Simulizi: Mchezo wa Kirafiki

Halfan Hamisi

New Member
Sep 11, 2021
4
7
FAIR PLAY
(Mchezo wa kirafiki)

Sehemu ya................01

Saa 2:30 Asubuhi, ZAMBE.

Gari aina ya Land cruiser lilikuwa likienda kwa kasi sana katikati ya mji wa Nzambe.

Ndani ya gari hilo walikuwamo watu wanne wote wakiwa wamefunika nyuso zao kwa vitambaa vyeusi.

Katika siti ya nyuma alikuwepo binti mmoja mdogo amefungwa miguu na mikono Aliitwa PENINA

Macho yake yalikuwa mekundu sana

ilionyesha kuwa Binti huyo alikuwa amelia kwa muda mrefu.

Mji wa Nzambe ulikuwa kimya kabisa hawakukutana na gari wala mtu yeyote tofauti na ilivyokuwa kawaida ya mji huo

Ni baada ya wataalam wa teknilojia ya ardhi kutabiri kuwa kutatokea tetemeko kubwa la ardhi ambalo lilikadiriwa kuleta madhara
makubwa hasa kwenye mji wa Nzambe uliokuwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi.

Kwa kuliona hilo Serikali iliwaomba wakazi wote wa mji wa Nzambe waondoke Mara moja na ndivyo ilivyokuwa.

****

Penina alitazama huku na huku hali akionyesha wasiwasi mkubwa Hakujua watu hawa walimteka kwa lengo gani na ni kwanini wamemleta eneo la Nzambe ambako Serikali haikuruhusu mtu yeyote kuingia.

Baada ya mwendo wa dakika 15 hatimae gari lilisamama mbele ya jengo moja kubwa la kisasa, ilikuwa ni ghorofa.

Penina aliinua macho taratibu na kutazama nyumba hiyo haraka akaitambua. Ilikuwa ni nyumba yao waliyohama muda mfupi baada ya Serikali kutoa tamko la wao kuondoka katika mji huo.

Wakati Penina akiendelea kushangaa Mara mlango wa gari ulifunguliwa kwa nguvu. Bila hata kuuliza Penina alinyenyuliwa juu juu
kuelekea ndani ya nyumba yao.

Walipanda hadi ghorofa ya juu kabisa, wakaingia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa kitupu.

Penina alitupwa juu ya sakafu kisha wale watu wanne wakasimama mbele yake wakimtazama.

Penina aliwatazama mmoja baada ya mwingine kwa zamu, hakika walitisha.

"M..mnataka nini se..me..meni Baba atawa..wa. aaaaah" Penina aliongea kwa hofu lakini kabla hajamaliza alilia kwa maumivu makali baada ya buti zito kutua tumboni mwake.

Taratibu yule mtu aliempiga alichuchumaa huku akitoa kitambaa kilicho uziba uso wake wakatazamana na Penina.

"Doctor Rahabu?" Penina aliita kwa mshangao mkubwa. Alikuwa ni mwanamke aliefanya kazi na Baba yake istoshe alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa Baba yake, wote walikuwa ni Madaktari waliofanya kazi hospitali moja

" Ooh! Unakumbukumbu nzuri binti" alisema Dr rahabu huku akiuinua Uso wa Penina kwa Kidole kimoja kisha akamkazia macho,

"Unasema baba yako atatupa tunachokitaka si ndio!?"
Alihoji Dr rahabu kisha akamsogerea zaidi na kumnong'oneza

"Tunataka uhai wakeee,,," kauli hii iliyomshtua sana Penina.

Dr aliongea kisha akacheka kwa nguvu sana Mara simu yake ikiita akapokea na kuweka sikioni.

"Ndio tuyane.....Sawa..... Sawa....nimekuelewa chief...Sawa" Alimaliza mazungumzo akaiweka simu chini sakafuni kisha akamtazama tena Penina.

"Unajua ni kwanini, tunataka afe!?" Aliuliza Dr Rahabu kisha akaendelea kuzungumza
"Kwa Sababu ni yeye ametuomba tumuuwe"

Dr rahabu alisimama na kuwapa ishara watu wake wamfuate. Wakatoka nje ya kile chumba.
Penina aliwasikia wakijadili kitu ambacho yeyeto hakukielewa.

Penina alibaki akitafakari maneno ya Doctor rahabu, hakika yalimchanganya.

Wakati akifikiri mara aliiona simu ya Dr Rahabu pale sakafuni
Haraka alijivuta na kuishika
Japo alikuwa amefungwa mikono lakini uliweza kuishika vizuri.

Bahati nzuri simu haikuwa imefungwa
Akabonyeza namba kadhaa nakupiga ilikuwa ni namba ya Baba yake.

"Samahani namba ya simu unayopiga inatumika kwa sasa".

Penina alikata simu kisha akavuta kumbukumbu ya namba nyingine.
Akaikumbuka namba ya rafiki yake.

Safari hii simu iliita, na mara ikapokelewa.

"Hallow Balton, ni mimi Penina njoo nyumbani haraka nime..."
Kabla hajamalza kuongea Mara simu ikachukuliwa ghafula ikifuatiwa na kipigo kizito.
Alikuwa ni Doctor Rahabu na watu wake.
Penina alilia kwa maumivu makali huku damu zikimtoka mdomoni na puani.

" Hallow, hallow ,hall. ..," Balton alikuwa akiongea
upande wa pili na mara simu ikakatwa.

"Unataka ufe mapema eeh!, usijali kufa utakufa tuu". Dr Rahabu alisema kwa hasira kuhu akichukuwa saa
moja kubwa ya ukutani akaiweka mbele ya Penina

" Sasa ni saa 4: 31, Bado dakika 29 tu hilo
Tetemeko litokee, utafia huku na Baba yako Sawa mtoto mzuri"
Aliongea Dr rahabu huku akitabasamu kisha akasimama na kaondoka
watu wake wakamfuata.

Penina alisikia sauti ya mlango ukifungwa na
funguo.
Baada ya dakika kadhaa alisikia pia mlio
wa gari likiwashwa na kaondoka.

Chumba kilikuwa kimya kabsa, mshare
wa saa pekee ndio uliosikika
Penina aliitazama saa,
zilikuwa zimesalia dakika 21.

Penina alifikiri ni namna gani angeweza kujisaidia lakini hakupata majibu, hakuwa na nguvu ya kusimama wala kufanya lolote
Aliendea kulala chini huku machozi yakimtililika,

Hatimae , zilibaki dakika 10,
Penina alijikatia tamaa mwenyewe sasa alikuwa tayari kwa lolote,

"Hivi ni kweli Tetemeko litatokea?, mbona hii ni kazi ya mungu, kivipi Binadamu wa kawaida akajua tetemeko litatokea, tena hadi muda, hapana hii haiwezekani"
Penina alikuwa akiwaza kuifarji nafsi yake.

Sasa zilibaki dakika tatu, mbili, mmoja na hatimae sekunde,
Penina alifumba macho kwa hofu.

Alipofumbua tayari zilizidi dakika mbili, na Hakuna kilichotokea.

Penina alitoa tabasamu hafifu akiamini sasa yuko salama,
Taratibu alijivuta hadi kwenye Dirisha kubwa la vioo,
Akachungulia nje kuhakikisha, ni kweli hali ilikuwa shwari kabisa hakukuwa na dalili zozote mbaya.

Wakati penina akichungulia nje kwa mbali alimuona mtu akija anakimbia kuielekea nyumba yao ilikuwa ni ajabu kidogo kwani kwa wakati huo hakuruhusiwa mtu yoyote kuingia ndani ya mji wa Nzambe
Penina alikaza macho kumuangalia mtu huyo aliyezidi kusogea

"Mungu wangu, ni Baba!!" Penina aliita kwa mshangao mkubwa.
Ni kweli mtu aliyekuwa anakuja huku akianguka na kuinuka
mara kadhaa alikuwa ni Baba yake Penina aliitwa Doctor Mwasaga.

"Penina, penina mwanangu, peninaaaaaa!!" Doctor Mwasaga aliita huku akiendelea kukimbia kuielekea nyumba yake.

Akiwa amebakiza hatua kadhaa kufika mara alisimama ghafula
Ni kama alihisi kitu, akatazama chini ya miguu yake,,,,,,
Ardhi ilikuwa ikitetemeka.

"TETEMEKO!!" Dr mwasaga alisema hali akiwa haamini.

alisimama kwa Dakika mbili mfululizo akiwa amepigwa na butwaa, mtikisiko wa ardhi ulikuwa ukiongezeka kadri muda ulivyo kwenda.

Kishindo kikubwa kilichosikika nyuma ya Dr Mwasaga ndicho kilimshtua kukoka katika hali ya mshangao.

Alipogeuka nyuma alishuhudia baadhi ya maghorofa kadhaa yakianza kuporomoka kutokana na mtikisiko mkubwa wa ardhi, sasa mji wa Nzambe ulianza kuchafukwa.

Dr Msigwa aliiona hatari kubwa iliyokuwa mbele yake na binti yake Penina ambao bila shaka ni wao wawili tu waliokuwa katika mji wa Nzambe, alifika hapo baada ya kupigiwa simu na watu wasiojulikana wakamwambia mwanae ametekwa na kupelekwa kwenye nyuma yake ya Nzambe, Dr msigwa alichanganyikiwa haswaa.

alianza tena kukimbia huku akianguka kutokana na mtikisiko mkubwa wa ardhi , hali akijaribu kukwepa vitu vilivyoanguka kutoka juu.

Hatimae alilifikia geti la nyumba yake akalishika kwa nguvu na kutazama juu ghorofani katika chumba alichofungiwa mwanae Penina
wakatazamana Uso kwa Uso.

"Huwezi kufa mwanangu" aliwaza Dr Mwasaga huku machozi yakimtoka.

JE NI NINI KITAFUATA!?
USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA PILI.
 
Haya mambo ni poa kakini sasa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom