“Sawa, unastahili haya yote,” Cindy alisema kwa upole, “sijawahi kuona mtu asiye na haya kama wewe anayemtongoza mchumba wa mtu mwingine.”
"Unasikika kana kwamba una hisia ya aibu." Eliza alibaki kwenye kiti bila kujisumbua kuinuka. Ingawa ilimbidi kuinua kichwa chake kumtazama Cindy, bado alionyesha sura kali. “Angalau nilipata nafasi katika tasnia ya burudani kutokana na uigizaji wangu. Na wewe je? Kama mwimbaji, uliiga kazi za rafiki yako bora wa zamani. Kama mwigizaji, ungeweza kushinda tuzo kama Chester asingefanya michongo? Kuwa mkweli, kwa nini unataka kuwa mwigizaji? Kazana tu kumhudumia Chester vizuri kitandani. Labda ataweza kukununulia tena tuzo ya mwigizaji bora mwaka ujao.”
Loida alitetemeka mwili mzima huku akitazama hali ya baridi ya Eliza. Jinsi Eliza alivyokuwa na uthubutu kuwa na ugomvi na Cindy, ilimtia hofu sana.
“Umefanya vizuri, Eliza. Nitakumbuka kila neno ulilosema na kumjulisha Chester kulihusu. Kwa hilo, kazi yako ya uigizaji itaishia hapa.” Cindy aligeuka huku akitetemeka. Baada ya kujizoeza kuwa mtulivu na mwenye busara kwa miaka, hakumshambulia Eliza mwishowe.
Alipiga teke tu mlango wa sebule kwa nguvu wakati anatoka. Mara wale waliokuwa wakiangalia tamthilia hiyo pale mlangoni walipoona sura ya Cindy ya hasira, walimkwepa kwa kuhofia kwamba wangeteseka.
Kwa wasiwasi, Loida akaelekeza macho yake kwa Eliza. “Bi Robbins, najua unamchukia Cindy, lakini ulimfanya aonekane mbaya sana. Baada ya yote, yeye ni mchumba wa Bwana Choka. Hata mkurugenzi Mutui inabidi aongee naye kwa heshima.”
“Ni sawa. Nikishindwa kuwa mwigizaji, unaweza kuungana nami kuanzisha biashara siku zijazo,” Eliza alisema kwa njia nyepesi, “Ujuzi wangu wa ujasiriamali ni bora kuliko ustadi wangu wa kuigiza.”
Loida alikosa la kusema. “Naomba usinidanganye. Umewahi kuanzisha biashara lini? Zaidi ya hayo, ni rahisi sana kwa familia ya Choka kumwangamiza mtu yeyote.”
“Najua.” Eliza alicheka huku sauti yake ikiwa na kejeli.
Hakuna mtu aliyeijua vizuri zaidi yake kwa sababu yeye ndiye alikuwa ameharibiwa hapo awali.
Baadaye, Director Kalulu alifanya mkutano wa dharura. "Kwa kuwa Cindy anaolewa mwishoni mwa mwaka huu, anaweza kukosa wakati wa kutosha wa kushoot filamu. Baada ya kujadiliana na kampuni yake, tumeamua kumbadilisha na Eliza. Sasa Eliza atakuwa kiongozi kinara wa kike. Mwigizaji msaidizi wa kwanza atajiunga na waigizaji siku inayofuata kesho, ili kila mtu apumzike kwa siku mbili zijazo. Eliza, unaweza kuanza kupitia script ya kiongozi kinara wa kike kwa sasa."
“Sawa.” Eliza alichukua script chini ya mshangao wa kila mtu.
Hakuna aliyeamini kwamba Cindy aliondolewa ghafla hivyo kwa sababu ya harusi yake.
Labda ni kwa sababu uigizaji wa Eliza ulikuwa mzuri sana. Ikiwa Cindy angeendelea kuwa kiongozi wa kike, angepigwa chini na asingeonekana kama nyota wa filamu hiyo. Kwa hivyo, hakukuwa na chaguo ila kumfanya Cindy kuachia nafasi hiyo kwa Eliza. Hiyo ndiyo sababu pia Eliza na Cindy walikuwa na ugomvi mchana huo. Lakini, kila mtu alikuwa mwerevu vya kutosha kunyamaza.
Sura ya: 732