Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA 29
SURA yake ilikuwa imebadilika kabisa, macho yakabadilika na kuwa ya rangi nyekundu, mwili wake ukaanza kutetemeka kama mtu aliyekuwa na homa kali, Victor Fedorov akauona utajiri wote aliokuwa nao haukuwa na maana kwake kama tu angewakosa watoto wake ambao kwa hakika alikuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha ili kuwapata na sasa walikuwa katika hatari nyingine ya kifo kama tu asingetimiza jambo alilotakiwa kulifanya ndani ya saa chache alizopewa.
Kwa muda wa dakika tano aliendelea kutafakari na hakuelewa ni kwa nini mtekaji huyo alifanya tendo hilo, akavuta kumbukumbu zake nyuma akijaribu kufikiria watu wote aliowahi kuwakosea na kuwadhulumu lakini hakuna alichokumbuka.
Mara kadhaa taswira ya Ditrov ilimjia lakini akatupilia mbali mawazo juu ya mtu huyo na kuamini kwamba tayari alishakufa.
“Nilimuua ili kuficha siri sikuwa na tatizo jingine kabla!” alisema akitembea kukielekea kiti kilichokuwa mbele yake. Huku jasho jingi likimtiririka, akakisogelea kiti na kuketi, moyoni mwake akiwa na hofu juu ya watoto wake.
“Nitatoa kiasi chochote cha fedha atakachohitaji mtu huyo ili mradi tu niwapate watoto wangu!” aliwaza akijifuta machozi.
Alipotupa macho yake kwenye saa yake ya mkononi hofu ikazidi kumwingia, mbele yake kulikuwa na saa kumi tu zilizobaki katika saa ishirini na nne alizopewa na muuaji.
Haraka akanyanyuka kitini na kusogelea tena simu akapiga namba zilezile alizobonyeza mwanzo kisha kuiweka simu sikioni, alikuwa hapo kuzungumza na mtu huyo ataje kiasi hicho cha fedha na sehemu ambapo angezikuta na yeye kupata watoto wake wakiwa salama.
***
Ilikuwa ni familia yenye furaha kupita kawaida, kila mtu aliyewaona aliona wivu, hakika walivutia, walikuwa na kila sababu ya kuitwa mke na mume. Lakini pamoja na mambo yote hayo kutawala maishani mwao, jambo moja tu lilikuwa likiwasumbua ni wapi wangepata mtoto.
Kwa mwanamke halikuwa tatizo sana, kazi kubwa ilikuwa kwa mwanaume ambaye alitumia muda mwingi kufikiria namna gani angeitwa baba kama ilivyowahi kutokea miaka mingi kabla.
“Darling” (mpenzi), Phillip aliita siku moja asubuhi.
“Yes baby!” (Ndiyo mpenzi)
“Ni miaka minne sasa tupo kwenye ndoa lakini mimi sina uwezo wa kuzaa nataka tuliongelee jambo hili ili tufikie muafaka juu ya nini cha kufanya, napenda niitwe baba hata kama mtoto huyo atakuwa si wa kwangu,” alisema Phillip.
“Unamaanisha nini Phillip?”
“Sina nia mbaya, ila nataka nikupe nafasi ya wewe kuzaa kwa sababu huna tatizo lolote.”
“Mh!” Lina akaguna.
“Ni ukweli mke wangu nakupenda sana lakini nitakupenda zaidi utakapofanikiwa kuniletea mtoto.”
“Phillip mbona sikuelewi, mtoto atoke wapi? Ni kweli mimi sina tatizo lakini nitampata wapi mtoto ili hali wewe ndiye mume wangu na tayari una tatizo?”
“Tafuta mwanaume yeyote ambaye atakuwa tayari kuzaa na wewe Lina halafu mimi nitalea mtoto huyo!” alisema Phillip akilengwalengwa na machozi.
Ilikuwa ni kauli ngumu sana kuitamka mdomoni hasa kwa mwanaume aliyempenda mke wake kupita maelezo, lakini haikukwepeka kwa sababu walihitaji mtoto ndani ya nyumba ambaye angekuwa mrithi wa mali zote walizokuwa nazo.
Lina akamwangalia Phillip kwa muda, hakuwa tayari kuamini kauli aliyoisikia mdomoni mwa Phillip, kwani katika muda wote walioishi pamoja ndani ya nyumba Phillip alionyesha kumpenda na mara kadhaa akimwomba kuwa mwaminifu katika mapenzi yao.
“Phillip!” Lina aliita.
“Yes honey” (ndiyo mpenzi) aliitikia Phillip huku macho yake yakimwangalia Lina kwa huruma.
“Unamaanisha unachosema?”
“Hakika, wala sina utani juu ya hilo.”
“Ni kwa nini umefikia hapo, hivi kweli unanipenda?”
“Nakupenda kupita maelezo wewe mwenyewe unafahamu.”
“Sasa?”
“Nataka kuitwa baba.”
“Phillip hutaumia kugundua kwamba mkeo unayempenda kwa dhati amekutana na mwanaume mwingine kisha kupata ujauzito?”
“Nimekaa na kufikiria kwa muda mrefu si kwamba sitaumia, ninachohitaji ni wewe kufanya kila unachoweza upate ujauzito halafu mimi nitautunza mpaka utakapojifungua mke wangu.”
“Phillip kumbe hunipendi,” alisema Lina akibubujikwa na machozi.
Phillip akanyanyuka kitini na kusogea karibu kabisa na kiti alichoketi Lina kisha kumkumbatia wote kwa pamoja wakaanza kulia.
“Uamuzi wangu si mbaya, ninachohitaji wewe uwe na furaha mke wangu matatizo yangu mimi yasikufanye ukakosa kuitwa mama maishani mwako,” aliongea huku akimpigapiga Lina mgongoni.
“Phillip hivi utajisikiaje kuona mimi ni mjamzito halafu si wa kwako?”
“Kwa sababu nimetoa idhini mimi mwenyewe sitaumia, ninachotaka ni wewe uitwe mama na mimi baba basi.”
“Ni ngumu Phillip, mimi siwezi kulisaliti penzi letu acha tubaki hivihivi bila mtoto naamini Mungu alikuwa na makusudi juu ya hilo.”
“Unasema?” aliuliza Phillip akinyanyuka kitini, alikuwa hatanii bali alimaanisha alichokuwa akikisema. Haja ya moyo wake ilikuwa ni kuitwa baba bila kujali ni wapi mtoto huyo angepatikana.
“Phillip.” Lina akaita huku akijaribu kumfuata.
“Lina nataka mtoto!”
“Phillip haiwezekani mimi siko tayari kusaliti penzi letu.”
“Unanipenda?” Phillip aliuliza kwa kujiamini.
“Nakupenda sana mume wangu.”
“Basi nataka mtoto!” aliongea Phillip huku akitembea kuondoka eneo hilo.
“Mungu wangu! Ni papa?”alijiuliza huku akinyanyua taa yake ndogo na kumulika eneo hilo huku akitetemeka kwa hofu.
Akayatoa macho yake yote kuangalia mbele lakini kwa sababu ya mwanga mdogo uliokuwepo hakuweza kuona vyema. Woga ukazidi kumwingia na wazo pekee lililomjia kichwani kwa wakati ule lilikuwa ni kugeuza mtumbwi wake haraka na kurejea alikotoka, jambo ambalo hakuwa na uhakika nalo kama lingesaidia kuokoa maisha yake.
Akiwa hapo alishuhudia mtumbwi wake ukiyumbishwa huku na kule, akajua tayari amejiingiza kwenye hatari.
“Leo ninakufa huku nikijiona,” alisema Oleg Malenko huku machozi yakimbubujika kwa wingi mashavuni. Hofu kuu ilikuwa imemkumba na hakuna alichokuwa anakisubiri zaidi ya kifo, tena cha kuliwa na papa.
Aliifanya kazi ya uvuvi kwa kipindi kirefu lakini hata siku moja hakuwahi kukutana na dhahama kama ile. Zaidi alifanya kusimuliwa na wavuvi wenzake kwamba watu wengi hufa baharini, hasa wavuvi baada ya mitubwi yao kuvamiwa na kupinduliwa na samaki wakubwa.
Kwa Oleg Malenko siku hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia tukio hilo, akaamini kabisa kwamba kifo kilikuwa kimemkaribia. Taswira za mke na watoto wake zikawa zinapita kwa kasi kichwani mwake kama filamu ya kusisimua, machozi ya uchungu yakawa yanamtoka.
Akiwa katika mawazo hayo, haraka alipata wazo la kupiga kasia kwa nguvu na kugeuza mtubwi wake kwa kasi kurejea upande aliokuwa mara ya kwanza lakini tayari alishachelewa, akahisi mtumbwi ukivutwa kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu.
“Nakufaa! Nakufaa!” alisema kwa lugha ya Kirusi akiomba msaada.
***
Muda mfupi baada ya kuzamishwa baharini akiwa amefungwa jiwe kubwa mwilini mwake ili asipate nafasi ya kujiokoa kwa lengo la kupoteza ushahidi, Ditrov alirejewa na fahamu baada ya kupigwa na baridi kali. Alijaribu kufurukuta kwa kupiga mbizi ili kujiokoa lakini hakufanikiwa.
Alipotumia nguvu za ziada alizokuwa nazo mwilini mwake, bado aliendelea kutapatapa na sasa akawa anavutwa kuelekea chini ya bahari na lile jiwe kubwa alilokuwa amefunganishwa mwilini. Akiwa katikati ya hali ya kupoteza fahamu na uzima, alikumbuka picha ya tukio zima lililotokea ofisini kwa bosi wake, Victor Fedorov hadi wakati ule. Alikumbuka jinsi alivyofyatuliwa risasi bila huruma ambazo zilipenya kwenye mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
Akiwa katika hali hiyo kwa takribani dakika kumi nzima, aliendelea kujivuta huku na kule ndani ya maji ili kujiokoa lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu kwake. Akawa anazidi kuzama! Ditrov alizidiwa nguvu na maji, akaanza kukata tamaa lakini upande mwingine wa akili yake alikuwa na matumaini makubwa ya kusalimika na kifo.
“Ma…ji!” alitamka kwa tabu akiwa bado anatapatapa, moyoni akasikia sauti ikimwambia kuwa hapaswi kukata tama kwani kufanya hivyo kungemaanisha kifo chake.
“Sitaki ku…fa!” akatamka tena kwa tabu.
Hali yake ilizidi kuwa mbaya, uwezekano wa kutoka baharini akiwa salama ukazidi kupungua kutokana na maumivu aliyokuwa anayahisi baada ya risasi kuupenya mwili wake na kusababisha atokwe na damu nyingi. Pamoja na kuwa jabali, Ditrov hakuwa na uhakika kama angesalimika lakini bado hakukata tamaa.
Ghafla akiwa katika hali ya kukata tama, alikumbuka kitu. Wakati anaingia ofisini kwa Victor Fedorov, ndani ya mfuko mmoja katika suruali yake alikuwa na kisu kidogo cha kukunja, akaamini huenda kingemsaidia kuokoa uhai wake.
Kwa nguvu zake zote alijitahidi kuingiza mkono mfukoni lakini hakufanikiwa, akajaribu tena upande mwingine wa suruali yake na kukumbana na maumivu makali.
Licha ya maumivu hayo alijaribu tena kuusogeza mkono wake zaidi mpaka akaufikia mfuko wa suruali, kwa taabu kubwa akafanikiwa kugusa kitu kigumu na kuamini kwamba kilikuwa chenyewe.
Akiwa katika hali ya kutapatapa akafanikiwa kuupenyeza mkono mfukoni na kuchomoa kisu, kwa taabu kubwa akakishika vyema na kujaribu kuikata kamba ili ajinusuru na umauti uliokuwa ukiinyemelea roho yake.
Hakuwa tayari kukutana na kifo. Ni kweli alifahamu wazi kwamba kila binadamu angeonja mauti lakini hakuwa tayari kufa kikatili kiasi hicho.
“Nitajaribu mpaka mwisho, ikishindikana basi,”aliwaza akilini mwake.
Kwa nguvu kidogo alizokuwa nazo alikishika vyema kisu kidogo alichokuwa nacho mkononi, licha ya maumivu makali aliyokuwa nayo upande wake wa kulia, aliikamata vyema kamba aliyokuwa amefungwa shingoni na kuanza kuikata.
“Krii!Krii!Krii!” aliendelea kusugua kisu katika kamba ili ikatike na kumwacha huru. Kwa takribani dakika tano nzima aliendelea kung’ang’ana na kisu lakini zoezi hilo lilionekana kumshinda. Akaanza kuhisi fahamu zikipotea na nguvu kidogo alizobakiwa nazo zikamwishia. Licha ya hayo yote, bado hakuchoka, alitaka kuendelea kujaribu.
***
“Ngrii!Ngrii!Ngri” Ulikuwa ni mlio wa simu ndani ya nyumba ya Victor Fedorov. Aliinuka taratibu huku akitetemeka na kuisogelea simu hiyo ili aipokee akiwa haelewi ni nani alikuwa akipiga.
“Ndiyo,” akajibu huku akitetemeka.
“Muda unazidi kuyoyoma! Ninachohitaji kutoka kwako ni kiasi cha dola milioni 290 ili niweze kuwaachia watoto wako. Ningependa fedha hizo nizipate ndani ya Msitu wa Beloomut, kusini mwa Jiji la Moscow kwa usalama zaidi.
“Msitu wa Beloomut?” aliuliza lakini kabla hajapata jibu kutoka upande wa pili wa simu, alisikia sauti za watoto wake wakimwita.
“Daaaady!” (Babaaaa!) kilio kikali kilifuatia nyuma yake, Fedorov akazidi kuchanganyikiwa akili.
Je, nini kitaendelea? Victor Fedorov atakuwa tayari kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuwakomboa watoto wake? Ni kwa nini muuaji ametaka fedha hizo zipelekwe kwenye Msitu wa Beloomut?
ITAENDELEA,