Simulizi kumi kali nilizowahi kuzisoma hapa JamiiForums

Wakipekee

JF-Expert Member
Aug 21, 2019
5,354
9,217
Habari wapendwa? Poleni na jukumu zito la ujenzi wa nchi yetu nzuri ya Tanzania. Ama baada ya salamu niende kwenye maada moja kwa moja. Leo nimeona nilete simulizi kumi kali nilizowahi kusoma hapa JF. Haimaanishi kwamba hizi ndio bora kuliko zingine ambazo sijazitaja hapana bali nimeamua tu kushare hizi chache na nyie mpate kuburudika kama ni mpenzi wa masimulizi najua zipo zingine kali sana nawewe pia sio vibaya ukitaja hapa nasisi pia tupate kuburudika.!
Karibuni


10.Goodness of fit:Love,Loyalty na Betrayal
Shukurani kwake KigaKoyo kwa hii simulizi niliipenda sana hasa namna anavosimulia inavutia sio siri. Anazo simulizi zingine kali lakini kwangu hii niliipenda zaidi.


9. THE LAST SUMMER IN TANZANIA
Kutoka kwa mtunzi Nyemo chilongani hii simulizi ni habari nyingine kabisa nazani bongo movie wamtafute huyu jamaa wafanye nae kazi trust me it will pay more! Asante kwa Abdallahking kwa kuileta hapa JF.



8.MSAKO WA HAYAWANI
Hii ililetwa na idawa lakini mtunzi ni Eddie Ganzel. Najua wahenga mnayo mengi kuhusu huyu mtunzi alikua balaa. Alale pema peponi.


7.SAFARI SABA ZA SINBAD
Hii ni simulizi ya kusisimua sana hasa inatukumbusha kua tusikate tamaa kwenye maisha. Ni kisa cha kale kilicholetwa hapa JF na mkuu Bujibuji. Itafute utafurahi


6. PENZI LA MFUNGWA
Kwa wale wapenzi wa masimulizi huko FB jina la mtunzi Alexis wa milazo sio geni ila ilieletwa humu na Sharobaro la jf. Simulizi ya kichawi inayosisimua sana.

5.KIJIJINI KWA BIBI
hii inatoka kwa mtunzi Alex kileo ila ileshushwa hapa na the_legend. Kuna nini huko kijijini ? Kaisome mwenyewe.


4. TAI KWENYE MZOGA
Kama unapenda simulizi za kijasusi basi hii n "baba lao". Bonge moja la riwaya toka kwa mtunzi nguli wa stori za kipelelezi muite KELVIN e. MPONDA ama jasusi kama yeye mwenyewe anavopenda kujiita. Shukurani kwake the banker kwa kiluleta huu uhundo hapa JF. Ukipata muda kaipitie utanishukuru nakwapia.


3. BAO TATU ZA MGENI
kama unazani ni zile bao za chota chama wa simba au za saidoo yule wa yanga basi unakosea sana. Hapa kuna mwamba alipiga mabinti wa watu mimba karibia kijiji kizima. Yaani alikua anakula tunda kimasikhara sana. Wanawake walidata na bao tatu za mgeni. Chombezo hili ni balaa la mtunzi Jack Mambo lakini lililetwa hapa na madau wa kuitwa Dampa. Isome utafurahi mwenyewe ila kama hauna mpenzi bro! My sister chunga sana utajikuta upo ngome kongwe ya CHAPUTA.


2. ANGA LA WASHENZI NA JOANA ANAONA KITU USIKU.
Ohoo! Unawajua washenzi kweli wewe? basi tulia usije ukaniuliza kwani washenzi wenyewe wanasemaje? Hilo swali tayari mtunzi kichwa SteveMollel alishalijibu. Hii ni moja kati ya stori za hapa JF iliyonifanya nikeshe usiku kucha kuisoma maana ni full mzuka ndo maana Zuchu alipoisoma akajua utamu wake balaa tupu yaani ni su..ka..ri. Sugar sukari!!!...


1. PENIELA
Hili dude nililisoma hapa mwanzoni mwa mwaka 2017 hakika ni hadithi ya kiwango cha nyota maana iko juu sana. Ndio ilinifanya nianze kupenda hadithi za kipelelezi heko kwake PATRICK CK. nazani wadau wadau wa JF tulipaswa kutoa tuzo kwa huyu mtunzi maana hii simulizi iliyotikisa zaidi anga la wasomaji hapa JF hadi neno "alosto'' likaingizwa kwenye urahibu wa kumiss simulizi. Kama unazani ni hadithi ya kuipotezea tu unakosea sana mazee! maana hadi leo ilishagonga " Viewers" zaidi ya milioni moja na ushee wa hapa jukwaani. Shukurani kwake mkuu LEGE kwa kutuletea hii burudani na nyingine nyingi kali. Ipitie utafurahi sana.

Mwisho!!!.
Cc Wakipekee
 
Kuna story za ukweli na zakutunga. Mimi napenda nisome zile za kweli ni zipi kati ya hizo ni za kweli ili nisome.


Kwangu Mimi hii ni the best kuliko zote,japo jamaa alizingua hakumaliza nadhani kutokana na ujuaji mwingi was watu.
Ni stori ya kweli.


Sijawahi vutiwa kusoma stori,
Hata hizo alizoweka jamaa pale juu nilijaribu kusoma nikashindwa .
Lakini hii ndiyo stori pekee niliyoshawishika kuisoma mstari kwa mstari.
 


Kwangu Mimi hii ni the best kuliko zote,japo jamaa alizingua hakumaliza nadhani kutokana na ujuaji mwingi was watu.
Ni stori ya kweli.


Sijawahi vutiwa kusoma stori,
Hata hizo alizoweka jamaa pale juu nilijaribu kusoma nikashindwa .
Lakini hii ndiyo stori pekee niliyoshawishika kuisoma mstari kwa mstari.
Asante. Hii niliisoma pia ila nadhani haikufikia mwisho iliishia njiani.
 
Sawa. Umeitendea haki 'Peniela" na Anga la Washenzi

11. Makaburi ya Wasio na hatia.

Tatizo la simulizi nyingi huwa hazifiki mwisho. 'The End' na kufanya ziharibu uzuri wa simulizi husika.
Ndo maana nikachagua ambazo zilienda mwanzo hadi mwisho
 


Kwangu Mimi hii ni the best kuliko zote,japo jamaa alizingua hakumaliza nadhani kutokana na ujuaji mwingi was watu.
Ni stori ya kweli.


Sijawahi vutiwa kusoma stori,
Hata hizo alizoweka jamaa pale juu nilijaribu kusoma nikashindwa .
Lakini hii ndiyo stori pekee niliyoshawishika kuisoma mstari kwa mstari.
Kwakweli hiyo stori ni noma sana sema Mimi nimechagua zile za kutunga tu ila hiyo naielewa nazani kwa mikasa ya ukweli iliyowahi kutokea watu hii n shida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom