SEHEMU YA 152
Rose alikuja kushtuka na kugundua kuwa alilala pale usiku mzima na kazinduka kesho yake huku mwili wa mama jack ukiwa kwenye siti ya nyuma ya gari lake kama alivyouweka, alishangaa sana kisha kuanza tena kuendesha gari kwa haraka haraka hadi akafika nyumbani kwa mganga ila alimkuta akiwa amechukia sana, kwani aliposhuka tu kwenye gari lake na kukutana uso kwa uso na Yule mganga alishangaa akifokewa na Yule mganga,
“Ndio umefanya nini sasa Rose?”
“Sielewi”
“Huelewi nini na umemtoa kafara rafiki yako? Nenda kamzike sasa”
Rose alihisi kuishiwa nguvu kabisa kwani hakutegemea kama rafiki yake atakuwa amekufa,
“Nisamehe mganga”
“Na bora ungewahi jana ile ile, sasa mwili umeshapoa kabisa ndio unamleta kwangu? Nenda kazike tu”
“Nisamehe tafadhari sijui cha kufanya”
“Hujui nini? Nenda kazike”
“Sijapanga kumtoa kafara rafiki yangu hata sijui imekuwaje”
“Hivi wewe mwanamke una akili gani? Mwanzo si nilikutuma na dawa mtoni wewe nikakwambia ukimwaga utamuona mwanao kitandani halafu msukume mtoni, ila wewe ukamuona sijui Moza wako ukakimbia na hukuweza kumsukuma, sasa nimekupa dawa umwage mlangoni kwako, usiongee na mtu yeyote zaidi ukifika ndani uanze kutaja majina ya unaowatoa kafara. Ni kweli hujaongea chochote ila umeanza kumtaja rafiki yako huyu, ulikuwa na mpango gani nay eye zaidi ya kumtoa kafara tu. Na hiyo kafara haikusaidii chochote ni kama umetoa sadaka tu, haya nenda kazike mzoga wako”
Rose alijikuta akikosa nguvu kabisa kwani haya mambo yalivyoenda ndivyo sivyo yalizidi kumchanganya akili na akaona kunapoelekea sasa hata yeye binafsi atajikuta amejiua kwa presha au kwa namna nyingine yoyote maana hakuelewa chochote, hakujua aanzie wapi kuzika au aishie wapi.
“Sasa mimi nitamzikaje?”
“Kwani hujui watu wanazikaje? Wewe mwanamke ni mjinga sana, rafiki yako kakusaidia kakuleta kwangu halafu umemtoa sadaka, yani wewe mwanamke ni mpumbavu”
“Nakuomba mganga tumsaidie rafiki yangu kwa namna yoyote ile”
“Tumsaidie nini na mwili umepoa huo? Labda utoe kafara ya watoto wako wote”
Rose alichanganyikiwa kabisa, ila Yule mganga aliondoka na kwenda kwenye chumba chake cha uganga na kumuacha Rose akiwa na mawazo yasiyo na kifani.
Aliwaza kuhusu watoto wake na kuona kuwa vyote alivyovifanya kwa kipindi chote ni kazi bure,
“Hivi mimi si ndio nilimtesa yule mwanaume yani Patrick na kumfanya kama ndondocha sababu ya watoto wangu! Nilitaka waishi vizuri, wale raha ya maisha, yani leo nikawatoe wote kafara kweli! Hao wawili wenyewe nilikubali kwa shingo upande, naweza kuwatoa kafara watoto wangu kweli! Kuna sababu gani ya mimi kuendelea kuishi na kutafuta mali kwa haj azote ikiwa watoto angu nimewatoa kafara, kuna faida gani ya kuishi vizuri huku nikinyooshewa vidole na watu kuwa niliwatoa kafara watoto wangu! Nawapenda sana, niishi bila Sara, Kulwa, Doto na Ana kweli! Hapana kwakweli, na huu mwili wa rafiki yangu sijui nitafanya nao nini”
Aliwaza sana bila ya jibu la mawazo yake na alijihisi ni mkosanji kila alipofikiria kwani aliona anapoelekea sasa sio kuzuri, yani awatoe watoto wake wote.
Yule mganga akamtuma mtu ambaye alienda kumuita Rose na kuingia kwenye chumba cha mganga, na baada ya kuingia tu aliulizwa alichokiamua,
“Utaenda kumzika rafiki yako au utawatoa watoto wako kafara?”
“Nitaenda kumzika rafiki yangu”
“Yani wewe naelewa sasa kwanini wachawi wenzio hawashirikiani na wewe, yani wewe uchawi wako mkubwa ni kutegemea nguvu za waganga wa kienyeji, hakuna mchawi ambaye hatoi kafara, wewe ni mchawi gani wewe? Nakuuliza mara ya mwisho, utaenda kumzika rafiki yako au utawatoa watoto wkao kafara?”
“Nitaenda kumzika rafiki yangu”
Mganga ilibidi acheke huku akisikitika, alimuangalia kwa makini sana Rose halafu akamwambia tena,
“Nakupa machaguzi ya mwisho, nenda kafikirie kati ya kumzika rafiki yako na kuwatoa kafara watoto wako”
Rose alitoka tena na kukaa chini ya mti huku kichwa chake kikiwa kimejawa na msongo wa mawazo.