beb njoo umsaidie mzee mgaya huku
ha haaaaaa wataka aongezewemzee mgaya kunifurahisha,ila bado naona mama kulwa kichapo hakijamkolea
Jumatatu kesho mzigo kama kawaidaHuku mbona panaenda taratibu sana
Jack Daniel vip leoJumatatu kesho mzigo kama kawaida
shukrani boss moneytalk njoo bebSEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
Siku tatu baadaye Mzee Mgaya alipokea barua iliyomtaka afike kituo kidogo cha polisi, kilichoko karibu nyumbani kwake kwa bibi mkubwa, Cha kushangaza barua ile haikuwa na muhuri wa polisi, na pia haikuwa inamuamrisha aripoti moja kwa moja bali, ilimtaka afike kwa mazungumzo ya kawaida ya kirafiki.
Akiwa anatazama kwa umakini sahihi ya muandikaji, akiwa anamfahamu vyema kabisa, alitabasamu huku akitupia Samson lile karatasi.
Samson alilisoma huku, uso wake ukianza kubadilika kwani alihisi hatari inayomkabili baba yake, huku akijua ni kuhusu kupigwa kwa mama Kulwa, huku akijiona ni msababishaji, aliwaza mbali sana Samson, alianza kuiona shule ni chungu mno kwake kwani angekuwa kijijini kwao yote yale yasingetokea.
Samahani sana baba mkubwa najua Mimi ndiye niliyekuponza, sasa nilikuwa naomba kama inawezekana, unipe tu nauli niweze kuondoka, sijisikii kukaa hapa kwa kweli.
aliongea kwa sauti yenye upole Samson.
Kwanini unawaza hayo Samson,
Wewe usijali, Mimi nitakuacha hapa na mama yako mdogo Tausi, naenda kumsikiliza huyu afande anasemaje, maana hapa nimeitwa na yeye,ngoja nikamsikilize.
aliongea kwa kujiamini mzee Mgaya.
Mume wangu usichukulie vitu kirahisi hivyo suala lako ni zito, Hadi Leo siku ya tatu upo hapa hujui muhusika anaendeleaje, kachukua hatua gani, halafu unapokea ujumbe kama huo unaanza kuleta dharau, kweli?
Mimi binafsi naona muongozane na Samson maana lolote linaweza kutokea, unaweza kuwekwa ndani huku tukishindwa kujua kinachojiri.
alishauri Tausi huku akizidi kumtisha zaidi Samson.
Si mbaya ngoja nikawasikilize wanasemaje, aliongea Mzee Mgaya huku akiingia ndani ya gari pamoja na Samson wakiwa kama wanarudi kwa mama Kulwa ambako ndiko kwenye kituo Cha polisi alikoitiwa na yule afande.
***************************************
Mama Kulwa alikuwa nje akipunga upepo huku akiwa anamuelekeza housemaid wake mambo fulani, Kwa kifupi hakuwa na maumivu makubwa kama alivyokuwa anawaaminisha watu wengi, ila hadi siku ile alikuwa safi tu.
(Geti likagongwa)
Sukuma tu mlango mdogo, ingia.
Alimwelekeza mgeni wake.
Binti machachari aitwaye Cathy ambaye lile suala alilivalia njuga kana kwamba ni mzazi wake, aliingia huku akikaribishwa hadi ndani kabisa,
Enhee niambie mama yangu, unaendeleaje kwasasa, maana Jana nilitoka kidogo nilikuwa nje ya mji huu. aliongea Cathy Mara baada ya kukaribishwa akae.
Mmmh mwanangu niendelee vipi,
Hapa Mimi najiona kama kilema tu, maana hapa nilipo mkono haufanyi kazi, ingawaje Doctor alisema eti upo sawa haoni hitilafu yeyote, lakini maumivu nayopata hapa MUNGU mwenyewe ndiye anajua,
Pia maeneo ya kiunoni Nako kunauma kwani nashindwa hata kuinama nikafanya kazi zangu kwa uhuru Kila kitu kimekataa kabisaaa najiona wa kufa muda wowote.
alilalamika mama Kulwa.
Sawa, vipi baba yupo wapi
alizidi kupeleleza Cathy.
Awe wapi unafikiri, azma yake ya kutaka kuniua alishatimiza, nadhani ni MUNGU tu ananisaidia Hadi leo hii pengine yeye akili zake zinamwambia
kuwa nimekufa, alizidi kulalamika mama Kulwa.
Mmmmh sikuwahi kufikiria kuwa Mzee Mgaya ndivyo alivyo, yaani hii inadhihirisha kuwa alidhamiria kwa alichokifanya, maana ingekuwa bahati mbaya, pengine angekuwa kasharudi eidha kukuomba msamaha au kukupeleleka hospital kabisa.
Sasa vipi ile Jana ulifanikiwa kwenda polisi tena?
aliuliza Cathy.
Ndiyo, nilienda ila sikuridhika sana na majibu yao kwani Kila nikidai kufungua kesi, wao wanadai haya masuala yanazungumzika, kitendo ambacho sikukielewa, ndiyo Mimi nafahamiana na maaskari wengi hapo wapo tunaosali nao, wapo tunaoshirikiana mambo mengi tu, hali kadhalika baba Kulwa yeye ndiye anajulikana zaidi. Nadhani kujulikana kwetu si sababu ya wao kunipuuza maamuzi yangu, Ina maana hadi nije kuumizwa vibaya au nife kabisa ndiyo watamchukulia hatua baba kulwa?
alilaumu mama Kulwa.
Sasa mama, kwanza wewe ni mteja kama wateja wengine, hakuna rufaa yeyote ungeomba ili mkasikilizwe mbele zaidi? alihoji Cathy.
Waliniambia hivyo kuwa wanapenda tungekutana Mimi na mume wangu kwanza tuongee na wao kisha, yakishindikana nitaenda mbele, ila kwa uelewa wangu niligundua wanampendelea baba Kulwa hivyo nikawaambia kama kufungua kesi inashindikana basi watanielewa siku wakija kuokota maiti yangu.
aliweka kituo mama Kulwa huku akionekana dhahiri hakuwa na maumivu yeyote.
*************************************
Karibu sana mzee wetu, karibu sana.
Hivi kidogo ungenikosa maana leo natoka mchana huu hadi kesho asubuhi. aliongea afande mmoja wa makamo ambaye Hadi umri ule hakuwa na cheo chochote kikubwa.
Huyu ni nani mzee Mgaya,
aliuliza yule afande.
Ni kijana wangu anaitwa Samson.
Sawa, tunaomba angekusubiri nje kabisa kama itawezekana samahani lakini, aliongea yule afande huku akimpiga piga Samson mgongoni akimuelekeza sehemu ya kukaa.
Akiwa kazungukwa na maafande watatu yeye akiwa wanne, lawama zilianza kwake huku akisimangwa vyema kabisa,
Kiukweli shemeji, umejivunjia heshima mno kwa kitendo ulichokifanya kwa mkeo ambaye mnaitafuta jubilee ya pili kwa mujibu wa taratibu za kanisa letu,
Nyinyi mmekuwa mfano wa kuigwa kwa sisi wengi wetu, sijui kama mnajijua kuwa maisha yenu ni mfano kwa wengine? Lakini kwa hili ulilolifanya kwa mke wako na umri huo nimekudharau mpaka basi, na ushukuru mama Kulwa hakutaka kuwa na mambo mengi vinginevyo sheria ingechukua mkondo wake, sidhani kama ungekuja hapa Ukiwa inaendesha gari mwenyewe.
alilalamika afande yule wa kike huku akionekana kumchukia Mzee Mgaya.
Jamani ni stori ndefu juu ya sababu iliyopelekea Mimi kugombana na mke wangu.............
Mzee Mgaya hatujakuita hapa uje utueleze maisha unayoishi wewe na mkeo, badala yake tumekuja kukukanya uache hiyo tabia, uzee huo umaarufu na ushawishi uliokuwa nao hatukutegemea kuwa unaweza kufanya vitendo viovu na vya kufedhehesha,
Hebu fikiria mkeo ni daktari mkubwa, katumikia fani na utaalamu wake, huku akijizolea umaarufu mkubwa,
Amestaafu kwa heshima, mna watoto wale wote nawajua vizuri, mmesomesha, mmewaandalia urithi Bora kabisa ambao ni elimu. Lakini Cha ajabu umekuja kumdhalilisha mkeo tena Kwa kipigo! aliongea afande mwingine kwa uchungu huku waliongea kwa sauti kiasi Cha baadhi ya maaskari kusogea Kila mtu amuone huyo Mzee aliyemuumiza mkewe.
Tumeambiwa, shida eti ni mtoto ndiye kasababisha hayo yote,
Kwani kulikuwa na ulazima gani wa kukaa naye? Kama kweli ulikuwa na huo uwezo wa kumsomesha, si ungempeleka boarding huko?
Waliongea maaskari wale kwa pamoja bila kumpa nafasi Mzee Mgaya.
Mara akaingia afande mmoja mwenye cheo cha juu akiwa na umri mdogo kabisa,
Alipigiwa salute, na baadhi ya maaskari Kisha akauliza akiwa kamshika Samson mkono.
Jamani nimemuona huyu dogo hapo nje na nimemuuliza unafanya nini hapa kanijibu anamsubiri baba yake, nikapata mashaka nikaona ni vyema anithibitishie huyo baba yuko wapi.
Akaoneshwa Mzee Mgaya.
Vipi Mzee wetu ana shida gani tena, au ni yule niliyeambiwa kaibiwa jana maana wajihi wake kama anafanana na nikivyoekekezwa. aliongea yule afande.
Hapana huyu ni yule ambaye alikuja yule mama daktari mstaafu akitaka kumfungulia kesi mkuu, walijibu wale maaskari huku wakiwa wamenyooka.
Ahaaaaah huyu ndiye yule mzee mshenzi, Sasa mnaendelea kupiga naye stori za Nini?
Muwekeni ndani Hadi pale atakapo kuja mkewe, sisi hatuna shida naye mwenye shida naye ni mkewe, aliongea yule afande Kisha akatoka nje na walinzi wake wakatokomea.
Kama masihara, kama utani Mzee Mgaya alianza kuvua mkanda huku akiwabembeleza maaskari wale ili waongee kiutu uzima, lakini walimkatalia kwamba yeye mwenyewe anajua wazi amri imetoka kwa nani.
Hayo yote yalifanyika huku Samson akiona , akaruhusiwa aondoke akimuacha baba yake kimasikhara akiwa selo.
Samson, alipata wakati mgumu sana, aliwaza aende kwa mama Kulwa, je atamuelewa kwa atakachomwambia hasa ukizingatia yeye ndiyo chanzo cha mvurugano katika familia?
Akawaza aende kwa Tausi akatoe taarifa kuwa baba yake yupo kituoni kashikiliwa? akaona na Giza hili linaloingia kule kwenyewe sijakujua vizuri, Bora hapa kwa mama Kulwa ni karibu najua Nina siku ya tatu sijatokea lakini liwalo na liwe lazima nikatoe taarifa..
Je, samson anavyochukiwa, ataeleweka?
Kumbuka wametoka kwa Tausi wakaenda kituoni moja kwa moja bila kupitia kwa mama Kulwa
Itaendelea..............
Mzigo utakuja hivi pundeJack Daniel arosto ndugu yngu
Shukrani bossMzigo utakuja hivi punde
beb moneytalkMzigo utakuja hivi punde
Yes babe
Tuendelee kusubili nyama ipo chini bebYes babe
mkuu ungetupia na yale kabsa nduguSEHEMU YA THELATHINI
Samson alianza kurudi nyumbani kwa mama Kulwa taratibu, huku akiwaza anaenda kusema nini au ataanzaje,alikuwa na majibu ya kila swali alilojiuliza, Kila kilichotokea alijikuta yeye ndiye msababishaji.
Hatimaye akarikaribia geti la nyumbani pale akabisha hodi akafunguliwa, alishangaa kukutana uso kwa uso na Dotto mmoja ya watoto mapacha na wa mwisho kwa Mzee Mgaya.
Walisalimiana kwa kukumbatiana huku mwenzake akiwa na furaha baada ya kumuona Samson, lakini hali ilikuwa tofauti kwa Samson kwani alihisi pengine mambo yatazidi kuharibika.
Samson twende zetu ndani kwa Kulwa maana tulimuuliza Mama siyo muda kuwa uko wapi hata hajatujibu .
aliongea Dotto huku wakiingia ndani/chumbani kwao na kumkuta Kulwa ambapo wote walifurahi sana kumuona Samson.
Vipi Sam ulikuwa wapi maana tumefika hapa kama masaa matatu yaliyopita, hatujakuona ila si mbaya tutajadili masomo yetu kwa pamoja au sivyo Sam? Tunahitaji kubadilishana madini.
aliongea Kulwa huku akigundua Samson hajachangamka kama kipindi kile walichomuacha.
Walitizamana wale mapacha, huku Dotto akiropoka,
Vipi ndugu mbona kama haupo sawa vipi? sisi hapa tumekuja tutakaa kama siku tatu tu, kisha tunaondoka tena hapa penyewe tumefanya kuiba tu ujue, Sasa tulitegemea tutakuja kusoma na kufurahi kwa pamoja mbona hivyo tena Sam?
Samson hakujibu kitu badala yake aliwauliza kuhusu mama yao yuko wapi,
Mama yupo tumeonana naye, tumeishia kusalimiana tu, kisha akatoka nje alikuwa anamsindikiza mama dada mmoja hivi, lakini alisema atarudi siyo muda. alijibu Kulwa.
Wote watatu, watoto wanaosoma kidato kimoja, kasoro ubora wa shule, na pia ni rika moja wakiendana kwa vitu vingi huku wakitofautiana sehemu ndogo sana, ni kwamba samson alikuwa handsome sura ambayo ni ya mama yake mzazi huku akina Kulwa wakifanana kwenye familia ya Mgaya Mzee ambaye ni Babu yao.
Wakati huo Samson hakuongea lolote kuhusu taarifa ya baba yao kuwekwa lock up, aliona si watu sahihi kuwaambia, wakatoka nje wakiwa wamekaa kibarazani wakiulizana maswali kadhaa huku Samson akishangaa baadhi ya definitions kwenye maswali anayoulizwa zikitofautiana, lakini akigundua zote zina maana ile ile.
Baadaye sauti ya mama yao ilisikika, wakakimbilia kufungua geti huku Samson akiwa nyuma nyuma pale getini, macho yakagongana na mama Kulwa.
Mwanangu cathy, njoo kwanza shoga yangu maana, Kuna vitu nikikusimulia unaweza sema mama ana mdomo Sasa njoo ujionee mwenyewe.
aliongea Mama Kulwa.
Mama Kulwa bwanaa mwenzio ninachelewa tena, ujue nilikuleta ili uwahi tu na hili giza mamangu?
alilalamika Cathy huku akiingia ndani ya geti,
Heee, huyu mtoto amerudi tena, mtoto ana roho ngumu sijawahi ona, mwangalie kwanza kama ana laana vile, kwani msimrudishe kwao? Watoto wengine wanakuwaga wachawi ujue, huwezi jua nyumbani kwao wapoje ndiyo maana ujio wake umetibua Kila kitu, wewe ndani maelewano hamna, Mara mtake kuuana unafikiri Kuna nini mama.
aliongea Cathy akimsimanga Samson.
Wewe unafikiri hapa atafute nini, wamesikia sijakufa ndiyo maana amerudi kuja kunimalizia, Sasa Sina Cha kusema maana Kuna kitu umeongea mwanangu nimekuelewa sana, hapo kwenye uchawi, kwenye uchawi hapo nashikilia na kupakamata, ooooohooo Mimi naingia zangu ndani mwanangu.
Waliagana na Cathy huku akina Kulwa wakishindwa kujua wamuulize nani kuhusu yanayoendelea pale maana hawakujua chochote.
Cathy alitokea kujenga chuki mbaya kwa Samson, haikufahamika Mara moja lakini ilishangaza sana,
Mama Kulwa na wanaye waliingia ndani huku wakimtaka Samson aingie ndani lakini akawa ana hofu sana hakuweza kuingia ndani, dada wa kazi alimuhurumia Samson, ikabidi amuite nje waongee vizuri lakini Samson hakuongea chochote zaidi ya kulia kilio cha kwikwi.
Haikujulikana akina Kulwa waliambiwa Nini na mama yao, kwasababu hawakuonesha kumjali Tena Samson waligawana vyumba Kisha kwenda kulala, dada wa kazi akitambua Samson hawezi kusogea mezani kuja kula alipakua chakula akamletea Samson nje,
Kula, kula mdogo wangu, Mimi nadhani ni bora umwambie baba akurudishe kijijini kwenu maana, nahisi hali hii inazidi na utaumia hapa mjini. alishauri housemaid.
Samahani dada, naomba umwambie mama kuwa baba yupo ndani kituo Cha polisi Cha (akitaja jina).
aliongea Samson.
Mmmmh mama kaingia kulala, hebu ngoja nikajaribu kumgongea nimwambie habari hizi, aliongea dada wa kazi huku akienda usawa wa chumba Cha mama yake.
Samson naye akapata chance ya kuingia chambani kwake kulala, alivyoingia tu kwanza aligundua godoro juu ya kitanda halipo , maana tangu afike pale aliishia kudakwa na akina Kulwa na kushindwa kujua vilivyomo ndani hakukuwa na shuka Wala nini, angemwambia nani au angemuuliza housemaid halafu angemsaidia nini, akajikunja akalala chini sakafuni.
Usiku wa saa nane, Samson alisikia akiitwa , kutega sikio vizuri alikuwa ni mama Kulwa, Kwa uoga, na kwa kutetemeka akahisi labda ni mwisho wa uhai wake, akidhani pengine ni mama Kulwa anataka kumuangamiza.
Samson alifungua mlango huku moyo ukimdundadunda, akaambiwa aje Hadi sebuleni ambapo alikaa mama yake,
Samson nimekuita kwasababu wakati nakaribia kulala niliambiwa taarifa fulani na dada yako, ila niliipuuza na sikuipuuza tu Bali nilifurahi kama yaliyomkuta Mzee Mgaya ni ya kweli, lakini Mimi ni binadamu tu, naamini ni mwenye dhambi nakosea kama watu wengine, siwezi kulala usingizi ikiwa my husband baba Jose yupo sehemu isiyokuwa nzuri hebu niambie kwani ilikuwaje?
aliuliza mama Kulwa.
Kwanza Samson, alishangaa upole wa ghafla wa mama Kulwa, ndipo alipotulia na kumweleza tangu walipopokea ile barua, wakiwa kwa Tausi, Hadi wanafika kituoni na mwisho wa siku baba yake akawekwa kizuizini.
Sasa mbona hukunieleza mapema, yaani tunakula vizuri hapa , tunafurahi na wanangu kwakuwa siku nyingi hatujaonana kumbe mume wangu yupo mahabusu jamani, aliongea kwa uchungu mama Kulwa.
Samson alitamani aseme jambo baada ya kulaumiwa eti, kwanini hakusema mapema, lakini alikaa kimya kwani alijua kusema lolote ni kujipalia makaa ya moto.
Yaani hapa nasubiri kupambazuke tu nikamtoe mume wangu wasiniletee ujinga, halafu pia samson mgongee dada yako mwambie akupe godoro na vitu vingine , aliongea mama Kulwa akiinuka na kuingia chumbani kwake.
Samson hakumuamsha mtu Wala nini alirudi kulala huku akishindwa kupata tena usingizi maana ilikuwa karibu kunakucha.
***************************************
Usingizi hauna adabu, si mama Kulwa Wala Samson aliyekumbuka kujihimu badala yake samson aliamshwa na makelele ya lawama za Mzee Mgaya pale sebuleni akaamka kwenda kusikiliza Kuna nini.
Mimi nakuapia Mzee mwenzangu, nakwambia yule mtoto nitahakikisha anahama, hawezi kunidhalilisha yule mtoto, yaani kupandishwa cheo kufikia pale ndiyo kuingilia mambo ya wengine, yule wakunilaza ndani Mimi yule? Nikwambie tu ukweli nitahakikisha anahama hapa labda kama si Mimi James Mgaya nakwambia. alibwata Mzee Mgaya akionesha kumlaumu afande aliyemuweka ndani.
Hivi Mzee mwenzangu kama nisingepewa taarifa hizi nikaja kukutoa pale Ina maana ungelala siyo. aliuliza Mzee fulani wa miraba minne pande la mtu ambaye ni rafiki wa mzee Mgaya.
Wewe acha tu hata hivyo nitajua namna ya kupambana na yule kijana, Mimi simjui vizuri , ila kwakuwa wewe unamjua nitadili naye, alizidi kutoa vitisho Mzee Mgaya.
Hatujui yule , hajui kama sisi ndiyo tunaamua nani awe kitengo, hiki na nani awe nani. Waliendelea kujibizana kwa ukali na sauti za juu kana kwamba wamegombana kumbe ni stori zinazomuhusu afande aliyetoa amri Mzee Mgaya akae ndani.
Wakati huo samson hakujua kinazungumzwa nini, na mama Kulwa alikuwa pembeni akisikiliza maneno ya wale walevi wawili kwani walilewa ipasavyo, akaanza kufikiria
Samson anasema huyu baba yake aliwekwa selo mbele yake, Sasa katoka muda gani, na walikuwa wapi mbona wamelewa hivi?
Alijiuliza hakupata majibu ya harakaharaka, hatimaye yule mgeni akaondoka, wakabaki wanafamilia.
Itaendelea........... ......
Yepi hayo mkuumkuu ungetupia na yale kabsa ndugu
hahahaa hatimaye tumezifikiaTuendelee kusubili nyama ipo chini beb
Nlichapia mkuu nlimaanisha ya janaYepi hayo mkuu