Simulizi: Msichana wangu wa kwanza

leadermoe

R I P
Feb 15, 2017
1,392
4,573
************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)

Upepo na jua ni mahasimu wa toka zamani, mara nyingi ubishani wao wa kutaka kujionyesha yupi ni bora kuliko mwenzie, ndio sababu pekee ambayo hutupatia jua kali sana. Jua ambalo huua mazao yetu na kusababisha ukame upelekeao kupotea kwa maisha ya binadamu, sijua peke vilevile hata upepo ukiwa kwenye ubishi huo, huweza kuvuma kwa kasi kikubwa ambachohumfanya binadamu apate tabu katika macho yake dhidi ya vumbi izolewayo na upepo.

Ilikuwa mida ya saa sita, kamili mchana mida ambayo wanafunzi washule nyingi za Tanzania hutolewa darasani kwa ajili ya kwenda makwao,kupata chakula chamchana ili waweze kurudi shuleni na kusoma pasina kuwazia chakula. Wakati yote hayo yakiendelea, ziliweza kusikika sauti za marumbano katika pande za duka la kina Nurdini, sauti zile zilikuwa zikibishana juu ya uandishi wa maneno uliokua ukiendelea kwenye moja kati ya karatasi iliyochanwa kutoka kwenye daftari ya mahesabu.

"Unatakiwa uandike i luv u, eti we boya unaandika kiswahili" Ni maneno ya Samir, aliyokuwa akimwambia rafiki yake Nurdin. Huku akiwa ameinyooshea kidole karatasi iliyokuwa ikiandikwa.

"poa lakini mbona huku chini tume sahau kuandika saini, unadhani mtoto atajua imetoka kwa nani?" Lilikuwa ni swali kutoka kwa nurdin, swali alilomtupia rafiki yake samir.

" we nurdini ni boya kichizi, hivi unataka tuandike saini ili iweje . Je, barua ikikamatwa na mwalimu unadhani utasalimika, jaribu kutumia akili hapa chamsingi ni kuandika bila saini kisha nikimpelekea nitamwambia imetoka kwa nani, kwanza malizia fasta;fasta kwani sasa hivi ni saa saba na dakika kumi na tano, zimebaki dakika ishirini tu wanafunzi waingie madarasani, si unajua wakiingia madarasani kumpata ilivyo inshu jombaa." Aliongea maneno yale samir na kuukata mzizi wa fitna juu ya swala la kuandika saini katika karatasi ile.

"Tayari nimeikili, ngoja nikusikilizishe maneno atakayo yasikia mtoto na ku acept my request" Aliongea nurdini.

"ok isome mzazi ilinimuwaishie dogo, siunajua tena hii ndo mida yenyewe?"

Baada ya kuruhusiwa na samir basi nurdini alianza kuisoma barua ile ambayo ilikuwa inasomeka hivi:

MPENZI WAKO,
S.L.P. MOYO,
2/1/2009.

Dear sumayah......

Salamu sana, natumaini utakuwa mzima wa afya, japo hofu inaendelea kunitanda ila naamini hivyo. Kuhusu mimi, usiwe na shaka kabisa, kwani mimi nipo safi ki afya. Dhumuni la barua hii si kwa ajili ya salamu pekee, bali kuna jambo nyeti ninalotaka kukujuza.

Mpendwa sumayyah dhumuni la barua, nikukujuza kuwa, nimezunguka mashariki na hata magharibi, bila kusahau kusini na kaskazini lakini kama wewe sijamuona. tafadhali naomba unikubalie ombi langu kwani ni wewe pekee ambae umeuteka moyo wangu. Kila ni kinywa maji huwa na kuona kwenye grass, hata nikilala huwa nakuota , shahidi ni rafiki yangu alie kuletea barua hii tafadhali nakuomba kubali ombi langu ili uuokoe moyo wangu.

Sumayah, wewe nimegundua wewe ni zaidi hata ya mambo yote muhimu ikiwemo chakula, malazi, na hata mavazi kwani kila wakati huwa nakuwaza wewe, misikufichi hadi muda mwingine huwa nachanganya mahesabu ya dukani kwa sababu yako sumayyah. U mrembo sana sumayah, maana kila ukipita karibu yangu huwa na jihisi kama nimetembelewa na malikia wa dunia.

Mapenzi si barafu eti yataganda na baadae kuwa kimiminika, wala mapenzi si dafu eti utayala na kuyanywa. Tafadhali unusuru moyo wangu, moyo ambao umeangukia ndani ya bahari ya mapenzi. Nadiliki kusema kuwa wewe ni mvuvi ulie livua pendo langu kama samaki na kuliweka kwenye mtego, halifurukuti wala halijinasui juu yako. Nakupenda tafadhali kubali ombi langu...

... Mwisho....

Endapo kuna makosa yoyote katika barua hii basi ujue ni machozi yaliyodondoka kipindi naandika barua hii.

Wako akupendae ......

**********

"Ewaaa, maneno matamu sana nurdin na, nina amini mtoto atakubali kwani vitu ulivyoandika vinateka sana moyo wa mtu. Imependeza japo nilikwambia uandike neno 'I luv u' ila hata hilohilo likopoa sana mwanangu cha msingi, ipulizie unyunyu hiyo barua na uiweke vizuri katika bahasha ili hata akiishika ajue imetoka kwa kijana smati au sio mwanangu?". Aliongea samiri, na kukazia baadhi ya pointi.

"Ndio, hivyo mwanangu alafu tuweke na karatasi nyngine kwa ajili ya majibu au vpi mwanangu?" Ulikuwa ni ushauri kutoka kwa Nurdin.

"Acha uboya Nurdini majibu utafata mwenyewe unamuogopea nini huyo, au uliambiwa ana kunya keki,kisha anakojoa soda?. Acha mambo yako mtoto wa kiume huwa haogopi nyau, wewe utafata jibu mwenyewe kiume au sio mwanangu?"

"poa, lakini siunajua jinsi anavyonioneaga aibu hivi unadhani ataweza kunijibu kweli au unaniambia tu wangu"

"we utaöna mwenyewe kwa maneno yaliyomo humu ngoja kwanza mimi niende nikamtegee kwenye ile kona anayopenda kupita akiwa anaenda shule."Aliongea Samir na kuanza kujiondoa taratibu...

Alifika maeneo ya shule na kuketi katika moja kati ya mawe yaliyokuwapo eneo lile, punde kidogo Samir aliweza kumuona Sumayah akipita katika maeneo yale, kwakuwa hakutaka kujionyesha kuwa yupo pale kwa ajili ya kumsubiri sumayah, basi alijifanya yuko bize na kufunga nyuzi za viatu vyake.

Sumayah alipofika mkabala na Samir alimpa salamu ya kiislamu.

"Asalaam alyk Samir" Alisalimu Sumayah huku akiwa ameuelekeza mkono wake karibu na kichwa cha Samir, ambae kwa muda huo alijifanya yuko bize na kufunga nyuzi za viatu vyake.

Baada ya kuskia salamu ile ndipo Samir alijifanya ameshtuka kusikia sauti ya Sumayah kana kwamba hakutegemea kama angeweza kuiskia sauti ile.

"waalaykum salam Sumayah. Vp umetokea wapi au nawewe ni mzimu nini"

" jamaani Samir unavituko, mbona mimi nimetokea njia yangu ya kila siku."

"ahaa, lakini umenishtua. Enhe leta story mrembo."

" Samir mbona unaniita mrembo, mi spendi kuitwa mrembo, warembo wapo kwenye makopo ya mafuta, labda na waigizaji kama kina Aishwaria rai, Kajor , Pretty zinta, na kina... kina....." Kabla hata Sumayah, haja maliza maelezo, Samir akaingilia.

Sumayah, unajua we hujui tu kiasi gani ulivyo mrembo. Wewe ni mzuri Sumayyah, hebu tazama macho yako,midomo unavyo ikunja dah," Sumayyah, akatabasamu kidogo kwa kusikia vituko vile, na Samir akatumia tabasamu lile kama spana ya kukazia maneno yake.

" Tazama tabasamu lako lilivyo zuri, kwa tabasamu hilo hata Kajor inabidi akasome, dah cheki unavyonikosha mtoto wakiume na dimpozi zako, sikutofautishi na Prettyzinta alieigiza movi ya Soldier akiwa na Bob-deo."

Furaha ya Sumayah ilizidi kumjaa, hata kumpelekea ashindwe kukabiliana na tabasam lake.

Samir aliendelea kukomaza sifa mbele ya Sumayah, na kumfanya asitamani kutoka maeneo yale iliendelea kupata sifa kem,kem, kutoka kwa Samir .

"Sumayah mtoto mzuri, tena uliyejawa na urembo kwenye sura yako. tafadhali chukua ujumbe huu, uusome na uuzingatie"

"ujumbe!! ujumbe gani huo?, na umetoka kwako au kwa nani ?" Ni maneno yaliyomtoka Sumayyah, huku akiwa kwenye bumbuwazi na maswali lukuki.

"anhaa, tulia muigizaji wa nafsi yangu, mbona unakuwa na haraka utadhani mkojo wa asubuhi?, ok, ujumbe huu umetoka kwa rafiki yangu kipenzi, mpole, mcheshi, mwenye wingi wa vituko tena zaidi yangu nae simwingine bali ni NURDIN"

Sumayah baada ya kuskia vile, alishangaa sana, kwakuwa hakuw na mazoea na Nurdin.

" Nurdini!!! Mmh!!, haya acha niwahi shuleni nitausoma nikifika nyumbani"

"sawa Sumayah wewe wahi shuleni siunajua limwalimu lenu lile la zamu linavyojifanyaga linajua kuchapa"

ok, baadae Samir

Sumayah, baada ya kuaga, hakuwa na la ziada ila kuondoka maeneo yale na kwenda maeneo salama. Akiwa katika hatua zake, huku nyuma Samir alibaki hoi na kujisifu kwa ushujaa wa kufanikisha kufikisha kile ambacho kilikuwa ni ahadi kati yake na rafiki yake.

Ingawa muda ulikuwa unazidi kuyoyoma, lakini Samir hakuondoka maeneo yale, aliendelea kutabasamu na kujipongeza kwa kazi ile ya kishujaa.

"dah, huyu boya amepata kisu kichizi, najua mishe itatiki na lazima au bebe mzigo. Na kwa jinsi jamaa alivyooza, sijui tu atakuaje." Ni maneno aliyoongea Samir huku akiwa anaendlea kutafakari na kuzidi kulichanusha tabasamu lake.

Kengele ya kuingia madarasani ilipogongwa, Samir hakuingia na badala yake aliamua kurudi kwa rafiki yake ilikwenda angalau kumpasha habari juu ya yaliyotokea.

Alifika na kumpa habari ya yaliyotokea, lakini katika masimulizi yake, chumvi ndio ilisheheni kwenye maneno yake. Mara mtoto akachelewa darasani, mara tumekaa nae zaidi ya nusu saa, ilimradi tu, kuzidisha chumvi katika maneno yake.

" Kwa hiyo umemwambia kabisa na jina langu alafu akafurahi?" Aliuliza nurdin.

"unanichezea mimi wewe. Mtoto nimemtupia maneno mpaka yeye mwenyewe akarespekti na hawezi kuchomoa maana, inaonyesha wazi kabla hata hajasoma maudhui , kichwa cha habari kimeweza kusadifu yaliyomo" Aliongea Samir katika hali ya kujigamba mfano wa mwanajeshi asimuliapo matukio ya vita alizo pigana kwa kuitetea nchi yake. Ilikuwa ni furaha tu kwa rafiki yake na aliamua kumuagiza kwa mama ntilie maarufu maeneo yale ili afate ukoko. Ikiwa ni kama kipongezo cha kazi nzuri waliyofanya.

"Dah, mzee Samir, singo la leo tamu au we unaonaje?" Aliongea Nurdin kuusifia ukoko ule.

" singo ni tamu kwa sababu mambo yanaenda fresh, na hii ni ishara nzuri ya kuonesha jinsi gani mtoto atakubali tena bila kuzingua" Aliongea Samir , huku akiendlea kukokoa ukoko.

"Nakuaminia sana mtu wangu kwa show zako, hebu nipe tano kwanza". Aliongea nurdin, na kugongesha tano.

" ebana ee mimi ndio Samir , mkali wa show za kibabe, mzee wa michongo yenye kuchongoka, mtaalam wa michongo ya busara kuliko panya kadogo aliefanikisha kumfunga paka kengele". Aliongea Samir kwa majivuno huku akitamba utadhani yupo jukwaani.

" we ngoja tusubiri majibu, mtoto amesema ataisoma akifika mahome kwao"

"ok, sasa mbona wewe hurudi skuli siunajua nyie ni L.Y "

"usijali Nurdin minitatia tim kesho,coz leo nishaharibu kuna dogo mmoja ameniletea class nikamchukua mkono, ameenda kusema kwa mwalimu kwa hiyo skul pamenuka"

"Dah, pole sana mkali wangu lakini huo ndio uanaume boya akikuzingua mfanyizie amanini mwanangu?" Aliongea nurdin na kumalizia kwa swali.

Waliendelea na maongezi yao mpaka ulipofika muda wa wanafunzi kurudi makwao, ndipo Samir alipotoka kwenye duka la rafiki yake Nurdin na kuanza kujongea ilikuelekea kwao kwa ajili ya kubadilisha nguo iliawe huru, hakuwaza chakula kwakua tayari alishapata kwa rafiki yake Nurdin

Akiwa njiani Samir aliweza kukutana na rafiki zake wengne na kuwauliza yaliyojili baada ya yeye kumpiga mwanafunzi mwenzake na kwenda kusema kwa mwalimu. Wanafunzi wenzake walimuhakikishia kwamba hakuna tatizo na kumfanya ajisikie huru, Samir alipofika nyumbani kwao alibadili nguo pamoja na kuoga. Baada ya kuoga aliamua kujipumzisha geto kwake na kuanza kukumbuka jinsi alivyokuwa akimchekesha Sumayah.

Usingzi ulimchukua, hata alipoamka aliamua kwenda moja kwa moja hadi kwa rafiki yake Nurdin kwa ajili ya kupanga mipango ya kumuwinda Sumayah.

"Oy, mzee Samir yule mtoto amejipitisha hapa muda tu wewe ulipoondoka."

"Mtoto yupi huyo Mkali wangu?"

"mmmh, unajifanya humjui. Si mtoto Zulfa, amesema kakumis ile mbaya."

"Huyo nae, mimi nisha mwambia simpendi, mbna si muelewa huyo msichana. Mi sipendi hata kumuona," Aliongea Samir huku akionesha kukasirika.

"Tena staki habari za sijui Zulfa"

"poa kaka ila sio fea"

Waliongea meng muda ule. Hatimae ilifika usiku na wakaenda kumuwinda Sumayah maeneo ya kwao.

" Mkali mbona hatokei inamaana leo hatumwi hata mafuta ya taa, au ndio tuseme mafuta yao ya jana yapo hadi leo!" aliongea maneno yale Nurdin huku akibadirisha pozi katika mawe yale waliyokuwa wamekalia.

"Aaaah,,gundu hizo mwanangu. Mbona unajichulia, we unadhani mafuta yale waliyo yanunua jana yanaweza yakatosha kubaki hadi leo acha mambo yako, mtoto atapita tu kwenda dukani we skilizia kiaina siunajua sisi wapiga mingo tulivyo"Aliongea Samir maneno ya kuwatia ujasiri wa kuendelea kubaki maeneo yale.

Walikaa takribani saa nzima huku wakipongezwa na mbu ambao waliwauma na kuwafanya wajiwashe makofi kila mara katika miili yao kwa minajili ya kuuwa mbu, kuachilia mbali mbu wale waliokuwa wakiwauma kwa zamu, vile vile kulikuwa na baridi kali:baridi ambalo waliweza kulivumilia kwakua walikuwa wakimsubiri msichana yule lakini laiti kama angelikuwa mtu mwingine basi wasingeliweza kulivumilia baridi lile.

"oyaaaa Samir sio yeye huyo anatoka nyumbni kwao"

"ndio yeye Nurdin, hapa chamsingi mfate moja kwa moja kabla hata hajafika dukani ili akupe jibu letu mapema sisi tuambae geto tukatulie amanini mwanangu"

"ya, ndo hivyo jombaa". Hayo yalikuwa maongezi waliyo yaanzisha baada ya kumuona Sumayah kwa mbele na bila kupoteza muda Nurdin alienda mpaka alipokuwa sumayah...........

Je Nurdin atafanikiwa mpango wake kwa Sumayah?
 
Mwendelezo ni kila siku.
Santo sana Cuzoo akee mambo ni bampa to bampa hakuna kupoaa!!
Ngoja nitulie niisome vizuri!
Bantu Lady Tayukwa baby zu Lovelovie
 
Cuzoo akee umefanyaje trena wamekuban doh !! kwahio mwendelezo hadi utoke kifungoni?????🙄
 
"Njmezunguka mashariki na hata magharibi, bila kusahau kusini na kaskazini"😂😂😂
Watu wana menenoo🙌😂
 
Weee acha zako cuzoo Kwani walikufanyeje kule???
Tena leo nasubiria baraka zako kulee cuzoo uje utubles one time buana!
Acha tu mama mambo yasiwe mengi. Niko naanda kitu sana.
Ile picha kama kweli ni yako. Nakufahamu vizuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom