Simulizi Huru Media Production

MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 01.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

DAR ES SALAAM:
"Kwa Majina naitwa EPIPHANIA WILNERY MKOMBO Au Mama Bright Kama ilivyozoeleka hapo mwanzo" Sauti ya Kigugumizi iliyoanza na utambulisho wa majina ilianza kusikika karibia kila kona ya ukumbi.

Kila mmoja sasa alikua tayari kusikiliza mkasa wa Kweli wa bidada huyu aliyejitambulisha kwa jina EPIFANIA, kulingana na mengi aliyopitia, Eppie aliamua kuweka wazi sasa mambo yaliyomsibu hadi kufikia hapo. Aliitwa katika mkutano mkubwa wa waandishi wa habari na mkutano huo kupewa jina la MACHOZI YA DAMU.

Waandishi walitamani haswa kujua ni kipi haswa kimsibu mwandada Eppie hadi kutumbukizwa gerezani kwa kosa la Mauaji?. Mkasa wake ukasimuliwa kama ifuatavyo;

“Mimi ni mwanamke nisiyezidi hata miaka thelathini na nne, Mzawa wa Wilaya ya Madaba iliyopo mpakani mwa Mkoa wa Ruvuma na Njombe. Kiasili mimi ni Mbena kabisa niliyechanganyika na Ungoni na Matengo kwa mbali, kilichonileta hapa ni kuhusu huu ushuhuda wa Machozi ya Damu ambao umepitia katika maisha yangu. MACHOZI YA DAMU!, MACHOZI YA DAMU!, MACHOZI YA DAMU! "

Alirudia Mara kadhaa maneno hayo kwa kutuweka sawa na vifaa vyetu ili tupate mkasa kamili, jambo lililoendelea kutia hamasa zaidi ya watu kusikiliza makini ni machozi ambayo yalikuwa yanamtiririka mwanadada huyu, kila mmoja akijiuliza kuna kipi kilichomsibu hadi kuporomosha machozi mzito mithili ya damu? na kwanini Mkasa wake aliupachika jina la MACHOZI YA DAMU???. Tukabaki vinywa wazi kusubiri majibu.

“NDUGU Waandishi, Ndugu Wasikilizaji, Ndugu Wanaume na Ndugu Wanawake wenzangu, najua Tanzania nzima sasa imetega sikio na jicho lake kusikia na kuona kile ambacho natamani kusimulia. Sidhani kama nitafanikiwa kuyatoa maneno yote ya moyo wangu kutokana na machungu yaliyonishika. Moyo wangu unauma sana na kujihisi nina hatia, labda ni kwa sababu ya maamuzi ambayo niliyachukua baada ya kuteseka kwa muda mrefu, Nimesababisha kifo mimi ndugu Waandishi ah, oh, Ohah ha ha ha ha mimi Eppie... Eh Mungu Jitahidi kunisamehe kosa hili japokuwa wanasema halina msamaha!" Eppie aliendelea kuongeza kilio kidogokidogo na kuacha hudhuni itawale chumba kizima. Kabla hajaanza kusimulia vizuri tayari kila mmoja mule ndani alianza kuonesha kumhurumia. Aliendelea.

“Nilizaliwa Tar 25/10/1998 hadi leo hii 2030 nipo mahali hapa nimeshatimiza miaka 32.

Nilizaliwa wakati wa wazazi wangu wote wawili wakiwa wanapatana, wote wakiwa wazima hadi leo hii ninapoongea nanyi. Nilimaliza Elimu yangu ya Msingi na Sekondari hukohuko Wilayani Madaba na Shule ya Upili nilimaliza pale shule ya sekondari ya Wasichana wilayani Masasi mkoa wa Korosho-Mtwara. Kwasababu za kufanya vizuri katika masomo yangu, Mungu akaniadhibu sasa kwa kinipeleka kusomea Kozi ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lakini katika tawi la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kwa miaka mitatu ya shahada ya kwanza.

Kipindi chote hicho tayari nilishaanza kujiweka wazi kuwa nitasimamia msimamo wangu wa kuishi maisha yangu, na sitakuja kulia kisa Mapenzi. Na leo nasimama mbele yenu na chozi la damu likitiririka kama mvua. Ah, jamani!, jamani! Jamani!, Omba tu uendelee kusimuliwa. Maisha ya mapenzi yanalaana. Yana laana ndugu zangu...." Eppie aliendelea kuongea akisogeza kitambaa chake chepesi na kuyafuta machozi yake yaliendelea kutiririka. Akaweka sawa kora yake sare ya magereza na kuendelea.

"Hapohapo chuo nilikutana na kila aina ya wanaume, warefu, wafupi, wembamba, weupe, maji kunde, chotara, wenye pesa na wasio na pesa lakini moyo wangu uliendelea kutulizwa kuwa hakuna mwanaume hapo ambaye anaweza kukidhi haja ya moyo wangu. Wote nilihisi ni wababishaji tu. Wakaka wa chuo? Ah, hapana kwa kweli. Labda kwasababu ya mazingira niliyotoka nikawa nawachukilia wanaume kawaida tu. Na pia labda kwa sababu pengine labda sikupata yule nyonga mkalia ini ambaye amethubutu kuucha’chafya moyo wangu na kujikuta nauhifadhi kwake!. Nikaendelea kutunza usichana wangu. Niliiutunza, kumtunzia mwanaume ambaye hakuwa na shida na moyo wa mtu. Mwanaume ambaye alibadili Eppie mimi kutoka utulivu na hofu ya Mungu hadi kuwa mhusika wa kifo chake. Nikaitwa Muuaji. Eppie mimi ni muuaji jamani haaaah!"

HADI hapo Eppie aliweka kwanza nukta na kuendelea kushusha machozi. Moyo ulinisuta sana kutaka kujua nini ambacho kipo ndani ya mkasa wa Eppie, Kwanini ajutie vile maisha yake kiasi cha kumkosoa hadi Mungu? Kwanini awe muhusika wa mauaji? Kamuua nani?, na kwanini???


Indelea...
Karibu Simulizi Huru Media Production. Sapoti kazi zetu katika mitandao yote ya kijamii. @SIMULIZI_HURU_MEDIA_PRODUCTON




MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 02.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

HADI hapo Eppie aliweka kwanza nukta na kuendelea kushusha machozi. Moyo ulinisuta sana kutaka kujua nini ambacho kipo ndani ya mkasa wa Eppie, Kwanini ajutie vile maisha yake kiasi cha kumkosoa hadi Mungu? Kwanini awe muhusika wa mauaji? Kamuua nani?, na kwanini???

CHOZI LA PILI...
"Ndugu Waandishi, Mwishoni kabisa mwa mwaka wa tatu, alikuja mtu maarufu sana chuoni kwetu, alikuja kutupa baadhi ya mambo ambayo yanaendelea mtaani hasa katika shida ya upungufu wa ajira.

Mtaalamu yule aliichambua vizuri sana Tanzania, alikuja na ushaidi wake wa data na takwimu nyingine mbalimbali. Akafanikiwa kuniteka pia katika suala lake la mahusiano, kauli yake bado haijatoka katika kumbukumbu zangu, nakumbuka! Nakumbuka alisema kuwa eti “Tafadhali huu ndio muda mzuri wa kupanga maisha yako.. Mwanamke! tafuta mwanaume wa maisha yako. Mtaani mambo sio poa. Jaribu sasa kumuweka mwanaume mmoja ambaye hisia zako zimekuweka huko. Mpende, mjari, mheshimu, kwa maana usipokuwa na msimamo sasa na kujiandaa katika maisha ya familia, utajikuta unapoteza muda mwingi sana kujifunza vitu vipya na vigumu ukiwa ndani ya ndoa. Nawashauri kwa kuweka hazina!. Jifunze kuchagua na kupenda. Jifunze kuwa na msimamo”: kauli hii aliitoa yule mtaalamu wa saikolojia katika mkutano mkubwa wa wanawake. Nikaichukua kama ilivyo, sijui niielewa vibaya au la lakini niliitendea kazi.

Tokea siku hiyo nikafungua kufuri la moyo wangu kwa kuanza kutafuta mwanaume ambaye atakuwa ndoto za maisha yangu. Nikaacha kufikilia mambo mengine na sasa kujikita zaidi katika masuala ya kuchunguza wanaume na sifa zao, yote hiyo ni kujua nani nitampa sehemu zangu za siri na akazitunza!, hatimaye nikaangukia katika mtego wa nguruwe. Mtego ambao hadi kufikia hapa sijajua ni nani aliutega? Na alikuwa anakusudio gani?. Kama kuniua basi amefanikiwa... Eppie mimi leo sina ndoto wala malengo tena. Miaka Thelathini na mbili tu nimeshazikwa tayari... Jamani mapenzi.."

Eppie aliendelea kutoa mkasa wake huku machozi yakiwa kama kinywaji. Kila neno aliloongea alionesha kuwa na uchungu mno. Bila shaka alikuwa anajuta, anajuta na atajuta sana. Sasa kwanini awe muuaji? Bado ukumbi ulikua kimya kumsikiliza.

"Kabla ya kufanya mtihani wangu wa mwisho wa kuhitimu elimu ya chuo kikuu shahada ya kwanza, nikakutana na mwanaume wa maisha yangu. Mwanaume ambaye ameacha kovu kwangu, ‘labda mtu alikua sahihi ila muda ndio haukuwa sahihi…’

Ah, Ilikuwa ni katika Uzinduzi wa Kampuni ya SIMULIZI HURU MEDIA PRODUCTION pale UBUNGO PLAZA. kwa kweli nilikua mpenzi sana wa simulizi za kusisimua. Simulzi zilinijenga sana. Nilijutia maisha wapitayo wahusika katika simulizi ila sikuamini kwamba kweli wandishi wanaandika mambo yanayotokea katika jamii.. Nilihisi ni visa tu vya kubuni na wameandika ili kujipatia kipato.

Kwa kuwa nilikua mpenzi wa Simulizi na mdau mkubwa wa Simulizi nilikuwepo siku ya uzinduzi ili nikutane na waandishi wangu watano muhimu ambao kazi zao nilikua nikizipenda kila kuchwao... Naomba niwataje tu hata kwa majina kwani nao yaweza kuwa ni wahusika wakuu wa mkasa huu... Aaaaah jamani.. Jamani... Jamani.. Mapenzi!.

Ah, naomba nimtaje Ibrahim Hussein katika nafasi ya kwanza.. Huyu alinikosha na mkasa wake wa Talaka kwa Mke Mwema. Twende kwa Talhat Moudy nae alinisukumia katika mkasa wa mwanamke mwenzangu ambaye Alishindwa kumsahau Mtunza moyo wake. Sam Darfur kama Mwenyekiti wa Simulizi Huru Media Production alinigusa kwa mikasa kadha wa kadha naomba nitaje tu huu wa Nani Kaniambukiza nikajifunza namna bora ya kutunza siri zangu usije yakanikuta yale mambo ya UKIMWI na nikashindwa kutambua nani ameniambukiza!. Marcus Cona pia alinikosha kwa visa vyake vya hapa na pale, kaka mcheshi sana huyu nilianza kumpenda toka ya kwanza anapandisha simulizi yake ya THIS IS DAR ES SALAAM huko YouTube katika Channel yao hiyo hiyo ya Simulizi Huru Media Production.

Naomba nimalize na huyu mwandishi. Beloved One, My Heart Beat, My Heart Master, Kipenzi Cha Wapenzi.. Aliniandikia PENDO HURU na simulizi ya MKUKI WA MAPENZI na kunichoma kabisaa!! Aliutumia huo mkuki kunichoma kabisa, kwa kweli alinipata, na huyu ndio sababu ya yote haya hadi leo hii nipo hapa kutoa ushuhuda huu, nikampa hadi uhusika katika moyo wangu nikiamini kuwa anaweza kuunda kama aundavyo vyema hadithi zake. Lakini....!! Da!. Da! Daa!


Inaendelea
Karibuni Wakubwa
FB_IMG_1619616896093.jpg
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 03.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

Naomba nimalize na huyu mwandishi. Beloved One, My Heart Beat, My Heart Master, Kipenzi Cha Wapenzi.. Aliniandikia PENDO HURU na simulizi ya MKUKI WA MAPENZI na kunichoma kabisaa!! Aliutumia huo mkuki kunichoma kabisa, kwa kweli alinipata, na huyu ndio sababu ya yote haya hadi leo hii nipo hapa kutoa ushuhuda huu, nikampa hadi uhusika katika moyo wangu nikiamini kuwa anaweza kuunda kama aundavyo vyema hadithi zake. Lakini....!! Da!. Da! Daa!

CHOZI LA TATU...
"Kama nilivyo eleza hapo mwanzo, ilikua ni siku ya uzinduzi wa Kampuni ya Simulizi Huru Media Production, katika pilikapilika za hapa na pale nikafanikiwa angalau kukumbana kikumbo na MR. XAVERY. Sikutarajia!, sikutarajia kwa kweli... Niliona hata aibu kuinua macho yangu kumwangalia mwanaume yule ambayo nilihisi kabisa nipo na hisia nae.

Nilibaki kuchezea mtandio wangu macho yakiwa chini kwa aibu na kusubiri mwanaume huyo aondoke pale ili nami niwe huru kusogea, lakini haikuwa hivyo; mwanaume yule aliendelea kuganda tu, nikijaribu kuinua macho yangu basi yanakutana na yake. Alikuwa kama mtu aliyefikwa na bumbuwazi. Moyo wangu ulikua kasi sana kutamani uhuru kwa dakika tu. Nilihisi hata kuzitoa pumzi zangu pia nakosea. Nikajistukia tu kwa kughuna kidogo na kumsalimia.

"Ah, Samahani.. Samahani sana. Bahati mbaya! Sorry" nilibabaika mno kutoa maneno hayo. Sauti yangu ilikua inapishana sana. Labda kwasababu ya woga ulionikumba.

Yule Bwana aliendelea kuganda tu palepale akiitazama sura yangu. Hata ile samahani yangu haikufika katika masikio yake. Yeye alikua makini kuniangalia usoni utadhani anachagua chunusi katika uso wa mlimbwende ambao ni nadra kuzipata. Alibaki kunishangaa tu mwanaume yule. Bila shaka uzuri wangu pia na jinsi nilivyovaa ilikuwa ni mvuto kwake.

Nilijichekesha kidogo na kuivuta kwa juu nguo yangu ndefu iliyofika hadi miguuni, nikamega hatua mbili za wasiwasi huku moyo ukingojea kugombezwa au kuitwa kwa kuwa nilifanya kosa la kumpiga kikumbo, lakini haikuwa hivyo. Mr. Xavery alinitazama hadi napotea. Nilipofika mbele niliketi katika kiti cha wageni kwa kuendelea na ufutiliaji wa ule uzinduzi.

Huwezi amini ndugu waandishi... Toka hapo nilitamani kuonana na Mr Xavery kila saa. Hata naye aliporudi kuketi sehemu yake ya mbele, jicho langu lilikuwa kwake tu. Nilishindwa hata kusikia kile kinachoendelea katika ukumbi. Nilihisi sauti ya Mshereheshaji inanisindikiza katika penzi jipya lililostawi mda mchache.

Basi kuna muda nilikua nazubaa mwenyewe na kuwaza ikawaje siku moja niwe na Mr. Xavery sehemu tumetulia, upepo ukitusogelea kwa bashasha za kutusifu kuwa tumependeza.

Moyo wangu ulianza kujadili habari za Mr. Xavery, ukataka kufahamu kila kitu kuhusu huyo mtu. Nikawa nabinyabinya tu kifundo cha mtandio wangu mda mrefu bila kujua, mara ghafla nilishitushwa na Sauti nzito kidogo iliyishiba mahaba, ilitoka kwa upole na kuushitua moyo wangu. Hizi ndio zile sauti ambazo wanasema kuwa zinatoa nyoka pangoni.

"Please, tunaweza pata picha ya pamoja" Aisee.. Ndugu waandishi. Nawashauri, kabla hujampenda mtu kupitiliza jitahidi kwanza kuushinda moyo wako usikupeleke mputa.

Mimi nilishindwa kudhibiti mihemuko yangu. Aliponigusa na mkono wake na kulia mwili mzima ulisisimka. Hakunishika sehemu mbaya za hisia, ila bega. Bega tu! lakini kama aligusa mbavu zangu. Nilisisimka mno na kujikuta napata na ujasiri wa kumtazama machoni. Aseeee!. Aseee!!! masekunde yalipita tukiwa tunaangaliana tu kama watu waliotamani kubadilishana vimiminika. Tuliganda hivyo kama waigizaji wa filamu za kikorea

Yeye alikiwa ameduwaa na uso wangu wenye weupe kwa mbali, dimpozi zikiwa kama zinataka kutoka nje ya mwili lakini zinaogopa. Kope za macho yangu zilisimama wima bila kutikisika. Ilikua ni Paap Kwa Paap.. Ana kwa ana. Eppie kwa Xavery! Waaaaho!!!"

EPPIE alisimulia kwa hisia sana kipengele hiki, ukumbi mzima ukashuhudia ni kwa jinsi gani mapenzi yalivyo, hasa ukimkabidhi mwanaume au mwanamke moyo wako. Unakuwa kama umechanganyikiwa hivi. Eppie sasa hata ule machozi uliotiririka mwanzo, ulikauka. Macho yalikuwa makavu sana kuelezea ni namna gani alipenda. Aliendelea kusimulia.

"Ndugu waandishi, hata mimi pia nilikua na fikra za kumchambua mwanaume huyo, alikuwa na sura ya upole sana, alikuwa mtu mwenye weusi wa kung’aa usoni, alionesha pia ni mtu mwenye mazoezi kidogo kutoakana na misuli yake ya kichwa ilivyojipanga. Mimi Eppie nikajikuta nimefia hapo. Nimekufa.. Nimekufa.

Inaendelea…





MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 04.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

"Ndugu waandishi, hata mimi pia nilikua na fikra za kumchambua mwanaume huyo, alikuwa na sura ya upole sana, alikuwa mtu mwenye chunusi kiasi usoni, alionesha pia ni mtu mwenye mazoezi kidogo kutoakana na misuli yake ya kichwa ilivyojipanga. Mimi Eppie nikajikuta nimefia hapo. Nimekufa.. Nimekufa!.

CHOZI LA NNE!

"Baada ya kila mmoja kutosheka kumwangalia mwenzake Mr. Xavery alinishika mkono na kuninyanyua taratibu hadi mbele. Lilikuwa ni tukio la haraka sana kwani hadi nanyanyuliwa sikujitambua kwa kweli.

Kwa kweli hadi picha inapigwa, mimi nilikua sipo kabisa katika pozi. Bado niliendelea kuupongeza moyo wangu kwa jambo lililotokea. Niliposhangaa kidogo tu, sikumuona tena Mr. Xavery nilimtafuta kwa macho kila kona sikumuona. Hapo hapo nikaanza kupatwa na wivu, nilitaka kuanza kumchunga kama mume wangu wa ndoa. Aseee Jamani, Mapenzi uchizi eti, ivi kweli mimi nilikua najielewa kweli?"

Eppie alisimama kidogo kusimulia na kuutazama ukumbi. Alipeleka macho yake huku na kule kama kuna mtu ana mtafuta hivi. Baada ya sekunde kadhaa alirejea kipaza sauti chake. Akakohoa kidogo na kuendelea..

"Basi, shughuli za uzinduzi zilihitimishwa vyema katika Kumbi hiyo, sikuweza kumuona tena Mr. Xavery.

Nikafanikiwa kurudi salama sehemu niliyopanga, kilikuwa chumba akimoja chenye kitanda, kabati na vifaa vya kupikia nilivyonunua kupitia msaada wa pesa zangu za serikali (Boom). nikaoga mapema sana na bila kula nikajikuta natafuta mda wa kuzifichua hisia zangu. Nilitaka nipumzike ili ile picha iliyonitokea mwanzo pale ukumbini basi inirudie tena.

Nilijilaza mtoto wa watu mwili ukiwa juu ya kitanda, macho yakiwa juu sambamba na feni. Kadiri feni inavyozunguka na ndipo akili yangu iliponipeleka kule nako hitaji. Unajua mda mwingine nilihisi kabisa ni uchawi!. Au ni kwa sababu ni pendo langu la dhati la mara ya kwanza?.

Niliwaza sana na mda mwingine kujikataa kwamba sio akili yangu kumng'ang'ania mwanaume kiasi kile. Swali ambalo lilikuwa linaniumiza Kichwa ni lile la Je kama akiwa ameshaoa?.
----

Siku zilivyozidi kwenda mbele nikaanza kubadilika kabisa. Nikawa najiandaa kuwa mke wa mtu haswa. Mwanaume yoyote yule akiniuliza au kunihusisha tu na suala la mapenzi ninampa taarifa kuwa nimechumbiwa na ni mke wa mtu ambaye anaheshimu sana mume wake mtarajiwa. Tayari nilishamkabidhi hisia zangu mwanaume ambaye sikuhisi kama anahisia na mimi kwa muda huo. Ila nilikua na iamani tu.

Nilipoteza hata baadhi ya marafiki wa kiume ambao nilijua tu nao walikuwa nami kwa kigezo cha urafiki ili wapate kuishawishi katika uhusiano wa kimapenzi.

Tukiende mbele zaidi, kuna siku ambayo nilipata nafasi ya angalau kutuma ujumbe mfupi wa WhatsApp Mr. Xavery ambapo namba yake nilipata katika makundi ya kulipia ya Simulizi Huru Media.

Sikua hata na la kusema lakini nilipapasa maneno moyoni mwangu na kutoka na maneno machache tu;

“Habari!, Pole na Kazi.. Nakutakia siku njema” ujumbe huu uliganda hewani bila kufunguliwa hadi saa tano za usiku. Jibu lake likaibua tena hisia zangu na kuzidisha upendo wa dhati, upendo ambao umenibandika leo jina la Muuaji. Je machozi yangu ndio sababu ya kifo chake? Labda!. Siwezi kutoa jibu wakati mahakama imeshatoa maamuzi. Mimi ni muuaji.

Basi, ujumbe wake uliorudi ulisomeka hiuvi “Asante, Sijakupata lakini”. Kwa hakika jumbe hii niliisubiri kwa hamu sana.

Ilinichukua muda kujitambulisha hadi mhusika anatoweka mtandaoni. Nikiendelea kuirudiarudia kusoma ule ujumbe hadi usingizi ukanipitia. Ebu tazama!, Ujumbe wa maneno matatu tu alioutuma niliusoma lisaa lizima hadi kulala?. Waandishi naomba wenyewe ndie mpime nini namaanisha!. Nilipenda kweli jamani. Nilipenda mimi mwenzenu na kwa vile bado nilikua na usichana wangu ndo ukaanza kunisumbua kabisa. Yani kama niliuchochea hivi…

Nilikuja kuujibu ujumbe ule siku ya pili yake na hapo mawasiliano yalianza lakini yalikuwa kwa kusuasua. Mungu mkubwa kuna siku alikuja mgeni pale napohishi. Alikuwa ni mwanmke aliyestaharibika vyema. Aliweka shungi hadi kufunika nywele na masikio yake. Alikuja na kunipa bahasha kisha akaomba kuomba kuondoka. Nilipomuuliza ni kutoka kwa nani alisema maelezo yote yapo humo ndani ya bahasha, basi nikamsindikiza.

Nilipofika ndani niligundua mtu yule kama kuna sehemu nilishawahi kumuona. Yes! Alikuwa ni mwanamke kutoka Simulizi Huru Media Proction. Ni mwandishi kwa jina la Talhat Moudy. Kichwa change kikang’amua hivyo.

Nikitoka mbio kurudi hadi pale nilipoishia kumsindikiza yule mwanamke; hakukuwa na mtu. Alishatoweka Talhat. Nikarudi ndani na kuparamia ile bahasha. Niliichana na ndani nikakutana na karatasi moja gumu nyeupe, lililosheheni rangi za mahaba na maandishi machache mazuri. Pembeni kulikuwa na ka-ua ka’plastiki kumaanisha jumbe hizo zililenga huduma ya mapanzi....

ITAENDELEA…


Pata Simulizi Hii kwa Tsh 2000 tu. Ipo full kwa Vipande 25.
Namba ni 0672493994
Natuma Wasap.
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 05.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

Nikitoka mbio kurudi hadi pale nilipoishia kumsindikiza yule mwanamke; hakukuwa na mtu. Alishatoweka Talhat. Nikarudi ndani na kuparamia ile bahasha. Niliichana na ndani nikakutana na karatasi moja gumu nyeupe, lililosheheni rangi za mahaba na maandishi machache mazuri. Pembeni kulikuwa na ka-ua ka’plastiki kumaanisha jumbe hizo zililenga huduma ya mapanzi....

CHOZI LA TANO..
"Hi Eppie!, Nisamehe kwa kuchanganya herufi za jina lako, japo sijatoka katika uhalisia.
Nimekuwa katika wakati mgumu sana wa kufanya uamuzi huu. Japo itakushitua kidogo lakini hakuna namna nyingine ya kunusuru moyo wangu.
Nimekuwa na wakati mgumu tokea nikutie machoni kwa siku ya kwanza. Nikawaza na kuwaza. Nikatamani kila pande ya kuta za chumba changu nikuone wewe tu. Nilifanikiwa. Nikachukua picha yako na kutandaza katika kuta za cha chumba changu.
Ok. Eppie, nimekufuatilia sana, kila sehemu, nikakujua vizuri kabla hata sijaandika jumbe huu. Hivyo ninahakika Kwetu wamepata Mkwe.
Nakupenda Eppie.
Ni mimi Mr. X"

BAHASHA niliyofungua ilikua na ujumbe mzito namna hiyo. Roho yangu ilipaa haswa. Nilinyanyuka kitandani na kusimama. Niliisoma tena ule ujumbe vizuri. Nikakaa. Nikasimama tena na kurukaruka. Nikakaa, nikasimama tena na kumalizia kunusa ua lililoambatanishwa na hile barua ambalo halikuwa na marashi kabisa ila nilihisi lina harufu ya peponi.

Upande wa pili wa lile karatasi la ujumbe lilikuwa na picha kubwa iliyonata karibia kila pande ya karatasi. Ilikua na rangi zile 'Original' zenyewe, mimi nikiwa kushoto na Mr. Xavery akiwa kulia. Alooo!

Nilipata wehu kwa muda. Nilihisi hata kujikojolea. Ni bahati gani hii ambayo imenikuta mimi?, yani bila kuchezewa usichana wangu hatimaye ninatimukia kwenye ndoa?.

Nikawaza hata kutoa taarifa zile kwa mama yangu mzazi lakini nikaghaili baada ya kuona taarifa hile haikuwa na uzito bado.

"Yanipasa nipate uhakika kwanza. I Love You Mr. Xavery. Mume wangu mtarajiwa" nilijisifia mno nikiwa mwenyewe. Kwa kweli habari zile nilitamani sisambae kwa haraka sana. Kwa wale ambao wamewai kupenda au kupendwa kweli, wanaelewa nazungumzia nini.

Basi haukupita mda nilikuta na ujumbe mwingine WhatsApp wa salamu. Niliujibu haraka sana. Tukachati na aliomba kukutana na mimi uso kwa uso.

Nilipanga hata kuvunja vipindi vya chuo ili nionane na laazizi huyu lakini alinipoza na sauti yake ya WhatsApp ya mahaba alisema,

"Anhaa.. Hapana. Kuwa kwanza huru, jaribu kuweka siku ambayo haitakuathiri kabisa hata kisaikorojia. Ebu kuwa huru kwanza"
Aliongea na hapo ukawa mwanzo wa mapenzi na mawasiliano mazuri kati yangu na marehemu mume wangu Mr. Xavery.

Wanasema, fuata nyuki ule asali... Mimi nilivalia njuga hisia zangu na nikapata faida sana juu ya hii.
Nilipanga siku ya Jumamosi kuwa ndiyo siku ambayo tutakutana mimi na mume wangu mtarajiwa. Nadhani siku hii ndio chanzo hasa ya kuutoa uhai wake. Alinipa sumu ambayo niliishi nayo moyoni hadi kumuua nayo yeye mwenyewe. Siku hii nayo imeingia katika historia ya maisha yangu.

"Ah, karibu Eppie. Karibu kuketi" Nilipofika tu eneo husika nilipokelewa na sauti yenye tabasamu nzito usoni. Nilikaa.

Alichukua dakika kama moja hivi nayeye kukaa, alinitazama huku akitabasamu kila wakati.

"Hallo, watumia nini?" aliniuliza na kunitazama usoni. Bila shaka alipendezwa na aibu yangu. Kila mda nilijitahidi kuficha macho yangu yasionekane. Yeye hakujali hilo aliendelea kuachia tabasamu lake hadimu kila mda. Nilimjibu kuwa nakunywa chochote kile, hasa kile atachoagiza yeye.

Hakuangaika kupaza sauti kuita mhudumu, alinyanyuka mwenyewe na kuelekea sehemu ya huduma. Alivuta bilauri mbili za juisi na kuja nazo.

"Karibu" alinikaribisha. Na kunisihi niwe huru kila wakati.

Katika maongezi hayo nilikua msikilizaji kwa kiasi kikubwa mno, ili niweze kumsoma mwenzangu na labda naweza nikagundua madhaifu yake.

"Unasoma eh?" alinuiliza na nikaitikia kwa kichwa. Aliuliza swali ambalo majibu yake aliyafahamu.

"Mwaka wa tatu?" aliuliza swali lingine lakini hakuniangalia kama nimeitika au la. Alimimina kinywaji chake taratibu kinywani na kukishusha.

"By the way! Vyote hivo navifahamu na nisamehe sana kwa kukufuatilia kinyemela.
Ah, Eppie. Natamani nifumbe macho na nitamke maneno haya."NAKUPENDA" Sijajua utalichukuliaje suara hili, ila naomba niliwasilishe kwako tafadhali. Toka nikuone machoni mwangu, nimeshindwa kupata usingizi, kazi hazifanyiki. Moyo unahitaji mtu sasa na wewe ndiye sahihi kwangu. Nakuomba..." aliongea taratibu na kumalizia kinywaji chake.

"Kwani.. Ah. Kwani wewe hauna mke jamani?" nilijikakamua kuuliza swali ambalo sikujua hata limetokea wapi. Lakini nilijipa ahueni kwamba nitafahamu kitu kuhusu yeye.. Nikatega sikio kusikiliza jibu ambalo lilipa mwanga wa kutengeneza kifo chake. Pumzika kwa amani kipenzi Mume wangu!
.
.
Tuna patikana Youtube na Katika Ukurasa wetu wa Facebook #SIMULIZI HURU MEDIA PRODUCTION.

Inaendelea....
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 06.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

"Kwani.. Ah. Kwani wewe hauna mke jamani?" nilijikakamua kuuliza swali ambalo sikujua hata limetokea wapi. Lakini nilijipa ahueni kwamba nitafahamu kitu kuhusu yeye.. Nikatega sikio kusikiliza jibu ambalo lilipa mwanga wa kutengeneza kifo chake. Pumzika kwa amani kipenzi Mume wangu!

CHOZI LA SITA....
"Haha, Swali zuri sana Eppie" Alijibu na kisha kukaza macho kunitazama. Nami nilianza kula nae sahani moja, niliondoa na mimi ule woga wangu. Tukabaki tunashangaana kwa muda kabla hajaendelea kuongea.

"Yahp!, nipo na Mke" Ah, Nikishituka sana niliposikia kauli hii. Mapigo yangu ya moyo yalianza kudunda kwa nguvu hadi kutikisa meza.

Nilianza na kutetemeka mwili mzima. Sasa, anae Mke, mimi ananipendea nini au kwanini awe kiburi cha kulopoka neno zito kiasi hiki mbele yangu si hata angeniongopea tu jamani. Nilikua radhi kupokea uongo kuwa aniambie tu hana mtu hata kama yupo.

"Haha Mke ninaye!, mzuri!, Mwalimu!, mcheshi kwa lugha, kipenzi cha wengi pia. By the way, sina mwanamke mwingine zaidi ya Fasihi. Naipenda sana Fasihi, huyu amekuwa mke wangu kwa mda mrefu sasa. Nilipokuona wewe nikaongea nae na akanikubalia kuongeza mke wa pili. Nakupenda Eppie" Alifafanua alichomaanisha na mwishowe kuomba tena upendo wangu kwake. Yaani alimaanisha baada ya mimi kuna kitu kingine ambacho alikuwa anakipenda kupita amaelezo, kilikuwa ni fasihi.

Huyu mwanaume alikuwa ananichezea kwa kweli. Alijua kuendana na mazingira sana. Nilifumba macho na kumshukuru Mungu kunipa mwanaume mzuri na bora ambaye alitambulika kwa hisia zangu tu.

Mr. Xavery akapata kibali cha kupendana na mimi. Akakaa kiti cha mbele kabisa katika moyo wangu. Kiti ambacho kilikua kizima kabisa. Kilipambwa kwa rangi nzuri za kuvutia. Sikujua kama kitakuja kumwangusha na kumzika mazima. Sikujua ndugu waandishi. Labda ndio sababu ya mimi kuwepo hapa na kuwapa ushuhuda huu.

Nilimkubalia palepale na nikapata nafasi ya kumuuliza maswali mawili matatu na yote akajibu kama nilivyohitaji. Alinipa historia fupi ya maisha yake kabla hata hatujaachana sehemu ile.

"Kwa majina matatu ni Xavery Emmanuel Luoga. Napenda kujitambulisha kama Mr. X.
Maisha yangu yalianzia utotoni huko mjini Songea, nilimaliza Elimu zangu za msingi huko na kumalizia shule za upili mkoani Songwe.

Nilibahatika kusomea Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na kumaliza shahada yangu ya kwanza. Hapohapo ulipomaliza wewe lakini nilikutangulia madarasa kama matatu hivi.

Toka hapo sikuhangaika kabisa na soko la ajira. Moja kwa moja nikajikita katika taaluma ya fasihi. Hadi hapa leo ni Wanachama wa Simulizi Huru Media kitengo cha Habari.

Sikubahatika kujihushisha kabisa katika mahusiano ila nipo na marafiki wengi wa kike. Labda kwasababu niliempenda mwanzo alipoteza maisha. Toka hapo, Mungu akanionesha wewe!. Nikakupenda. Nakupenda. Nakupenda Eppie" Historia yake aliimaliza hivyo na kumalizia tena neno lake lile lile.

Nilitabasamu na kufurahi sana. Hiyo ndio siku ambayo iliunda siku nyingine zaidi ya mia moja. Moyo wangu ukamwamini mwanaume mmoja tu. Mr. Xavery.

Siku na Miezi vilizidi na kuzidi. Ukaribu wetu uliongezeka sana na mara moja moja alikua anakuja hata chuo kunisabai. Jambo ambalo hata marafiki wangu hawakuamini ni kuwa hatukuwai kuongea wala kugusia kipengele cha kufanya mapenzi. Labda haya mabusu madogo madogo ndani ya gari lake. Tena tulipeana kama watu waliokumbukana kwa muda mrefu. Nilifurahi nilipata mtu nilie mwamini sana.

Habari zilifika hadi nyumbani kwa mama kuwa baada ya masomo yangu ya shahada ya kwanza natarajia kuchumbiwa, yakiwa maandalizi kabisa ya kuvaa Shera. Ni wachache sana walivaa ili vazi katika ukoo wetu hivyo kila mtu alikua na hamu ya kushuhudia. Jambo hilo lilifanya chuo kimalizike mapema sana. Nikamaliza chuo ndugu waandishi.
----

Ah, ilipata mwezi mmoja baada ya kuhitimu chuo. Bado niliendelea na kukaa palepale nilipopanga mwanzo, huduma zote nilikua napata kutoka kwa mume wangu mtarajiwa. Kutokana na upendo huu nilifanikiwa tena kupoteza marafiki wengi sana, hasa wa kiume. Haikunipa shida. Nilikua na wa kuniliwaza jamani.

Kama jinsi tulivyo wanawake, nilianza kulialia kwamba anichukue tukaishi wote nyumbani kwake lakini aligoma. Aliendelea kusisitiza kuwa yupo na hulka na hisia na mimi, na hapendi kukatisha imani yake na ahadi yake aliyoiweka mwanzo. Alisema eti siku Mungu akihidhinisha kuwa mimi na yeye ni Mke na Mume ndipo itakuwa siku ya mimi na yeye kuanza kijidai pamoja. Aligoma Mr. Xavery, alikua na msimamo sana,

Jambo ambalo nikikua silipendi, ni kusikia anamahusiano ya kirafiki na wanawake wengine. Mchezo huu sikuutaka kwake lakini sikutaka kuonesha kabisa niliogopa kujenga wasiwasi. Nikaendelea kuishi na dukuduku langu.

Mwezi wa Kumi na moja mwaka 2021, nilipata shahada ya kwanza ya ualimu. Mwezi huohuo nikapata na shahada nyingine ya Ndoa. Alhamdulillah! Nikawa Mke halali wa Bwana Xavery Luoga. Mke wa Ndoa ya Dini...
.
.
.
Tusaidie kuupenda Ukurasa wetu wa Simulizi Huru Media
.
Inaendelea....
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 07.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

Mwezi wa Kumi na moja mwaka 2021, nilipata shahada ya kwanza ya ualimu. Mwezi huohuo nikapata na shahada nyingine ya Ndoa. Alhamdulillah! Nikawa Mke halali wa Bwana Xavery Luoga. Mke wa Ndoa ya Dini...

CHOZI LA SABA....
Hakuna aliyehamini tukio hili, kila mmoja ilimpasa kushuhudia kwa macho yake mawili. Nikaweka rekodi ya kuwa kati ya wanawake wachache duniani ambao wamefunga ndoa wakiwa bado na usichana wao.

Kila kitu kilienda sawa na harusi ilikuwa kubwa tu. Ukumbi mkubwa, mambo makubwa, hata ndugu zangu wasio na uwezo wa kutembea walikuja jijini kwa usafiri maalumu ulioandaliwa kwa ajili yao hadi siku ya kurudishwa.

Hakukuwa na sababu iliyoonekana kwa mtu kukosa shughuli hii. Tulipunguza changamoto nyingi sana na hii ilimaanisha kweli Mume wangu ananipenda kwa dhati. Nilifurahi mno.

Hatimaye Eppie nikawa ndani ya Nyumba. Nyumba ilikuwa maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam karibu kabisa na jengo kubwa la vioo linaloimurika Kariakoo

Nilikua ni mtu mwenye furaha sana kwa kweli, ndani kulikua na kila kitu, televisheni, redio, na vifaa vikubwa vya muziki. Getini hakukuwa na hata mlinzi, kulishatandazwa waya za umeme kutahadharisha wezi na wavunjifu wa amani katika nyumba za watu. Unadhani juu ya yote hayo nini nilikosa?

Mtu wa kuongea nae kutwa nzima. Kama wewe ni binadamu wa kawaida basi huwezi siku nzima ukakaa pekee kutazama tu televisheni au kucheza na vyombo vichafu, hususani sisi wanawake?, lazima utafute kijisehemu cha kushikiza hata maneno mawili watatu.

Niliongea na mume wangu kuwa nahitaji nikae na mtu kipindi yeye yupo kazini, lakini hakupenda kuongelea suala hili. Halihakikisha tu atokapo asubuhi kila huduma inayomuhusu yeye ameiacha. Sikupata shida kwa kweli.
--

Kuna siku nilipata nafasi ya kutoka na kuzunguka baadhi ya maeneo jijini, yote ni kutafuta vifaa na vyakula vingine vya kwenye jokofu. Niliona hakuna shaka pindi nitakapotafuta hata fundi wa kunifunga nywele zangu ili ziwe katika mwonekano tofauti.

Kwa kusema kweli, Mume wangu hakuwai nikataza kabisa nisitoke. Nilikua huru katika kila kitu. Hata wikiendi akitoka kazini basi hunichukua majira ya jioni na kuumaliza usiku katika mahoteli makubwa kubadili hata radha ya hali ya hewa.

Huko nilipoenda kujishikiza nywele nikakutana na washauri nasaa. Jamani kuna wanawake wanaongea!. Wanaongea hadi naogopa. Ikaja maada amabayo inanilenga moja kwa moja mimi, lakini niliogopa kuchangia. Nikakaa tu kusikiliza.

"Unakuta mwanaume anakupa kila kitu ndani, kila kitu kipo mwaya, lakini akitoka, basi ametoka. Tena wanaume wengi ndio hujishikiza haswa katika kukupa kila kitu ili uridhike tu na usiweze kumfuatilia katika mambo yao.." Dada Msusi aliongea. Aliendelea kusema kuwa,

"Mimi Mume wangu alikua ananifanyia mchezo huuhuu, akitoka nyumbani anaacha kila kitu, anenda kazini huko hadi mida ya kwenda kwa malaya zake. Mimi si niliridhika tu na vyakwangu jamani, kumbe kuna wahuni wapo tu nao wanajilia mume wangu.." yule Dada aliongea sana.

Japokuwa sikuchangia chochote lakini nilitoka na kitu. Wivu ukaanza kunijaa haswa. Nikamsubiri mume wangu aje na kumuomba anipeleke anakofanya kazi. Hakubisha, akanipeleka tena alinipeleka hadi ofisi za viongozi wake.

"Kaka Sam, huyu ndiye Mwandani wangu, Mke wangu. (akinigeukia) Mke huyu ndie Mkurugenzi hapa Simulizi Huru Media. Hakika najivunia kufanya kazi naye.." Alinitambulisha kwa kila mtu sehemu hile.

Nilifurahi kwa kuwa alisikiliza kile ambacho nataka. Lakini roho yangu haikuridhika kabisa, nilitamani anipeleke hadi marafiki zake wa kike lakini alikili kuwa marafiki zake wengi wanakutana Online, lakini alianza kupata wasiwasi juu ya wivu wangu.

"Mke wangu nini shida?, nachelewa kurudi nyumbani au kuna utofauti umeuona kutoka kwangu?" aliniuliza swali hilo na likakosa majibu kabisa. Sikujua cha kujibu kwani hakukuwa na utofauti kabisa kati yangu na mume wangu. Alikuwa mhumini vilevile, Mcha Mungu na mtu anayempenda sana mke wake.

Kimbembe kilianzia hapa!, ni siku ambayo nilitapika sana mbele yake. Nilichukizwa na hali hii ya kutapika tena ikinirudia zaidi ya maramoja, lakini yeye aliniangalia na kuniambia tu,

"Bado utakuwa chini ya uangalizi wangu mke wangu" Aliongea hivyo na sikuelewa anazungumzia nini. Tuliivusha siku ile bila kugombana. Kwa maana nilijikuta tu ninakisilani ajabu.

Siku iliyofuata nilianza tena kuhisi kuwa sipo peke yangu, kuna kiumbe kingine kimeanza kusumbua tumboni mwangu. Nikainua simu na kupiga.

"Please! Najihisi vibaya.. Wahi nyumbani mara moja" kisha nilikata. Sikujua kwanini nimefanya hivyo lakini ikatokea. Jamani ni shetani gani anawapanda wanawake katika kipindi kama hiki? Ewe mwanaume muelewa wa hali hii wafundishe wanawake jinsi ya kuhimili hulka zao za mimba. Mwanamke akiwa na mimba kama atashindwa kujihimili basi atawachukiza wengi sana.

Basi tulienda hospitali na kukutwa nina ujauzito. Hakika ilikua furaha sana hasa kwa mume wangu. Bila shaka alisubiri kwa muda mrefu sana hali hii. Hii ilionesha tu pindi alipozidisha mapenzi kwangu. Yaani sinahakika alinipenda sana mume wangu, lakini sasa je Kwanini Nimuue???..
.
.
.
Kuanzia kesho zitakuwa zinaruka mbili
#Machozi_Ya_Damu
#TALAKA_KWA_MKE_MWEMA

ITAENDELEA...
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 08.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

Basi tulienda hospitali na kukutwa nina ujauzito. Hakika ilikua furaha sana hasa kwa mume wangu. Bila shaka alisubiri kwa muda mrefu sana hali hii. Hii ilionesha tu pindi alipozidisha mapenzi kwangu. Yaani sinahakika alinipenda sana mume wangu, lakini sasa je Kwanini Nimuue???..

CHOZI LA NANE...

Hadi kifikia hapo Eppie alianza tena kulia. Hapa hakuna aliyejitahidi hata kuongea kitu. Waandishi walifuta vumbi katika vioo vya kamera zao na kuweka tena sawa kwaajiri ya kurekodi. Eppie alikua anasimulia polepole na mda nwingine kwa kucheka, kufurahi, na kulia kama mtu aliyebanwa na kwikwi. Alipoona yupo tayari aliendelea kusimulia.

"HAKIKA sijawai kupata Upendo kama huu toka niingie kwenye ndoa. Hapo ndipo nikaamini kuwa kumbe wanaume nao wanahisia...

Alikubali lolote nililosema hata kama linaonekana wazi kuwa ni uongo. Siku za kliniki basi naye hawezi kufunga safari kwenda sehemu nyingine, anatayarisha gari mapema ili mke wake na mwanaye kijacho wakae na kuwapeleka kituo cha afya.

Wivu wangu ulijaa mara dufu, sikujua labda ni sababu ya ujauzito. Lakini Hapana!. Ndio nifanye vitu kama vile?. Nilihitaji kumuona mme wangu kwa ukaribu sana. Nikasahau kama anamajukumu ya kuandika Simulizi na kuendeleza kikundi chao cha SIMULIZI HURU MEDIA PRODUCTION kilichomtoa kimaisha hadi kujipatia ka gari na nyumba ambazo sasa tunatumia.

Sikumpa hata mda wa kupumzika mume wangu, kadiri mda ulivyokuwa unaenda; akiweka makalio chini tu, basi namuagiza tena kunichukulia au kunifanyia kitu...

"Baba, jokofu halina kitu.. Si ungejaza kabisa!" Mda mwingi nilikua natoa amri. Hakupinga!. Hakupinga sababu aliweka matumaini kwa kiumbe chake. Anasimama na kutekeleza jukumu aliloagizwa.

Kipindi hiki nipo mjamzito mume wangu alikuwa mshika dini sana, Jumapili wote kanisani, jumamosi anachezea tumbo langu kutwa nzima. Siku nyingine ni mara mojamoja sana ndio huenda kazini.

"Unaenda wapi baba"

"Kazini!"

“Jamani kwani hujui kama mimi naumwa.. Dah, basi niandalie kabisa samaki"

Hayo ndio yalikuwa maneno yangu. Mume wangu hakuwa mkasilikaji hata kidogo. Akatabasamu, akalegeza tai yake. Akachomolea shati lake na kuingia jikoni. Hata iwe sa kumi na moja asubuhi anapika hizo samaki ambazo nakua hata sina hamu nazo kula kwasababu ya mafuta yake.
--

Ilikuwa ni takribani miezi saba sasa tangu nikuze kiumbe changu. Maisha yangu yalikua na furaha sana kwa kuwa na mume anayenipenda na kuwa karibu naye kila wakati. Lakini akaleta Wazo. Wazo jipya na lenye umuhimu kwetu.. Lakini likawa pia sababu ya kuhusika na kifo chake.. Ewe Mungu nisamehe mimi kiumbe mdhambi.

Mume wangu alikuja na wazo…

"Mke wangu, hii miezi yahitaji mtu, niina maana msaidizi... Kufua, kupika, kukuangalia kila mara, pia maandalizi ya mtoto... Si unajua sisi wanaume wazito sana kununua madishi na vifaa vya kujifungua?" aliongea kifasihi zaidi lakini nilimuelewa.

Kweli alihitajika mtu sasa wa kuwa karibu. Kwamaana mume wangu hakuwa mzuri katika kuchagua rangi wala 'Size', usije akaninunulia Soksi za kike kwa mtoto wa kiume bure!. Wazo likapita la kuelekea kumchukua msaidizi.

Baada ya siku mbili alielekea huko Mkoani Ruvuma Wilayani Mabada. Alitumia usafiri wake kwenda kusalimia wazazi wangu na kumuomba mdogo wa kike Vaileth ambaye alinifuata, kuja kunisaidia shughuli za mwishoni mwa ujauzito. Kila kitu kikaenda sawa.

Anaitwa Vaileth Mkombo, ni mdogo halali wa Epifania Mkombo. Tulizidiana miaka miwili tu mimi nikiwa mkubwa wake. Kwa umbo lake lilivyo unaweza kudhania ni mtoto aliyehitimu kidato cha nne hapo juzi. Tulifanana kidogo sana sura kutokana na kila mmoja kurithi upande wake. Vai na Mr. X wote walifika nyumbani salama.

"Wao Dada ake!, hapa nilikua nawaza kweli kama utakuwa umebadilika... Hivi umegoma kabisa Kusuka?" Yalikuwa ni maongezi baada ya kupokea kila kitu.

"Dada... Wanajeshi na kusuka wapi na wapi?, nasukia maadui au?, kwanza nina hasira sana sikuhudhuria siku ya ndoa yenu" aliingea kwa kubinya midomo huku akituangalia wote kwa zamu mimi na mume wangu.

"Hivi hukuwepo Shem?" alidakia mume wangu huku akicheka kwa mfululizo.

"Niwepo wapi? Mda huo Kozi za Jeshi ndio ziliumana!.. Hakuna likizo, hakuna kutoka, labda nijikoshe tu kwa picha" Aliongea na kunyanyuka katika sofa alilokaa, alisogea hadi ilipopicha kubwa ukutani. Ilikua ni picha ya siku ya ndoa. Ilikua ni full BLACK AND WHITE (Nyekundu na Nyeupe). Baba Ndani ya Suti na Mama ndani ya Shela...

Mdogo wangu alikua mcheshi sana... Sitaki kumshushia lawama kuwa naye alihusika katika kifo cha mme wangu. Hivi kweli mdogo wangu Vain awe ulihusika katika huu makasa!. Ona sasa hadi sheria imechukua mkondo wake....
.
.
.

ITAENDELEA...
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 09.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

Mdogo wangu alikua mcheshi sana... Sitaki kumshushia lawama kuwa naye alihusika katika kifo cha mme wangu. Hivi kweli mdogo wangu Vain awe ulihusika katika huu makasa!. Ona sasa hadi sheria imechukua mkondo wake....

CHOZI LA TISA...
Nilianza kukaa na mdogo wangu siku baada ya siku, alikua mchapakazi sana kama nilivyomfahamu. Vitu vingi sana alivifanya kijeshi kutoka na mazoea. Mdogo wangu alikua katika kozi maalumu za Jeshi la kujenga taifa huko mkoani Iringa baada tu ya kuhitimu kidato cha nne. Hadi sasa yupo kwanza nyumbani kusubiri matokeo ya uchaguzi wa ajira za kazi hiyo.

Mume wangu alipata kupumua sasa kwani aliendelea kwenda kazini kila siku, lakini alichelewa kutoka nyumbani na pia aliwai kuja nyumbani. Kweli alikua ananipenda mume wangu.. Lakini najua bado mnajiuliza kwanini sasa nimuue!

Aaah ha ha ha, sitaki kuikumbuka hii hatua kwa kweli. Sihitaji waandishi.. Kweli NDOA kumbe ndio ina mazuri na mabaya kiasi hiki? Lakini mbona mazuri nilivumilia... Kwanini nishindwe mabaya?. Inasikitisha kweli jamani... Au alilipa yale ambayo mimi nilikua namfanyia? Kumchelewesha kazini, kumkalipia, kumgomea, kumsumbua.. Hivyo tu. Hivyo tu jamani. Au yeye alikua ananiigizia. Ah!. Bora.

Bora hata nimemuua mume wangu. Nili-choka jamaniiii...." Aliongea kwa kasi sana Eppie. Ndani kukalipuka tena kwa machozi. Alilia sana Eppie. Bado kuna dukuduku lilikua linamsokota. Lilimkaba haswa, alikua anatafuta namna ya kulitoa. Sasa akaendelea...

"Dada, umepata mume Bora sana!. Tena amenifunza mengi sana kuhusu wanaume. Hapo mwanzo sikua na upeo huu ambao leo mume wako amekuwa Darasa kwangu, nilikua nawachukulia wanaume ni binadamu kutoka uzao mmoja wa ukatili na watu wasio na huruma kwa wanawake.. Kumbe nilikosea na kuishi hapa nimepata kama Darasa. Mambo kama haya jeshini hayapo kabisa.." Mdogo wangu aliniadithia mema ya mume wangu siku moja tulipoketi kupunga upepo nje nyumba kubwa mimi na yeye. Nilitabasamu tu na kuishia hapo. Nilishamzoea mume wangu. Nikaona kawaida kufanya mema kwa mdogo wangu.

Hekaheka na pilikapilika za tarehe za kujifungua zikakaribia... Mdogo wangu Vai aliniwahisha kituo cha chafya kwa haraka zaidi. Hakuchelewa kwani msaada mkubwa ulitoka kwa daktari binafsi aliyelipwa na mume wangu kuja kunipima kila baada ya siku mbili. Aliniomba niwai hospitali haraka kwani inaonesha kuwa mapigo ya moyo ya mtoto yanapungua.

Nilipofikishwa hospitali nilipimwa na kuambiwa kuwa njia ya mtoto imeonekana kukamilika na napaswa kudungwa sindano za uchungu kumuita mtoto.

Mume wangu alipewa taarifa na haraka kuwahi hospitali.. Nilipata tu habari yupo nje ya chumba cha kusubiri wagonjwa wanaotoka kujifungua.. Kwa hulka za mume wangu nilijua kabisa ameshikilia mlango kuchungulia kiumbe chake kinavyopatikana.. Nusu niropoke kwa manesi wa zamu kuwa "Mtoeni Mume wangu pale mlangoni ananichungulia.. Nashindwa kusukuma kwa kuona aibu" hayo ndio yalikuwa mawazo yangu.

Ndugu waandishi, nisiwadanganye kuwa huu ndio ulikua mwisho wa mapenzi ya dhati kutoka kwa mume wangu... Huu pia ulikua kama mwanzo tu wa dalili za kutengeneza kifo chake. Nashindwa kuhadithia sehemu hii kwa sababu sikujielewa wala kuelewa nini kimetokea. Nilizimia baada ya kujifungua.
---

Baada ya muda nisioujua nilizinduka nipo kitandani na watu tele wakinisimamia. Pembeni kulikua na kijitanda maalumu kwa kuweka wachanga. Nilikivuta kwa shauku ya kuangalia hata jinsia ya mwanangu: hakuna mtoto.

Nilijaribu kutaka kujiinua ili niangalie vizuri lakini waliniwai na kunituliza kitandani. Kila mmoja aligeuka upande wake kwa kunionea aibu. Niliwaangalia kwa hasira mno. Mdomo ulikua mzito hata kutoa salamu. Niliwaangalia wote na kugundua ni Ndugu wa karibu na baadhi ya majilani lakini mtu mmoja hakuwepo mahali pale. Baba wa mtoto.

Wakati najitahidi kuuliza alipo Baba wa Mwanangu gahfla nilisikia mlango unafunguka na watu wawili wakiingia. Mmoja alivaa mavazi ya heshima huku kile kifaa cha kupima mapigo ya moyo kikibembea kifuani kwake.

Mwingine alikuwa ni kijana mrefu kidogo, maji ya kunde, chunusi zake za mda mrefu zilionesha kupotea kwa tabasamu lake. Alikuwa ni mume wangu. Baba wa mtoto wangu.. Mr. X

Aliponiona tu namuangalia aliachia meno yake wazi na kuruhusu tabasamu. Nami nikajibu kwa tabasamu lilelile, nilikuwa namkejeri kila siku.

Yule daktari alipaza sauti yake nzito kiasi kuomba watu wampishe katika kazi yake mara moja. Dakika tu walijikusanya na wote kutoka nje hadi mume wangu.

"Epifania! Unajisikiaje?" Alinijulia hali huku akinisaidia kunifunika mapaja yangu meupe yasio na doa.

"Salama, Nipo vizuri kidogo" nilijibu

"Sawa, Naitwa Dokta Fransis Kadudu. Ni muhusika na matibabu yako hadi kujifungua.." aliongea huku akiniangalia usoni. Niliitikia tu kwa kichwa.

"Ah, Pole sana na Hongera sana kwa hilo. Hakika wewe ni shujaa sana.." aliongea tena kidogo kisha kutabasamu.

"Muda wa takribani lisaa limoja lililopita ulifanikiwa kujifungua kwa njia ya kawaida kabisa, ah, jambo ambalo si la kawaida mtoto alikua na mapungufu kidogo, i mean.. Aa, kuna sehemu hazikukaa sawa. Ahh, anavidole ishirini na nne yaani mikononi sitasita na miguu pia, ah, pia sikio moja na pua vimeungana na sehemu ya ubongo. Kwa taarifa za kidaktari tunaita "ABNORMAL" na zimeonesha mtoto ameshindwa kupumua hata kwa dakika tano tu, hivyo baada ya kujifungua tu, tumempoteza"
.
.
.
Full ni Tsh 2000. Namba ni 0672493994 jina ni Xavery Luoga

Inaendelea
 
MTUNZI: XAVERY E. LUOGA
RIWAYA: "MACHOZI YA DAMU"
SEHEMU YA 10.
WhatsApp NO. 0672493994.
#SimuliziHuruMediaProduction
×--------------SHUMP---------------×

"Muda wa takribani lisaa limoja lililopita ulifanikiwa kujifungua kwa njia ya kawaida kabisa, ah, jambo ambalo si la kawaida mtoto alikua na mapungufu kidogo, i mean.. Aa, kuna sehemu hazikukaa sawa. Ahh, anavidole ishirini na nne yaani mikononi sitasita na miguu pia, ah, pia sikio moja na pua vimeungana na sehemu ya ubongo. Kwa taarifa za kidaktari tunaita "ABNORMAL" na zimeonesha mtoto ameshindwa kupumua hata kwa dakika tano tu, hivyo baada ya kujifungua tu, tumempoteza"


CHOZI LA KUMI...
Hakika taarifa hizi ziliusumbua sana moyo wangu. Nilipatwa na ganzi ya kushindwa kuuliza wala kujibu chochote kile. Machozi yalikwa yananitoka na nilishindwa hata kufumba macho.. Nilibubujikwa na machozi huku mboni ya macho yangu ikiwa usoni mwa daktari lakini taswira yangu ilikua mbali sana.

Ilikua anamuona jinsi mwanangu anavyocheza kwenye maua na baba yake, jinsi anavyolishwa chakula kizuri na baba yake.. Anavyoshushwa kwenye gari na kumpungia mkono baba yake pindi anapopelekwa shule… Kwa kweli roho iliniuma sana. Kwikwi zilinikamatana na kujikuta naishiwa tena nguvu. Macho yakawa mepesi na kufumba ghafla. Nikazimia tena..
*****

Kama wasemavyo wahenga kuwa, tabasamu huficha hisia za maumivu. Nikizinduka na kukuta uso wa mume wangu ukitabasamu mbele yangu. Niliona aibu sana kwa kushindwa kumletea mtoto wake akiwa hai. Machozi yalianza kunitoka tena.

Mwanaume huyu wa tofuati duniani alikusanya shati lake na kunifuta machozi.

"Nyamaza Jasiri wangu. Nafurahi sana umeniletea Kidume japo mungu amemchukua. Tushukuru sana Mungu kwa kufanya hivyo mapema. Kwa hali nilimuona nayo basi bila shaka kama angekuwa hai angekuwa anakuliza kila siku. Au ungeweza kukaa na kiumbe ambaye hawezi kuongea, kusikia, kutembea hata kupumua? Tumshukuru Mungu Mke wangu" aliongea na kunifuta machozi. Ndani humo tulikua mimi na yeye tu.

Aliniinua kwa upendo kabisa na kuniketisha chini. Alisimamisha mkoba wa maji uliokuwa unapeleka maji mwilini mwangu kwani ulikua umeshaisha.

"Pole na Hongera.. Haya nimekuandalia kitu hapa, nikifanya Haaa, unaachama mdomo na mimi naweka mchuzi wa nyama... Aphuuuuu! hauna moto kabisa huu" Hakika huyu alikua mtu wa tofauti sana. Machozi yangu yakakauka palepale na kuendelea kumshangaa kwa vituko vyake. Nilikua nawaza tu nitakua naonekanaje kwenye jamii.. Uzazi wa kwanza na... Na... Na kuzikaaa aaah jamani..."

EPPIE alianza tena kulia kwa sauti. Safari hii alilia hadi mwandishi mmoja wa kike alisogea na kumkumbatia. Alimbembeleza mara kadhaa na kumpa pole. Alimuambia maneno ha kumtia moyo ili arudi katika hali yake. Bila shaka mwandishi yule na yeye alipitia wakati mgumu kama Eppie kiasi cha kuguswa hadi kutoka mbele kabisa ya jukwaa.. Hakika haya ni MACHOZI YA DAMU.

Baada ya dakika tano yule mwandishi wa kike alimaliza kazi yake. Eppie alirudi katika hali yake na kuanza kwa kutabasamu... Naaaam bika shaka anaendelea kukumbuka tabasamu la marehemu Mume wake.

"Ah, Samahani sana jamani sikuja hapa kwa nia ya kuonesha udhaifu wangu hadharani. Bali kutoa sababu na kujibu maswali yenu ya kwanini niliua mume wangu kwa mikono yangu mwenyewe!.

Basi pale, Tulirudi nyumbani na mume wangu pamoja na mdogo wangu Vai. Njia nzima nilijiona ni mkosaji sana kwa kushindwa kutimiza haja ya mume wangu. Kila nikikumbuka kuwa alikuwa ni jinsia ya kiume moyo ulizidi kuniuma sana. Bado mume wangu aliendelea kuwa karibu sana na mimi kwa kila kitu. Nikiwa naye najihisi kama hakuna tatizo kwa ucheshi wake ila akiwa mbali na mimi tatizo ndio hujirudia.

"Mke wangu!! mwanangu hajafia tumboni. Ulijifungua kabisa. Hivyo nimempa na jina. Atakuwa mwanangu wa kwanza kabisa.. Na nimempa jina la BRIGHT kuashiria Mwanga, Akili na nguvu. Hakika alikua mwenye maajabu yake..." Yalikua ni maneno ya ufariji sana. Kama kuna wanawake wenzangu wanasikia hii basi lazima wataonja tu mapenzi haya japo yananitoka kwa machozi. Toka hapo nikamwita Baba B (Bright) na Nami akaniita Ma Bright ili kumuenzi mtoto wetu…

Nisiwe mkosefu wa shukurani pia kwa mdogo wangu na dada yangu kwa wakati mmoja. Vai alikua bega kwa bega na mimi. Alionesha mapenzi ya dhati na kuwa mshauri wangu kila siku. Sikutegemea kama kuna siku naye nitamuhusisha katika tabia mbaya za mume wangu ambazo zilipelekea kifo chake. Daaa...
.
.
.
.


ITAENDELEA...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom