Simulizi: Milango ya mafanikio

Maskini Samson, ulivyo malaya sasa unaweza kumparamia madam usiku wakati matatizo yako ndio kwanza yameanza
 
Ahahahahah eti uteuzi.....huko ofisini samson atawafyeka wanawake wote
 
Purukushani moja hv enz za usichana Wang khaaa basi tu naogopa kusimulia hako kastor Mkuu
Hata mimi episode imenikumbusha mbali sana, enzi hizo niko fomu foo
though sikufuzwa lkn nilisepa home saa sita usiku
tumetoka mbali na kupitia mengi
 
Hata mimi episode imenikumbusha mbali sana, enzi hizo niko fomu foo
though sikufuzwa lkn nilisepa home saa sita usiku
tumetoka mbali na kupitia mengi
kidogo ifanane na ya kwang sema Huwa nkikumbuka nataman kujipiga vibao walahi vile
 
Reactions: ram
SEHEMU YA SABINI NA TANO

Samson aliwaza mambo mengi akiwa pale kitandani huku akiwa na mawazo mengi, alishindwa wa kumlaumu akijikuta kila lililoendelea hakuna aliyemuonea.

Aligeuka alimwangalia Madam ama mwalimu wake, akagundua usingizi umeshamchukua, akaamua kuinuka pale kitandani na kuja sebuleni lengo likiwa ni kutafakari upya nini kifanyike aliziangalia zile pesa akiamini ni kweli zingeweza kumfikisha nyumbani kwao mkoani lakini aende akafanye nini, wazazi wake wanategemea siku mtoto wao akirudi aje na habari njema Sasa itakuwaje ikiwa tofauti?
aliwaza sana Samson.
Usingizi ulimchukua saa ngapi hakujua, alishtuka akiamshwa na Madam pale kwenye kiti huku akishtuka baada ya kuona mandhari tofauti na akili ikirudi akigundua yupo ugenini na si kwa mama Kulwa.

Hujambo Samson,
Alisalimia Madam.

Samson akaitikia Salamu ile, huku akimpa heshima yake mwalimu wake.

Nakumbuka nilikwambia uje ulale ndani Sasa huku ulikujaje? aliuliza Madam.

Ni mawazo tu mwalimu, nadhani hata Jana sikukusimulia ipasavyo kifupi sioni nikiendelea na shule kwani watu ninaowategemea hawataki hata kuniona.
alijibu Samson.

Sawa, Sasa sijui itakuwaje maana usiku ule nimekuonea huruma ndiyo maana nikakupa hifadhi, lakini suala la wewe kukaa hapa haiwezekani, nadhani mchana huu inatakiwa utafute namna ya kuwasiliana na wazazi wako ili mjue mnayajenga vipi, lakini hapa kwangu haiwezekani tena kwanza mazingira yenyewe umeyaona tunawezaje kuishi wote lakini pia haiwezekani Mimi nikakaa na mtu ambaye sijui kafanya kosa gani, haiwezekani.na Sasa najiandaa kwenda shule na wewe inatakiwa uitumie siku hii ya leo vizuri uhakikishe unapata jibu aidha urudi kwenu kama unavyosema au upatane na walezi wako. Mimi sina cha kukusaidia na halafu familia yako wale wazee ni watata sana ni ngumu mtu kwenda kukuombea msamaha ni wajuaji sana. aliweka kituo Madam huku akimlazimisha Samson atoke akaangalie ustaarabu mwengine mbele.

Samson aliingia mtaani na begi lake huku mawazo yakizidi kumsonga, pengine umri na alichofanyiwa ilikuwa tofauti, aliendelea kuzunguka asijue anaenda wapi, aende kwa mama Kulwa ili aombe msamaha, akahisi hatasikilizwa, au aende basi kwa Tausi ili angalau apate utetezi lakini akikumbuka Tausi ndiye aliyekuwa anashikilia na kutoa msimamo wa yeye kufukuzwa.

Wazo likamjia kuwa Mzee Mgaya ana marafiki wengi sana tena wa maana anaweza kuwafuata baadhi awaeleze yanayomsibu pengine atasikilizwa, lakini Kila akijaribu kuvuta picha namna atakavyoulizwa maswali na ikiwa atasema ukweli basi ataonekana ni kijana asiyekuwa na adabu basi alikata tamaa hakutaka tena.

Hadi kufikia saa tisa alasiri hakuwa ametia kitu mdomoni, pesa alikuwa nayo lakini hakuwa na hamu ya kula mawazo yalimvuruga sana. alitafuta sehemu ajipumzishe baada ya kuzurula muda mrefu, akiwa hana hili Wala lile ghafla Kuna gari ilipaki karibu na yeye huku wakishuka watu watatu wanaume wawili na mwanamke mmoja huku dereva wa gari akiwa hajashuka kwenye gari.

Mwanaume mwenye miraba minne huku akiwa nadhifu kimavazi , alianza kumuuliza maswali kadhaa Samson.

Sihitaji salamu yako ni kwamba nataka kujua wewe ni nani na unafanya nini hapa, Kuna watu Wana wasiwasi na wewe kwani tangu asubuhi unazunguka mtaa mmoja kiasi cha kuwatisha wakazi wa eneo hili , hawakuelewi. aliongea jamaa huku akiwa makini .
Licha ya Samson kutaka kujibu lakini alitupiwa swali lingine ikawa ni ngumu kujibu, ajibu swali lipi aache lipi.

Unaona afande huyu ni mwizi Hawa wanatabia ya kuchora ramani mchana ili usiku iwe rahisi kuja kutuibia . alizidi kuchochea moto mwanamke aliyekuwa pale.

Wewe mama usijali, Hawa ndiyo tunawatafuta siku zote, alijibu yule afande ambaye alianza kupekua begi la Samson huku akizikuta nguo za shule,

Heee jamani majirani huu ni ushahidi hii sare ya shule ya (akitaja jina)

Ndiyo , masikini kumbe huyo mtoto mwizi eeeh, yaani ukute amesababisha mtoto wa mtu asiende shule kwa kumuibia. alizidi kuchochea moto mwanamke yule huku afande akimzuia Samson asijibu chochote, licha ya kujitetea mara nyingi lakini walimwambia ni mwizi na akae kimya, aliendelea kupekuliwa huku msala ukawa mkubwa zaidi baada ya kukutwa na kiasi fulani cha pesa, alianza kupigwa na yule afande huku wananchi wenye hasira Kali wakimtaka afande awaachie ili wadili naye maana wamechoka kuibiwa lakini walizuiliwa na afande mwingine ambaye alibaki ndani ya gari kama dereva lakini kwa kuokoa maisha ya Samson aliamua kushuka kwenye gari huku akiwa na silaha na kuwafanya baadhi ya raia warudi nyuma huku wakitukana matusi yote ya Duniani.

Mtoto mdogo umri huo ulipaswa uwe shule, lakini unaiba unadhani wizi utakufikisha wapi na leo hii ungekuwa ni marehemu mjinga wewe, mshukuru huyu afande , alishuka kwenye gari na kukutetea Mimi ningekuwa peke yangu ningewaachia wakugeuze kama nyama, aliongea yule afande huku Kila saa akimpiga vibao Samson., Huku Samson Kila akijaribu kuongea maafande wakimzuia na kumwambia akiendelea kuwasumbua watamshusha katikati ya raia ashughulikiwe.

Walifika naye kituoni huku wakimsukuma na kumwambia avue viatu tayari kuwekwa Lock up kama mahabusu, Samson aliomba MUNGU kimyakimya huku sauti ya mama yake mzazi ambaye yupo kwao kijijini ikimwambia mwanangu kumbuka kusali, kwenye Kila hatua ya maisha na masomo yako mshirikishe MUNGU. Kauli ile alipewa siku wakati akisindikizwa kwenye kituo cha basi tayari kuja jijini Dar es salaam mahali anakoishi baba yake mkubwa Mzee Mgaya.

Wewe mjinga vua viatu , unajiliza nini, unatafuta huruma , yaani unajifunza wizi ukitegemea nini, unadhani serikali imelala eeh hebu kwanza sogea huku mpumbavu wewe. aliongea mmoja wa maaskari waliokuwa pale huku wengine wakicheka sana. Wakati huo Kuna afande alishangaa kuona kumbe anayeambiwa ni mtu anayemfahamu.

Hebu afande subiri kwanza huyu mtoto mbona kama namfahamu, huyu anakaa kwa yule mzee wanamuita nani sijui, kwao siyo mbali ni kama robo saa tu, eti unaitwa nani wewe na kwanini uibe. aliuliza mmoja ya maafande waliokuwa pale kaunda

Ndipo Samson alipoanza kujieleza vizuri huku akiwa haachi neno maana alijua ukweli utamuweka huru.
maaskari waliangaliana huku wakiridhika na maelezo Yale kwa kiasi fulani hata wale ambao walimpa kichapo kwenye gari walianza kuona huruma huku wakitoka nje kwa kuzuga Wana majukumu mengine.

Lakini msiamini maneno yake huyu kijana lazima mzazi wake aje hapa aturidhishe kama ni kijana wake, hatuwezi kukubali kirahisi, au hamjui wezi na vibaka wanavyojua kugeuza maneno na kujieleza vizuri, alizidi kupigilia msumari afande mmoja aliyekuwa anahesabu hela za mahabusu fulani aliyetoka kupewa dhamana na jamaa zake.

************************************
Mama Kulwa alifika pale kituoni huku akimalizana na maafande na kumchukua Samson, mama Kulwa alimwangalia Samson huku wakiwa hawajasalimiana na hawajaongea lolote, mama Kulwa alitia gia huku Samson akishangaa mama Kulwa akiendesha gari kwa mkono mmoja mwingine akifuta machozi huku akiwa hataki Samson ajue kama analia. Gari ilikuwa inaelekea sehemu siyo lakini Samson hakuuliza kitu hatimaye wakafika kwenye zahanati moja iliyokuwa inasifika kwa huduma nzuri , baba tafadhali mwambie daktari Kila kitu usimfiche sehemu yeyote unahohisi una maumivu nayo. aliongea mama Kulwa huku akionesha ni mnyonge sana. Haswa baada ya kulaumiwa na polisi kuwa kwanini anachukua majukumu ya kumfukuza mtoto mdogo nyumbani Tena nyakati za usiku, na kusababisha raia wamuhisi mtoto vibaya hali ambayo ingepelekea kupoteza maisha ikiwa raia wangejichukulia sheria mkononi, huku polisi wakijivua na kudai wao hawana makosa.

Samson alipewa matibabu kisha akatoka huku daktari akimshauri kuwa akiona mabadiliko basi asisite kurudi tena,wakati anafika pale reception alishangaa kumuona Mzee Mgaya ambaye alimfuata Samson na kumkumbatia huku akimbusu kwenye paji la uso.

Mmmmh mke wangu, unajua huyu mtoto tungempoteza leo,aliongea Mzee Mgaya huku akiwa bado kakumbatiana na Samson.

Baba Jose naomba acha habari hizo utaniumiza mwenzio , hapa nilipo moyo unanienda mbio ningeanzaje kuwaambia kule kijijini, aliongea mama Kulwa huku safari hii machozi yakiwa hayajifichi.

Mzee Mgaya alipanda kwenye gari lake na kutokomea sehemu nyingine, huku Samson akipanda gari na mama Kulwa na kurudi nyumbani wakiwa hawaongei chochote njiani.

Milango ya mafanikio ipo mingi sana, kwa Dunia ya Sasa tunaamini katika Elimu ndiyo inaweza kufungua milango hiyo, je milango yenyewe ni rahisi kufunguka au Kila mlango una funguo zake?
Tiririka na Samson.

Itaendelea.........................
 
Hii imeniumiza mnooo jamani hadi chozi walahi
 
Nimelia kama mama kulwa🥲
 
Nimelia kama mama kulwa🥲
Mnakuwaga na machozi ama vilio vya furaha na vya huzuni ama maumivu na vingine vya kinafiki jamani. Yaani unalia kabisa inaonekana umeumia kumbe una act. Na kilio kingine Cha utamu ,eti unasema bebi nitwange taratibu unaniumiza kwa utam¥¥ so huwa hamueleweki.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…