na mimi. Hajaongea na mimi kwa wiki sasa.

Nikaamua kumtumia na nyingine tena; "Okey mume wangu, nakufikiria kweli nakusubiri kwa hamu" akaijibu mapema kwa kuniambia;

"Acha upumbavu Vicky"

Nikamtumia nyingine iliyosema "please njoo nyumbani ulale na mimi leo. Nimekubali nilikosea. Nahitaji kurekebisha na wewe. Tafadhali nipe nafasi nyingine. Nakupenda my baby"

Akanijibu "Okay"

Nilifurahi sana nikaondoka haraka na ku-drive mpaka Game supermarket mlimani City nakununua matching lingerie (nguo ya usiku yenye mvuto wa kimahaba). Nikanunua foot massage kit na body massage oil.

Nilisoma kwenye google kwamba kumfanyia mwanaume massage ya miguu na mwili kunaweza kufanya maajabu na mume akashawishika kushiriki tendo na wewe. Pia nikanunua lubricator. Google ilinifundisha vingi mno.

Baada ya kumaliza manunuzi nika-drive haraka kupitia barabara ya sam Nujoma, nikanyosha barabara inayoelekea Coca cola Mwenge na kukatisha kulia kuelekea barabara inayoelekea clouds media group.

Nikafika nyumbani mida ya saa moja usiku, nikaandaa chakula ambapo nilimpikia Tony fried rice na kuku. Mpaka kufikia mida ya saa mbili usiku nilikuwa nimeshamaliza kila kitu na nimejiandaa kumpokea Tony.

Nilikaa kwenye sofa nikiangalia Movie iitwayo 'Me before you' huku nikiwa nimevaa lingarie ambayo kwa hakika ilikua inavutia kwani ilikua imenichora vizuri umbo langu namba nane ambalo Tony alikuwa akisema linamvutia mno.

Nikajaribu kumpigia Tony lakini akawa hapatikani kwenye simu. Nikasubiri! Lakini hakutokea..nikaendelea kumpigia lakini sikuweza kumfikia...

Usingizi nao haukuniacha salama, nikaanza kusinzia na kuona watu wawili wawili kwenye TV...mwishoe nikapitiwa na usingizi kabisa kwenye kochi.

Nikaamshwa na mlio wa mlango ukifunguliwa, nikatizama saa na kukuta ni saa moja asubuhi. Tony hakurudi ule usiku, instead alirudi asubuhi.

Akaingia, akanitizama kwa sekunde kadhaa na kupitiliza moja kwa moja kwenye chumba cha wageni kubadili nguo kama kawaida yake bila kunisemesha lolote.

Nikainamisha kichwa changu, nikalia mno, nikaomboleza zaidi pale alipojifungia ndani. Nilipatwa na uchungu mwingi....kwa mara ya kwanza nikamlaumu Mungu...

ITAENDELEA.....
 
NDOA YANGU

EPISODE -05

Jumamosi asubuhi Tony aliporudi nyumbani asubuhi nikaamua imetosha sasa liwalo na liwe. Hakuwa na haki ya kuendelea kulala nje ya nyumba yetu eti kwa sababu ya hasira.

Nilikuwa tayari ninamsubiri afike na alipoingia tu nikasimama nikamzuia mlangoni na kumuuliza kwa jazba.."Eheee unafikiri ulikuwa wapi Mr. Tony?"

Akanitizama kwa mshangao kama nimeota mapembe na kwa mshangao akanijibu kwa mkato.."Bahari Beach Hotel."

"Kwaio ndio huko unakolala siku zote?" Nikamuuliza huku nikiwa na uhakika hatanijibu palepale.

"Yes nilichukua chumba pale" akanijibu huku akinitizama. "Ni hayo tu?" Tony akaniuliza

"Hapana Tony, sio hayo tu na usinifanye mimi mpumbavu. Umekuwa ukilala nje takribani wiki tatu sasa na ninakuuliza unanijibu kwa dharau" niliongea huku nikiwa nimejawa na hasira!

"Madam, umeniuliza nilikokuwa na nimekujibu vizuri tu, ni kivipi nimekuonesha dharau?"

"Tony, kwa mara nyingine nakuomba unisamehe"

"Okay nimekusikia. Kuwa muwazi basi unaomba msamaha wa nini?
"Well, nisamehe kwa kukunyima tendo la ndoa na kufunga bila makubaliano na wewe. Samahani kwa kutokujali hisia zako. Please tunaweza tukarudi kuwa kama zamani tulivyopendana?"

"Okay, nimekusikia" akanijibu huku akitizama saa yake.
"Tony sasa hivi please. Unataka niseme au nifanye nini unisamehe?"

"Vicky nimesema nimekusikia. Please don't stress me. Nataka nikafanye mazoezi na baiskeli yangu kidogo, umenielewa?"

”Okay that is fine. Nataka unipe ahadi kwamba kuanzia leo utabaki nyumbani"
"Yes nakuahidi nitabaki, kwahiyo unaniruhusu niende nikabadili na kwenda kufanya mazoezi?"

Nikatikisa kichwa na kumpisha njia na akaenda chumba cha wageni na kuvaa nguo za mazoezi. Siku zote alikuwa akivutia na kuonekana handsome akivaa nguo za mazoezi zilizokuwa zikimbana na kuonesha misuli yake iliyotuna sawasawa.

Nikaenda kumkumbatia nikitegemea atanikatalia lakini akanikumbatia vizuri tu na kuondoka na baiskeli yake ya mazoezi. Asubuhi ile nilifurahi mno na nikaamua nimpikie breakfast nzuri ale akirudi kutoka mazoezini.

Baada kama ya dakika 30 hivi nikapigiwa simu iliyobadili maisha yangu kabisa. Huku machozi yakinitoka nisijue kwanini, nilichukua funguo za gari yangu na kuwahi Hospitali ya TMJ nilikoelekezwa.

Nilikua bado siamini kama kweli nimeambiwa Tony amepata ajali!! Ni dakika 30 tu zimepita tokea aondoke nyumbani, alienipigia simu hakuweza kuniambia ajali ilikuaje na ukubwa wake.

Nikakutana na foleni kubwa. Nikajaribu kupiga simu ya Tony ili kupata details lakini simu yake ilikuwa imezimwa. Nikataka kuwapigia ndugu na marafiki lakini nikajiambia natakiwa nijue hali yake na ukubwa wa ajali aliyoipata kwanza kabla sijamwambia yeyote.

"Oh Mungu wangu nisaidie mwanao. Wewe mwenyewe ulisema hatutakufa bali tutaishi. Tafadhali Mungu mponye mume wangu, sitakuwa mjane nikiwa kijana hivi oh Mungu"

Maneno ya kusali yakaniishia, sikujua hata namna ya kuomba. Baada ya saa moja hatimaye nikafika hospitali ya TMJ. Nikapaki gari Myfair plaza na kuvuka upande iliko hospitali ya TMJ.

Nikatembea haraka haraka kuwahi mapokezi huku nikiwa nina hofu na uoga mkuu nisijue ni nini naenda kukikuta huko......

ITAENDELEA....
 
NDOA YANGU.

EPISODE -06

Kama masaa nane hivi nilikuwa nimekaa ofisini kwa daktari nikisubiri kupewa maelezo ya kina kuhusiana na hali ya Tony. Nilichoambiwa wakati nikisubiri ni kwamba Tony yuko hai na ameingizwa kupigwa 'ultrasound' na baadae afanyiwe upasuaji.

Manesi hawakutaka kuniambia ukubwa wa ajali aliyoipata Tony, nilikuwa nikilia tu nakupiga kelele kama nimechanganyikiwa. Baadae nikampigia simu wifi yangu ambae alikuja haraka kusubiri nami huku akinibembeleza.

Nilitoka hospitali mara moja na kwenda Myfair plaza kwenye mashine ya ATM ili kutoa pesa maana sikuwa hata na mia, ilikuwa tayari saa kumi na moja kasoro jioni na sikuwa nimekula wala kunywa kitu tokea jana yake jioni.

Baada ya kurudi hospitalini, nikaonana na daktari mwenye asili ya kihindi na akaanza kunieleza kilichojiri.

"Mrs Tony, Asante sana kwa uvumilivu wako" mimi nikamkatisha haraka.

"Mr. Daktari, please just go straight to the point, acha kuanza kuzunguka zunguka. Anaendeleaje? Nini kimetokea? Upasuaji ulikuwa wa nini? Yuko salama? Upasuaji umefanikiwa?

"Madam, nitakujibu maswali yako yote, ila nataka utulie kwanza acha papara"

"Okay, samahani, endelea nakusikiliza"

"Mume wako yuko salama, na upasuaji ulikuwa wa mafanikio. Alipatwa na kitu kwa kitaalamu kinaitwa 'testicular trauma' ni injury inayotokea kwenye korodani za mwanaume.

"Kwa wanaume korodani au testicles zinakaa nje ya kitu kama kipochi hivi kinachoitwa kwa lugha ya kitaalam scrotum. Kutokana na location yake, aina nyingi za ajali zinazotokea husababisha kuumia kwa korodani.

"Mfano wa ajali hizo ni kama vile kupigwa kwa mpira au kitu chochote ktk maeneo nyeti, ajali ya pikipiki na ajali ya baiskeli ambayo kwayo ndio mume wako alikumbana nayo.

"Mungu wanguu!!!!! unaona matatizo haya..unamaanisha nini daktari? Kwamba mmezitoa, mume wangu hana korodani tena? Mamaaa tutapataje mtoto sasa uwiiii nafwaa mie...Tony ataniuaaaa woiii!!!" Nilichanganyikiwa!

"Tafadhali binti hebu relax basi, mbona unadandia treni kwa mbele. Mimi sijakueleza kwamba mume wako hana korodani hapa. Ni rapture tu ndogo ilitokea na kuhama kwa testicles na ndio maana ikatubidi kumfanyia upasuaji haraka"

"Upasuaji kama nilivyokwambia ulikuwa wa mafanikio na tumeweza kuzirudisha mahala pake na tuna uhakika haitasababisha asiwe na uwezo wa kuzaa hapo baadae"

"Ofcourse ninashauri akae mbali na Sex kwa muda kama wiki tatu hivi mpaka apone vizuri kabisa ili asiweze kupata kitu kinaitwa 'hernia'. Vinginevyo kila kitu kipo sawa sasa, tumshukuru Mungu.

"Asante sana daktari, kwaio lini tutaruhusiwa kurudi nyumbani?"
"Nataka nimtizame usiku huu kuhakikisha yuko sawa. Akiamka kesho vizuri nitaruhusu muondoke"

Usiku ule dada yake aliondoka baada ya kuhakikishiwa Tony yuko salama.

Mimi nilikaa hospitali chumba alicholazwa Tony nikiwa pembeni ya kitanda chake, huku machozi yakinitoka usiku kucha, nilikumbuka mambo mengi sana enzi za uchumba wetu jinsi tulivyopendana na kuona ulimwengu wote ni wangu.

Asubuhi yake baada ya kufanya malipo tuliruhusiwa kutoka, Tony alikuwa mkimya asiongee hata neno moja. Nikiwa na-drive nikawa kichwani nawaza kama Tony hataamsha tena hasira zake juu yangu.

Nikawa nikimuomba Mungu kimya kimya Tony asianze masuala yake tena.

"Darling uko sawa?" Nilimuuliza baada ya kufika nyumbani na kumlaza chumbani.

"Vicky, siko sawa. Unajua nini? Ninajuta kukuoa wewe. Sidhani kama kweli mwanaume apatae mke amepata kitu chema na kupata kibali kutoka kwa Mungu kwa sababu wewe ndio chanzo cha mimi kutokuwa na furaha na kujawa na huzuni.

Nikamshangaa Tony, sikumuelewa!!!

"Unajua nini, nilipoamua kukuoa wewe nilikuwa na mipango mingi. Nilifahamu ni nini ninataka. Nilitaka mwanamke ambae atanipenda na kunifanya niwe na furaha. Nilitaka maisha ya furaha, faraja na amani.

"Nilitaka kujenga nyakati nzuri zenye ubora wa hali ya juu katika ndoa yetu wawili tu mimi na wewe kabla hata hatujaanza kuzaa.

"Ila sijafanikiwa kupata lolote kati ya hayo, ikawa ni matatizo tu hili baadae linakuja hili. Tupo kwenye ndoa kwa miezi tisa tu na tayari nimeshachoka"

"Tony, kwanini unanilaumu mimi kwa hayo? Kwanini? Kipi cha msingi ambacho mimi nimekifanya ambacho kimeharibu hiyo unayosema furaha yako?"

"Nisikilize Vicky, baada ya ndoa tu ilinichukua wiki mbili nzima wewe kuniruhusu kufanya tendo la ndoa na kuiondoa bikira yako. Honeymoon yetu hata sikuifurahia kwakuwa ulikuwa ukinizuia kufanya tendo la ndoa.

Baadae sana Baada ya kuniruhusu kutoa bikira yako kwa mbinde kweli ukaanza wenge lako la kutaka mtoto na kufanya tendo la ndoa liwe linaboa kila mara.

"Kila nikikueleza kwamba tusubiri kwanza tufurahie ndoa yetu kabla hatujaanza kuzaa na kulea wewe unakua mbogo. Kila nikitaka kufanya tendo la ndoa kwa style tofauti wewe hutaki unataka missionary style kwa madai kwamba ndio style nzuri ya kupata ujauzito.

Kwa wenge lako la kutaka mtoto mapema baada ya miezi mitano tu ukaanza huo mfungo wako na kwa sababu ya mawazo na frustration ulizonipa nikawa sina furaha na stress juu.

"Jana asubuhi nikaenda kufanya mazoezi na baiskeli yangu na kutokana na stress na mawazo uliyonisababishia wewe nikapata ajali.

"Unafahamu wewe ndio umenisababishia haya? Nilikuwa nikikufikiria wewe mpaka nikapoteza concentration na shetani alivyo mpumbavu was trying to crack a joke, testicular trauma? I am tired madam"

Nilikaa kimya nisijue lipi la kuongea, zaidi zaidi hasira zikawa zikinipanda.

"Unathubutuje kuniambia hayo Tony? Kwanini unanilaumu mimi kwa kuwa na huzuni na kukosa hiyo furaha yako! Kila siku naamka kukuombea na hii ndio namna unavyonilipa?

"Sio wewe ambae wakati unanioa mtaji wa kampuni yako ulikua na kufikia kutengeneza faida kubwa? Unathubutuje kunitukana na kunilaumu mimi sasa hivi!! Sitaruhusu shetani aendelee kukutumia tena Tony, amekutumia vya kutosha!

"Haya maongezi yameisha Tony, sasa hivi fanya lolote unalotaka. Nikasimama pale kitandani na kutoka nje huku nikiwa nimeghafirika mno. Na kwa mara ya kwanza tena nikaona bora ningekuwa single tu.......

ITAENDELEA.....
 
NDOA YANGU

EPISODE -07

Maongezi yangu na Tony yalinifanya nitambue kuwa Tony hanithamini tena kama mke wake hivyo basi nikafanya maamuzi ya kumpa nafasi.

Nikampigia simu mama yangu na kumwambia narudi nyumbani kuwasilimia na nitakaa kwa wiki moja. Nilimshawishi kwa kumdanganya kuwa Tony amekubaliana na mimi.

Mama alikubali na nikapaki begi langu vizuri tayari kwa safari ya kwenda kwetu. Asubuhi yake nikamwambia Tony kuhusiana na safari yangu.

"Nilikusikiliza yote uliyoniambia jana Tony na nimeonelea wote tupeane nafasi kwanza. Nachukua break naenda kwetu kwa wazazi wangu" nilimweleza Tony.

Tony akatikisa kichwa chake na kusema, "unatakiwa ujionee hata aibu Vicky. In fact hata wakisema wanawake bora wasimame inatakiwa ufiche uso wako kabisa kwa aibu. Umeshindwa kutunza nyumba yako, umeshindwa kumridhisha mume wako na baada ya kutatua hayo matatizo umeonelea bora uyakimbie?"

Tony, nimekataa wewe kunidhihaki na kunitukana. Nilikaa kimya wakati unanitukana jana na sio kwamba mimi nitaendelea kukaa kimya tu uendelee kunitukana. Umesema uwepo wangu unakupa huzuni, sasa hivi nataka nikupe nafasi. Naenda kuchukua muda wangu kuomba kwa ajili yetu."

"I don’t freaking need your prayers madam. In fact hata Mungu hatajibu hayo maombi yako kwa sababu Mungu ameshakueleza kila kitu cha kufanya kwa mume wako katika Biblia. Sitaki uniombee mimi."

"Eee kwahiyo ile siku nimenunua lingarie na mafuta ya massage na ukaniacha nikining'inia tu usiku kucha usitokee nyumbani nayo utasemaje? Sikuwa natimiza majukumu yangu? Umechanganyikiwa Tony. Hujui ni nini unataka!"

"Unataka kuondoka? Sawa! Get the hell out but you just might not meet this marriage when you come back...nakwambia hutaiona tena hii ndoa ukirudi"

"Kama nilivyokwambia Tony, nachukua muda mbali na wewe naenda kuiombea hii ndoa, hayo maneno yako yakashindwe. Mungu ata-sustain nyumba yetu" nikamwambia Tony.

Akatingisha tena kichwa chake, akafumba macho, akavuta shuka akimaanisha amemaliza maongezi na mimi. Nikachukua mabegi yangu na kuelekea Airport.

Nikaenda ofisi za wakala wa usafiri wa anga na kununua tiketi ya ndege ya Fastjet ya kuelekea kwetu Mwanza iliyokua ikiondoka saa nne asubuhi.

PASIANSI, MWANZA, TANZANIA.

Usiku wake nikiwa nimeshafika nyumbani mapema tu mchana, nikiwa nimekaa na wazazi wangu sebuleni mama alikuwa akijaribu kunipigisha story za hapa na pale.

"Ehee kwaio kwanini Tony amekupa ruhusa ya kuja huku mama angu?"

"Mama, Tony yuko busy na kazi, hata baba nimemwambia hapo kabla"

"Kwaio ameshindwa hata kuja kutusalimia mara moja pamoja na wewe halafu ageuze hata kesho. Hatujamuona tokea ile siku ya harusi."

"Si ndio maana nipo hapa mama? Atleast umeona hata mmoja wetu, ukiniona mimi umemuona Tony..si unajua tu mwili mmoja hahaaa." Nikamwambia na kucheka.

"Ahaa, hamna tatizo. Nimejaribu kumpigia baada ya wewe kufika kumwambia kwamba nimempokea mke wake lakini hajapokea simu" mama aliongea.

"Nina uhakika atakupigia kesho, atakuwa amepumzika mapema leo ukizingatia ni weekenda halafu mimi sipo." Nilimwambia mama.

”Sawa mwanangu, ila Vicky vipi maisha ya ndoa? Ninaimani unamtii mume wako na kumjali vya kutosha." Mama aliongea.

"Mama, kwani Tony amelalamika kwako? Najitahidi kadiri ya uwezo wangu."

"Mbona unajishuku Vicky? Kila kitu kipo sawa kweli huko ulikotoka? Ninajua kuchelewa kupata ujauzito hakukupi pressure."

"Hapana mama, tuko sawa kabisa. Kila kitu kipo vizuri."

"Usiwe na pressure ya mtoto. Hata mwaka haujaisha bado. Mimi na baba yako tulisubiri miaka mitatu kabla hatujampata kaka yako wa kwanza na baada ya hapo mambo yakatuendea vizuri. Hivyo usijali kila kitu kitakuwa sawa." Mama alimaliza.

"Nafahamu mama...." Mara tukasikia mtu akigonga mlango.

"Mama unategemea mgeni yeyote usiku huu. Ni saa tano na nusu sasa na baba ameshaenda kulala."

"Hapana mwanangu sina ugeni wowote, inaweza kuwa mmoja wa majirani zetu anahitaji kitu nenda na ufungue mlango."

Nikiwa ninaosogelea mlango ili kuufungua, niliangushwa chini kwa nguvu na mlango uliofunguliwa kwa nguvu. Macho yalinitoka na kupiga kelele, walikuwa watu wanne waliovalia kofia zilizoziba uso mzima na kubakiza mdomo, macho na pua wakiwa wameshika mapanga. Nilifunga macho yangu na kuanza kusali.

"Sawasawa sali kwa bidii mtoto mzuri, unaweza ukakipata unachokiomba" sauti nzito na mbovu ilisikika kutoka kwa mmoja wapo wa wale watu watatu.

Mara wakaanza kunivuta nywele zangu na kunipeleka mpaka sebuleni. Nikamuona mama yangu akiwa amejibanza kwenye kona ya sebule akilia mno, bila shaka alisikia zile purukushani.

Tulikuwa tumevamiwa na majambazi!

SIKU TANO BAADAE.

Niliamka tena huku nikiwa napiga kelele kama kichaa. Imekua ni kawaida yangu kushtuka na kupiga kelele kama mwendawazimu tokea ule usiku mbaya kabisa katika maisha yangu. Usiku tuliovamiwa na majambazi.

Baba yangu alikuwa pembeni yangu, akinifuta machozi yaliyokuwa yakinitoka kwa wingi.

"Usijali Vicky. Upo sawa na salama kabisa. Baba yako nipo hapa."

"Baba naogopa, Tony bado hajaja."
"Nafahamu mwanangu, Tony hajaja. Nitampigia simu tena. Jitahidi uwe na nguvu kwanza, sawa mwanangu?"

"Hapokei simu zangu baba, tokea umemwambia like tukio hajapokea tena simu yangu baba!!"

"Usijali mwanangu atakupigua tu, labda alipatwa na mshtuko baada ya mimi kumsimulia lile tukio. Tusubiri atulie atakupigia tu"

Baba alipotoka chumbani kwangu na kuniacha peke yangu nikaanza kukumbuka lile tukio. Usiku mbaya kabisa katika maisha yangu...naweza kuuita 'evil night'.

SIKU TANO NYUMA.

Nakumbuka baba yangu alifuatwa chumbani na wale majambazi na wakamtaka awape pesa. Nakumbuka walimpiga na ubapa wa panga na kusachi chumba kizima. Aliwapa shilingi laki tano hivyo wakadhani anazo pesa nyingine kwani asubuhi yake alikuwa ametoka kuuza ng'ombe zake 88 huko wilayani Magu.

Baba hakuwa na Cash, pesa zote aliweka benki. Nakumbuka niliwaongezea shilingi laki moja niliyokuwa nayo na mwanaume mmoja kati yao akaniambia ninamtukana kwa kuwapa shilingi laki moja tu.

Nikiwa ninawaomba msamaha, yule jambazi aliniangalia kwa macho fulani ambayo nilijua anataka kufanya nini kabla hajaniambia.

"Tafadhali jamani, mimi nimeolewa. Ninawaombeni msinifanye mnachotaka.kunifanya. Nawaomba for christ sake!

"Kwaio kama umeolewa unafanya nini nyumbani kwa baba na mama. Mume wako hakuridhishi ee mama? Ngoja nimsaidie hilo suala. Anahitaji msaada." Yule jambazi aliongea.

Niliomboleza na kuwaomba wasinibake, mama na baba nao wakaomboleza kwa kuwapigia magoti wale watu wabaya na jawabu walilowapa ni kwamba wamesikia ombi lao na kitu pekee watachokifanya sio kunibaka mbele yao.

Majambazi wawili wakabaki sebuleni wakiwalinda baba na mama na wengine wawili wakanivuta mimi mpaka chumbani. Nilipigana kadiri ninavyoweza lakini walinizidi nguvu.

Mmoja akanishikilia na mwingine akafanya mambo yake, maumivu niliyoyapata sijawahi kukumbana nayo. Nilimkumbuka mume wangu Tony, nikajilaumu kwanini niliondoka kwa mume wangu, kwanini niliwadanganya wazazi wangu...

Nikakumbuka jinsi Tony alivyonizuia nisiondoke na kumwacha. Nililia mno, yule jambazi aliendelea kunifanyia kitendo cha kinyama na dakika 30 baadae akawa amemaliza.

Baada ya yuke jambazi kumaliza, wakaambizana waondoke haraka...wakaondoka na kutokomea kabisa!

Niliumia mno, kwa mara ya pili tena nikamlaumu Mungu na kumuuliza maswali mengi. Ukimya wake ulinipa simanzi na nikajidharau mno!

MUDA HUU.

Zimepita siku tano tokea nifanyiwe like tukio la kinyama ule usiku, siku tano baada ya baba kumpigia simu Tony na kumtaarifu na siku tatu tokea nitoke hospitali ya Bugando, bado Tony hajaja na hapokei simu tena....

Sina nilichobakiza kusema nitaiishi kesho, nipo radhi nife hata sasa hivi......

ITAENDELEA....
 
NDOA YANGU

EPISODE -08

Baada ya miezi mitatu ya kumpigia simu Tony bila mafanikio yoyoye hatimaye nikakata tamaa. Nikajua ndoa yangu imeshavunjika. Nililia vya kutosha, na hasira zilinifikia kiwango cha mwisho kabisa.

Nikajidharau nafsi yangu hata nguvu ya kusali ikanikimbia..sikuwa nasali tena. Nilijaribu kutafuta maana ya ukimya wa Tony kwa njia tofauti lakini jibu lake ilikuwa ni kwamba Tony hanipendi tena kiasi cha kupigania ndoa yetu.

Nilimtumia text za aina mbalimbali, lakini kwa miezi yote mitatu hakuwahi kujibu hata moja ingawa zilikuwa zikipokelewa. Sikuweza kuelewa inakuaje mwanaume anakua kimya kiasi hicho wakati amesikia kabisa mke wake kuwa amebakwa!!

Ile Ijumaa mchana Kama kawaida yake mama alikuja chumbani kwangu na kuniuliza ni nini kimetokea kati yangu na mume wangu. Alikuwa ameshaanza kugundua kuwa kuna tatizo katika ndoa yetu ila kila siku nilikua ninamkatalia na kumwambia kila kitu kipo sawa.

"Vicky, unajua nini? Mimi na baba yako tumejaribu vya kutosha. Umekaa nyumbani kwetu mwezi wa tatu huu na mume wako hata simu hapokei. Huwezi kusema hakuna tatizo huko ulikotoka. Mimi nimeolewa mwaka wa 35 sasa na ninajua mengi ya ndoa kuliko wewe uliekaa miezi 12 tu"

"Mama, please sina hata nguvu za kuanza kubishana hapa."

"Sawa, kama ndio hivyo mimi na baba yako tumeonelea kwamba huwezi kuendelea kuishi hapa. Hatuwezi kutunza mke wa mtu sisi. Na kwa kuwa wewe na mmeo mmeshindwa kutuheshimu kiasi ya kutafuta ushauri kwetu, basi ni bora urudi kwa mume wako au kokote kule utakapoona wewe panakufaa ila hauwezi kuendelea kukaa hapa na wakati wewe ni mke halali wa mtu."- mama alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hasira."

Nikiwa bado nashangaa maneno mazito aliyoniambia nikamwita; "Mama?"
"Ndio mwanangu"
Nikawa sina namna nyingine tena, maji yamenifikia shingoni! Sina Plan B!!

"Mama, Tony na mimi tuna matatizo makubwa, ndoa yetu ndio kwanza ina miezi 12 na bado hatujui ni namna gani tutasonga mbele."

"Sawa mwanangu, sasa nieleze kila kitu, mimi nakusikiliza, usinifiche chochote."

Hivyo basi, nikakaa saa moja nzima nikimuelezea kila kitu kilichotokea katika ndoa yetu kuanzia ule usiku baada ya sherehe ya harusi nyumbani kwa Tony, honeymoon mpaka ile siku nimeondoka kwa Tony!

Kwa mshangao wangu mama hakuingilia kati wakati namwelezea wala hakunikaripia. Nilitegemea aanze kunifokea wakati nikiendelea kumuelezea lakini hakufanya hivyo, alitulia kimya akinisikiliza. Utulivu wake ulinishangaza.

Baada ya kumaliza kumsimulia mama akaanza kuongea...."Heheheeee Vicky weeee mwanangu"...akaanza kuongea kwa kisukuma huku ameshika kichwa (akimaanisha nimeharibu dunia)

"Mama, kipi mimi nimekosea? Inakuwaje Tony amenitelekeza hapa? Mapenzi yake ni ya mashaka mama, hanipendi kama mke wake mama!!" Nikamweleza mama huku nikiwa na hasira na kukata tamaa.

"Jambo la kwanza mwanangu lazima uhame hilo kanisa. Hiyo aina ya mama mchungaji wa kanisa lako sio mtu mwenye hekima kabisa na hukupaswa kumsikiliza. Kwanini hukunipigia mimi mwanangu? Kwanini hukuongea na mtu mwingine mbali na mama mchungaji wa hilo kanisa lako?"

"Mama, wewe ndiye uliyenieleza kwamba masuala ya ndoa yangu yawe siri."

"Hapana mwanangu, sio wakati mambo yanatuendea kombo, wote hua tunahitaji msaada"
"Sawa mama, sasa tunafanya nini? Unafikiri kuna nafasi ya Tony na mimi kurudiana tena?"

"Ndio mwanangu, mimi na baba yako tumekabiliana na vita vikubwa sana katika kipindi cha ndoa yetu. Ndoa inapigwa vita sana, tunapigana, tunashambulia, tunashinda. Na kesho tena vita mpya inaibuka.

"Kamwe hatukukata tamaa, vita hii huisha pale unapositisha mapigano. Vicky endelea kupambana mpaka ushinde hii vita, hakuna mwisho hapa. Ulifanya maamuzi ya hatari na ukachukua hatua zisizo sahihi hata kidogo."

"Mama, vipi kuhusu Tony? Nae amechukua maamuzi yasiyo sahihi pia."

"Ndio, nitaongea na Tony lakini nataka niongee na wewe kwanza. Nilikwambia usijipe pressure ya kupata mtoto. Atakuja tu! Hukutakiwa kufunga na kumnyima mume wako tendo la ndoa, sio mimi nilekwambia chakula akipendacho mume kuliko vyote ni tendo la ndoa? Mbona umeniangusha mwanangu?

Hata Biblia iko wazi kabisa katika hili, Waraka wa kwanza wa paulo mtume kwa Wakoritho 7:3-5 paulo anawaambia, "Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; Vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu."

"Vicky, mumeo hakupatana na wewe kuhusu kufunga, ulilifanya hili jambo pele yako..hata hivyo ulitakiwa umpe haki yake ya ndoa kati ya saa kumi na mbili jioni unavyofungua na mwisho saa sita siku inapoanza.

"Vilevile Vicky hukutakiwa kukimbia nyumbani kwako bila hiyari ya mumeo na kuja kujificha huku. Kukueleza ukweli, Ni mpaka Mungu aingilie kati kwa Tony kuja kulala na wewe tena."

Umesahau yale niliyokuusia kipindi unaolewa? Ngoja nikukumbushe yale maneno mwanangu nilikueleza haya;

Nilikufundisha jinsi ya kuheshimu mume, na kutokuwa na hasira zisizo na msingi. Lakini kama utafanya vinginevyo, hutakuwa binti yangu niliyekuzaa bali mwanamke mwenzangu.
Binti yangu, nilikueleza unamuona mumeo? Ni gentlemen haswa! Ila usichukulie faida ya yeye kuwa gentlemen kumletea mizengwe.

Nilikwambia Usilete ujinga dhidi yake. Mwanangu unaona hili kovu kwenye paji langu la uso? Baba yako ndio alinipa hili kovu.
Alinivumilia muda mwingi sana, ila siku moja from nowhere nilimuudhi tena, najua halikuwa lengo lake ila hasira zilimfika hapa akanipiga mara moja na kunumiza.

Mamii, Wanaume wanachukia pale unapomwambia "HUWEZI". Anajua anaweza akafanya zaidi ya hapo lakini anafanya hivyo kukulinda asikuumize. Nilikueleza Binti yangu pale kutakapokuwepo na kutouelewana, jaribu kunywa maji, huwezi ukaongea huku maji yapo mdomoni.

Nikakueleza kuwa sasa una familia mbili. Una bahati sana mamii, Vumilia na heshimu familia yako kama ulivyokua ukifanya hapa. Jifunze kuwakarimu watoto wa majirani zako, na karibuni watoto wako wataizunguka meza yenu kwa upendo mkila pamoja chakula kwa furaha.

Nikakuonesha lile hotpot langu kubwa! Nililinunua wakati bado sina hata mtoto mmoja, kabla ya kuwazaa ninyi. Lakini mara kadhaa nilipika chakula na kulijaza na kula pamoja na watoto wasio na pa kula.

Nilikifunza kuwa mkarimu, wakarimu wageni walau hata kwa maji ya kunywa. Usinyanyapae wageni, usidharau ndugu wa mumeo bali walete kwa pamoja. Jifunze ku appreciate jitihada ndogo zinazofanyika na karibuni watajifunza mengi kutoka kwako na watakupenda.

Nilikwambia Pale kutakapokuwa na kutokuelewana, usirudi hapa nyumbani. Msuluhishe wenyewe huko huko na jenga nyumba yenye furaha. Nilijenga yangu na baba yako amekuwa akifurahia mpaka kesho.

Nikakwambia wazi kabisa kwamba Mamii wanaume wanapenda chakula kizuri. Wanapenda vyakula vyote cha jikoni na cha chumbani. Usimnyime chakula cha aina yoyote eti kwa sababu hamna maelewano. Hiyo ni sumu katika ndoa!

"Wote wawili mmeharibu mambo. Hili tatizo halikutakiwa kufikia hatua hii. Jambo la kwanza kesho asubuhi , tutarudi wote Dar es salaam, tunaenda kumuona mume wako."

KAWE, DAR ES SALAAM.

NI Kweli, Jumamosi asubuhi tulipanda ndege ya saa mbili, tukafika Dar es salaam saa tatu asubuhi. Mpaka saa tano asubuhi tulikuwa tumefika nyumbani kwangu. Nilipouona tu gari ya Tony imepaki uani, moyo wangu ukaanza kudunda kwa kasi mno.

Nikatamani asiwepo nyumbani, ingawa mama alishampigia simu jana usiku kumuelezea ujio wetu. Tulipoukaribia tu mlango Tony akaja kutufungulia. Nafikiri alituona kupitia dirishani wakati tukiingia.

Akamsalimia mama kwa kisukuma, lakini mimi akanipotezea....hakunipa salamu kabisa, mama akatabasmu! Nikawaacha sebuleni mimi nikapitiliza moja kwa moja chumbani kwangu. Kila kitu nilikikuta kama nilivyokiacha na kwa uchunguzi wangu sikuona dalili yoyote ya mwanamke kuishi na Tony.

Nikamsikia mama akiniita sebuleni na haraka haraka nikaenda kujiunga nao.

"Mama, Vicky hataki ndoa. Kwa mwaka mmoja tu wa ndoa yetu ameshanionesha dharau, kiburi na kutonitii kwangu na kwa nyumba hii. Me nimechoka.kwa hayo. Hafikirii angekuwa mwanaume mwingine, asingeanza kuchepuka kwa hivyo vituko alivyokua akinionesha??"

"Mama mimi Nimekua muaminifu pale Vicky aliposhindwa kuwa muaminifu kwenye majukumu yake kwa ndoa, nimevumilia kipindi chote hicho mama sikuwahi kumsaliti hata siku moja......." Tony akawa akiongea kwa hasira huku akilengwa na machozi......

_____________________________

Je vipi kuhusu hali ya afya Vicky?, Je kwanini Tony alikaa kimya muda wote wa miezi mitatu asipokee simu wala kujibu texts za Vicky? Je vipi kuhusu mustakabali wa ndoa yao? Ama hakika maswali ni mengi, Usikose sehemu inayofuata...

ITAENDELEA...
 
NDOA YANGU


SEHEMU YA MWISHO

"Tony tafadhali usitudanganye sisi kuhusu uaminifu. Kwahiyo unataka tukupe tuzo kwa kuwa sio msaliti? Nikadandia na kumkatisha aliyokua akiongea kwa kumwambia hayo!

"Funga mdomo wako Vicky, tena utulie kabisa, stupid woman" mama akanikaripia huku Tony akitingisha tu kichwa chake akionekana kusikitika. Nikajisikia aibu mama kunikaripia mbele ya Tony.

Nikawa kimya nikisikiliza mama na Tony wakiongea. Nikasikiliza mambo ya ukweli kabisa Tony aliyokua akimuelezea mama na nikayaona maumivu yake dhahiri kabisa alipokua akimsimulia mambo niliyokua ninamfanyia.

Nikaelewa uzito wa makosa niliyokuwa nikimfanyia Tony. Muda alipoanza kuzungumzia tu lile tukio la mimi kubakwa, nikaona machozi yakimtoka. Akakaa kimya, akainamisha kichwa chake chini...akachukua kitambaa chake na kujifuta machozi, kiukweli na mimi niliumia mno!

"Mama, nilimuonya Vicky. Nilimuonya asiondoke nyumbani. Mpaka leo hii sijaweza kuiondoa picha ya hilo tukio la mke wangu kubakwa kichwani kwangu. Ninaanzia wapi? Alikuwa akikataa kufanya tendo la ndoa na mimi kwa kisingizio cha mfungo na kwenda kumpa tendo la ndoa jambazi kirahis rahisi tu..aaah mama naumiaaa!!!"

"Tony, tafadhali usiseme alimpa jambazi kirahisi. Ule ulikuwa uvamizi na walikuwa na silaha. Wote bado tunayo maumivu juu ya lile tukio hasa mke wako.

Maumivu aliyonayo juu ya lile tukio ni makubwa mno. Anahitaji muda mwingi sana mpaka asahau na kuwa sawa tena. Na tushukuru Mungu kwani ameshapima mara sita sasa hajaambukizwa ugonjwa wa zinaa wala hakupata ujauzito." Mama akaongea.

"Nilimuonya mama, nilimuonya lakini." Tony akaendelea kusisitiza.

"Ni kweli mwanangu Tony, majaribu hayana budi kuja, ni vile tu kuwa na moyo imara wa kusamehe"

Mama akaanza kuongea na Tony kuhusu sisi kuwa na mawasiliano mazuri, kuelewana na kuwa wepesi kusameheana. Akaongea mengi mno ambayo yalinigusa moyo wangu moja kwa moja na nikajawa na huruma nyingi na majuto kila nilipokuwa nikimuangalia Tony usoni.

Nafsini nikajiambia huyu ni mume wangu, kati ya wanawake wote amenichagua mimi peke yangu, kwa kweli sikustahili kumfanyia yale niliyokuwa nikimfanyia, naijutia nafsi yangu!!

Baada ya ushauri na maneno mengi ya busara kutoka kwa mama, Tony akaanza kuelewa na kupunguza hasira juu yangu.

"Wote wewe na mmeo mnatakiwa mfanye maombi, muwe wavumilivu na mjifunze kuwasiliana na kukubaliana jambo."

"Mama, kusema ukweli, mimi sina uhakika kama hii ndoa bado ipo. Kwa sababu mimi sijui hata nitaanzia wapi na Vicky."

"Tony mwanangu, msimpe shetani ushindi wa mezani kiwepesi hivyo, wote mnatakiwa muanze kwa kusameheana kwanza na baada ya hapo mambo mengine ni hatua kwa hatua. Mnaanza na maongezi, yale maongezi ya karibu sana yatakayounganisha mioyo yenu, mshirikiane maumivu na hofu na baada ya muda fulani wote mtajikuta mkiwa vizuri tena."

"Sawa mama, asante sana."

Kwa kuwa mama alikuwa na tiketi ya kwenda na kurudi, Saa moja baadae mama akaondoka na kuelekea Airport kurudi Mwanza. Akagoma kabisa kubaki hata kwa siku moja tu akidai amemkumbuka mume wake na anahofu kumuacha peke yake na wala hakutaka tusimsindikize bali akataka tumkodie tax tu.

Na kwa hilo nikajifunza jambo jingine kubwa tu, kuwa karibu na mume wako kadiri unavyoweza!

Baada ya mama kuondoka tu, nikamfuata Tony na kumkumbatia kwa nguvu.

"Baby, I am sorry, nisamehe kwa yote niliyokufanyia nakiri kwako na mbele za Mungu sitarudia tena, kuanzia sasa nitakua nikikusikiliza wewe tu, na zaidi wazazi wako na wangu basi...i love you my Tony!"

"Vicky, i am sorry too, nisamehe kwa kuwa sikuwa na wewe katika kipindi kigumu cha maumivu ya kutendewa unyama na wale mafedhuli.

"Ukweli ni kwamba nilichanganyikiwa baada ya baba kunieleza lile tukio na mpaka sasa hivi sijui nitawezaje kuliondoa lile tukio kichwani mwangu" Tony akanieleza hayo huku nae akiwa amenikumbatia.

”We will babe”, nikamwambia Tony kwa kujiamini ”we will, one day at a time”.

LEO HII.

Tupo likizo Nchini China, mimi na mume wangu Tony na mwanetu Jayden akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu. Siku zote namshukuru sana Mungu kwa kunipa Tony wangu! He is such a darling...i love him to death!!!

T H E E N D !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom