bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
MTOTO WA MAAJABU: 1
Mariam alikuwa na mawazo sana kutokana na ile
mimba aliyobeba kupitiliza muda wa kawaida wa
kujifungua yaani miezi tisa kwani kwasasa mimba
yake ilifikisha miezi ishirini na nne yani miaka miwili
bila ya dalili zozote zile za kujifungua na kumfanya
awe na mawazo zaidi, ukizingatia ameshajaribu njia
nyingi ila imeshindikana na hakuwa kabisa na dalili
ya kujifungua wala nini.
Mumewe alimuona mkewe jinsi ambavyo anakosa
raha kila siku, mara kwa mara huwa anamuuliza ila
leo aliamua kukaa nae na kuongea nae vizuri,
alimuuliza
“Mke wangu tatizo ni nini?”
Ila Mariam hakujibu kitu kanakwamba hakusikia
chochote, hii ni kutokana na mawazo ya mbali sana
aliyokuwa nayo hadi mumewe ikabidi amuite kwa
sauti,
“Wewe Mariam, wewe!!”
Ndipo Mariam alishtuka na kumuangalia mume
wake kisha akamuuliza,
“Kumbe unaongea na mimi?”
“Ndio, unajua nakuona huna raha kabisa”
“Naitoa wapi raha mume wangu? Mimba gani hii
jamani! Kwanini hii mimba inanieleleza hivi?
Nimekosa nini mimi? Miaka miwili hii imepita na
mwezi huo unakatika yani mimba imekaa miezi
ishirini na tano kweli!! Hakuna dalili ya uchungu
wala nini halafu hospitali wanasema nisubiri tu,
kwakweli nimechoka”
“Halafu tumbo limekuwa kubwa sana mke wangu
kupita kawaida!”
“Yani hadi kero mume wangu, nachukia hatari basi
tu ila hii hali inanikera sana”
“Ngoja, kesho tutaenda tena hospitali ili kujua ni
kwanini inakuwa hivi ili kama inawezekana hata
operesheni wakufanyie”
“Kila tukienda wanazingua, mimi nimechoka
kwakweli”
“Sawa, ila tutaenda hospitali nyingine lazima tupate
suluhisho la hiyo mimba mke wangu. Mimi binafsi
sijapenda”
“Bora iwe hivyo, kwakweli nimechoka tena
nimechoka sana. Hata mimi sipendi kabisa hali hii,
mtu unakaa na mimba kama unataka kuzaa tembo!!
Ndio mambo gani haya!”
“Pole mke wangu”
Kwakweli Mariam hakuwa na raha kabisa kutokana
na ile mimba, sababu ilimkosesha raha kabisa na
alishindwa kufanya mambo yake mengi sana.
Kesho yake kama ambavyo walipanga na mumewe,
walienda hospitali kwaajili ya kuangalia maendeleo
ya ile mimba na kwanini ilipitiliza muda wake kiasi
kile, waliamua kubadilisha hospitali kwani waliona
labda hospitali ambayo huwa anaenda hawana ujuzi
mzuri kwani alikuwa ameshachoka kuibeba ile
mimba, moja kwa moja walikutana na daktari
ambaye alikuwa ni mtaalamu wa mambo ya
wanawake na kuongea nae na kuhusu swala zima la
kupitiliza kwa ule ujauzito,
“Umesema imepita miaka miwili?”
“Ndio, tena sio miaka miwili tu maana na mwezi
ushakatika sasa, imepitiliza miezi ishirini na tano.
Kwakweli nimechoka, wakati watu hubeba mimba
kwa miezi tisa tu!! Sasa kwanini mimi inakuwa hivi
jamani!”
“Pole sana, ila ngoja kwanza tukakupige ultrasound
halafu nijue ni kitu gani kinaendelea”
Walikubali na moja kwa moja walienda kwenye
vipimo, majibu yalipotoka walienda kuongea na
daktari,
“Kwanza hongera
sana, inaonyesha umebeba mapacha wa kiume”
“Kheeeee mapacha tena!”
“Mbona unashangaa sasa? Hupendi mapacha au?
Wanawake wengi sana hupenda kuzaa mapacha,
kwani ni raha kuishi nao utapata shida kidogo tu
kwenye malezi kama kipato chako kidogo ila
mapacha ni watoto wazuri sana kwahiyo unatakiwa
kufurahi”
“Haya tuachane na hizo habari dokta, nitajifungua
lini maana nishachoka”
“Sijaona tatizo lolote kwenye mimba yako,
utajifungua tu kawaida”
Basi mume wa Mariam akamwambia daktari,
“Hivi kwani hakuna uwezekano wa mke wangu
kufanyiwa tu operesheni bila kusubiria huo
uchungu?”
“Kwahiyo mnataka kwa operesheni sio!”
“Dokta, nimechoka mimi sijui kama umenielewa
nilivyokwambia kuwa mimba hii imepitiliza miaka
miwili nadhani kitoto kitakachotoka hadi kitakuwa
kinatembea”
Dokta akacheka kidogo huku akitikisa kichwa na
kusema,
“Sawa, ngoja niwapangie siku ya kuja kufanya hiyo
operesheni”
Dokta akaangalia ratiba yake pale na kuwaambia
kuwa waende kesho kutwa kwaajili ya kufanya hiyo
operesheni.
Mariam alifurahi kwani alishachoka kwakweli, basi
walimaliza pale na kuondoka zao kurudi nyumbani
kwao.
Walipofika nyumbani waliongea kidogo ambapo
mume wa Mariam alimuuliza mkewe,
“Nakumbuka mara ya mwisho tulipopiga ultrasound
tuliambiwa ni mtoto mmoja, sasa leo imekuwaje
tena ni mapacha?”
“Yani na wewe unashangaa tu habari za mapacha
badala ya kushangaa swala la kukaa na mimba
miaka miwili jamani!! Yani mimi nimechoka, hata
wawe mapacha sijui vitu gani watoke tu, nimechoka
kwakweli”
Kiukweli Mariam hakuwa na raha kabisa ukizingatia
hii mimba ndio imesababisha hadi yeye na
mumewe kwenda kuhamia sehemu ya mbali kwani
akikumbuka watu wanaomfahamu walikuwa
wakimshangaa sana kuwa bado hajajifungua! Na
yeye ilikuwa inampa hasira sana wakimshangaa
ndiomana na mumewe waliamua kuhamia mbali na
kuishi wenyewe bila ya watu wanaowafahamu vizuri
kuwa karibu.
Mumewe alimuuliza Mariam,
“Leo ungependa kula nini?”
“Kama kuna chakula cha kuleta uchungu basi mimi
ndio nakitaka hiko chakula, sijui kama na wewe
unanielewa kuwa nimechoka!”
Mumewe hakuongea sana kwani alikuwa akijua wazi
muda mkewe njaa ikimshika basi huwahi kwenye
majungu mwenyewe na kutafutiza chakula, ila muda
huu sababu ana hasira ndiomana alijibu hivi.
Siku ilifika ambapo Mariam alitakiwa kwenda
kufanyiwa upasuaji, kwahiyo walijiandaa na vifaa
pamoja na mumewe na kwenda hospitali,
hawakuwaambia ndugu maana sio kwamba hii ni
mara ya kwanza kuamua hivi hapana, ila ilishawahi
kutokea na haikuwa na mafanikio.
Na ndivyo ilivyokuwa hata kwa siku hii, ilionekana
presha ya Mariam ipo juu sana kiasi kwamba
ilikuwa ngumu kwa yeye kufanyiwa upasuaji,
kwakweli Mariam alichukia sana na kurudi na
mumewe nyumbani.
“Jamani Juma, hali hii hadi lini mimi nimechoka”
“Pole mke wangu, ila mimi naamini tu kuwa
mambo yatakuwa sawa”
“Kama hao mapacha si watoke tu, loh nimechoka
sana”
Mariam aliamua kwenda kulala, wakati huo Juma
alimpigia simu mama yake na kumueleza kile
ambacho kimetokea,
“Kheeee mlienda tena hospitali halafu yametoka
kama yale yale?”
“Ndio mama”
“Khaaaa, mimi nataka mjukuu jamani. Kuna mtu
namsubiri kaniambia ataniletea dawa nyingine ya
kieyeji”
“Unadhani hiyo itafanya kazi vizuri mama?”
“Ndio, aliyeniambia safari hii namuamini, hana
mambo ya longolongo kabisa, kwahiyo hata msijali”
“Sawa mama”
Juma alienda kumpa hiyo habari Mariam na
kumfanya Mariam afurahi sana,
“Kheeee afadhari yani, nimechoka sana loh!”
“Usijali, hata mimi nakuonea huruma”
“Ila isiwe kama ile midawa ya kipindi kile jamani,
hakuna kitu kinafanyika wala nini!”
“Mama kasema kwasasa ni uhakika”
Basi Mariam alifurahi sana, na hapo hata kula siku
hii alikula vizuri tu.
Siku hii, alifika mama mkwe wa Mariam na
kumkaribisha pale kwao kwa furaha sana kwani
Mariam alichokuwa anataka ni kupata dawa tu, basi
yule mama alianza kuongea na Mariam pale kuhusu
dawa aliyomletea,
“Kwanza pole mwanangu unajua ni nini,
nimehangaika yani kuipata hii dawa balaa, unajua
mwanzoni nilijua umechezewa yani umerogwa!”
“Ndio nimerogwa mama”
“Hamna Mariam, nasikia kuna kosa umefanya”
“Kheeee kosa gani sasa ambalo mimi silijui?”
“Mimi silijui pia, ila nasikia kuna kosa umefanya,
kuna kitu ulikatazwa kufanya sijui kukila wakati una
mimba halafu wewe ukakifanya na ndio kimekuletea
matatizo hayo”
Mumewe akadakia,
“Inawezekana mama, maana wakati Mimba changa
khaaa Mariam alikuwa anakula hovyo hovyo yani”
“Hata mimi nakumbuka, yani mimba za wenzie
zikiwa changa huwa utakuta tunapatwa na
vichefuchefu na kula kula hovyo hatuwezi mpaka
mimba iongezeke kidogo ila Mariam khaaa ulizidi
mkwe wangu jamani nakumbuka kuna siku
nimekukuta unakula hadi mbegu za mapapai”
“Jamani mama, yani huwezi amini wakati mimba hii
ilivyokuwa changa nilikuwa natamani kila
kilichokuwa kinakuja mbele yangu na nilikuwa
sishibi, nakumbuka kuna vyakula vingine vilikula
hadi aibu kuvisema ila mbegu za mapapai ni dawa
mama”
“Kweli ni dawa ila sio kwa mtindo ule ambao
ulikuwa unakula wewe”
Mumewe akasema,
“Mimi nakumbuka, kuna siku Mariam ulikamata
kindege kidogo ndani ukakinyonga na kukichoma
halafu ukakila khaaa nilikushangaa sana, kwahiyo
inawezekana kweli ulikula vitu vya ajabu”
“Na ndio nilivyoambiwa wanangu, tunaambiwa
hakuna cha mchawi wala nini, inasemekana Mariam
hakurogwa wala nini ila kuna kitu alikosea, ila
nimepewa hii dawa itaenda kumsaidia”
Mariam hakutia neno kwa wakati huu kwani yeye
cha msingi alitaka kusaidiwa tu maswala ya kula
kula hovyo kwanza hakuona kuwa ni tatizo kwani
wenye mimba wengi huwa wanatamani hata vitu
visivyokuwepo, kwahiyo alikuwa akiwasapoti tu
sababu alikuwa akitaka dawa tu kwa muda huo.
Mama mkwe wa Mariam alitoa dawa ambazo
zilikuwa zimefungwa kwenye vifundo vitatu na
kuanza kumuelekeza Mariam namna ya kutumia,
“Ni Hivi, hili fundo la kwanza utaoga siku ya kwanza
yani unachanganya kwenye maji ya kuoga.
Ukishaoga mwenyewe unajimwagia haya maji ya
dawa, hili fundo la kwanza linabeba miezi yote kumi
na mbili yani mwaka mmoja ambao mimba hiyo
imepitilia, halafu siku ya pili utachanganya hili fundo
la pili kwenye maji na lenyewe litabeba mwaka
mzima, halafu hili fundo la tatu utachanganya
kwenye maji siku ya tatu na kuoga, na lenyewe
litabeba huo mwezi mmoja uliopitiliza, baada ya
hapo utapata majibu yake mkwe wangu, lazima
ujifungue, yani nitafurahije jamani! Nataka mjukuu
mimi. Halafu siondoki hivyo, ndio nimekuja moja
kwa moja kwani najua wiki hii hii mambo yatakuwa
tayari”
“Ooooh asante mama, kwahiyo naanza kuoga leo?”
“Ndio, leo leo Mariam, hujalichoka hilo tumbo au?”
“Nimelichoka tena nimelichoka sana”
“Haya, itabidi uanze leo”
“Ngoja nikaianze sasa hivi”
Mariam alichukua ile dawa na kwenda nayo ndani
huku akienda kujiandaa kuoga, basi mama mkwe
wake alibaki na mwanae pale wakiwa wanaongea
ongea kidogo.
“Kwakweli mama nakushukuru sana, nahitaji mke
wangu awe mzima”
“Usijali, mbona huyu anapona kabisa, hakuna tatizo
yule mzee niliyekutana nae unajua hajachukua hata
mia yangu. Kasema kambo yakiwa mazuri basi
nitaenda kumpa zawadi”
“Kheeee kweli huyo ni mganga mama”
“Ni mganga sana, ndiomana kasema ukweli kuwa
Mariam hajarogwa wala nini ila kajiroga mwenyewe”
“Ila sijawahi kusikia mambo haya kabisa mama,
yani nahisi kuna kitu kimejificha hatukijui mama
yangu”
“Tutajua tu hata usijali”
Basi wakaendelea tu na maongezi pale ila Mariam
hakurudi tena pale sebleni wala nini.
Mariam alipomaliza tu kuoga kwa ile dawa akaanza
kujihisi tofauti tumboni, yani kama vile wale watoto
wamefunga kamba tumboni wakiruka ruka.
Alikosa raha na amani kabisa, basi moja kwa moja
akaenda kulala, mumewe akamfata kumuuliza,
“Vipi tena, unajihisi vipi Mariam?”
“Kheeee makubwa yapo hapa jamani, yani hawa
watoto kamavile wanaruka kamba tumboni, yani hii
mitoto itakuwa mikubwa kabisa, mbona kunieleleza
hivi mimi jamani!”
“Pole mke wangu, ila hiyo ya watoto kuruka kamba
tumboni, kweli ni kioja ngoja nikamwite mama”
Mume wa Mariam alimuita mama yake ambapo na
yeye aliambiwa vile vile na Mariam, yule mama
aliupumua kidogo tu na kumwambia Mariam,
“Usijali Mariam, vumilia tu kila kitu kitakuwa sawa.
Naamini kuwa mambo yatakuwa sawa tu, vumilia
Mariam”
“Asante mama”
Basi walimuacha Mariam pale aweze kupumzika
huku wakiendelea na mambo mengine kama
kumtayarishia chakula maana waliona hali yake sio
nzuri kwa wakati huo ila sababu walitaka kuona ile
dawa ikifanya kazi, ilibidi tu wawe wapole na
wavumilie.
Usiku ule ndio Mariam alisema kuwa kidogo tumbo
limetulia na aliweza kukaa na kula chakula kwasasa
huku akiongea na mama mkwe wake,
“Siku hizi utaalamu mwingi, ushajua ni mtoto gani?”
“Mmmmh mama, kwasasa hata jinsia ya mtoto sio
ya muhimu kwangu, cha muhimu ni kushusha huu
mzigo tu”
Mumewe akasema,
“Ni mapacha mama, dokta kasema ni mapacha wa
kiume”
“Ooooh hongera mtoto wangu, ndiomana kuna
mambo ya ajabu yamefanyika hapa kumbe hawataki
hii baraka ije kwetu khaaa!! Hongera sana
mwanangu, umri wako umeenda ila kumbe utapata
mwanamke na atakuzalia uzao wa kwanza midume
miwili”
Mume wa Mariam aliangalia chini tu kiasi kwamba
mama yake alimuuliza,
“Mbona hishangilii sasa?”
“Nishangilie nini mama ikiwa mke wangu anateseka
kwa kiasi hiko? Sikujua kama mapacha ndio
wanasumbua hivi yani, bora angezaa mmoja tu”
“Hamna bhana, huyu uzazi tu umemuendea vibaya,
wala mapacha hawasumbui wala nini ila huyu uzazi
umemsumbua tu huu, sio sababu ya kubeba
mapacha tumboni wala nini!”
Mariam alikuwa kimya kabisa kwani alikuwa
akitamani tu muda ufike aweze kujifungua basi na
sio kuongelea kuhusu watoto aliowabeba tumboni
kwa zaidi ya miaka miwili.
Siku ya pili, Mariam anaenda kuogea tena ile dawa
kama ambavyo alipewa maelekezo na mama mkwe
wake ila baada ya kuoga tu akamsikia mtoto
tumboni kama akibinuka sarakasi na kumfanya
Mariam achukie sana.
Akaenda kwa mama mkwe wake kumlalamikia,
“Mama, yani huyu mtoto kama anabinuka sarakasi
tumboni”
“Khaaaa Mariam, si mapacha hao!! Watakuwa ndio
wanajiandaa kutoka”
“Jamani mama hadi tumbo linaniuma”
“Pole sana”
Mariama akaondoka zake na kwenda kulala ila
kiukweli leo hata kulala hakuweza maana tumbo
lake lilikuwa linacheza cheza muda wote na
kumkosha raha kabisa.
Basi alijigeuza hadi usiku ulifika na hata kula
aligoma kwa siku hii kabisa, yani kwa jinsi
alivyokuwa akijihisi tumboni ilimlazimu kuamua
kwenda kuoga usiku ile dawa ya siku ya tatu kabla
hata siku yenyewe haijafikia vizuri kwani alijihisi
kukereka kwa yale maumivu ya mtoto kujibinua
tumboni.
Sasa alipoanza kuoga na hii dawa akasikia sauti ya
mtoto mdogo,
“Mama, ndio hutaki niendelee kubaki tumboni
mwako?”
Mariam hakutaka kuifatiliza hii sauti wala nini bali
alijimwagia tu ile dawa ila alirudi akiwa na maumivu
makali sana,
“Jamani nakufa, jamani sijawahi kupatwa na
maumivu kama haya, nakufa jamani”
Mama mkwe wake alimfata na alivyomsikiliza vizuri
Mariam akajua tu ni uchungu umemuanza,
“Kheeee mbona mapema kabla hata hujamaliza
dawa?”
Mariam hakumjibu kitu kwani kiukweli alishamaliza
dawa, ule uchungu ulikuwa unamchanganya akili
yake haswaa, yani alikuwa akijihisi vibaya sana.
Basi usiku ule ule mume wa Mariam ilibidi
akatafute usafari ili waweze kuwahi hospitali ili
aweze kujifungua kwa huduma nzuri.
Damu nazo zilianza kummwagika Mariam na
kuonyesha kweli hapo mambo yameiva sasa, mama
mkwe aliendelea tu kumpa moyo,
“Jikaze Mariam, ndio ukubwa huo”
“Mama nakufa mimi, sirudii tena mimi khaaaa ndio
uchungu wenyewe upo hivi! Nakufa jamani, sio kwa
maumivu haya loh!”
Mariam alikuwa akipiga kelel tu, basi usafiri
ulivyofika moja kwa moja waliingia kwenye gari na
kuelekea hospitali.
Walivyofika hospitali, moja kwa moja Mariam
alipelekwa leba maana alionekana kuwa na hali
mbaya tayari.
Daktari alimpiga pale na kusema,
“Khaaaa mtoto katanguliza miguu, hapa hakuna jinsi
ni operesheni tu”
Basi wakaenda kuchukua karatasi za kusaini
waweze kumpeleka Mariam kwenye operesheni ila
muda ule ule wote walishangaa pale Mariam
akijilaza kitandani na mtoto akitoka vile vile akiwa
ametanguliza miguu, yani Mariam alijifungua
kawaida kabisa ingawa mtoto alikuwa katanguliza
miguu.
Kitu ambacho kilimshangaza Mariam, hakujifungua
mapacha bali alijifungua mtoto mmoja, kitu
kilichowashangaza pale leba wote ni kuwa mtoto
wa Mariam baada ya kuzaliwa alikaa mwenyewe
pale kitandani.